Ukweli kuhusu Mradi wa NSSF wa Dege Beach Kigamboni

Hivi tunaharibu ya zamani, siyo? Ndiyo tulishauriwa tusiharibu haya?? Maswali kwa mleta mada.
 
pole Sana msemo na genge lako, hayo kayaeleze mahakamai/pccb/cag
 
Hii ni sawa na Rugemalila aliyetoa ardhgi kwa IPTL,akaja kuvuna mabilioni ya hatari mpaka yakamchanganya akaanza kutoa sandakalawe.


Inaonekana huyu mkurugenzi mpya wa NSSF ni mtu wa majungu na kupenda kukomoa,
sijui hata lengo lake la kuufanyia ufukunyungu management iliyopita ni nini wakati yeye tangu ashike madaraka hajaweza hata kufanya mradi mmoja hata wa kutengeza kalavati tu ili nae tujue kweli anafaa pale,

sasa hiyo kesi ya kimajungu hata upeleke mahakamani utamshinda nani zaidi ya kupoteza mda wa watu?,
hopelless kabisa huyu
 
Yaani Azimuo hana hata mia. Maana hiyo 35% ya hela ya mtaji ambayo alitakiwa atoe,alitaka kuikopa NSSF yenyewe. Yaani at the end NSSF ingekuwa imejenga mradi wote kwa hela zake yenyewe halafu hao matapeli wangepewa 55% share ya mradi bila kutoa hata shilingi moja. Halafu watu wanateteta upuuzi hapa
 
Kuna watanzani wana Dharau sana kama huyu- kuna haja yakuanzisha mahakama yao
 
Mkuu Samvulachole huo ufisadi unaweza kuwa sahihi kama unavyotajwa, unachotakiwa kujua ni
  • Hilo eneo lilikua na ekari ngapi/ viwanja vingapi vilivyopimwa?
  • Gharama za mradi zilikua kiasi gani?
  • Hiyo 20% ya gharama zote ni sh. ngapi? kisha gawanya kwa idadi ya viwanja.
Navyojua kwa miradi kama hii kwa nchi zetu za Africa huwezi kukosa ufisadi.
 
Reactions: 911
Hana ubunufu unategemea atatea vipi kibarua chake zaidi ya majungu na kutafta mchawi unafkiri alivojua anakabdhiwa nssf alijua anatoa lecture udsm
kumbe ni lecture huyu mtu?,ndo maana wahitimu wetu wanamaliza vyuo hawajui hata umombo,kwa malecture kama huyu,it means anajua kushika chaki na duster na si kuongoza shirika kubwa kama NSSF
 
Picture this, mmekubaliana kuendesha mradi za hotel, mwenzako atafute nyumba alipe kodi na kununua vifaa, wewe ulete chakula na kuajiri wafanyakazi. Na vitu vyote hivyo vina thamani tangible na ndio uwekezaji na hisa zenu.

Unakuja kugundua kuwa mwenzako kodi aliyolipa na vifaa alivyonunua i.e uwekezaji wake kazidisha bei mara 10. Je utakuwa haujaibiwa.

Kwa maelezo yao ni kwamba walipaswa kuwekeza katika ardhi, na wakasema thamani ya ardhi yenyewe ni mil 800 wakati kiuhalisia ni mil 25. Wakati huo huo wanasema wana acres 20,000 wakati wana acres < 4,000.

No matter how technical you want to explain this, it doesn't cut.
 

asante sana. taarifa kama hizi husaidia sana kunoa bongo zetu
 
kijana wa leo ngoja nikupe explanation for dumb ,

imagine wewe una kiwanja cha heka moja hapo kibaha ambacho tusema thamani yake waweza muuzia mtu kwa milion 10,

wanakuja wawekezaji wanataka kuweka mradi wa kujenga maghorofa ya kupangisha na wanataka wakupe milion 10 uwaachie kiwanja,
unapiga hesabu ya mradi utakaowekwa hapo na kuona utakuwa na thamani ya bilion 100,unaona kuuza kiwanja kwa milion 10 utakuwa umewapa watu ulaji,
unakataa kuuza,wanakubembeleza hatmaye unakubali kuingia nao ubia na mnapanga katika mradi huo upewe hisa 20%,ambayo kama sikosei ni thamani kama milion 200.

Kumbuka mwanzo thamani halisi ya hiyo heka yako moja ni sh milion 10,
lakini kwasababu umeingia mkataba wa land for equit sasa thamani yako katika mradi huo ni milioni 200.

