Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Status
Not open for further replies.
Tafadhali ndugu yangu usijivue nguo kwa kuonesha ulimbukeni wako, watu kama hao uliowataja hawawezi kuwa msingi wa arguement kwani wanajulikana walivyo na huwezi kuona hata mara moja amekuwa qouted au kuwa refered katika academic writings. Nilifikiri watu hap JF wanauwezo wa kujua trashes ni zipi na vitu genuine ni vipi ili kuendeleza majadiliano makini. Kumbe watu wanataka mabishano ya kijiweni na majibizano ya mihadhara????

Eti ulipokuja mjini, ukakuta shule tupu duh! hii ni nini sasa? Huu ndio msing wa arguement?
Mla chapati utamjua kwa jina na muelekeo wa mawazo.

Ukweli utabaki pale pale mkuu Dar es salaam haijengwi na wazaramo tu bali na wakuja, tena wengi tu.
If you think the best you can do is to express your self in english then youd better start feeling sorry for your self my dear, crooked mouth.

Kwangu you sound like a mediocre half acheiver, who is loud on the mouth. The best thing that you can use your mouth is gobble a couple of Indian chapatis that are not indigenous to your self anyway.

Mkuu Domo kaya nakushauri kubadili jina lako as it seems nothing intelligible can come out of your infertile senses.
 
Mada kamwe haiwezi kutoa msingi wa arguemennt(argument), arguement(argument) inafanywa na mtu. Tatizo kubwa ulilonalo wewe na hapa umelieleza ni kufikiri kila mtu akitoa arguement(argument) hapa aidha apendelee uislamu au ukristo! Hasha. Hapa watu wana prob tatizo na kuliona tatizo lipo, makundi yanayobaguliwa yapo mengi tu, hata kundi la wana maombi linabaguliwa. Mtu mmoja ana wazo lake anadhani kundi fulani linabaguliwa natoa ushahidi wake wewe badala ya kujibu ushahidi unatoa prejudices ukitaka kila mtu awe upande fulani bila kuzingatia ukweli ni nini. Soma mawzo ya mtu na wala si kummuliza yeye yuko upande gani.

Mkuu ungejieleza tu kwa kiswahili fasihi unachokielewa.

Natangulia kukusahihisha kiingereza (in red) ulichokiboronga ili upate kueleweka.

Pili, ubaguzi na hisia zilizoibuliwa na mada hii ndio inayopelekea kuwa na mjadala huu.Kwa bahati mbaya mada inajaribu kulaumu upande mmoja kuwa ndio ulikuwa unapendelewa kwa sababu za makusudi kabisa.Sasa ni juu yako Domo kaya kupitia mada zote na kuelewa msimao wangu juu ya mada nzima.

Ubaguzi ni ubaguzi tu uwe wa dini ukabila au vinginevyo.

Sasa mada inahama kutoka kwenye Uisslamu/Ukristo, Uarabu/Uzungu na kuingia katika ukabila.

There is no fine line here, ndio maana nasema inahitaji common sense zaidi kuliko maneno matupu kupata common ground kwa mada iliyopo.

Huwezi kuibua tuhuma nzito na ukafikiri yatajadiliwa yale unayopenda wewe tu.There are some carried over feelings that affect the whole society.

Ukiutetea uislamu basi makundi mengine yanajitazama yanasimamia wapi kutokana na tuhuma zako.
 
FM ni nani?,au ndio wewe Fundi Mchundo.Mbona ulikataa kuitwa Amandla!.Unaandika majina unayoyaogopa mwenyewe.
Mimi nilikuwa nakujibu wewe na wala si mwengine.Lakini hii habari ya kuchanganyikiwa unapobanwa na hoja zako za kijinga ni utamaduni wako.
Unamkumbuka bwana mmoja anaitwa Zomba hapa JF,siku hizi simuoni sijui yu hai au anaumwa.Alikubana mwaka 2008 na mada yako uliyoianzisha.Nani aliyeleta biashara ya utumwa hapa kwetu.Ukamkimbia jukwaa la dini na imani, akakufuata huko huko ulikokwenda
Ulipochanganyikiwa ukasema hivi.Kwa hivyo wewe unajaribu kukanusha na kutetea mambo ya waislamu na wakristo,lakini si kwamba unajua chochote cha maana bali kwa haja ya kuleta fujo tu.Ndio maana nikamshauri Muhammed asitishike na wewe.Hueleweki kabisa.

Kweli debe tupu haliachi kulia. FM ni acronym ya Fundi Mchundo sasa kwa nini nikatae kuitwa FM? "Amandla" ( Power) ni kiibwagizo cha kusalimiana kilichokuwa kikitumika na wapiganaji wa African National Congress ya Afrika Kusini. Kiitikio kilikuwa "awethu" au "ngawethu", wakimaanisha "To us". Kilio hiki sasa kinatumika na baadhi ya wanaharakati katika vita dhidi ya ugandamizaji ( oppression).

Kumbe umekuwa ukinifuatilia tangu 2008? Kwa nini basi haukujiunga wakati ule ili uchangie katika mjadala. Mimi niliondoka katika Jukwaa la dini kwa sababu paliacha kuwa sehemu ya kuelimishana pakageuzwa na hao wakina Zomba kuwa sehemu ya kuonyeshana nani anayeweza kuitusi zaidi dini ya mwenziwe. Sababu nyingine ni kuwa niliamini kuwa pana haja ya kupanua wigo wa kujadiliana kuhusu biashara ya utumwa. Kubakiza mjadala kwenye jukwa la Dini kuligeuza mjadal kuwa kati ya ukristu na uislamu, kitu ambacho hakikuwa sahihi. Huyo Zomba, kweli alinifuata huko nilikouamishia tukaendelea aikuwa la mwisho na lilisema nini! Huyo Zomba, ambae naona ulikuwa unamuabudu, mwenyewe unakiri kuwa ametokomea. Kilichomfukuza bila shaka ni kufungiwa kwa jukwaa la dini ambako alilitumia kusambaza sumu yake ya udini na chuki dhidi ya watu wengine. Hakuwa na uwezo wa kujadili mambo mengine ambayo hayahusu dini. Sishangai kuwa ulikuwa mshabiki wake. Huyo Fundi Mchundo unayedai alichanganyikiwa bado yupo anapeta ndani ya hii Forum yetu. Wewe unanishangaa kuwa nimeweza kutetea waislamu? Nimetetea mashoga, nimemtetea Rostam Aziz na wengine bila kujali wengi wamesimamia wapi! Wewe umechangia nini katika Jukwaa hili nje ya kushabikia uovu na chuki dhidi ya wenzako? Watu kama nyinyi ni vidonda katika uso wa huu ulimwengu wetu.

Kumbe Muhammed alitishika na Fundi mchundo? Mbona alidai anajitoa kwa sababu ye ni muungwana na biashara ya kuvunjiana heshima hawezi. Kumbe aliniogopa! kweli mtu ukiwa na rafiki kama wewe, hauhitaji adui.

Naona kujibishana nawe hakutasaidia kitu maana haujajaaliwa uwezo wa kuchambua unachokisoma au kusomewa! kwa sababu hiyo nitafuata ushauri niliompa Jasusi na kujitoa katika kulumbana na wewe.

Amandla.........
 
Hapa, Mkuu, unaanza kuchemsha.

Hivi kweli unatumia mambo yaliyofanyika zamani kuhalalisha ya sasa? Ni nchi gani ya magharibi inayojiita kikatiba ya kikristu? Kutokana na yale waliyojifunza awali, nchi hizi msisitizo wao mkubwa ni kutenganisha dini na utawala. Ingawa wengi wanaoongoza ni waumini wa ukristu lakini kanisa halina sehemu kikatiba katika uongozi wa nchi. Hata Uingereza ambako malkia ni kiongozi wa dini hana nguvu juu ya waziri mkuu! Kutokana na maovu ambayo watu wa magharibi waliona yalitendeka wakati dini iliposhirikishwa kwenye utawala imekuwa mwiko kwao kuunganisha vitu hivyo. Busara ya kutenganishwa huko tunaiona hivi sasa katika nchi zinazodai zinazoongozwa na dini. Wote tuliona yaliyotokea Afghanistan wakati wa Taliban. Na hii ndiyo inayochangia kwa namna moja hata wengi wa wa waislamu wasomi wanaohama kwao kukimbilia nchi za magharibi na sio Saudia, Sudan au Iran. Wakienda kwenye nchi za kiislamu wanakimbilia zile ambako utawala hauruhusu dini kutawala kila nyanja. Wanajazana Dubai, Oman n.k. ambako mtu hakatwi mkono akiiba! Au kupigwa mawe kutokana na uasherati.

Hivi kweli unaamini kuwa OIC ndiyo panacea ya matatizo ya waislamu? Si itakuwa yale yale ya kutegemea mtu kutoka nje akukwamue katika matatizo yako? Linakuwaje tusi pale mtu anapoambiwa aangalie uwezo wake kabla ya kungojea fadhila kutoka kwa wengine?

Wapi watu wamepinga kuanzishwa benki ya kiislamu? Ninavyojua mimi watu ( kwa makosa) walipinga benki moja (Stanbic) kuwa na kitengo kitakofuata maagizo ya sharia katika kutoa huduma zake. Ninavyojua mimi viongozi wengi katika hiyo benki ni wakristu , sasa utasemaje kuwa wakristu hawataki benki ya kiislamu? Halafu Benki ipi ni ya wakristu? Kama ni kwa sababu waliozianzisha au/na wanaoziendesha ni wakristu basi vile vile utatuambia kuwa unga na lambalamba za Azam ni za kiislamu! Au iliyokuwa Greenland Bank. Au Meridien Bao. Hizi nazo zilikuwa za kiislamu kwa sababu wamiliki wake walikuwa waislamu? Hivi nchi ambayo rais wake ni muislamu, waziri wake wa fedha muislamu, gavana wake wa benki kuu ni muislamu, katika nchi ambayo karibu nusu wa raia wake ni waislamu, kweli itazuiwa na mkristu wa mtaani kuanzisha au kuruhusu benki ya kiislamu kama waliona kuna tija? Hapa si unarudia kosa lile lile la wakina Mohamed Said la kuona mkono wa mkristu hata kwenye yale ambayo yamewashinda wenyewe?

