Ukweli kuhusu kwanini unaamini dini unayoiamini

Ukweli kuhusu kwanini unaamini dini unayoiamini

Huu ni uongo kama Ukizaliwa Kwenye Ubudha "Budha" ndo itakuwa dini yako na zingine zote utaona Ni uongo kwa kuwa umeisoma Dini yako na umeaminishwa ni Kweli kuliko.zingine..
Ukizaliwa Kwenye Uislam Vile vile ,Ukristo,Shinto,Judaism na hata Uhindu..

Hakuna Kitu kinaitwa Dini Ya kweli..
Ni Bora kusema Dini Iliyonizunguka...
Japo Dini zote ni sawa...

Ukienda kwa Wayahudi Wao wanaamini Dini yao ni Bora kuliko Ibrahimic Religion zote..
Na wao wana mafundisho tofauti ns Dini zingine zote..
So usijitie Simanzi hakuna Dini ya kweli..
Ila kuna Dini uliyopo Na dini Ulikulia na Dini uliyo bahatika kuwa karibu kimazingira
Kuna kaukweli ndan yake
 
Mambo ni mengi sana.

Mimi huwa napenda kuacha mambo yaende kama yalivyo au yatakavyokuwa as longer as sivunji sheria wala simuudhi mtu,the rest siku nifunge macho nikaone huko kukoje?hakuna kingine!
 
  • Thanks
Reactions: 511
Ndio maana Mungu ameahidi moto Kwa watu wasiojielewa kama wewe

Unataka ushahidi wa kisayansi kuwa ulimwengu uliumbwa Kwa siku 6?

Wakati hao wanasayansi wako wa NASA Hadi Leo hii bado hawajamaliza kujifunza kuhusu ulimwengu
Hebu tushiriki mimi na wewe kwenye hili jaribio la kufikirika,
Assume, umekaa tu nayako, halafu nikaja mimi, nikakwambia kuwa nimekuja na habari ya Mungu wa kweli anaitwa "Kekova" , nikasoma kitabu cha kwanza kwenye vitabu 12 alivyonipa Kekova kwenye mlima Kilimanjaro

Aya inasema "Hapo mwanzo kulikua na Kekova na watoto wake wawili wakiume, wakaamua kuumba binadamu kwa mfano wao, wakawaweka Serengeti"

Kekova aliumba ulimwengu mzima kwa siku 23, akapumzika siku 4....

Tu pause kwanza hapa kwa mda tu, hii injiri yangu utaikubali au utaikataa, na kama utaikataa utatumia vigezo gani (sahau kwanza kuhusu dini yako) nataka unipe sababu za wewe kukata hii stori nzima ya Mungu Kekova kuwa ni ya uongo, nipe sababu kwanini ulimwengu haukuumbwa na Mungu Kekova kwa siku 23
 
Kuna asimilia fulani ya imani ya kweli katika kila dini -- hata zile ambazo zinaeneza uongo wa wazi.

Ukweli unaweza kuchanganywa na uongo ilimradi tu uvutie akilini mwa watu wanaopenda kudanganyika na kudanganywa.

Aidha, ukweli halisi wa Mungu haujifichi na wala hauna sababu ya kujificha.

Kanuni ya ukweli ni kudhihirika kama nuru ya adhuhuri, isiyohitaji wala umahiri kuing'amua.

Kanuni ya uongo ni kujificha kama giza la usiku wa manane, linalohitaji kutia maanani ili kupata utambuzi wa ziada ili kubaini kinachoendelea duniani.

Tatizo la wengi sana si kwamba hawaujui ukweli.

Shida ipo kwenye maslahi binafsi wanayohofu yatavurugika iwapo wakiufuata ukweli.

Maslahi (mali, kipato, fedha, familia, marafiki, mazingira, mfumo, mipango fulani fulani, nk)

Shida ipo kwenye utaratibu mpya wa maisha watakaolazimika kuufuata iwapo wakiukubali ukweli huo.

Shida ipo kwenye raha na starehe potofu watakazolazimika kuzivua kwa vile zinakinza ukweli mpya ambao hawana budi kuupokea.

