Ukweli kuhusu namba 666 (Nero Caesar)

Ukweli kuhusu namba 666 (Nero Caesar)

Venus Star

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2018
Posts
26,519
Reaction score
78,311
Wapenzi wasomaji wangu leo ninaendelea na kufumbua macho watu. Mwenye macho haambiwi tanzama, na mwenye akili zake ataweza kung'amua na kuelewa ukweli wa mambo.

Leo katika bandiko langu hili nitajikita kuongelea suala la alama ya 666 kama ilivyoandikwa katika kitabu cha ufunuo 13:18

Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita. Ufunuo wa Yohana 13:18

Kitabu cha ufunuo na kitabu cha Daniel ni vitabu vilivyo na ufanano kwa namna Fulani.

Kwanza kabisa tunatakiwa kuelewa tamaduni za wayahudi kipindi kile kwamba waandishi na manabii walikuwa wakitoa unabii kwamba wayahudi yanawatokea mabaya kwasababu ya kutenda mema. Walikuwa wakitabili na kuwaeleza kuwa manyanyaso yao yatakwisha. Lakini waliendelea kutawaliwa ndipo sasa wakaja na namna nyingine ya uandishi.
Apocalyptic literature, ndio namna mpya ya uandishi na unabii wakawa wanatumia. Moja wapo ya vitabu ni kitabu cha ufunuo na Daniel.

Leo naongelea sehemu ndogo tu ya kitabu cha ufunuo na tafsiri yake sahihi. Namba 666.

Ikumbukwe kuwa hawa wayahudi wanamna yao ya Numerology inaitwa Gematria. Wana encode maneno kwenye number.

Kitabu cha ufunuo kiliandikwa kipindi cha utawala wa Nero. Huyu alikuwa akitesa sana, na ilikuwa lazima uwe na certificate ya kufanya jambo lolote. Kwamba uwe na chapa yahuri wa Nero.

Kwahiyo Jina Nero Caesar ni kama ifuatavyo:

Screenshot_20220112-150905~2.png
 
Apocalyptic literature
Apocalyptic literature is a genre of prophetical writing that developed in post-Exilic Jewish culture and was popular among millennialist early Christians. Apocalypse is a Greek word meaning "revelation", "an unveiling or unfolding of things not previously known and which could not be known apart from the unveiling".

Kama nilivyo tangulia Kusema hapo awali baada ya wayahudi kuwa na manabii wa kila namna wakitoa unabii na kuwatia moyo wayahudi ilifikia wakati wakachoka.

Basi baada ya hapo ndipo wakabadilisha upepo namna ya uandishi wakiwaeleza kuwa hayo yanayotokea kuna vita ambayo inaendelea katika ulimwengu wa roho.

Sana sana matukio yaliyokuwa yakiendelea wakati huo. Sasa basi kwa sababu kipindi kile cha Nero na ukristo ulikuwa ndio unanza ndipo sasa mwandishi wa kitabu cha ufunuo aliye jitambulisha kwa jina la Yohana aliye kuwa amefungwa katika kisiwa cha Patimo akileta huu unabii. Ikumbukwe kuwa Nero alijiua baadae Mwandishi wa kitabu hiki alikuwa makini sana huku akiungamisha maandiko yaliyoandikwa kwenye kitabu cha Daniel kwa ustadi mkubwa.

Katika mfululizo wa makala zangu hizi nitakichambua kitabu cha Daniel na Ufunuo A-Z namna vilivyokuwa vinatumika na namna ya mapikeo ya wakristo na kutoa tafsiri ambayo si ya ukweli. Ni tafsiri inayo wafaa kwa muda huu.
 
Gematria
Gematria is a Jewish form of numerology in which the letters of the Hebrew alphabet are substituted with corresponding numbers. The first ten letters are given number values that increase consecutively from 1 to 10. The next eight letters are given number values that increase by a factor of ten from 20 to 90. The final four letters are given number values that increase by a factor of one hundred from 100 to 400. In Hebrew, gematria is often used as an alternative to Arabic Numerals when recording numbers. Hebrew dates are generally written using gematria
images.png

.
 
MTASHIKANA NA KURUSHIANA MPIRA HADI LINI? TAFUTA UGALI MKUU ACHANA NA MAMBO AMBAYO HATA HUNA UHAKIKA NAYO
 
Ukisoma kwa makini Historia ya Nero itagundua nguvu ya wanamke. Mama yake Agrippina Younger alikuwa na ambition ya kuwa mtawala tangu akiwa mtoto.

