Hapa, Mkuu, unaanza kuchemsha.
Hivi kweli unatumia mambo yaliyofanyika zamani kuhalalisha ya sasa? Ni nchi gani ya magharibi inayojiita kikatiba ya kikristu? Kutokana na yale waliyojifunza awali, nchi hizi msisitizo wao mkubwa ni kutenganisha dini na utawala. Ingawa wengi wanaoongoza ni waumini wa ukristu lakini kanisa halina sehemu kikatiba katika uongozi wa nchi. Hata Uingereza ambako malkia ni kiongozi wa dini hana nguvu juu ya waziri mkuu! Kutokana na maovu ambayo watu wa magharibi waliona yalitendeka wakati dini iliposhirikishwa kwenye utawala imekuwa mwiko kwao kuunganisha vitu hivyo. Busara ya kutenganishwa huko tunaiona hivi sasa katika nchi zinazodai zinazoongozwa na dini. Wote tuliona yaliyotokea Afghanistan wakati wa Taliban. Na hii ndiyo inayochangia kwa namna moja hata wengi wa wa waislamu wasomi wanaohama kwao kukimbilia nchi za magharibi na sio Saudia, Sudan au Iran. Wakienda kwenye nchi za kiislamu wanakimbilia zile ambako utawala hauruhusu dini kutawala kila nyanja. Wanajazana Dubai, Oman n.k. ambako mtu hakatwi mkono akiiba! Au kupigwa mawe kutokana na uasherati.
Hivi kweli unaamini kuwa OIC ndiyo panacea ya matatizo ya waislamu? Si itakuwa yale yale ya kutegemea mtu kutoka nje akukwamue katika matatizo yako? Linakuwaje tusi pale mtu anapoambiwa aangalie uwezo wake kabla ya kungojea fadhila kutoka kwa wengine?
Wapi watu wamepinga kuanzishwa benki ya kiislamu? Ninavyojua mimi watu ( kwa makosa) walipinga benki moja (Stanbic) kuwa na kitengo kitakofuata maagizo ya sharia katika kutoa huduma zake. Ninavyojua mimi viongozi wengi katika hiyo benki ni wakristu , sasa utasemaje kuwa wakristu hawataki benki ya kiislamu? Halafu Benki ipi ni ya wakristu? Kama ni kwa sababu waliozianzisha au/na wanaoziendesha ni wakristu basi vile vile utatuambia kuwa unga na lambalamba za Azam ni za kiislamu! Au iliyokuwa Greenland Bank. Au Meridien Bao. Hizi nazo zilikuwa za kiislamu kwa sababu wamiliki wake walikuwa waislamu? Hivi nchi ambayo rais wake ni muislamu, waziri wake wa fedha muislamu, gavana wake wa benki kuu ni muislamu, katika nchi ambayo karibu nusu wa raia wake ni waislamu, kweli itazuiwa na mkristu wa mtaani kuanzisha au kuruhusu benki ya kiislamu kama waliona kuna tija? Hapa si unarudia kosa lile lile la wakina Mohamed Said la kuona mkono wa mkristu hata kwenye yale ambayo yamewashinda wenyewe?
New York kinachopingwa na wengi si kujengwa kwa msikiti bali mahali panapotakiwa kujengwa hicho unachokiita kuwa ni msikiti wakati ni community centre yenye sehemu ya maombi. Vile vile hao sauti kubwa zinazotetea ujenzi wa msikiti huo zinatoka kwa wakristu, wakisema kuwa mbona kwenye eneo hilo tayari kuna misikiti miwili? Rome kwa hao wakatoliki penyewe pana msikiti, tena mkubwa sana. Sasa wewe nitolee mfano wa kanisa au kasehemu ka kuabudia wakristu lililopo Riyadh, Jeddah, Tehran au Sanaa? Huko unakolaumu, waislamu wametengewa sehemu ya kuabudu katika Pentagon, ambalo baadhi ya waumini wa kiislamu walijaribu kulilipua? Hii inawezekana kweli kutokea huko mashariki ya kati?
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
Amandla...