Ndicho kilichotokea,halafu watu wanatumia umbumbu wa watu kutojua haya mambo kwa kuwapaka watu matope kuwa kuna ufisadi,
sasa swali ukipeleka mahakamani hii kesi utashinda au ndo yaleyale ya Dowans
 
Tunajua wewe ni mmojawapo wa wanufaika sasa majibu yako huku hata kusaidia nenda mbele ya kamati waeleze hayo,
Wacheni uwendawazimu nyie watu; kila siku mnaleta mambo hayohayo ya kizushi tu. Mlimpa hadi umiliki wa timu ya ligi Kuu England. Leo mnampa umiliki wa kampuni, kwani kawachukulia wake zenu?

Rekodi ya Dau hapo NSSF ni superb, ingekuwa vema nanyi mkawa wabunifu kuliendeleza shirika. Wenyewe mnakiri (japo na kiingereza cha jongoo) kuwa shirika lina aseti za na uimara kuliko mashirika yote ya hifadhi za Jamii Afrika Mashariki. Maprofesa wetu ni mabingwa wa ku-google tu sio zaidi. Tutakutana hapa JF muda mfupi ujao mkimkubuka Dau kutokana na hali ya shirika itakavyooza. Kenge
 
Inaelekea huyu Mkurugenzi Kahyarara amekosa ubunifu kiasi kwamba anaanza majungu kumpiga vita Mkurugenzi aliyepita.
Ninachokiona hapa, Dr Dau alikuwa na ubunifu na uthubutu wa kuwekeza na inaonekana aliaminiwa na BWM pamoja na JK ndiyo maana akadumu kwa miaka mingi pale, na kwa kweli mambo aliyoyafanya pale NSSF ni makubwa.
Huyu Kahyarara aache majungu, uprofesa wa vitabuni siyo sawa na kupractise live. Ngoja tuoneu ubunifu wake lakini so far namuona kama mchumi wa theory zaidi kuliko vitendo!
 
Kumbe ukiacha unazi wa Lumumba hua unaongea mambo ya maana! umeotoa point na mswali ya msingi sana
 
Tatizo inasemekana hao wawekezaji hawakuwa na ela mfukoni! ela walitaka wamkope huyo wanayetaka kuwekeza nao!!
 
Mkuu unapothaminisha ardhi kuna vitu vinaangaliwa kama vinaendana na thamani halisi,kulikuwa na factors zipi zilizofanya thamani ya ardhi kupanda kiasi hicho? kumbuka ni lazima kuwe na existing factors ili kupandisha thamani ya eneo. Huwezi kusema hili eneo lina thamani kwa sababu chuo kikuu UDSM kitahamia hapa, ukamuuzia mtu kwa thamani ya chuo kikuu kuwa pale wakati hakipo. Kama hilo eneo lilikuwa wazi na wakalivalue kwa thamani isiyo halisi, hapo mtu anashtakiwa kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi. Huwezi kusema eneo hili milioni 800 wakati eneo linalopakana na hilo linauzwa milioni 25 na halipati wateja.
 
Kinachowaumiza NSSF ni power struggle , kugombea madaraka. Viongozi 12 wamesimamishwa . Nafasi Zao kuna watu wanakaimu.

Hawa wanaokaimu Haswa haswa Mbette (utumishi) Tikyeba (Fedha) Mmuni (Operations) wanafanya kila njia na njama ili Chiku (utumishi) Mrosso (Fedha) na Magori (Operations) wasirudi wafukuzwe kazi ili wao wanaokaimu wachukue nafasi hizo.

Kwa Sababu hiyo walipoenda kwenye kamati za Bunge wakiulizwa Maswali wanajifanya ukweli hawaujui na njia nyepesi ni kuwalaumu kina Mrosso na wenzao ili waonekane hawafai.

Ndio maana kwenye Mkutano wa Wadau hivi karibuni Arusha Tikyeba aliwaambia Wadau viongozi wa zamani mafisadi na kwamba wao ni wageni wapewe Muda wasafishe. Kauli hiyo Kairudia kwenye kamati ya Bunge.

La ajabu ni kuwa Kama kina Mrosso mafisadi mbona CAG katoa Hati safi ya hesabu? Mbona huo ufisadi kwenye ripoti ya CAG haupo?

Tikyaba na wenziwe wajue vyeo havipatikani kwa kufitini wengine
 
Kwanini NSSF hawakununua kiwanja wakakiendeleza wenyewe na maeneo ya wazi yapo mengi tu Kigamboni? One million dollar question.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…