Alipo pata nafasi ya kuolewa na mjomba wake Claudius (Roman Emperor) alihakikisha anapata influence katikati ya wakuu wote katika serikali ya Claudius. Baadae aliweza kushawishi Claudius aweze kum adopt mtoto wake "Lucius Domitius Ahenobarbus" na akabadilishwa jina na kuwa "Nero Claudius Caesar Augustus Germanicus". Agrippina alikuwa mshauri mkuu wa Claudius na alipewa mamlaka ya kusign nyaraka mbalimbali za serikali. Agrippina aliweza kujikusanyia mali nyingi sana. Baada ya kuona muda mwafaka wa mwanae kuweza kutwaa uongozi alipanga mpango na kuweza kumuua Claudius, alimuwekea sumu kwenye chakula na alikufa huku anajitazama. Agrippina haraka alifanya mpango na kumuweka mwanae kuwa kiongozi akiwa na umri wa miaka 17. Nero aliweza kuongoza empire kwa kusikilia mashauri kutoka kwa mama yake.

Nitaendelea kuongelea why Nero anatajwa kuwa 666.
 
Lini Kitabu cha Ufnuo kiliandikwa
Wana theology wanasema kwamba kitabu hiki cha ufunuo kiliandikwa mwaka 65AD. Kwamba kiliandikwa kipindi Nero akiwa anatawala.

Kipindi hicho Paul na Peter waliuawa. Na wakristo walikuwa wakisakwa na kuuawa.

Mwandishi wa kitabu hicho hajulikani. Lakini ukikisoma mwanzoni yule aliyeona maono alijiita Yohana alikuwa katika kisiwa cha patimo. Wengine wanasema kwamba aliyeandika kitabu hicho ni Yohana mwanafunzi wa Yesu ambaye alifungwa katika kisiwa cha Patimo baada ya kushindikana kuuawa. Kwamba alitupwa kwenye pipa lililochemka mafuta lakini hakuweza kufa. Lakini Yohana alikuwa ni mtu ambaye hakusoma kwamba isingewezekana kuandika kitabu hicho ambacho ndani yake kuna Nyaraka ambazo zimeandikwa kwa ustadi katika makani saba

(1) Efeso (Ufunuo 2: 1-7) — kanisa lililoacha upendo wake wa kwanza (2: 4). (2) Smurna (Ufunuo 2: 8-11) — kanisa ambalo litapitia mateso (2:10) (3) Pergamumu (Ufunuo 2: 12-17) — kanisa ambalo lilihitaji kutubu (2:16). (4) Thuatira (Ufunuo 2: 18-29) — kanisa lililokuwa na nabii wa uongo (2:20). (5) Sarde (Ufunuo 3: 1-6) — kanisa lililokuwa limelala (3: 2). (6) Filadelfia (Ufunuo 3: 7-13) — kanisa ambalo lilikuwa la uvumilivu (3:10). (7) Laodikea (Ufunuo 3: 14-22) — kanisa lenye imani si baridi wala si moto (3:16).

Kwa mantiki hiyo na mambo mengine mwandishi wa kitabu hicho cha ufunuo sio Yohana mwanafunzi wa Yesu. Na ikumbukwe kuwa Yohana lili kuwa ni jina common wakati ule katika jamii ile

Upande mwingine mwandishi wa Ijili ya Yohana na Mwamdishi wa Ufunuo ni waandishi wawili tofauti. Maana namna ya uandishi ni tofauti. Mwandishi wa Injili ya Yohana alikuwa professional write na alikuwa anaijua lugha, lakini mwandishi wa kitabu cha ufunuo alikuwa haijui lugha, maana kwenye original document ya ufunuo kulikuwa na mistakes nyingi za grammar. Kwa hiyo mwandishi wa kitabu cha ufunuo siyo yule aliyeandika kitabu cha Injili ya Yohana.

Kwa maana hiyo, kutokana na kuchanganya changa kwa taarifa zilizomo kwenye kitabu cha ufunuo kwamba style ya uandishi, kwa sehemu ili copy kitabu cha kutoka, kwa sehemu ili copy kitabu cha Daniel, kwa sehemu ili copy Nyaraka za mitume na sehemu zingine kwenye injili na agano la kale. Kwahiyo sasa hakuwa mwandishi mmoja aliyeandika kitabu hiki cha ufunuo. Ni kwamba waandishi kadha wa kadha zilikusanywa documents zao na kuwekwa pamoja na mtu ambaye alikuwa makini sana.
 
Unaposema Yohana hakuwa na elimu hivyo hakuwa na uwezo wa kuandika. Tambua kuwa kama Mungu alitaka Yohana afikishe ujumbe wake, Roho Mtakatifu anaweza kumshukia na akajazwa elimu.

Kama Roho wa Mungu aliweza kumshukia binti kigori Maryamu na neno likageuzwa kuwa mwili mbona haya ni madogo sana kwa Mungu.
 
Naona mleta mada ameanza kudemka, nakushauri ukomee hapo ulipoishia kuliko kuendelea kupotosha
 
Mwisho wote tutakufa..na hakika hatujui tutaenda wapi...NAWASHAURI TENDA KAMA VILE SAUTI YAKO YA NDANI INAVYOKUAMURU
 
Back
Top Bottom