Ukweli kuhusu mieleka/wrestling, mchezo au maigizo

Hivi yeye amesema aliingia akaona UHALISIA,je wewe umeona uhalisia wa WWE kuwa ina uongo au hauna.Mbona tunakuwa na akili fupi sana,wewe ukiona jambo usiloliweza usidhani kuwa wengine hawawezi ndo maana kuna exceptional,kuna watu wanavunja/wanaweka record za dunia katika matukio mbalimbali napo watu wanasema uongo...kama hujui kaa kimya ueleweshwe kama huna uhakika kuwa muwazi sio unakataa tu bila hoja
 
Haya tuludi kwenye mchezo wenyewe.... John Cena atatetea mkanda wake dhidi ya Rusev leo kwenye Payback ?
 
no, sio maigizo ndugu, formally walikuwa wanauana sana. Mimi ni mpenzi wa mieleka, nimeanza kutazama Botswana tv wakati ule wa hack ogan, chris jericho etc.

Yale ni MAIGIZO kwa asilimia 98. Ndio maana Marekani na internationally, huo "mchezo" hauorodheshwi miongoni mwa SPORTS bali inawekwa chini ya ENTERTAINMENT. Wafahamu hayo???
 
Niko radhi kuangalia mieleka for an hour than kuangalia hizi ngumi za kina mayweather kwa dk kumi
 
Ushaambiwa ni WWE the E is for Entertainment what do you think it is?
 

soma vizuri kama nimetaja vidonge vya KUONGEZA NGUVU ?
 
soma vizuri kama nimetaja vidonge vya KUONGEZA NGUVU ?

kuna vidonge huwa wanatumia ili wasichanike hovyo,kwa mwaka mara mbili full dose ni dollar 8000


Haya...Kolo Toure aliwahi kutumia dawa za kupunguza uzito, na bado akala adhabu.
 
Mjadara mtamu sana hila umejaa ubishi wa watu wasiopenda soma mstari kwa msitar kwenye comment za wenzao....Mambo kama haya tunayaona mpaka kwenye KATIBA watu hawaisomi wanabaki pitia migongo ya wanasiasa mara ni nzuri mara haifai tunabaki ambiwa tu....Ndo sawa na mjadara huu watu hawasomi commeti za wenzao wanabaki mkosoa mtu......F.Mombasa katoa ushuhuda wake watu wanapinga bila hoja thabiti....kakaJambazi:unapinga mieleka kuchezewa S.A wakati jamaa wa mieleka wanakujaga cheza pale....Jamaa mwingne kataja mpaka jina la hizo dawa za kupunguza maumivu na kuchanika bado mtu anakuja mbeleni anauliza tena jina la dawa hizo why?.....Jamani tuwe tunasoma mstari kwa mstari toka page ya kwanza tusikimbilie hoji maswali ambayo majibu yapo page za mwanzoni.....95% ya huu mchezo ni kweli zinazobaki ni kumfanya mtazamaji hasiboleke,akina tyson,myweather,swazniger nawengine wameshindwa mana hapa ngumi ni za kweli na nzito...Hawajamaa ni majiant tena brave ndo mana unaitwa😛ROFC-NAL TRAINING PERFORMANCE.
 
kuna vidonge huwa wanatumia ili wasichanike hovyo,kwa mwaka mara mbili full dose ni dollar 8000

VINAUZWA wapi hivyo vidonge? navihitaji sana maana mimi nasafir safiri sana na mabasi hapa Tz nadhani vitanifaa na hizi ajali zinazotokea kila siku
 
Doh! Nimeiona. Inatia huruma sana. Maana jamaa apigwa vibaya sana akatupwa nje, kisha ile anarudi tuu, akapigwa teke la upande wa kushoto wa kichwa... Hakunyanyuka. Mchezo hatari sana huu.

Maana kama wanaoigiza wanakufa, vipi unaemuiga anaeigiza?

Huo mchezo hatari sana mkuu
 
Yale ni MAIGIZO kwa asilimia 98. Ndio maana Marekani na internationally, huo "mchezo" hauorodheshwi miongoni mwa SPORTS bali inawekwa chini ya ENTERTAINMENT. Wafahamu hayo???

So wataka kusema ile mtu anapigwa RKO juu ya meza ya wale commentators mpaka meza inavunjika ni uongo?? Kama ndio mbona basi wanazichomoaga kwanza zile TV pale mezani? si wangeziacha tu maana hata mtu haumii kweli bali wanaigiza tu
 
Hakuna ukweli, hata lile jukwaa limejaa masponji ndo mana wanajirusha rusha
 
So wataka kusema ile mtu anapigwa RKO juu ya meza ya wale commentators mpaka meza inavunjika ni uongo?? Kama ndio mbona basi wanazichomoaga kwanza zile TV pale mezani? si wangeziacha tu maana hata mtu haumii kweli bali wanaigiza tu
hatusemi kwamba ni uongo,,,, bali wanakuwa wamepanga ... kwamba next move ni hii wewe utalegea dakika kadhaa match atashinda fulani
 
Daaah mkuu umenikumbusha jamaa yangu mmoja wakati tukiwa form four ukimwambia mieleka uwongo anaanza kulia
Teh teh teh

Mkuu hapa nina ndugu yangu dingi zima linapambana kuganya watu kuwa mieleka ni ukweli.
 
Samahani kwa kutoka nje ya mada. Hivi wale tunaowaona kwenye movie au sinema wakila romance na hatimaye uroda huwa inakuwa ni kweli au viini macho?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…