Mkuu wangu soma hoja ya mtu kwa kuelewa anachohoji yeye kisha jibu kulingana na... Mimi nimeweka bandiko langu kwa kumjibu Pasco ambaye kama umemsoma vizuri utagundua kwamba majibu yangu yoote yametokana na hoja yake na zaidi ni kumfahamisha chimbuko la kuingia dini Tanzania na tofauti ya tawala baina ya Mzungu na mwarabu.
Hakuna mtu anayezungumzia Utawala wa Uingereza leo hii uko vipi, na hata huyo Mohamed Said anapohoji kukandamizwa kwa Waislaam, hazungumzii leo isipokuwa wakati wa Nyerere na ndio maana sisi tunapinga kuwa udhalimu huo haukuwepo zaidi ya waislaam kuwezeshwa. Kuhusu Ulaya na hasa hiyo Uingereza nakuhakikishia mkuu wangu nenda kasome hiistoria utakuta karibu nchi zote zoteza Ulaya zimepatikana Uhuru wao kwa kupitia dini ya kikristu na ndio maana ktk kila nchi hizi bado wana Wafalme na wanaheshimika.. .
Kisha basi ni lazima ufahamu kwamba dini ndio Culture ya wazungu hivyo sii kweli ati wazungu wanatenganisha dini na Utawala hali utamaduni wao umetokana na dini..Kinachofanyika leo ni kupingana na baadhi ya culture hizo za kidini na hakika nakuhakikishia kama wewe sii muumini wa dini zao (ukristu) huwezi kutawala nchi zao lakini unaweza kuwa kizazi kilichohamia hapo na ukatawala..Foundation ya uhuru wao ni dini hilo kataa uanvyopenda lakini ukweli utabakia palepale.
Mabadliko ya Uingereza kuingia demokrasia ni hatua nyingine baada ya nchi kupata Uhuru wake lakini ktk fungu la kidini.. Na ka sikosei wao walijitenga na Ukatoliki kwa sababu King Henry alimpa talaka mkewe kinyume cha sheria za kidini hivyo yeye akachukua jukumu la la kuwa head of the church of England na kutoka Ukatoliki ( sina hakika na jina la King mwenyewe).
Marekani hadi kesho wanasema wao wenyewe kwamba nchi yao imepoatikana kutokana na dini ya Kikristu na hawa wametawaliwa vile vile..Na nenda hadi kule Romania ambako kwa yule mtu wa kutisha Dracula, historia yake alikuwa pia kiongozi wa dini na mfalme lakini nao wakaja kuwa Wakomunist baadaye.
Na unapozungumzia Rome kumbuka tu kwamba nchi hiyo ilitawaliwa na Waislaam na hadi leo ndio Rome ina msikiti mmoja. Sasa sijui kama umefuatilia kwa nini miaka yoote ile haukujengwa msikiti hadi majuzi tu. Na kisha yaonyesha wewe unasikiliza saana CNN pasipo kupima. Yanayotokea Saudia na Vatican hayahusiani na fikra zako wewe kwani wakati wa mtume kulikuwa na makanisa Saudia kwa taarifa yako..
Sasa kwani msikiti ukijengwa barabara mbili toka 9/11? ndio ina maanisha kitu gani kama sii kusema hawaamini Waislaam. Those guyz wa 9/11 were Arabs, tena WaSaudia ambao wameyafanya waliyoyafanya kwa sababu they want America out of Saudia.
Msikiti ni wa Waislaam sawa na Sinagogi iliyopo mitaa hiyo hiyo ya 9/11, iweje wao (jews) iwe sawa lakini sio kwa Waislaam kama sii kuwabagua...Labda nikukuguse wewe, Ati Waafrika tutake kujenga jengo la jumuiya yetu tukatazwe kujenga sehemu kwa sababu WaSomalia walihujumu Wamarekani lakini Wachina, waarabu na Wahindi na watu wengine woote wanaruhusiwa kujenga majenog ya jumuiya zao.. Ooh nilitaka kusahau kama unataka kuona makanisa google utayaona mengi moja wapo ni Zanzibar na Mombasa ambako kulikuwa na Waislaam kwa asilimia 99 bado kuna makanisa. Wee google utayaona makanisa tena toka enzi na enzi yamesimama..
