Ukweli kuhusu kwanini unaamini dini unayoiamini

Utoto huo Mimi siwez jadili huo utoto
Mkuu nimekuuliza hivyo kwasababu nahakika hujaelewa vizuri mantiki ya mada

Hapa tunatafuta ni namna gani huyo mungu wa “kweli” anahakikisha watu wote wanamjua? Na sio watu kuamini kwasababu tu za kimalezi jiografia na historia
 
It takes one generation to forget about God, The next generation will know nothing about God....

Kila mtu huzaliwa Atheist mpaka pale anapo aminishwa kuna invisible creature beyond the sky anaitwa Mungu...
Mkuu watu wengi inawawia vigumu kuamini hiki ulichoandika hapa lakini ndio ukweli
Dhana ya Mungu imejaa maswali bila majibu
 
Tuache tu mkuu
 
Mkuu Dini inahusisha kuamini katika nguvu kuu kuliko zote(Mungu, jini nk nk)
Hata hao mababu zetu walikua na DINI zao pia
Imani ni matarajio tu
Nikikukopesha naamini utanilipa

Lakini dini ni mfumo wa maisha kulingana na nguvu kuu unayoiamini
 
Hoja kubwa hapa ni nini ROLE ya Mungu wa kweli ili watu kumjua?
Mungu ndiye anaanzisha harakati zote hadi mwanadamu amjue na kumwamini.

Kila mtu anayo nafasi hiyo 100% licha ya mazingira ya kijiografia au historia ama hali na wakati aliopo.

Ibrahimu alizaliwa upaganini 100% lakini akawa muumini wa Mungu wa kweli.

Utashi ni wa mtu mwenyewe kuamua; but ukweli uko wazi kwa yeyote yule apendaye.

Kwanini kumuamini Mungu ni matokeo ya historia jiografia na malezi na sio based na FACT?
Historia & jiografia ina sehemu yake katika imani, lakini havimfungi yeyote kubaki katika imani husika.

Wengi wanafungwa na utashi wao wenyewe -- hawako tayari kubadili hali iliyopo kwa kuhofia kupoteza kitu fulani wanachodhani kuwa cha thamani sana kwao.

Kwa hiyo tatizo siyo sana mazingira ya nje, bali yaleya ndani -- akili ya mtu mwenyewe.
 
Sababu ya mtu kuwa mkristo au muislamu ni sababu ile ile inayofanya mtu azungumze kiswahili au kifaransa

Jiografia.

99.99% ya wakristo, ni wakristo kwasababu wamezaliwa na kulelewa kwenye familia za kikristo, wamekabidhiwa dini na kuambiwa huu ni ukweli, kisha nao wakaipokea kama ilivyo, ni utamaduni.

Vile vile 99.99% ya waislamu, ni waislamu kwasababu wamezaliwa na kulelewa na familia za kiislam

Ukizaliwa Ulaya, kuna 99% chance ya kuwa mkristo, ukizaliwa Saudi Arabia kuna 99% chance ya kuwa muislam
 
Lete ushahidi wa kihistoria kuwa Ibrahim ni "binadamu halisi" aliyewahi kuishi

Lete ushahidi wa kihistoria na kijiografia kuwa "Gharika" iliwahi tokea, Nuhu alikua mtu halisi, na viumbe vyote duniani vilivyopo sasa vilitosha kwenye hio Safina ndogo kuliko boat za Azam

Lete Ushahidi wa kihistoria na kisayansi kuwa "Adam na Eva" walikua binadamu halisi, waliishi wapi? Na kivipi watu wote duniani walitokea kwa watu wawili bila athari zote za incestry

Lete ushahidi kuwa wana wa Israel waliwahi kuchukuliwa utumwa Misri licha ya kutokua na rekodi hata moja Misri kuhusu uwepo wao (Misri ya kale ime document almost kila kitu chao, hakuna hata single reference ya kuwepo kwa wayahudi hapo)


Lete ushahidi wa kisayansi kivipi dunia iliumbwa kwa siku 6
 
Huu ni uongo kama Ukizaliwa Kwenye Ubudha "Budha" ndo itakuwa dini yako na zingine zote utaona Ni uongo kwa kuwa umeisoma Dini yako na umeaminishwa ni Kweli kuliko.zingine..
Ukizaliwa Kwenye Uislam Vile vile ,Ukristo,Shinto,Judaism na hata Uhindu..