New York kinachopingwa na wengi si kujengwa kwa msikiti bali mahali panapotakiwa kujengwa hicho unachokiita kuwa ni msikiti wakati ni community centre yenye sehemu ya maombi. Vile vile hao sauti kubwa zinazotetea ujenzi wa msikiti huo zinatoka kwa wakristu, wakisema kuwa mbona kwenye eneo hilo tayari kuna misikiti miwili? Rome kwa hao wakatoliki penyewe pana msikiti, tena mkubwa sana. Sasa wewe nitolee mfano wa kanisa au kasehemu ka kuabudia wakristu lililopo Riyadh, Jeddah, Tehran au Sanaa? Huko unakolaumu, waislamu wametengewa sehemu ya kuabudu katika Pentagon, ambalo baadhi ya waumini wa kiislamu walijaribu kulilipua? Hii inawezekana kweli kutokea huko mashariki ya kati?

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Amandla...
Mkuu wangu soma hoja ya mtu kwa kuelewa anachohoji yeye kisha jibu kulingana na... Mimi nimeweka bandiko langu kwa kumjibu Pasco ambaye kama umemsoma vizuri utagundua kwamba majibu yangu yoote yametokana na hoja yake na zaidi ni kumfahamisha chimbuko la kuingia dini Tanzania na tofauti ya tawala baina ya Mzungu na mwarabu.

Hakuna mtu anayezungumzia Utawala wa Uingereza leo hii uko vipi, na hata huyo Mohamed Said anapohoji kukandamizwa kwa Waislaam, hazungumzii leo isipokuwa wakati wa Nyerere na ndio maana sisi tunapinga kuwa udhalimu huo haukuwepo zaidi ya waislaam kuwezeshwa. Kuhusu Ulaya na hasa hiyo Uingereza nakuhakikishia mkuu wangu nenda kasome hiistoria utakuta karibu nchi zote zoteza Ulaya zimepatikana Uhuru wao kwa kupitia dini ya kikristu na ndio maana ktk kila nchi hizi bado wana Wafalme na wanaheshimika.. .

Kisha basi ni lazima ufahamu kwamba dini ndio Culture ya wazungu hivyo sii kweli ati wazungu wanatenganisha dini na Utawala hali utamaduni wao umetokana na dini..Kinachofanyika leo ni kupingana na baadhi ya culture hizo za kidini na hakika nakuhakikishia kama wewe sii muumini wa dini zao (ukristu) huwezi kutawala nchi zao lakini unaweza kuwa kizazi kilichohamia hapo na ukatawala..Foundation ya uhuru wao ni dini hilo kataa uanvyopenda lakini ukweli utabakia palepale.

Mabadliko ya Uingereza kuingia demokrasia ni hatua nyingine baada ya nchi kupata Uhuru wake lakini ktk fungu la kidini.. Na ka sikosei wao walijitenga na Ukatoliki kwa sababu King Henry alimpa talaka mkewe kinyume cha sheria za kidini hivyo yeye akachukua jukumu la la kuwa head of the church of England na kutoka Ukatoliki ( sina hakika na jina la King mwenyewe).

Marekani hadi kesho wanasema wao wenyewe kwamba nchi yao imepoatikana kutokana na dini ya Kikristu na hawa wametawaliwa vile vile..Na nenda hadi kule Romania ambako kwa yule mtu wa kutisha Dracula, historia yake alikuwa pia kiongozi wa dini na mfalme lakini nao wakaja kuwa Wakomunist baadaye.

Na unapozungumzia Rome kumbuka tu kwamba nchi hiyo ilitawaliwa na Waislaam na hadi leo ndio Rome ina msikiti mmoja. Sasa sijui kama umefuatilia kwa nini miaka yoote ile haukujengwa msikiti hadi majuzi tu. Na kisha yaonyesha wewe unasikiliza saana CNN pasipo kupima. Yanayotokea Saudia na Vatican hayahusiani na fikra zako wewe kwani wakati wa mtume kulikuwa na makanisa Saudia kwa taarifa yako..

Sasa kwani msikiti ukijengwa barabara mbili toka 9/11? ndio ina maanisha kitu gani kama sii kusema hawaamini Waislaam. Those guyz wa 9/11 were Arabs, tena WaSaudia ambao wameyafanya waliyoyafanya kwa sababu they want America out of Saudia.

Msikiti ni wa Waislaam sawa na Sinagogi iliyopo mitaa hiyo hiyo ya 9/11, iweje wao (jews) iwe sawa lakini sio kwa Waislaam kama sii kuwabagua...Labda nikukuguse wewe, Ati Waafrika tutake kujenga jengo la jumuiya yetu tukatazwe kujenga sehemu kwa sababu WaSomalia walihujumu Wamarekani lakini Wachina, waarabu na Wahindi na watu wengine woote wanaruhusiwa kujenga majenog ya jumuiya zao.. Ooh nilitaka kusahau kama unataka kuona makanisa google utayaona mengi moja wapo ni Zanzibar na Mombasa ambako kulikuwa na Waislaam kwa asilimia 99 bado kuna makanisa. Wee google utayaona makanisa tena toka enzi na enzi yamesimama..

Na sijui kwa nini nakuelezea haya yote kwa sababu naamini kabisa mtu yeyote anayesukumwa na imani ya dini haweziu kuona haki hii isipokuwa yake mwenyewe.. Na ndio maana ya usemi wangu koote kule nilikotoka. You proved my point kwamba ni vigumu kwa mkristu kuona haki ya wengine pale yeye haoni haki isipokuwa yake yeye mwenyewe. Sijui kama umenielewa kifungu hiki?

Hakuna sehemu yoyote inayosema Taliban represent Islam isipokuwa ni binadamu wanaotaka ku preserve culture na dini yao ktk kuendesha maisha yao. Who the f.... sisi kuwaamulia wao maisha yao hata kama sisi hatuyapendi? hao hao Taliban waliondoa kabisa biashara ya Opium na moja ya chuki kubwa ya hawa watu ni kuondoa Bwimbwi ambalo linazitajirisha nchi za Ulaya kwa gharama ya maisha ya wananchi wao wenyewe.. Wakati Taliban yupo madarakani Bwibwi lilikuwa na bei kuliko Cocaine kwa sababu halikupatikana ( demand kubwa supply ndogo)leo wanalaumiwa ati kwa kulima madawa ya kulevya.. 90% ya Opium farms na production inatoka sehemu ambazo NATO wamezishika iweje taliban ndio walaumiwe hali American na majeshi ya NATO wanaweza kuweka vikwazo!

In your mind, hivi kweli unafikiri Marekani cares abaout hao wanawake wanaoonewa ati kwa kucharazwa bakora wasipovaa hijab? Mbona Saudia pia wanacharaza bakora na hatujasikia waki plan kuwaokoa wanawake wa huko. Na hiyo Afghanstan yenyewe ndio maskini kuliko hata haiti toka wamesaidiwa Na marekani kuwaondoa Urusi hawajapiga hatua hata moja under Taliba au baada.

Mkuu sasa unabisha kupingwa kwa benki ya kiislaam na wakristu?...yaani unakataa katu kwa kuelewa au....Na leo OIC ndio unajua umuhimu wa kutowategemea wageni lakini wanapoleta toka huko uzunguni kuja kwenu hakuna fikra hizo ila wepesi kusema Nanyi (waislaam) fanyeni kama sisi hamjakatazwa!..duh! basi mkuu wangu nadhani hatutaweza kuelewana hata kidogo..

All this shit about Taliban ni ujinga mtupu ambao mimi Mkandara will never buy it for a pennie.. Walioripua 9/11 ni Wasaudia (kama sii Wayahudi wenyewe) ambao maisha yao hawajawahi kuishi Afghan tan ila ikasemekana Osama na Al Queda huko ndiko kwenye makao yao makuu yao. Osama ambaye ni Msaudia na hakuwahi kuishi Afghanstan alipelekwa Afghanstan na Marekani wenyewe kuwawezesha wao kupenya ndani Taliban kumsinda Mrusi, leo iweje Marekani waishambulie Afghanstan hali kila kitu kilichotokea 9/11 hakihusiani kabisa na WaAfghanstan maskini ambao hata kula yao wenyewe ni shida!..Oooh mara Osama alionekana Torabora mara sijui katuma ujumbe mpya yaani wao ndio wanapata ujumbe kwa kila Osama analotaka kufanya hali wanadai hawajui aliko ila huwa wanaletewa tapes tu.. how can we be that stupid!

Marekani alitaka kuingia Afghanstan kuwaondoa Taliban na sio kwa sababu ya dini au matendo yao isipokuwa kuwawezesha kujenga bomba la Mafuta na gas toka Kuzestan hadi bahari ya Hindi. Niliyasema kama haya wakati wa Saadam kwamba hakuna WMD tena hapa hapa JF watu hamkuamini mkaniita mwongo na kadhalika. Kwa hiyo mkuu wangu nawe usichanganye dini na politics. Huku ndiko kuchanganya kwani Marekani wanaposhambulia nchi nyingine hutoa sababu za kidini.. wao wakienda vitani wanasema Lord Jesus awalinde lakini Muislaam akisema Allah Akbar basi huyo ni terrorist. Come on..
 
Mohamed Said anazungumzia mambo ya Mwembechai na kuzuiwa kwa kitabu cha Njoza (?) kama mfano wa ukandamizwaji wa waislamu. Wewe mwenyewe umeingiza suala la O.I.C. na kuzuiwa kwa benki ya kiislamu kama mfano wa kugandamizwa kwa waislamu. Vyote hivi ni vitu vimetendeka baada ya Nyerere kung'atuka na vingine baada ya kifo chake!

Ni nchi chache sana za ulaya zilipata waokupitia ukristu. Spain, Ugiriki na Ureno ndizo unazoweza kudai hivyo. Nyingi zilikuwa ni kutoka wakristu wenzao au mapinduzi dhidi ya utawala wa kifalme ambao wote walikuwa wakristu. Pili, ni lazima ujue ulaya hii tunayoiona sasa hivi ni ya hivi karibuni tu, hususan kuanzia karne 19 kwa sehemu kubwa. Kabla ya hapo sehemu kubwa ya Ulaya ilikuwa ni vifalme vidogo vikijitawala na kupigana baina ya wenyewe. Nchi kama Italy, Ujerumani n.k. ni za hivi karibuni tu. Ireland (nchi ya kikatoliki) ilipata uhuru wake kutoka kwa muingereza (mprotestant), Norway (mluteri) na Finland (mluteri) zilipata uhuru wao kutoka kwa Sweden (mluteri), Uingereza ( wapagani) walipata uhuru wao kutoka kwa warumi ambao tayari waliishaanza kuingiwa na ukristu, Spain ilikuwa sehemu ya Roman Empire hadi Empire hiyo iliposambaratika. Moors (waislamu) walipovamia Spain mwaka 711 waliikuta iko huru. Moors walitawala kwa miaka 700 hadi walipoondolewa tena na wakristu. Italy haijawahi kutawaliwa na waislamu bali ilikuwa ni sehemu ya Austria na walipigana vita 3 katika karne ya 19 ( 1848,1859 na1866). Ugiriki walikuwa chini ya Ottoman Empire (waislamu) hadi mapinduzi kati ya 1821-1830, walipopigana kwa kusaidiwa na majeshi kutoka nchi nyingine za ulaya dhidi ya majeshi ya Ottoman yakisaidiwa na Mistri na Tunisia. Moors walivamia Portugal mwaka 711 na walifukuzwa kutoka sehemu hiyo mwaka 868. Wafaransa wanahesabu Julai 14 (Bastille) kuwa siku yao ya Uhuru wakikumbuka siku ambapo jela ya Bastille mwaka 1789 na kuashiriwa mapinduzi dhidi ya utawala wa kifalme wa Louis XVI ( mkristu).

