Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Ndugu yangu mimi nazungumza kama Mtanzania wa kawaida tu ambaye anajali mustakabali wa nchi yetu. Si lazima niwe serikalini. Nimesema usinirudishe nyuma. Taja sasa hivi 2010 tufanyeje sisi kama Watanzania ili tuweze kusonga mbele sote pamoja kwa mshikamano na amani.
Sisusi ila sikuzoea kutoleana fedhuli hiyo si silka katika makuzi yangu. Kawaida yangu ninapoona lugha zinakuwa si za kiungwana basi mie hujiweka pembeni na kusema salama.
Ama hilo la kusema kuna kubwa kuliko kuandika kitabu kikachapwa na kikawa kitabu cha rejea katika vyuo vikuu duniani?
Au kuna kubwa kuzidi ya kualikwa katika midahalo ya kimataifa na kuzungumza kuhusu Uislam na Siasa katika Tanzania?
Au kuna kubwa kuliko kuwa mmoja kati ya waandishi wa Afrika wanaoandika Dictionary of African Biographies?
Au kuna mafanikio katika kuandika kuliko kitabu chako kikatiwa ndani ya Cambridge Journal of African History na kikatiwa katika catalogue ya Library of Congress, Washington?
Nimeingia JF kwa kuwa niliamini hii ni "forum ya great thinkers" na napenda nitoke humu nikiamini hivyo.
Umetia akili, umetia heshima, umeanza kuelewa jinsi jamvi linavyoendeshwa hapa, hakuna kususa susa, wanaondoka hawaagi, wanaoga hawaondoki, habari ndio hiyo. Hakuna kusema oooh hili nisingelijibu ila kwa vile nimeguswa kuambiwa najipendekeza kuwaletea udini kina Sykes, ukisusa umesusa, unaanza!FM nimependa jinsi unavyonasa mambo! Huu ndiyo usomi lakini ....
Adabu na kuheshimiana ndiyo mafunzo yetu na kauli njema ndiyo uungwana. Kwaheri.
Mohamed Said, unataja adabu na kuheshimiana na wakati huo huo unamponda kiumbe mwingine kama wewe ambaye pia ana haki ya kutoa mawazo yake kama wewe hata kama hamkubaliani yaani Rev. Christopher Mtikila. Kwa nini wewe uaminiwe kwa mambo ya kusimuliwa na si Mtikila ambaye yapo mengi labda kayashuhudia?Adabu na kuheshimiana ndiyo mafunzo yetu na kauli njema ndiyo uungwana. Kwaheri.
Mkuu wangu umedanganywa sana ktk habari hii. Waarabu waliokuja East Afrika hawakuileta dini isipokuwa dini imeletwa na kundi tofauti kabisa na wanazuoni kupitia Somalia.. Tofauti na Ukristu, watawala wetu hao wazungu walikuja na dini na ndio maana aliweza jenga makanisa ya kufundisha dini at the same time wakikusanya watumwa ktk makanisa hao hayo na kuwapeleka Ulaya..Wandugu, kwenye hili la maendeleo na shule za misheni, tunamlaumu Nyerere bure tuu, wazungu wa kwanza kuja barani Afrika walikuwa makundi matatu, wagunduzi, wapelelezi na wamishenari. Hawa walikuja karne ya 17 wakati Waarabu na Uislamu wao walikuja barani Afrika tangu karne ya 14.
Misheni ya kwanza kujengwa Afrika Mashariki ni Bagamoyo, then Zanzibar ndipo wakaja Dar. Waarabu na Uislamu wao, wao waliangalia biashara tuu yaani Trade, kujenga misikiti na madrasa zake. Wamishenari wao waliangalia investment potential areas ndipo wakajenga misheni kubwa kubwa, hali iliyopelekea maeneo yenye mazao ya biashara Kahawa, Chai, Pamba na Katani, kupata support kubwa ya misheni sio tuu kueneza dini, bali kutoa elimu dunia, hali iliyopelekea ndugu zetu wa Kilimanjaro na Kagera kupata dini na kupelekwa shule na pesa za kahawa, what had Nyerere got to do with this?!.
Mpaka leo ukiangalia baadhi ya makanisa makubwa, yako kwe the top prime area ya maeneo mengi ili hali Misikiti imejikita zaidi Uswazi, that was not a mare chance but long time vision.
Chelewa ufike, wenzetu Waislamu, Chuo Kikuu hicho hapo Moro, madrasa tujenge lakini na shule pia sasa ndio ndio hizo zipo. Enzi zile shule za sekondari zikiwa chache, mkoani Dar, Shule ya Sekondari ya Kinondoni ndio iliyokuwa ikiongoza kwa kuzungusha (Div=0) lakini bado makuwadi wa kilio cha kubaguliwa, wakiendelea kulia kuwa wanabaguliwa, kusoma msome wote, mwenzako apate Div=1, wewe upate Div=0 alafu unalalama unabaguliwa!.