Shida ipo akilini mwao kwamba jamii iliyowazoea wakiwa hivi itawaonaje ghafla tu wakiwa vile.

Shida ipo kwenye utashi wao ambao haujafanya maamuzi ya kina, wakidhani kwamba wana muda wa ziada kesho, ambayo kimsingi haitafika kamwe.
Huo ukweli unaojulikana ni upi mkuu?. Usijekuwa na wewe tayari ni mhanga/mwathirika kama mtoa mada alivyoeleza.
 
Lete ushahidi wa kihistoria kuwa Ibrahim ni "binadamu halisi" aliyewahi kuishi

Lete ushahidi wa kihistoria na kijiografia kuwa "Gharika" iliwahi tokea, Nuhu alikua mtu halisi, na viumbe vyote duniani vilivyopo sasa vilitosha kwenye hio Safina ndogo kuliko boat za Azam

Lete Ushahidi wa kihistoria na kisayansi kuwa "Adam na Eva" walikua binadamu halisi, waliishi wapi? Na kivipi watu wote duniani walitokea kwa watu wawili bila athari zote za incestry

Lete ushahidi kuwa wana wa Israel waliwahi kuchukuliwa utumwa Misri licha ya kutokua na rekodi hata moja Misri kuhusu uwepo wao (Misri ya kale ime document almost kila kitu chao, hakuna hata single reference ya kuwepo kwa wayahudi hapo)


Lete ushahidi wa kisayansi kivipi dunia iliumbwa kwa siku 6
Biblia inawafundisha kwamba jua lilitengenezwa siku ya 4,

Sasa sjui siku zilipitaje bila kuwepo jua
 
Ndio maana Mungu ameahidi moto Kwa watu wasiojielewa kama wewe

Unataka ushahidi wa kisayansi kuwa ulimwengu uliumbwa Kwa siku 6?

Wakati hao wanasayansi wako wa NASA Hadi Leo hii bado hawajamaliza kujifunza kuhusu ulimwengu
Pamoja na fallacy ulizoonesha hapo, lakini bado umedhihirisha kwahakika kabisa kuwa hakuna Mungu muweza wa yote mjuzi wa yote na mwenye upendo.

Right kama Mungu huyo angekuwepo asingeweza kuumba mtu asiyejielewa kama Kuchwizzy.
Mungu huyo si mkatili na mwenye kukosa upendo kwa viumbe wake kiasi cha kuumba mtu asiyejielewa halafu amchome moto.

Kumtisha mtu tu hilo ni tatzo linalomfanya mungu huyo asiwe mwenye upendo wote.


Unasuport hadithi za uumbaji kwa siku sita with no any evidence, tunaanzaje kuamini kitu cha kuambiwa tu kisicho hata na nusu ya facts?

Unakubali kwamba mungu aliumba jua siku ya nne?

Huoni kama hadithi ya uumbaji inautata mkubwa.

Then unafika mbali kuhoji eti kwamba Nasa hawajamaliza kujifunza ulimwengu, sasa inauhusiano gani hapo kwenye hoja zako?

Je unamaanisha Kutokumaliza huko kwa Nasa kujifunza ulimwengu huu ni uthibitisho kwamba dunia iliumbwa siku sita?
 
Kuna uongo mwingi sana kwenye hizi dini za duniani
 
Kuna uongo mwingi sana kwenye hizi dini za duniani
Nashangaa mtu unamkuta kazoroteka akili yake kabisa kwa mambo yakijinga kama hayo.

Dini inaharibu sana akili.

Jamaa mmoja alikuwa kwenye mjadala akaibua hoja kumuuliza muamini

Jamaa: Unaamini biblia wakati inauongo mwingi?

Muamini: unaweza kuonesha uongo kwenye biblia?

Jamaa: ukisoma marko 4:31 wanasema Mbegu ya Haradali ni ndogo kuliko zote duniani, je ni kweli

Muamini: Ndiyo ni kweli kulingana na neno la mungu

Jamaa: Unazijua mbegu za ostrich? Mbona kama ni ndogo kuliko hata hizo za haradali

Muamini: Huo ni mtazamo wako!!