Na sijui kwa nini nakuelezea haya yote kwa sababu naamini kabisa mtu yeyote anayesukumwa na imani ya dini haweziu kuona haki hii isipokuwa yake mwenyewe.. Na ndio maana ya usemi wangu koote kule nilikotoka. You proved my point kwamba ni vigumu kwa mkristu kuona haki ya wengine pale yeye haoni haki isipokuwa yake yeye mwenyewe. Sijui kama umenielewa kifungu hiki?
Hakuna sehemu yoyote inayosema Taliban represent Islam isipokuwa ni binadamu wanaotaka ku preserve culture na dini yao ktk kuendesha maisha yao. Who the f.... sisi kuwaamulia wao maisha yao hata kama sisi hatuyapendi? hao hao Taliban waliondoa kabisa biashara ya Opium na moja ya chuki kubwa ya hawa watu ni kuondoa Bwimbwi ambalo linazitajirisha nchi za Ulaya kwa gharama ya maisha ya wananchi wao wenyewe.. Wakati Taliban yupo madarakani Bwibwi lilikuwa na bei kuliko Cocaine kwa sababu halikupatikana ( demand kubwa supply ndogo)leo wanalaumiwa ati kwa kulima madawa ya kulevya.. 90% ya Opium farms na production inatoka sehemu ambazo NATO wamezishika iweje taliban ndio walaumiwe hali American na majeshi ya NATO wanaweza kuweka vikwazo!
In your mind, hivi kweli unafikiri Marekani cares abaout hao wanawake wanaoonewa ati kwa kucharazwa bakora wasipovaa hijab? Mbona Saudia pia wanacharaza bakora na hatujasikia waki plan kuwaokoa wanawake wa huko. Na hiyo Afghanstan yenyewe ndio maskini kuliko hata haiti toka wamesaidiwa Na marekani kuwaondoa Urusi hawajapiga hatua hata moja under Taliba au baada.
Mkuu sasa unabisha kupingwa kwa benki ya kiislaam na wakristu?...yaani unakataa katu kwa kuelewa au....Na leo OIC ndio unajua umuhimu wa kutowategemea wageni lakini wanapoleta toka huko uzunguni kuja kwenu hakuna fikra hizo ila wepesi kusema Nanyi (waislaam) fanyeni kama sisi hamjakatazwa!..duh! basi mkuu wangu nadhani hatutaweza kuelewana hata kidogo..
All this shit about Taliban ni ujinga mtupu ambao mimi Mkandara will never buy it for a pennie.. Walioripua 9/11 ni Wasaudia (kama sii Wayahudi wenyewe) ambao maisha yao hawajawahi kuishi Afghan tan ila ikasemekana Osama na Al Queda huko ndiko kwenye makao yao makuu yao. Osama ambaye ni Msaudia na hakuwahi kuishi Afghanstan alipelekwa Afghanstan na Marekani wenyewe kuwawezesha wao kupenya ndani Taliban kumsinda Mrusi, leo iweje Marekani waishambulie Afghanstan hali kila kitu kilichotokea 9/11 hakihusiani kabisa na WaAfghanstan maskini ambao hata kula yao wenyewe ni shida!..Oooh mara Osama alionekana Torabora mara sijui katuma ujumbe mpya yaani wao ndio wanapata ujumbe kwa kila Osama analotaka kufanya hali wanadai hawajui aliko ila huwa wanaletewa tapes tu.. how can we be that stupid!
Marekani alitaka kuingia Afghanstan kuwaondoa Taliban na sio kwa sababu ya dini au matendo yao isipokuwa kuwawezesha kujenga bomba la Mafuta na gas toka Kuzestan hadi bahari ya Hindi. Niliyasema kama haya wakati wa Saadam kwamba hakuna WMD tena hapa hapa JF watu hamkuamini mkaniita mwongo na kadhalika. Kwa hiyo mkuu wangu nawe usichanganye dini na politics. Huku ndiko kuchanganya kwani Marekani wanaposhambulia nchi nyingine hutoa sababu za kidini.. wao wakienda vitani wanasema Lord Jesus awalinde lakini Muislaam akisema Allah Akbar basi huyo ni terrorist. Come on..