Issue sio dini, issue ni visions, planing na strategy ya kufikia malengo. Nadhani nchi za emerging markets, Tiger nations zote ni za Kiislamu and have made it, hinyo tuache kuuhusisha uduni wa Waislamu na dini yao, dini kama dini, has nothing to do na uduni au ubora wa maisha, ila dini kama biashara, has got something to do, wenzetu walihubiri dini tuu kutafuta ahera ya milele, wenzao wakahubiri dini, huku wakijenga uwezo wa kiuchumi na matokeo ndio hii imbalance inayosababisha Nyerere kutaka kubebeshwa msalaba.
Nasubiria kusoma hicho kitabu!.
Hii habari ya kufikiri wenyewe waislamu ndio fani yetu,nyinyi tu tukionesha uwezo wetu wa kufikiri hamuna ubavu wa kuvumilia.Mfano ni hii kazi ya historia ya Muhammed Said,hapo hakuna mkono wa mkristu yeyote na hamuwezi kuipinga kitaalamu.Mkuu, unapoteza wakati wako. Huyu jamaa hawezi. Yeye ni mtu wa kufikiriwa, kufikiri mwenyewe inakuwa shida. Faraja yake kubwa ni kuwa yeye ni victim, Ukimuondolea hilo anabaki mweupe! Watu kama hawa wanajua zaidi kubomoa lakini kujenga hawawezi.
Amandla.......
Ikiwa ni hivyo hata tukikutajia cha kufanywa ni kwamba umejitayarisha kuleta dharau tu na mabezo.Ya kufanya kwa kifupi angalia utitiri wa malalamiko ya waislamu kwa Tanzania na labda uanze kutekeleza mwenyewe kwanza.Hii habari ya serikali unayotaka kujifanya mwakilishi wake hapa tuwachie wenyewe na Allah ataleta nusra isiyopingika.Ndugu yangu mimi nazungumza kama Mtanzania wa kawaida tu ambaye anajali mustakabali wa nchi yetu. Si lazima niwe serikalini. Nimesema usinirudishe nyuma. Taja sasa hivi 2010 tufanyeje sisi kama Watanzania ili tuweze kusonga mbele sote pamoja kwa mshikamano na amani.
Hii habari ya kufikiri wenyewe waislamu ndio fani yetu,nyinyi tu tukionesha uwezo wetu wa kufikiri hamuna ubavu wa kuvumilia. Mfano ni hii kazi ya historia ya Muhammed Said, hapo hakuna mkono wa mkristu yeyote na hamuwezi kuipinga kitaalamu.
Mwenye kutaka kuipinga asifuate mawazo yako ataaibika kwani hii historia iko mbali sana kufanyiwa kazi.Nyinyi kama ni watu wa kufikiri kweli wala musingeweza kusoma biblia.
Angalia sanaa za kiislamu zisivyoweza kulinganishika kwa uzuri na zile za kikristo. Pale Makka na Madina mwahala munamokusanya mamilioni ya waislamu kwa muda mfupi na katika eneo dogo pale hakuna fikra ya akina Fundi Mchundo.
Dharau zenu ndizo zilizopelekea Allah (s.w) akaibua watu wajanja na wadogo kuwasuta nyinyi na mukabaki kutukana tu.
Kuhusu kujenga na kubomoa angalia maeneo wanayoishi waislamu Tanzani na nje yake nani ni wajenzi wazuri na nani wabomoaji kweli.Umewahi kuona wajenzi wazuri kuliko waliojenga mji mkongwe wa Zanzibar,Rabbat na Cordova kule Spain?.Jee umejiuliza kuhusu ubomoaji unaoendelea kulea Iraq,Palestina,Afghanistan na kwengineko,na nani wabomoaji wake.
Fundi tumekuzoea kuleta dharau zisizo na mashiko kwa waislamu.
Maendeleo ni nini?..tuna mikoa mingapi Tanzania na ipi iloendelea kuliko mingine. itaje kisha anagalia population kubwa ya wakazi wake ni watu gani?.Mkuu Mkandara wanishangaza, sisi wengine ingawaje ni "watu wa kuja" hapa Dar es salaam, lakini tunaifahamu hii Dar kuliko wazaramo wenyewe.
Na nikisema watu wanacheza ngoma huna haja ya kwenda mbali, nanda tu nje ya Dar na ujionee hali ya kilimo na maendeleo kwa ujumla.
Halafu Mohammed Said aliandika kitabu hiki kwa ajili gani?
Ili tumwonee huruma au aipindue status quo?