Kisha basi ni lazima ufahamu kwamba dini ndio Culture ya wazungu hivyo sii kweli ati wazungu wanatenganisha dini na Utawala hali utamaduni wao umetokana na dini..Kinachofanyika leo ni kupingana na baadhi ya culture hizo za kidini na hakika nakuhakikishia kama wewe sii muumini wa dini zao (ukristu) huwezi kutawala nchi zao lakini unaweza kuwa kizazi kilichohamia hapo na ukatawala..Foundation ya uhuru wao ni dini hilo kataa uanvyopenda lakini ukweli utabakia palepale.

Unaposema culture una maana gani? Sehemu kubwa mno ya raia wa nchi nyingi za ulaya ni wakristu, hii haina ubishi. Utawala (Governance) wa utawala wa nchi hizo msingi wake ni tamaduni za kikristu na kiyahudi (Judae-Christian), nayo haina ubishi. Lakini hii haina maana kuwa kanisa ni sehemu ya utawala. Hakuna nchi ya ulaya ambapo kiongozi wa kanisa ana mamlaka ya kisheria kumhukumu raia wake. Katika theocracies za Iran na Afghanistan ya Taliban, muamuzi wa mwisho alikuwa kiongozi wa dini. Katika nchi zinazotawaliwak kwa misingi ya dini ya kiislamu, viongozi wa kidini wanaweza kumhukumu mtu kifungo, kukatwa kiungo, kuchapwa bakora na hata kifo!. Nitajie nchi hizo unazoitwa za kikristu ambapo Padri, Askofu, Kadinali au hata papa anaweza kumhukumu mtu kifungo hata kwa kuiba kuku! Sana sana wanachoweza kufanya ni kukutenga na kanisa lao. Na wao wakikosea wanapelekwa mbele ya sheria ambako atakayewahukumu anaweza kuwa myahudi, rasta, atheist au muumini wao! Katika nchi hizo mtu wa dini nyingine kutawala inakuwa vigumu ni kutokana na wingi na sio kwa sababu katiba inamkataza muislamu au myahudi kutawala. Katika representative democracy uchaguzi unafunywa na wapiga kura ambao wengi wanafanya maamuzi kutokana na imani zao pamoja na vitu vingine. Mtu mweusi ilikuwa vigumu kutawala marekani si kwa sababu katiba ilimkataza bali kwa sababu wengi wa raia wa marekani waliona ugumu kumpigia kura mtu mweusi. Mwanamke hivyo hivyo ingawa katika nchi za ulaya jinsia imekuwa si kikwazoo. Leo Marekani wanamwakilishi muislamu katika bunge lao. Nitajie nchi ya kiislamu yenye mwakilishi asiye muislamu katika bunge lao. Hapa kwetu mhindi au mchaga ni vigumu kupata urais , si kwa sababu katiba inawakataza bali kwa sababu raia wengi wana prejudice dhidi yao.

Mabadliko ya Uingereza kuingia demokrasia ni hatua nyingine baada ya nchi kupata Uhuru wake lakini ktk fungu la kidini.. Na ka sikosei wao walijitenga na Ukatoliki kwa sababu King Henry alimpa talaka mkewe kinyume cha sheria za kidini hivyo yeye akachukua jukumu la la kuwa head of the church of England na kutoka Ukatoliki ( sina hakika na jina la King mwenyewe).

Uhuru wa uingereza kutoka kwa nani?Uingereza ilikuwa sehemu ya Roman Empire lakini baada ya kusambaratika ikabaki ilivyo. Walivamiwa na wa-norman 1066 ambao walijichanganya wakawa sehemu ya uingereza. Uingereza haijawahi kuwa na mapinduzi dhidi ya watawala wao. Kilichofanyika uingereza ni kusainiwa kwa Magna Carta mwaka 1215 na mfale John ambayo ilimnyang'anya mamlaka mengi mfalame ( ambaye alikuwa mtawala na kiongozi wa dini) na ilimpa haki raia kuhukumiwa na wenziwe na sio uongozi wa dini au ule wa kifalme. Hayo mabadiliko unayozungumzia hayakuhusu haki ya raia wa kawaida bali yalimpa uhuru mfalme wa kuweza kuingia katika vita dhidi ya wenzie bila kungoja kibali kutoka Roma pamoja na hiyo ya kuoa anayemtaka.

Nitaendelea baadae.

Amandla.....
 
Fundi Mchundo,
Unachanganya vitu sana tu. Taifa kuwa huru na kupanga Uraia ni kitu tofauti sana na Uhuru wa wananchi wake. zanzibar wanaweza kusema wametawaliwa na Tanganyika na wakadai Uhuru wao, haina maana Zanzibar haikuwa nchi na huru ndani ya Tanzania. Tunachozungumzia hapa ni founding father of their nation. Mwisho wa maneno yako unazungumza kwa hisia za kidini zaidi kama Mohamed Said, yaani ni lugha inayofanana na - kama Zanzibaar (waislaam) wakija jitenga na watadai nchi mpya watasema walipata Uhuru wao kutoka bara (wakristu).

Najua unashindwa kusema matukio mengi ya Ulaya yalikuwa mapinduzi dhidi ya wao kwa wao kutokana na tofauti za imani ya kidini au kumuondoa mkoloni ambaye alikuwa dini sawa na wao lakini dhalimu. Kuna sehemu nimekwambia kwamba Demokrasia tunayoiona Ulaya ni itikadi zinazopingana na mila zile za kidini zilizokuwepo na nimesema wazi kwamba demokrasia iliytopo Uingereza ni hatua nyingine ktk upinzani wa itikadi na mfumo ulokuwepo..

Hao Ireland wakipingana na Muingereza kidini lakini ni serikali huoni picha nayojarigbu kuijenga hapa mkuu wangu kwamba they are all Christians..Acha political matters pembeni. Nakuomba tena rudia kusoma historia ya nchi za Ulaya utaona jinsi dini ilivyoweza kuchukua nafasi kubwa ya identity yao kuliko sisi tunaojitambulisha kwa makabila.

Mwanafalsafa anapopinga utawala wa monarchy na kujiita huru kisiasa kama walivyotangaza Canada walivyotangaza. Again hata sisi ipo siku tutakuja fikia demokrasia ya kweli na ni hatua mbele baada ya kuwa huru..ukiniuliza huru kutoka kwa nani ina maana hufuatilii historia ya nchi ila kwa haya unayoyaona leo.

Kifupi nachoweza kukuambia na ukanielewa vizuri pengine nitumie mfano wa Yesu...ni kwamba Jesus was a Jews na yeye ndiye aliyekuja pingana na Wayahudi hivyo haiwezi kuondoa haki yake ya Uzawa kama alikuwa Myahudi kwa sababu tu alikuja na imani mpya inayopingana na baadhi ya ibada za wayahudi..Huyo mtawala mwenyewe Pilato mroma alikuwa mhmyahudi A jew by faith)..Na hata kama isingekuwa dini kama Yesu angepingana na Utawala wa Pialato kisiasa isingeondoa imani yao kuwa tofauti kidini kwa sababu mmoja ni Myahudi kwa uzawa (ban Israel) na mwingine ni Mroma kwa uzawa.

Na kuhusu Uingereza, mkuu wangu hawakuwa Wapagan, hawa walitawaliwa na Waroma ambao walikuwa Christians (Claudian invasion). Kwa hiyo wenyewe wanasema walikuwa Romanised, na kumbuka tu kwamba mtawala wao Constantine 2nd alikuwa mtoto wa yule Mkatoliki Constatine the great na kama sikosei ndiye aliye declare the All Roman Empire should henceforth be Christian.

Huyo Arthur mwenyewe, mama yake alikuwa a descended kutoka ktk line ya Priestesses of Avalon hata dada yake mwenyewe Morgaine alikuwa Priestess of Avalon kwa hiyo sii suala la kubishana hali ushahidi unaonyesha wazi kwamba unaweza rudi nyuma hadi karne ya 50 Ukristu ulikuwepo tayari kama ulivyo Uislaam ktk nchi za Kiarabu..Mkuu wangu yaani hiyo Europe ndio usiseme kabisa ukielewa kwamba dini hii ilitumika sana ktk vita vya ku conquer Ulaya na kusambaza utamaduni huu - a way of life na uzima wa milele..

Mkuu wangu kuwa against Mkristu mwenzako haina maana unapingana na dini isipokuwa unapingana na udhalimu wa mtawala. Hiui ndio lugha nayojaribu ku preach hapa kwamba dini haihusiani kabisa na fikra za udhalimu wa aina yoyote ile ambayo watu wanaweza kuipinga. Na ndio maana napinga wale wanamshuku Nyerere kwa sababu tu ni Mkristu.

Naamini kama kweli alikuwa mtu mbaya basi hata kama angekuwa Muislaam angeyafanya mabaya yale yale. Mbona huyo Mwinyi kafanya mengi machafu kwa Waislam kuliko hata huyo Nyerere, je inamfanya yeye kuwa Mkristu au? Huu ndio mtazamo wangu kktk mada hii na sii vinginevyo kubishaa juu ya dini hii kama vile ipo bora kuliko nyingine.

Ama hivi leo sisi tunapopingana na JK au CCM haitufanyi sisi tuwe tofauti kiimani ya dini ya JK ndio tupate kulalamika. Huu ni ufinyu wa kufikiri kwani JK hakuna jambo lolote analofanya ktk uongozi wake ni la kiislaam na hata huyu Mkapa hakufanya lolote la Kikristu isipokuwa kama Mkapa anavyotaka kufanya.

halafu tukirudi ktk swwala la culture, mkuu unazidi kupotea na ufahamu wako. Ukristu sio kuwa na Padre au Askofu ila ni Imani ya kiroho inayomkubali Yesu kama ndiye mwokozi wako. Mnaweza tofautiana ktk hadithi na sunna lakini bado tamaduni zenu zina root moja. Haya maswala ya kusema nikutajie nchi hata moja ya Kikristu hali unajua fika kwamba chimbuko lao ni ukristu, sijui unataka niseme nini zaidi. haya umekuja na ya taliban tena wakati hujui maana ya Taliban..