 
Swali la MSINGI;

IN THE FIRST PLACE, KWANINI UNAAMINI KATIKA DINI UNAYOIAMINI?

Kabla hujaendelea kusoma be honest with yourself na ujijibu🙏

Ok tuendelee.
Kila mtu kwa mujibu wa imani yake amekua akijenga HOJA NZITO kueleza “UKWELI” na u HALALI wa Mungu wake huku akinukuu maandiko ya dini yake kwa ufundi mkubwa sana na kukosoa imani zingine.

UKWELI ni kwamba SIO KWELI kwamba dini unayo iamini ULIICHAGUA kwa hiyari yako baada ya kujiridhisha ni SAHIHI na ya KWELI

UKWELI ni kwamba 95% ya watu wote Duniani wanaamini dini wanazo ziamini ikiwa ni MATOKEO ya MALEZI/MAKUZI, GEOGRAPHY/HISTORY, nasio machaguo yao

MALEZI YA MZAZI.
Wazazi wanachangia pakubwa sana kupitia ile TRUST dhidi ya watoto...... kuna trust kubwa sana ya mtoto kwa mzazi. Mtoto toka mchanga anamuamini mzazi 100% na anaanza kuaminishwa na kujengewa hofu kuhusu Mungu husika hadi anapokua kijana.

Teenagers are suspicious, lakini hadi kufikia hapo inakua too late, brainwashed damage ya mzazi inakua beyond repair

MAKUZI YA JAMII
Namna jamii inavyoishi kwa kumkuza Mungu

Mitaani watu wataapa kwa jina la Mungu, kila kitu kikitokea watu watesema namshukuru Mungu au namuachia Mungu, jamii inatoa nafasi kubwa kwa viongozi wa dini kama kwenye misiba harusi nk

Majanga makubwa yakitokea viongozi wataingoza maombi ya kitaifa nk nk

Mtaani huko ukisema hadharani hakuna Mungu kila mtu atakuona unalaana au umechanganyikiwa, nchi nyingine una uwawa kabisa

GEOGRAPHY/HISTORY
Je wewe mkristo wa Iringa au muislam wa Tanga vipi kama ungezaliwa na wazazi wa kihindu India kwenye viunga vya Punjab ambapo 99% ni Budha?

Vipi ungezaliwa kule milimani China ambapo 100% ya wakaazi ni Budha?

Kwa mfano Tz watu zaidi ya 80% wanajua dini mbili tu ukristo na usilam, hawana kabisa access ya kujua dini zingine, hii ipo kwa nchi nyingi sana duniani kote. Nchi kama North korea hali ndio mbaya kabisa.

Huko China kuna majimbo ukiwauliza kuhusu Yesu au Mudi hawajui kabisa kama vile wewe ukiulizwa kuhusu dini kuu ya wachina na Mungu wao hujui chochote labda u google😂

JE, WEWE UPO KWENYE IMANI YAKO KWA SABABU GANI?

Kisha tafakari dhana nzima ya uwepo wa Mungu mmoja kama inawezekana kwa kuzingatia malezi makuzi jiografia na historia 🙏

JE NI NINI ROLE YA MUNGU WA KWELI KUHAKIKISHA WATU WOTE WANAMJUA?
mungu muweza wayote anafanya atakalo anafanya apendalo kwani huu ulimwengu niwake na hakuna ashindwalo.! Asa sijui watu wanavyokufa kule Gaza yeye inampendeza.😢.? natamani hata anijibi nielewe hii hua imekaaje kwa upande wake. mtu anafanya ubaya anakatisha uhaui wangu anadhulumu mali zangu. alafu me nakua sipo duniani . yeye mungu na huyo mtu wake wanaombana msamaa huyo jamaa anasamehewa akija kufa tunakutana peponi duh.! siwezi kumuelewa mimi kwanin kwenye huo msamaha hawakunishilikisha namimi mtendewa.?
 
Back
Top Bottom