Mimi si msomi lakini ni muelewa, kuwa sehemu nyingi walizo wenzetu waislamu,nyingi zina maendeleo duni hili halihitaji ubishi, lakini wote ni waTanzania lazima waendelee.
Cha msingi hawataletewa maendeleo kama mvua , lazima wayaanze wenyewe, na hili waliona tusi?
Ukweli unauma ndugu yangu, lakini mimi niko tayari kuchangia shule za sehemu hizo lakini sishule za kidini, kwa maan wote ni watanzania na maendeleo tunayahitaji wote.
Kila Mfalme wa nchi za Ulaya anahusiana kinasaba na Ukristu aidha wali break out of Roman Catholic na kuunda church zao au kugawana urithi..Na ndivyo walivyo spread hadi Afrika, Marekani na wanaendelea kutumia dini kuendesha serikali zao lakini kosa kwa waislaam kuendesha nchi zao kwa kutumia dini zao. Na hakika mada hii inachekesha sana kwani mnasema waislaam wenyewe waanzishe vitu vyao lakini wakisema wanataka OIC hamtaki, wafungue bank zao hamtaki wakati nyie mnafungua!..Wakristu jamani mnanichosha. Huko New York wanapinga kujengwa kwa Msikiti lakini wanalaani Kanisa likizuiwa kujengwa nchi za kiarabu.
Mohamed Said, unataja adabu na kuheshimiana na wakati huo huo unamponda kiumbe mwingine kama wewe ambaye pia ana haki ya kutoa mawazo yake kama wewe hata kama hamkubaliani yaani Rev. Christopher Mtikila. Kwa nini wewe uaminiwe kwa mambo ya kusimuliwa na si Mtikila ambaye yapo mengi labda kayashuhudia?
Mimi nimejizuia sana kuingia kwenye huu mjadala sababu kubwa ikiwa ni moja tu - ninayoyajua kumhusu Mwalimu Nyerere sikusimuliwa, niliyashuhudia na wakati tunapata uhuru mwaka 1961 tayari nilikuwa sekondari. Pamoja na kukumbuka mengi yaliyotokea kwenye miaka ya 1950s lakini hata siku moja sikuwasikia hao wazee wako - sijui nani alizuia wasisikike Tanganyika nzima, Nyerere au mkoloni ? Kanda ya Ziwa ni eneo mojawapo ambapo mwamko wa harakati za kudai uhuru ulikuwa mkubwa na idadi ya wapiga kura wake ilikuwa maradufu kama ilivyoshuhudiwa 1958.
Mpaka leo shukuru kuwa umeachiwa uwanja ukitamba na kumwaga sumu yako kwa habari zisizo sahihi bila pingamizi lakini ukae ukijua kuwa yawezekana kwa tendo lako hilo umeamsha zimwi lililokuwa limelala. Labda unadhani kwa kuuleta huu uwongo JF umefanya kazi kubwa lakini nakuhakikishia hapa umefika kwani kusukuma ukuta bila kuusogeza wahenga husema hakuna kazi imetendeka - nchi ya Tanganyika ilikuwa kubwa zaidi ya pwani ya Dar es Salaam. Umefanya kosa kubwa kupiga hodi hapa JF na hizi habari za kufinyanga, yawezekana ulipotea njia, hivyo rudi nazo huko huko.
Pole na kwaheri.
FM nimependa jinsi unavyonasa mambo! Huu ndiyo usomi lakini kaka kunifananisha na Mtikila aaahh bwana hapo mbona unanivunja nguvu? Anga za Mtikila mie siwezi kuvuka. Kitabu changu kinaitwa "corrective history." Kinasomwa kwa mlinganisho wa ile historia iliyozoeleka kama hii ya kwetu. Bahati nzuri sana ni kuwa hao walimu wa somo hilo wengi wamekuja hapa na kuzungumza nami na wengi wao wamebaki marafiki zangu kwa kipindi kirefu sasa.
Maendeleo ni nini?..tuna mikoa mingapi Tanzania na ipi iloendelea kuliko mingine. itaje kisha anagalia population kubwa ya wakazi wake ni watu gani?.
Kwa ufasaha wako wananchi waliopo chini ya kima cha umaskini wengi ni wakristu kwa sababu ndio idadi kubwa wanaishi vijijini kuliko mijini, sasa unataka kunambia kilichowafanya kuwa maskini hivyo ni kwa sababu wao ni wakristu?
Na hii sio hoja ilotuleta hapa kumjadili Mohamed said kwani wewe ulokotoka huko shamba ulisema waenda mjini kutafuta maisha. Huko mjini tayari kulikuwa na maendeleo. Acha hizi habari za kulinganisha watu kwa dini zao kwa sababu wewe na huyo Mohammed mnachotofautiana ni sawa tukizungumzia Urusi na marekani enzi za vita baridi..