Hivi mkuu umewahi kuuliza Wahabbi ni kina nani hata ukawachukulia kwamba hao ndio Waislaam pasipo kufahamu undani wao. Sasa leo hii mimi maadam siwezi kuhukumiwa na huyo Taliban basi mimi sio Muislaam? Huyo taliba au Mulla anayehukumu ni msomi wa shera za dini na shehebu lao hivyo ana qualify kwa mizani yao na sio yako wewe.. Mbona huyo Papa na vatican wameshindwa kuwahukumu walio wala witi watoto ndio niseme ni huo ni Ukristu gani au lawama zangu zinatakiwa kuelekezwa kwa Papa kama zipo.. Acha zako mkuu wangu acha maswla ya dini wewe bakia na imani yako usitake kuhukumu wengine hali kwako ni mtoto mtupu.

Haya umerudi tena na kusema ati Marekani bunge lao lina Waislaam wakati huo huo unatakataa kwamba Marekani sio nchi za kikristu.. sasa sielwi nini malengo ya swali lako. Ni wewe unayepinga kupatikana kwa mataifa ya Ulaya chini ya Ukritu lakini mwepesi kuutumia Ukristu ku define make of their Government ambayo umekataa haina mahusiano na Ukristu. Hata sikuelewi mkuu wangu,sema moja tujue unazungumza kipi.
Nchi za Kiislaam zinaitwa nchi za kiislaam wala hazijifichi, hivyo kwa kila wanachofanya inaeleweka bila kujificha nyuma ya pazia. Sheria zao ni wazi na unapoingia kwao (Rome) unaua utafanya kama Waroma. Sii hawa Wamarekani wanaolaani watu wengine wakiua lakini wao wepesi kudai casualties of war hali wamebeba silaha kubwa za kuua.. wananyonga watu au kupiga sindano za kuua lakini asihukumiwe mtu mwingine nchi za waislaam. Na the fact is Marekani wananyonga watu wengi kuliko jumla ya nchi zote za kiislaam kwa mwaka.

Hilo swali la mwisho unarudi kuel kule nilikoanzia huko juu. Labda nitasema kwa ufupi to kwamba walitawaliwa na ROMANS.....
 
Marekani hadi kesho wanasema wao wenyewe kwamba nchi yao imepoatikana kutokana na dini ya Kikristu na hawa wametawaliwa vile vile..Na nenda hadi kule Romania ambako kwa yule mtu wa kutisha Dracula, historia yake alikuwa pia kiongozi wa dini na mfalme lakini nao wakaja kuwa Wakomunist baadaye.

Kuna machizi marekani ambao sio tu wanadai nchi yao ni ya kikristu bali ni yakiprotestanti! Wakatoliki kama John F Kennedy walipingwa na baadhi ya watu kuwa ukatoliki si sehemu ya umarekani. Hivyo hivyo kuna baadhi wanapinga waislamu, wayahudi, watu weusi, walatino n.k. na kuwaona kuwa si sehemu ya umarekani. Kinachozungumzia umarekani ni katiba yenyewe na si imani ya walioiandika. Mbona karibu wote wa walioandika katiba hiyo walikuwa na watumwa, hawakuhesabu mwanamke na mtu mweusi kuwa sawa na mwanaume mweupe? Lakini katiba hiyo hiyo waliyoiandika, ikisisitiza usawa wa watu wote imetumika kuonyesha kuwa hawa wote ni sehemu ya jamii. Ndiyo maana Obama (Mkristu) amesema KIKATIBA ni haki ya mmarekani yeyote kuabudu dini anayotaka na kujenga nyumba ya ibada mahali popote (ili mradi havunji sheria). Wewe kuwatumia watu kama wakina Glenn beck na Sarah Palin kudefine wamarekani ni makosa.

Unamzungumzia Bram Stoker au Vlad III Dracula mtawala wa Wallachia? Dracula ambaye wengi tunamjua alikuwa ni mtu wa kufikirika. Bali Vlad III Dracula kweli alikuwepo na alikuwa katili sana. Pamoja na ukatili wake, anaheshimika Romania kwa kuwa alipigana na kuwashinda waturuki wa Ottoman Empire. Sasa uhusiano wake na wa Romania kuwa nchi ya kikomunisti wala siuoni maana alikufa mwaka 1462,miaka kibao kabla ya Romania kuwa nchi ya kikommunisti mwaka 1947. Rumania iliingia kwenye ukomunisti baada ya kutawaliwa na urusi (USSR) baada ya vita kuu ya pili. Adhabu hii ilichangiwa sana na kitendo cha Rumania kuungana na ujerumani dhidi ya warusi katika vita hiyo. Ingawa Runmania waligeuka baadaye na kupigana dhidi ya ujerumani, urusi haikuwasamehe. Ndiyo maana mara baada ya vita hiyo kwisha, vibaraka wake walimpindua Mfalme Michael na ktangaza jamhuri ya kikomunisti. Dracula hapa ameingia vipi?

Na unapozungumzia Rome kumbuka tu kwamba nchi hiyo ilitawaliwa na Waislaam na hadi leo ndio Rome ina msikiti mmoja. Sasa sijui kama umefuatilia kwa nini miaka yoote ile haukujengwa msikiti hadi majuzi tu. Na kisha yaonyesha wewe unasikiliza saana CNN pasipo kupima. Yanayotokea Saudia na Vatican hayahusiani na fikra zako wewe kwani wakati wa mtume kulikuwa na makanisa Saudia kwa taarifa yako..

Rome haijawahi kutawaliwa na waislamu. Labda kama unazungumzia Constatinople ya uturuki ambayo kweli ilikuwa sehemu ya Roman Empire. Ottoman walipowapindua wakristu wa Constatinople, Roman Empire iliisha sambaratika. Kama unazungumzia Italy, hii nayo haijawahi kutawaliwa na waislamu. Unless unataka kutuambia kuwa wa-Austria walikuwa waislamu? Rome inasikiti mkubwa kuliko misikiti yote iliyoko Ulaya. Msikiti ambao ulibuniwa na wakristu ( Paolo Portoghesi) kwenye kiwanja walichopewa na jiji la Rome. Hivi inawezekana kweli kujenga hata kajikanisa kaduchu karibu na Maka? Inawezekana kweli kwa utawala wa Saudi Arabia kutoa kiwanja kwa wakristu ili wajenge kanisa?

Mtume aliukuta ukristu. Kuzungumzia wakati wa mtume hivyo si sahihi. Wakati wa Mtume Makka walikuwa wanaabudu sanamu, kwa hiyo unataka kutuambia mpaka leo watu wa maka wanaabudu sanamu? Tunazungumzia Saudia aliyoiacha Mtume na hii iliyopo sasa. Je, kuna kanisa Riyadh na Jeddah?

Sasa kwani msikiti ukijengwa barabara mbili toka 9/11? ndio ina maanisha kitu gani kama sii kusema hawaamini Waislaam. Those guyz wa 9/11 were Arabs, tena WaSaudia ambao wameyafanya waliyoyafanya kwa sababu they want America out of Saudia.

Msikiti ni wa Waislaam sawa na Sinagogi iliyopo mitaa hiyo hiyo ya 9/11, iweje wao (jews) iwe sawa lakini sio kwa Waislaam kama sii kuwabagua...Labda nikukuguse wewe, Ati Waafrika tutake kujenga jengo la jumuiya yetu tukatazwe kujenga sehemu kwa sababu WaSomalia walihujumu Wamarekani lakini Wachina, waarabu na Wahindi na watu wengine woote wanaruhusiwa kujenga majenog ya jumuiya zao.. Ooh nilitaka kusahau kama unataka kuona makanisa google utayaona mengi moja wapo ni Zanzibar na Mombasa ambako kulikuwa na Waislaam kwa asilimia 99 bado kuna makanisa. Wee google utayaona makanisa tena toka enzi na enzi yamesimama..

Mohamed Atta kiongozi wa magaidi wa 9/11 alitoka Misri. Wasaudi walikuwa wengi lakini si wote walitoka Saudi Arabi. Wote hawa walijiita waislamu na walifanya waliyoyafanya wakiamini kuwa wanapigana kwa niaba ya uislamu. Hilo unalozungumzia la wao kutaka wamarekani watoke Saudia ni wewe unalileta. Wale jamaa usongo wao ulikuwa Palestine na sehemu nyingine ambako wanaamini waislamu wanayanyaswa. Watu hao waliona Marekani kama taifa la kikristu na kiyahudi kwa hiyo ni lengo halali katika vita yao dhidi ya wale wote wanaodhani wanahujumu uislamu. kama walivyofanya uingereza, hispania na hata Moroko.

Utasemaje hawaamini waislamu wakati karibu zaidi kuna misikiti miwili? Kama hawawaamini waislamu si wangesema kuwa ivunjwe? na hapo panapokusudiwa kujengwa hilo jengo la waislamu tayari waislamu wanafanyia maombi na hamna aliyewafukuza. Maombi ya kubomoa hilo jengo ili kujenga hiyo community centre yameishapitishwa na utawala wa New York. Mtetezi mkubwa wa msikiti huo si muislamu bali ni Meya wa New York Bloomberg. Maandamano yamefanywa kupinga kujengwa kwake na watu wengi tu wameandamana kuunga mkono! Hii ndiyo demokrasi.

Kama kuna synagogue karibu na Ground Zero lilikuwepo kabla ya matukio ya 9/11. Kama yalivyokuwepo makanisa na misikiti. Kukimbilia kwa wayahudi kunadhihirisha bias yako dhidi yao. Sinagogi lina haki kuwepo hapo kama ilivyo kwa kanisa na msikiti. Hilo la waafrika ni far fetched.

Hiayo makanisa yaliyopo Zanzibar na Mombasa yalijengwa wakati wa utawala wa waingereza. Ingawa Zanzibar si nchi ya kiislamu lakini niambie kuna makanisa mangapi mapya yamejengwa mithili ya yale ya Stone Town? Au kabla ya waingereza kuingia? Au wareno kabla yao?

Na sijui kwa nini nakuelezea haya yote kwa sababu naamini kabisa mtu yeyote anayesukumwa na imani ya dini haweziu kuona haki hii isipokuwa yake mwenyewe.. Na ndio maana ya usemi wangu koote kule nilikotoka. You proved my point kwamba ni vigumu kwa mkristu kuona haki ya wengine pale yeye haoni haki isipokuwa yake yeye mwenyewe. Sijui kama umenielewa kifungu hiki?

