Wandugu, kwenye hili la maendeleo na shule za misheni, tunamlaumu Nyerere bure tuu, wazungu wa kwanza kuja barani Afrika walikuwa makundi matatu, wagunduzi, wapelelezi na wamishenari. Hawa walikuja karne ya 17 wakati Waarabu na Uislamu wao walikuja barani Afrika tangu karne ya 14.
Misheni ya kwanza kujengwa Afrika Mashariki ni Bagamoyo, then Zanzibar ndipo wakaja Dar. Waarabu na Uislamu wao, wao waliangalia biashara tuu yaani Trade, kujenga misikiti na madrasa zake. Wamishenari wao waliangalia investment potential areas ndipo wakajenga misheni kubwa kubwa, hali iliyopelekea maeneo yenye mazao ya biashara Kahawa, Chai, Pamba na Katani, kupata support kubwa ya misheni sio tuu kueneza dini, bali kutoa elimu dunia, hali iliyopelekea ndugu zetu wa Kilimanjaro na Kagera kupata dini na kupelekwa shule na pesa za kahawa, what had Nyerere got to do with this?!.
Mpaka leo ukiangalia baadhi ya makanisa makubwa, yako kwe the top prime area ya maeneo mengi ili hali Misikiti imejikita zaidi Uswazi, that was not a mare chance but long time vision.
Chelewa ufike, wenzetu Waislamu, Chuo Kikuu hicho hapo Moro, madrasa tujenge lakini na shule pia sasa ndio ndio hizo zipo. Enzi zile shule za sekondari zikiwa chache, mkoani Dar, Shule ya Sekondari ya Kinondoni ndio iliyokuwa ikiongoza kwa kuzungusha (Div=0) lakini bado makuwadi wa kilio cha kubaguliwa, wakiendelea kulia kuwa wanabaguliwa, kusoma msome wote, mwenzako apate Div=1, wewe upate Div=0 alafu unalalama unabaguliwa!.
Issue sio dini, issue ni visions, planing na strategy ya kufikia malengo. Nadhani nchi za emerging markets, Tiger nations zote ni za Kiislamu and have made it, hinyo tuache kuuhusisha uduni wa Waislamu na dini yao, dini kama dini, has nothing to do na uduni au ubora wa maisha, ila dini kama biashara, has got something to do, wenzetu walihubiri dini tuu kutafuta ahera ya milele, wenzao wakahubiri dini, huku wakijenga uwezo wa kiuchumi na matokeo ndio hii imbalance inayosababisha Nyerere kutaka kubebeshwa msalaba.
Nasubiria kusoma hicho kitabu!.