Matumizi ya dini ktk maendeleo ya watu ni ufinyu wa hoja, hivi wewe leo ukiwa Muislaam utarudi kucheza ngoma au?
FM ni nani?,au ndio wewe Fundi Mchundo.Mbona ulikataa kuitwa Amandla!.Unaandika majina unayoyaogopa mwenyewe.Unaonyesha ujuha wako. Badala ya kumjibu FM unaandama wakristu na ukristu. Unataka kulinganisha kweli mamboa yaliyofanywa na wale wanaojiita wakristu na waislamu? Shule au hekima ya Mohamed Said inakusaidia nini wewe kama Ami? Udini kweli pazia la kiza.
Amandla.....
Salma Maoulidi said:Such singling out can, however, be contested as it was not just Muslims who were snubbed by Nyerere. Such a fate also befell some of his close friends like Oscar Kambona and Chief David Kidaha Makwaia, the latter a Roman Catholic. One of the most influential chiefs in East Africa, Chief Makwaia, facilitated the political rise of his long-time college friend Julius Nyerere by winning him British support as well as by securing the allegiance of Sukuma chiefs to TANU. Upon attaining uhuru Nyerere abolished the role of chiefs, and banished Chief Makwaia to the remote Tunduru District of the Southern Province for undisclosed reasons (Awam Amkpa, 2007).
Ha ha ha
Mkuu mkuki kwa nguruwe , kwa binadamu mchungu?
Hii mada inahusu nini haswa , si udini mtupu kwa kwenda mbele.Unapo utetea uislamu kwa kubagua dini nyingine ujue na wewe waweza kubaguliwa ndani ya huo huo uislamu.
Tatizo la mada hii ni kuona uKristo ndio adui ya Uislamu kwa kupitia Mwalimu Nyerere, na ndio msingi wa argument nzima.
Ha ha ha
Mkuu mkuki kwa nguruwe , kwa binadamu mchungu?
Hii mada inahusu nini haswa , si udini mtupu kwa kwenda mbele. Unapo utetea uislamu kwa kubagua dini nyingine ujue na wewe waweza kubaguliwa ndani ya huo huo uislamu.
Tatizo la mada hii ni kuona uKristo ndio adui ya Uislamu kwa kupitia Mwalimu Nyerere, na ndio msingi wa argument nzima.
Uislamu wenyewe kuna Ushia na Usunni, kuna misikiti hata hapa Dar es salaam waswahili hawaingii ndani kwa kuswali.Mkuu mkandara bisha juu hilo.
Ukija kwenye Ukristo kwa mlioko nje mnaona woote sawa, vile vile kuna tofauti.Kuna Ukatoliki ambalo ndio kanisa kubwa na lenye nguvu.Kuna vile vile Ulutheri, kanisa lenye nguvu ya wastani, na makanisa madogo madogo kama Moravian , AIC, Menonite na hata Seventh Day ADventists.
Ni mawazo potofu kufikiri Ukristo kwa pamoja ndio waliofaidika na Ukoloni, kwa sababu si kweli kama wewe mwenyewe Mkandara unavyo kubali.
Na ndio maana mada hii inakosa nguvu yenye mantiki kudai kuwa Nyerere, kama Mkristo aliwaonea kimaendeleo waislamu.Kwa maana ukizitafuta tofauti kati ya watanzania ziko nyingi sana, hata katika dini yako ziko nyingi tu!Huko Iraq Mshia na Msunni wanauana na huko Ireland Mkatoliki na Mprotestanti wananuana.
Hapa Tanzania ni kuupa kipaumbele umoja wa watu wote.
Mtoa mada anasahau kuwa hizi sehemu walizokaa wakoloni, pamoja na maendeleo waislamu wanasahau kuwa wakoloni wa kizungu vile vile walileta ushindani mkubwa na kiu ya hayo maendeleo.
Hatuwashukuru wakoloni kwa kututawala lakini nguvu yao ya kimaendeleo twaitaka, na tusiwe wanafiki.
Sasa turudi huko "shamba" unakodai mimi ndo nimetoka!
Haya maneno yananikumbusha Marehemu Dotopile kuwa "wakuja" wameingia mjini bila kuosha matongo tongo na hawajui hata kula chapati, !
Hatujasahau mkuu maneno ya aina hiyo.Ila usisahau kuwa wengi wetu tulipoingia mjini shule hapa Dar zilikuwa bwerere, waswahili darasani hawakuwepo!
Mbaya zaidi hata kazi serikalini walikuwa wanaishia udereva na umesinja.Ila chapati walikuwa wanakula kweli kweli!
Sasa mkuu Mkandara sujui uko kundi gani?