Sijakuelewa maana hakuna mahali ambapo umeonyesha kuwa waislamu wananyimwa haki zao kikatiba katika nchi za ulaya. Ubaguzi upo. Profiling ipo. Lakini chini ya katiba za huko wanahesabiwa kama raia yeyote na haki yao ya kuabudu haipingiki. Hii si kweli katika nchi zinazojiita za kiislamu. Tofauti na unavyotaka kusema, mimi naona ni wewe ndiye umedhihirisha jinsi udini unavyoweza kukuzuia kuoana ukweli. Mfano ni hii saga ya jengo la komuniti ya waislamu hapo Ground Zero. Badala ya kuwaona wakina Bloomberg, wakina Obama, wewe unawakazania kooks kamawakina Glen Beck na Palin ambao watakuthibitishia imani yako kuwa wakristu wanachukia waislamu. Kuna mashehe wangapi ambao wanafanya mihadhara kutukana ukristu? Unataka kutuambia wao ndiyo wanawakilisha uislamu? Au mtu kama Osama Bimn Laden ndiye sura ya uislamu? Wewe pamoja na kuwa palikuwepo na bado kuna sehemu za kuabudia waislamu hapo Ground Zero, unanyooshea vidole sinagogi ambalo hata halihusiki katika ishu yote hii. Unasahau kuwa pamoja na kuwa mawazo ya hao wanaopinga kujengwa hilo jengo hapo, hakuna hata mmoja wao anayesema kuwa msikiti usijengwe mahali poptote marekani. Ugomvi wao ni sehemu panapotakiwa kujengwa na sio dhana ya kujenga msikiti kama unavyotaka kupotosha. pasingekuwa na kellele kiasi hiki kama wangesema wataujenga Harlem kwa mfano.

Hakuna sehemu yoyote inayosema Taliban represent Islam isipokuwa ni binadamu wanaotaka ku preserve culture na dini yao ktk kuendesha maisha yao. Who the f.... sisi kuwaamulia wao maisha yao hata kama sisi hatuyapendi? hao hao Taliban waliondoa kabisa biashara ya Opium na moja ya chuki kubwa ya hawa watu ni kuondoa Bwimbwi ambalo linazitajirisha nchi za Ulaya kwa gharama ya maisha ya wananchi wao wenyewe.. Wakati Taliban yupo madarakani Bwibwi lilikuwa na bei kuliko Cocaine kwa sababu halikupatikana ( demand kubwa supply ndogo)leo wanalaumiwa ati kwa kulima madawa ya kulevya.. 90% ya Opium farms na production inatoka sehemu ambazo NATO wamezishika iweje taliban ndio walaumiwe hali American na majeshi ya NATO wanaweza kuweka vikwazo!

In your mind, hivi kweli unafikiri Marekani cares abaout hao wanawake wanaoonewa ati kwa kucharazwa bakora wasipovaa hijab? Mbona Saudia pia wanacharaza bakora na hatujasikia waki plan kuwaokoa wanawake wa huko. Na hiyo Afghanstan yenyewe ndio maskini kuliko hata haiti toka wamesaidiwa Na marekani kuwaondoa Urusi hawajapiga hatua hata moja under Taliba au baada.

Sasa Taliban walikuwa waislamu au hawakuwa waislamu? unaposema tusiingilie una maana gani? Hivi wakati tunaomba vikwazo viwekwe dhidi ya utawala halali wa Afrika kusini tulikosea? Kama hao wazungu walitaka kuwabagua wengine si ilikuwa juu yao?

Wamarekani ndiyo waliowapa silaha Taliban kwa hiyo kudai mambo yanayoendelea huko ni ya kidini ni upuuzi. Wamarekani wako huko kwa sababu Taliban walimhifadhi mbaya wao mkuu, Osama bin Laden. Hawakudai hata siku moja kuwa walienda huko kuwakomboa wanawake wa ki-Afghanistan. hayo ni matokeo tu ya vita yao dhidi kile wanachodai ni uislamu wa kigaidi. Mfano wako dhidi ya bwibwi hauna mantik vile vile. Afrika Kusini chini ya apartheid ilikuwa na amani kuliko ilivyo sasa. Unataka kutuambia basi warudishe mfumo huo kwa sababu ujambazi haukutamba kiasi cha hivi leo?

Mkuu sasa unabisha kupingwa kwa benki ya kiislaam na wakristu?...yaani unakataa katu kwa kuelewa au....Na leo OIC ndio unajua umuhimu wa kutowategemea wageni lakini wanapoleta toka huko uzunguni kuja kwenu hakuna fikra hizo ila wepesi kusema Nanyi (waislaam) fanyeni kama sisi hamjakatazwa!..duh! basi mkuu wangu nadhani hatutaweza kuelewana hata kidogo..

Kwa nini tuandikie mate wakati wino upo? Nitajie benki moja ya kiislamu iliyopingwa na kuzuiwa kufanya biashara tanzania na wakristu. Moja tu, Mkuu. Kupingwa katika demokrasi ni kama adha. Mbona kuna waislamu wanapinga kujengwa mabucha ya kiti moto, mabaa na kadhalika? Sasa utasema kuwa serikali ya muislamu Jakaya kikwete inawazuia wakristu kujenga bucha za kiti moto? Si utakuwa unamuonea? Wako wakristu watakaopinga chochote wanachodhani ndiyo mwanzo wa kuingizwa utawala wa sharia nchini. Hii haina maana kuwa serikali inazuia shughuli zozote zinazofanywa na jumuia ya kiislamu. Ni haki ya wakristu kupinga O.I.C. hata kama wanakosea lakini ni serikali peke yake ambayo inaweza kujiunga au kutojiunga na O.I.C. Na mimi ninavyojua nilipoangalia mara ya mwisho, kiongozi waserikali hiyo ni muislamu. Utawalaumuje sasa wakristu kwa serikali yake kutojiunga na O.I.C.? Niambie ni jumuia ipi ya kikristu ambayo serikali imejiunga nayo? Na ambayo inaleta misaada kwa wakristu peke yao? Matokeo ya makanisa mengi ni wamisheni waliokuja wakati na kabla ya ukoloni. Uhusiano wao na makanisa mama ndiyo iliyopelekea na inayopelekea wao kusaidiwa. lakini pamoja na mahusiano hayo, ni juhudi za waumini wa madhehebu hayo zinazoendeleza shughuli zao zote za kimaendeleo. Makanisa mengi unayoona yanaibuka hapa nchini ni matokeo ya michango ya waumini na si misaada kutoka nje. Ingekuwa wanategemea Bishop wa Cantebury na bishop wa Rome basi hayo makanisa yangeishakufa zamani. mafanikio yao yanatokana na ushirikiano wao wao na si utegemezi. Unachpkidai wewe ni kuwa waislamu hawawezi kufanya lolote kujikwamua kama ankal hatatoka nje. Na mbaya zaidi, huyu ankal ni lazima akaribishwe na serikali yetu sote. Mbona muislamu Aga Khan, anajenga shule, hospitali, makazi ya wazee wa jumuia yake bila kungojea mwaliko wa serikali. Hao O.I.C. wamekatzwa kweli kuwasaidia waislamu hadi hapo tu serikali itakapojiunga nao? Wao wana uchungu na waislamu wenzao au serikali ya Tanzania?

All this shit about Taliban ni ujinga mtupu ambao mimi Mkandara will never buy it for a pennie.. Walioripua 9/11 ni Wasaudia (kama sii Wayahudi wenyewe) ambao maisha yao hawajawahi kuishi Afghan tan ila ikasemekana Osama na Al Queda huko ndiko kwenye makao yao makuu yao. Osama ambaye ni Msaudia na hakuwahi kuishi Afghanstan alipelekwa Afghanstan na Marekani wenyewe kuwawezesha wao kupenya ndani Taliban kumsinda Mrusi, leo iweje Marekani waishambulie Afghanstan hali kila kitu kilichotokea 9/11 hakihusiani kabisa na WaAfghanstan maskini ambao hata kula yao wenyewe ni shida!..Oooh mara Osama alionekana Torabora mara sijui katuma ujumbe mpya yaani wao ndio wanapata ujumbe kwa kila Osama analotaka kufanya hali wanadai hawajui aliko ila huwa wanaletewa tapes tu.. how can we be that stupid!

Are you for real? Wamarekani kweli walisaidia wapiganaji wa taliban dhidi ya urusi lakini hili la kusema Osama ni muajiriwa wa C.I.A. ndiyo nalisikia kwako! Madai kuwa wayahudi ndiyo waliolipua hayakuanza kwako. Yote hayo ni kujaribu kukwepa ukweli kuwa ni watu wenye imani yako ambao walifanya uovu ule. Mtu mwenye msimamo huu ni extremist na ni vigumu kumbadili.

Unataka kukataa kuwa Taliban walimpa hifadhi Osama? Osama aliishi Peshawar mwaka 1979 akisaidia kupigana dhidi ya warusi. Mwaka 1984 alianzisha Maktab-al- Khadamat. Aliondoka 1990 kurejea Saudia. mwaka 1992 alikimbilia Sudan na 1996 alirudi Afghanistan ambako alianzisha makambi ya mafunzo ya kijeshi. Ingawa ni kweli kuwa ugomvi wake na utawala wa Saudia ni kuwepo kwa majeshi ya wasio waislamu Saudi Arabia lakini mtazamo huu umepanuka zaidi na kujiona kuwa ni mtetezi mkubwa wa uislamu popte duniani, si Saudi Arabia tu.

Wamarekani walivamia Afghanistan baada ya serikali ya Taliban kukataa kumkabidhi kwa bila masharti yeyote. Utawala wa Taliban ulikuwa tayari kumkabidhi kama watahakikishiwa atahukumiwa katika mahakama ya kiislamu. Hii haikukubalika na marekani hasa ukichangia haja ya kisasi baada ya 9/11.
Marekani alitaka kuingia Afghanstan kuwaondoa Taliban na sio kwa sababu ya dini au matendo yao isipokuwa kuwawezesha kujenga bomba la Mafuta na gas toka Kuzestan hadi bahari ya Hindi. Niliyasema kama haya wakati wa Saadam kwamba hakuna WMD tena hapa hapa JF watu hamkuamini mkaniita mwongo na kadhalika. Kwa hiyo mkuu wangu nawe usichanganye dini na politics. Huku ndiko kuchanganya kwani Marekani wanaposhambulia nchi nyingine hutoa sababu za kidini.. wao wakienda vitani wanasema Lord Jesus awalinde lakini Muislaam akisema Allah Akbar basi huyo ni terrorist. Come on..