Hakuna Kitu kinaitwa Dini Ya kweli..
Ni Bora kusema Dini Iliyonizunguka...
Japo Dini zote ni sawa...

Ukienda kwa Wayahudi Wao wanaamini Dini yao ni Bora kuliko Ibrahimic Religion zote..
Na wao wana mafundisho tofauti ns Dini zingine zote..
So usijitie Simanzi hakuna Dini ya kweli..
Ila kuna Dini uliyopo Na dini Ulikulia na Dini uliyo bahatika kuwa karibu kimazingira
 
Akijibu Nitag Mkuu
 
Allah alijifunua Kwa watu kupitia Taurati,Zaburi, Injili na Quran

Ebu tupe mistali ya huyo Mungu Zeus tuone na yeye anasemaje
 
Ndio maana Mungu ameahidi moto Kwa watu wasiojielewa kama wewe

Unataka ushahidi wa kisayansi kuwa ulimwengu uliumbwa Kwa siku 6?

Wakati hao wanasayansi wako wa NASA Hadi Leo hii bado hawajamaliza kujifunza kuhusu ulimwengu
 
Ukizaliwa Ulaya, kuna 99% chance ya kuwa mkristo, ukizaliwa Saudi Arabia kuna 99% chance ya kuwa muislam
Kuzaliwa Mwislamu au Mkristu au mpagazi zimwe wa upagani (hard-headed heathen), wala siyo hoja kubwa yenye mashiko hapa.

Nukta ya maana kabisa ni iwapo ama la hatimaye ^chekecho^ lake limepeta fifi na kusaza ngano safi.

Sijui unanielewa?

Mwislamu ama Mkristu ama mpagani huyo anapokeaje ^mabadiliko ya tabia-dini^ zilizoshamiri ulimwenguni?

Kuzaliwa ^mti^ ni hoja moja, kugeuka ^mtu^ ni nyingine tofauti kabisa.
 
Wenda hujaelewa hoja,
Factor kubwa iliyofanya na inayofanya watu wawe waumini wa dini fulani ni Jiografia na sio critical analysis unayosema hapa

Majority ya watoto tayari wanapokea dini za wazazi wao hata kabla hawajafikia umri wa kuchanganua mambo, mda gani wanafanya critical analysis ya dini kujua dini ipi waende based on "Fact"?

Mtoto wa miaka 5 madrassa au kipaimara anaweza vipi kufanya huo mchanganuo kama sio indoctrination

Wewe ni mkristo? Ume mpa nafasi mwanao kupitia dini zote ili ajue ipi itamfaa based on facts atakazokutana nazo au ume force ukristo kwenye kichwa chake?

Bado hujapinga hii hoja, kwanini selection ya dini ibase kwenye jiografia badala ya fact? Kwanini kuna chance kubwa ya mtu kuwa muislamu Saudi Arabia kuliko Russia au India?
 
Influence ya wazazi YES! Ila wengine tuliamua kuchunguza facts za imani yetu hadi kufikia hatua ya kuyumba kabisa ila tulipokuja kupata uhalisia ndipo tulipotuliza nafsi na roho kwa Kanisa Moja Takatifu la Mitume!

Huwezi kujua kweli kwa kumtegemea mchungaji wako bila kukubali challenge nje ya imani yako na kuzichunguza kiroho safi. Mimi sijawahi kumuamini Kristo sababu ya miujiza, au kuona watumishi wenye upako. Nilikwenda beyond kusikiliza hawa wahubiri tunaoona wamebeba hekima za kutosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…