Hapa ndipo unapoonyesha unakotokea. Hilo la bomba la mafuta ni la kwako. Sijasikia mmarekani akisema Lord Jesus amlinde, huo ni uongo. Wanachoomba ni Mungu awalinde. Watu hawaitwi terrorists kwa kusema Allah Akbar vitani. Sijasikia mtu akisema majeshi ya Iran na Iraq wakati wanapigana yalikuwa ya ma-terrorists! Wanamuita mtu terrorists kama anasema Allah Akbar wakati anamchinja mtu ambaye kosa lake tu ni kuwa mtu wa dini nyingine. Hivyo hivyo, mkristu aktakayejifunga mabomu na kumlipua mwenzake asiye na hatia kwa imani za kidini ni terrorist. Timothy McVeigh alikuwa terrorist. Period.

Amamdla....
 
Mkandara,

Hivi kwa vile kiongozi wa nchi fulani ni wa dini fulani basi ina maana kuwa nchi hiyo ni ya dini hiyo? Unamaana kuwa tanzania ilikuwa nchi ya kikristu wakati wa Julius na benjamin na ya kiislamu wakati wa Ali na Jakaya? Kama sio, basi utaziitaje nchi za ulaya na marekani za kikristu kwa sababu tu watawala wake ni wakristu? Dini haina sehemu katika utawala wa nchi ya marekani ndiyo maana kwenye bunge lao kuna muislamu, myahudi, mkristu asiye na imani. Kuna mashoga pia kwenye bunge hilo. Sasa kama kweli wangekuwa wanaongozwa na imani kama unavyodai, wote hao wangekuwemo? Nchi zinazoongozwa na imani ndiyo hizo za mashariki ya kati ambako hutakuta mtu wa dini nyingine.

Amandla.......
 
wana Jf wenzangu hizi mada za udini zimeanza lini? Unajua mwanzoni JF ilianza vizuri, lakini sasa naona kama inaingiliwa. Hii itasababisha tusijadili hoja makini na badala yake tukaishia kuulizana wewe dini gani, wewe chama gani,au wewe thehebu gani. Kama wadau mtakumbuka mwalimu Nyerere alituasa tuache hii dhambi. Ni mbaya sana!
 
Mohamed Said,Fundi Mchundo,Mkandara,Jasusi,domokaya,Lole Gwakisa,

..naona sasa tumeserereka mpaka kwenye malumbano kuhusu historia ya dunia.

..binafsi ningependa sana tupate michango ya wana soshiolojia watuchambulie kwanini kuna maeneo yako nyuma kimaendeleo kuliko mengine. ningependa na wachumi nao waingie humo wachangie.

..binafsi sielewi kwanini mkoa wa Pwani ukose mwamko wa elimu wakati upo karibu sana na kitovu cha maendeleo na serikali, yaani jiji la Dar-es-salaam. naomba mzingatie neno mwamko.

..zaidi ya tuhuma za kubaguliwa na Mwalimu Nyerere, kuna mtu anaweza kutuelezea sociological na economic factors na economic factors zinazosababisha Pwani wawe na shule chache za sekondari za wazazi kulinganisha na mkoa kama Kilimanjaro au Kagera?

..binafsi naelemea zaidi kuamini kwamba sera za Mwalimu ktk kupambana na ujinga,umasikini,na maradhi zilifeli. tatizo lililopo ni degree ya kufeli kwake toka eneo moja la Tanzania hadi lingine. ninasema hayo bila kuhoji nia njema na uadilifu wa Mwalimu Nyerere.

..vilevile kuna maeneo Tanzania ambayo kutokana na historia, mila na utamaduni, jiografia, shughuli za kiuchumi etc etc, yalishindwa kufaidika na juhudi za serikali ya Mwalimu ktk kupeleka maendeleo kwa wananchi wake.

NB:

..kwenye science kuna kitu kinaitwa test by elimination. mjadala hapa ni kwamba Waislamu hawakuendelea kutokana na hujuma za Mwalimu Nyerere. sasa ni miaka 25 tangu Mwalimu aondoke madarakani, je hali ikoje?
 
Excellent Jokakuu.
For some people everything has got to be thought out for them well in advance.
They cant strategize or chart out their own destiny, it is simpler to blame the other guy, even if the other guy wants to help out.
Thats what beats me
Mwalimu Nyerere must have been a villain in this planet
 
Mageuzi1998 na JokaKuu,

Unfortunately hatuwezi kukwepa maana mada nzima iko steeped kwenye historia na udini! Distortions of both zimejaa na ni lazima niziseme. Kwa kukataa kuzi-debate ndio hizo distortions zinageuzwa kuwa "facts". Kwa baadhi yetu, hii hatuwezi kuiruhusu. Na ndio maana ninamjibu Mkandara hivi:

Fundi Mchundo,
Unachanganya vitu sana tu. Taifa kuwa huru na kupanga Uraia ni kitu tofauti sana na Uhuru wa wananchi wake. zanzibar wanaweza kusema wametawaliwa na Tanganyika na wakadai Uhuru wao, haina maana Zanzibar haikuwa nchi na huru ndani ya Tanzania. Tunachozungumzia hapa ni founding father of their nation. Mwisho wa maneno yako unazungumza kwa hisia za kidini zaidi kama Mohamed Said, yaani ni lugha inayofanana na - kama Zanzibaar (waislaam) wakija jitenga na watadai nchi mpya watasema walipata Uhuru wao kutoka bara (wakristu).
Hapa sielewi unachosema. Zanzibar watadaije uhuru kama wako huru tayari? Sijawahi kusema Zanzibar ni ya waislamu na bara ya wakristu. Sasa kama unataka kutuambia kuwa usongo wa Zanzibar kwa Bara ni wa kidini kuliko kihistoria na kisiasa hiyo ni ishu nyingine. Huo si mtazamo wangu.

PHP:
Najua unashindwa kusema matukio mengi ya Ulaya yalikuwa mapinduzi dhidi  ya wao kwa wao kutokana na tofauti za imani ya kidini au kumuondoa  mkoloni ambaye alikuwa dini sawa na wao lakini dhalimu. Kuna sehemu  nimekwambia kwamba Demokrasia tunayoiona Ulaya ni itikadi zinazopingana  na mila zile za kidini zilizokuwepo na nimesema wazi kwamba demokrasia  iliytopo Uingereza ni hatua nyingine ktk upinzani wa itikadi na mfumo  ulokuwepo..
 
Hao Ireland wakipingana na Muingereza kidini lakini ni serikali huoni  picha nayojarigbu kuijenga hapa mkuu wangu kwamba they are all  Christians..Acha political matters pembeni. Nakuomba tena rudia kusoma  historia ya nchi za Ulaya utaona jinsi dini ilivyoweza kuchukua nafasi  kubwa ya identity yao kuliko sisi tunaojitambulisha kwa makabila.
Nashindwaje kusema wakati nimekupa mifano halisi ya nchi wakati wewe umeishia ku-generalise. Toa mfano wa nchi izinazothibitisha hypothesis yako ndiyo nitakuelewa.
Kwa kuweka mbele dini juu ya politics ndio unarudia makosa ya Mohamed Said. Kama yeye, unashindwa kuwaona wa-Irish kama nationalists waliokuwa wakipigania uhuru wao kutoka kwa waingereza bali wakatoliki waliokataa kuwa chini ya waprotestanti. Hii ni sawa na Mohamed Said anayedai kuwa wakina Sykes na waislamu wenzao walipigana kutetea uislamu dhidi ya ukristu wa mkoloni badala ya wazalendo waliokuwa wakipigana na udhalimu wa mkoloni.
Hauwezi kusema ati kwa sababu dini ni sehemu kubwa ya maisha yao ndiyo ilikuwa paramount juu ya uzalendo wao.

Of course katika mapambano na udhalimu, mtu unatumia kila silaha uliyokuwa nayo, dini ikiwemo. Ukijua wengi wenu ni waislamu basi utawahamisisha kwenye misikiti na utajitahidi kuwavuta mashehe na ma-imam. kuwa upande wako. Na kama wengi ni wakristu, utatumia kanisa na mapadri kuwahamasisha wananchi wako. Kama kwetu kwenye makabila, basi utatumia machifu na wazee katika jamii kuwahamasisha wananchi. Lakini pote lengo kuu ni utaifa na si udini au ukabila. Wale wachache wa dini au kabila nyingine nao wanakubalika katika mapambano hayo bila kubaguliwa. Si wazalendo wote wa Ireland walikuwa wakatoliki. Walikuwepo waprotestanti wachache na wasio na dini. Lakini kwa vile wengi wa raia wa Ireland ni wakatoliki hawa walikuwa wengi.

Mwanafalsafa anapopinga utawala wa monarchy na kujiita huru kisiasa kama walivyotangaza Canada walivyotangaza. Again hata sisi ipo siku tutakuja fikia demokrasia ya kweli na ni hatua mbele baada ya kuwa huru..ukiniuliza huru kutoka kwa nani ina maana hufuatilii historia ya nchi ila kwa haya unayoyaona leo.
Hapa unataka kusema nini haswa?

Kifupi nachoweza kukuambia na ukanielewa vizuri pengine nitumie mfano wa Yesu...ni kwamba Jesus was a Jews na yeye ndiye aliyekuja pingana na Wayahudi hivyo haiwezi kuondoa haki yake ya Uzawa kama alikuwa Myahudi kwa sababu tu alikuja na imani mpya inayopingana na baadhi ya ibada za wayahudi..Huyo mtawala mwenyewe Pilato mroma alikuwa mhmyahudi A jew by faith)..Na hata kama isingekuwa dini kama Yesu angepingana na Utawala wa Pialato kisiasa isingeondoa imani yao kuwa tofauti kidini kwa sababu mmoja ni Myahudi kwa uzawa (ban Israel) na mwingine ni Mroma kwa uzawa.
Hapa tena haujui unachokisema. Yesu alikuwa myahudi na wakati wa uhai wake hakupingana na imani yake. Yeye alipinga matendo na tafsiri za viongozi wa dini yake waliokuwepo wakati ule. Kila wakati alitumia maandiko ya waliomtangulia kujenga hoja ya aliyoyahubiri.

Pilato alikuwa mrumi aliyepelekwa Judae kuwa Prefect ( Governor). Alikuwa ni mwakilishi wa utawala wa warumi. Hawa hata siku moja hawajawahi kuwa wayahudi. Yeye na Yesu walikuwa na imani tofauti na uzawa tofauti. Ndiyo maana aliwaambia wayahudi wakamhukumu kwa sheria zao maana yeye hakumuona na hatia. Na wayahudi walimbana kwa kusema watamchongea kwa bosi wake ( Kaisari) kama atakataa kumhukumu mtu aliyejifanya mkubwa kuliko Kaisari. Soma historia yako, Mkuu.

Na kuhusu Uingereza, mkuu wangu hawakuwa Wapagan, hawa walitawaliwa na Waroma ambao walikuwa Christians (Claudian invasion). Kwa hiyo wenyewe wanasema walikuwa Romanised, na kumbuka tu kwamba mtawala wao Constantine 2nd alikuwa mtoto wa yule Mkatoliki Constatine the great na kama sikosei ndiye aliye declare the All Roman Empire should henceforth be Christian.
Waingereza waasili kama walivyokuwa wakazi wengi wa ulaya walikuwa wapagani. Stonehenge haikujengwa na wakristu. Vikings waliabudu miungu wengi tu n.k. Julius Caesar wakati anavamia uingereza (na mpaka anakufa) alikuwa mpagani.

Tiberius Claudus Caesar Augustus Germanicus alitawala Rome kati ya 41-54. A.D. ( kwa sisi tuliosoma zamani). Alimtuma Aulus Plautisus kuvamia uingereza mwaka 43. Uingereza ya wakati ule ilikuwa na makabila mengi yaliyokuwa yanapigana yenyewe kwa yenyewe. Kabila lililopigana na warumi lilikuwa Catuvellaum likiogozwa na mfalme wao Caratacus na ndugu yake Togomas. Hawa walishindwa. Hiyo ndiyo Claudius invasion unayozungumzia. Warumi wa wakati ule walikuwa bado ni wapagani hasa ukizingatia uvamizi huu ulitokea miaka michache baada ya Yesu kusulubiwa. Hata Mtume Paul alikuwa bado hajamtambua Yesu ( hapa nilikosea. Paul alimtambua Yesu kati ya 33-36. Lakini ilikuwa ni miaka 17 kabla ya Paul kuupeleka ukristu Rome).

Caesar Flavius Valarius Aurelius Constantinus Augustus, aliyetawala warumi kati ya 306-337 alikuwa ndiye mtawala wa kwanza wa kirumi kuwakumbatia wakristu. Kabla ya hapo wakristu walikuwa wanawashwa moto kumulika barabara za Rome.
Baba yake hakuwa huyo unayedai bali Favius Constius ambae alikuwa gavana na jenerali katika jeshi la warumi. Ingawa kabla ya kuwa mtawala mkuu wa himaya ya warumi, Constantine alitawala uingereza, gaul na hispania( baada ya baba yake kufariki) alifanya hivi kabla hajabatizwa na kuingia ukristu. Lakini hata wakati huo aliwavumilia sana wakristu ambao waliishaanza kujitokeza katika sehemu aliyokuwa akitawala.

Utadaije mtu aliyetawala miaka zaidi ya mia mbili kabla alikuwa mkristu?

Huyo Arthur mwenyewe, mama yake alikuwa a descended kutoka ktk line ya Priestesses of Avalon hata dada yake mwenyewe Morgaine alikuwa Priestess of Avalon kwa hiyo sii suala la kubishana hali ushahidi unaonyesha wazi kwamba unaweza rudi nyuma hadi karne ya 50 Ukristu ulikuwepo tayari kama ulivyo Uislaam ktk nchi za Kiarabu..Mkuu wangu yaani hiyo Europe ndio usiseme kabisa ukielewa kwamba dini hii ilitumika sana ktk vita vya ku conquer Ulaya na kusambaza utamaduni huu - a way of life na uzima wa milele..
King Arthur alitawala miaka karibu mia tano baada ya Claudian invasion. Anahusika vipi na ukristu uingereza? Usichangenye myths ( wakina Merlin, panga lake Excalibur n.k.) na historia. Yeye kama Robin Hood haijulikani hasa facts ni nini na myths ni zipi.

King Arthur alikuwa ameisha kufa wakati Mtume Mohamed anahubiri uislamu.

halafu tukirudi ktk swwala la culture, mkuu unazidi kupotea na ufahamu wako. Ukristu sio kuwa na Padre au Askofu ila ni Imani ya kiroho inayomkubali Yesu kama ndiye mwokozi wako. Mnaweza tofautiana ktk hadithi na sunna lakini bado tamaduni zenu zina root moja. Haya maswala ya kusema nikutajie nchi hata moja ya Kikristu hali unajua fika kwamba chimbuko lao ni ukristu, sijui unataka niseme nini zaidi. haya umekuja na ya taliban tena wakati hujui maana ya Taliban..
Mimi nimekuambia nitajie nchi moja ya ulaya ambayo kikatiba ni ya kikristu. Au unataka kutuambia kuwa kwa sababu wakristu ni majority katika nchi nyingi za ulaya basi nchi hizo ni za kikristu? Utaweza kweli kuzifananisha na Iran na Saudi Arabia? Ukristu kama tamaduni hauhusiani na kumkubali Yesu kiroho n.k. Ingekuwa hivyo basi makanisa ulaya yangekuwa yanajaa. Hivyo hivyo utawala kuongozwa na Judaeo-Christian principles hakuna maana kuwa nchi hiyo ni ya kikristu. Kwa mfano, India mfumo wa utawala wake uko based kwenye hizo principles. Ndiyo maana ingawa wengi wao sana ni wahindu lakini hakuna ubaguzi wa kikatiba dhidi ya dini nyingine.

Utaniambiaje sijui kuhusu Taliban wakati mtandao upo? Tunaishi enzi ambako ignorance ni chaguo. Au utasema mtandao nao ni wa wakristu?
Mimi nimekueleza ninayoyaua kuhusu taliban na wenzao. Itakuwa vyema ukieleza wapi nimekosea badala ya kusema tu kuwa siwajui Taliban! Wewe unawajua? Kwani wewe ni m-afghanistan? Au kwa vile tu ni muislamu mwenzao basi unawajua zaidi kwa symbiosis?

Hivi mkuu umewahi kuuliza Wahabbi ni kina nani hata ukawachukulia kwamba hao ndio Waislaam pasipo kufahamu undani wao. Sasa leo hii mimi maadam siwezi kuhukumiwa na huyo Taliban basi mimi sio Muislaam? Huyo taliba au Mulla anayehukumu ni msomi wa shera za dini na shehebu lao hivyo ana qualify kwa mizani yao na sio yako wewe.. Mbona huyo Papa na vatican wameshindwa kuwahukumu walio wala witi watoto ndio niseme ni huo ni Ukristu gani au lawama zangu zinatakiwa kuelekezwa kwa Papa kama zipo.. Acha zako mkuu wangu acha maswla ya dini wewe bakia na imani yako usitake kuhukumu wengine hali kwako ni mtoto mtupu.
Unajichanganya tena. Tunapozungumzia waTaliban tunazungumzia wale watawala wa Afghanistan waliotumia jina hilo. Taliban sio dhehebu la uislamu. Sasa utahukumiwaje na Taliban kama wewe hauishi Afghanistan? sana sana wanaweza kutoa fatwa dhidi yako lakini wote tunajua yaliyompata Rushdie.

Ingawa Papa amepata kigugumizi kuwachukulia hatua hao mapadri wake, wahusika wamewapeleka mahakamani ambako wengine wamefungwa na sehemu nyingine parokia kupigwa faini nzito. Sasa ingekuwa utawala ni wakikristu, wangewezaje kwenda kinyume na kiongozi wao? Au unataka kuniambia kuwa waliowahukumu hao mapadri na hizo parokia walikuwa waislamu?

Sina haja ya wala ubavu wa kuhukumu uislamu, uhindu, rasta, mabuddha, bahai, atheists n.k. Lakini pale amabpo mtu anakosea ntamsema bila kujali dini yake hata kama ni mkristu mwenzangu. Wewe unataka kuwa popo, kulaumu waislamu wenzako lakini vile vile kutumia uislamu kuzuia wengine ambao si waislamu kuwalaumu wenzako. Hiyo si sawa hata kidogo.

Haya umerudi tena na kusema ati Marekani bunge lao lina Waislaam wakati huo huo unatakataa kwamba Marekani sio nchi za kikristu.. sasa sielwi nini malengo ya swali lako. Ni wewe unayepinga kupatikana kwa mataifa ya Ulaya chini ya Ukritu lakini mwepesi kuutumia Ukristu ku define make of their Government ambayo umekataa haina mahusiano na Ukristu. Hata sikuelewi mkuu wangu,sema moja tujue unazungumza kipi.
Nchi za Kiislaam zinaitwa nchi za kiislaam wala hazijifichi, hivyo kwa kila wanachofanya inaeleweka bila kujificha nyuma ya pazia. Sheria zao ni wazi na unapoingia kwao (Rome) unaua utafanya kama Waroma. Sii hawa Wamarekani wanaolaani watu wengine wakiua lakini wao wepesi kudai casualties of war hali wamebeba silaha kubwa za kuua.. wananyonga watu au kupiga sindano za kuua lakini asihukumiwe mtu mwingine nchi za waislaam. Na the fact is Marekani wananyonga watu wengi kuliko jumla ya nchi zote za kiislaam kwa mwaka.

Hilo swali la mwisho unarudi kuel kule nilikoanzia huko juu. Labda nitasema kwa ufupi to kwamba walitawaliwa na ROMANS.....
Hauwezi kweli kuelewa logic ya kusema kuwa "hauwezi kuliita bunge la marekani la kikristu wakati ndani yake kuna watu ambao si wakristu au ambao matendo yao hayaendani na imani hiyo?" Wewe umedai utawala wa marekani ni wa kikristu, nikakuambia la hasha, mbona ndani kuna muislamu ( Keith Ellison) mwenye imani ya kiyahudi ( Joseph Lieberman) na wengine. Sasa wewe nitajie mjumbe mmoja katika bunge la Iran au Pakistan ambaye sio muislamu? Au mtu aliye katika utawala wa Saudi Arabia ambaye si muislamu? Au unataka kuniambia katika nchi hizo ( Iran na Pakistan) hakuna watu wenye imani tofauti?

Huko huko marekani si majimbo yote yenye hukumu ya kifo. Ingekuwa kweli kunyonga ni sehemu ya itikadi ya ukristu basi nchi zote unazodai kuwa ni za kikristu wangenyonga. Pope anapinga hukumu ya kifo lakini hana uwezo wa kuikataza marekani kunyonga. Kwamba serikali ya marekani imefanya maovu hamna anayekataa hayo. Lakini hii inahusiana vipi na ukristu? Tatizo la nchi kama Iran na Saudia kujiita ni za kiislamu na kusema katiba yao ni Quran, zinafanya basi matendo yote yanayofanywa na nchi hizo kuonekana kama ni interpretation ya uislamu. Iran wanapompiga mwanamke mawe hadi kufa kwa sababu wanamshutumu kuwa amezini, inatueleza kuwa hicho ndicho uislamu inachoongoza. Sasa watu wakiona hivyo na kuchelea chochote kinachohusiana na Sharia utawalaumu? Si wengi ambao tungekubali mabinti zetu wapigwe mawe hadi kufa kwa sababu tu wamefumaniwa. Hiyo ndio tofauti yetu.

Hiyo sentensi yako ya mwisho inajibu swali gani? Mbona sikuelewi.

Ushauri wa bure. Kabla ya kubandika vitu vya historia fanya "fact check". Ndiyo faida ya mtandao.

Amandla.....
.

Mkuu ungejieleza tu kwa kiswahili fasihi unachokielewa.

Natangulia kukusahihisha kiingereza (in red) ulichokiboronga ili upate kueleweka.

Pili, ubaguzi na hisia zilizoibuliwa na mada hii ndio inayopelekea kuwa na mjadala huu.Kwa bahati mbaya mada inajaribu kulaumu upande mmoja kuwa ndio ulikuwa unapendelewa kwa sababu za makusudi kabisa.Sasa ni juu yako Domo kaya kupitia mada zote na kuelewa msimao wangu juu ya mada nzima.

Ubaguzi ni ubaguzi tu uwe wa dini ukabila au vinginevyo.

Sasa mada inahama kutoka kwenye Uisslamu/Ukristo, Uarabu/Uzungu na kuingia katika ukabila.

There is no fine line here, ndio maana nasema inahitaji common sense zaidi kuliko maneno matupu kupata common ground kwa mada iliyopo.

Huwezi kuibua tuhuma nzito na ukafikiri yatajadiliwa yale unayopenda wewe tu.There are some carried over feelings that affect the whole society.

Ukiutetea uislamu basi makundi mengine yanajitazama yanasimamia wapi kutokana na tuhuma zako.

Nashukuru kwa kunirekebisha Kingereza asante sana na nakuomba pia hata ninapokosea kiswahili naomba unikosoe tu kiingereza tu na pia nashukuru kwa wewe kukubali kuwa umeweza kuwa carried na feelings na hata umeweza kusema haya uliyoyasema. Wengi wanajua mtu anapokuwa carried na feelings uwezo wake wa kufikiri unakuwaje. Asante sana kwa kuwajulisha wana JF mawazo yako hapa yanapatikanaje
 
Usijali sana mkuu, ni feelings na sentiments hizo hizo unazokuwa nazo na wewe unapoteteta uislamu!
And for good measure, for every action there is an equal and opposite reaction.
 
Mageuzi1998 na JokaKuu,

Unfortunately hatuwezi kukwepa maana mada nzima iko steeped kwenye historia na udini! Distortions of both zimejaa na ni lazima niziseme. Kwa kukataa kuzi-debate ndio hizo distortions zinageuzwa kuwa "facts". Kwa baadhi yetu, hii hatuwezi kuiruhusu. Na ndio maana ninamjibu Mkandara hivi:
Tunaishi enzi ambako ignorance ni chaguo. Au utasema mtandao nao ni wa wakristu?Ushauri wa bure. Kabla ya kubandika vitu vya historia fanya "fact check". Ndiyo faida ya mtandao.

Amandla.....[/SIZE][/FONT].

Nakuvulia kofia Mkuu FM kwa posts zako zilizoenda shule na logic iliyomo ndani yake.Bahati mbaya ni kuwa kuna wenzetu wengi wanaosoma lakini hawaelimiki!
 
Suala hili limefanyiwa research na wanazuoni wazuri tu katika nchi yetu, hebu jamani tuitafute hiyo research ambayo kitabu chake kimepewa jina la Religion and Politics in Tanzania. Maprofesa na Madaktari wa falsafa wenye kuheshimika sana nchi hii zaidi ya ishirini waliliona hili na wakalifanyia kzi na kutoa mapendekezo yao. Basi angalau tuanzie hapo, tutafute hayo maandiko tuyasome, mwenye mawazo tofauti ayasema na pengine kuyawakilsha kwao Nimabahatika toka majuzi kupitia maandiko hayo na najihisi kulielewa hili suala zaidi kuliko ilivyokuwa awali na kitu kizuri pengine hata kitabu cha Mohamed Saedy kimepitiwa katika literature review na reference. Sijui kinapopatikana kitabu hicho lakini kwa kuwa kimechapishwa na mchapishaji wa hapa Tanzania, E&D Vision Publishers waliopo pale Africa sana nyuma ya kona Bar (club Ambiance) naamini wanaweza kutoa maelekezo ya kufaa katika upatikanaji wa kitabu hicho.

Naamini hii itapunguza bias na prujudice tulizo nazo, sometimes watu wanakuwa taken na hizo feelings zao kiasi wanakuwa vipofu wa kuuona ukweli. Ukweli kwa kawaida ni mgumu hsa ukiwa unakugusa lakini ukweli unakuwa mgumu sana ikiwa unagusa kitu ambacho mtu una kiamini na umekuwa ukikiamini toka utoto wako, its some sort of addiction, kwa hiyo inahitaji professional rahabilitation kwa mtu kurudi kuwa normal. Kuna wengine ambao hawako addicted kihivyo angalau hao mind zao hazipo closed na wapo ready kupokea mapya tofauti na sisi wengine ambazo tulishazifunga. Angalau kupitia kitabu hicho somepart of my mind imekuwa tayari kupokea mapya na kukubali palipokuwa na makosa na pia kuona wengine walipokosea na ndio maana nimeona angalau niwashirikishe wana JF wengine wapate dawa ambayo mim i kwa kiasi fulani imeweza kunisaidia. Its nof fair kupinga kila wazo linalotolewa na unayemhisi wa upande mwingine kwa vile tu unafikiri na yeye amekuwa carried na emotion kama wewe. Tuipate hii research, tusome tuje tujadili findings zake, tuaanzia hapo
 
Kwanza kabisa.......mtoa mada Dk Mohamed Said,yeye ni mmanyema kama alivyo sema,na akaeleza kuwa wamanyema wana sifa kuu tatu
1.Maringo yaani kujisikia au kunata
2.Wanapenda ushari,mabishano
3. Hakuna mmanyema Mkristu kabisaaaaa na anamshuruku mungu katika hilo

Ina maana kwa yeye mtu kuwa mkristu ni kero…najisi sio…!(ndio maana anafura kwa kabila lake kutokuwa na wakristu)…..Sasa kwanini isionekane kuwa presentation yake ni chuki dhidi ya wakristu….!
 
Ana maringo ya bure mkuu na nafikiri asihusishe maringo yake na kabila lake!!
Stara Thomas ambaye namfahamu fika ni Mkristo,mcheshi, humble na muimbaji mzuri sana.
Hili kabila tumeoleana hivyo tunalifahamu.
Matatizo yake Mohammed Said asipakazie kabila lake.
 
Kweli debe tupu haliachi kulia. FM ni acronym ya Fundi Mchundo sasa kwa nini nikatae kuitwa FM? "Amandla" ( Power) ni kiibwagizo cha kusalimiana kilichokuwa kikitumika na wapiganaji wa African National Congress ya Afrika Kusini. Kiitikio kilikuwa "awethu" au "ngawethu", wakimaanisha "To us". Kilio hiki sasa kinatumika na baadhi ya wanaharakati katika vita dhidi ya ugandamizaji ( oppression).

Kumbe umekuwa ukinifuatilia tangu 2008? Kwa nini basi haukujiunga wakati ule ili uchangie katika mjadala. Mimi niliondoka katika Jukwaa la dini kwa sababu paliacha kuwa sehemu ya kuelimishana pakageuzwa na hao wakina Zomba kuwa sehemu ya kuonyeshana nani anayeweza kuitusi zaidi dini ya mwenziwe. Sababu nyingine ni kuwa niliamini kuwa pana haja ya kupanua wigo wa kujadiliana kuhusu biashara ya utumwa. Kubakiza mjadala kwenye jukwa la Dini kuligeuza mjadal kuwa kati ya ukristu na uislamu, kitu ambacho hakikuwa sahihi. Huyo Zomba, kweli alinifuata huko nilikouamishia tukaendelea aikuwa la mwisho na lilisema nini! Huyo Zomba, ambae naona ulikuwa unamuabudu, mwenyewe unakiri kuwa ametokomea. Kilichomfukuza bila shaka ni kufungiwa kwa jukwaa la dini ambako alilitumia kusambaza sumu yake ya udini na chuki dhidi ya watu wengine. Hakuwa na uwezo wa kujadili mambo mengine ambayo hayahusu dini. Sishangai kuwa ulikuwa mshabiki wake. Huyo Fundi Mchundo unayedai alichanganyikiwa bado yupo anapeta ndani ya hii Forum yetu. Wewe unanishangaa kuwa nimeweza kutetea waislamu? Nimetetea mashoga, nimemtetea Rostam Aziz na wengine bila kujali wengi wamesimamia wapi! Wewe umechangia nini katika Jukwaa hili nje ya kushabikia uovu na chuki dhidi ya wenzako? Watu kama nyinyi ni vidonda katika uso wa huu ulimwengu wetu.

Kumbe Muhammed alitishika na Fundi mchundo? Mbona alidai anajitoa kwa sababu ye ni muungwana na biashara ya kuvunjiana heshima hawezi. Kumbe aliniogopa! kweli mtu ukiwa na rafiki kama wewe, hauhitaji adui.

Naona kujibishana nawe hakutasaidia kitu maana haujajaaliwa uwezo wa kuchambua unachokisoma au kusomewa! kwa sababu hiyo nitafuata ushauri niliompa Jasusi na kujitoa katika kulumbana na wewe.

Amandla.........
Kwani umefahamu vipi huo ushauri unaopeana na Jasusi?.Huoni kwamba hiyo ni namna tu ya kukuokoa kutokana na mashambulizi ili usizidi kugaragara hapa jukwaani.
Wewe unachangia sana na kwa mkazo mkubwa,lakini kwa kweli kama Mkandara alivyokwambia unachanganya sana mambo mpaka inatoa ladha ya kusoma mchango wako.
Tukirudi kwenye mada.Jee una kitabu chochote kilichoandikwa kutokana na utafiti kumtetea Nyerere kwa zile fadhila zake za punda kwa waislamu?,na jee unapinga kwamba Nyerere hapaswi kupewa hadhi ya kuwa muasisi wa TANU pekee na kuwasahau waliomkaribisha yeye kwenye siasa?.
Na jee Fundi una mpango wa kupindua maneno na kuandika historia yako ya kubuni au utakubaliana na utafiti wa Mohammed Said?.
 
Mimi nilidhani tuko hapa kujadiliana na kuelimishana kumbe tuko hapa kushambuliana na kugaragazana? Aah, kumbe ndiyo maana umeniita mtu wa serikali, il hali hata hunijui ninafanya kazi gani na wapi?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom