Mohamed Said Salum Popo "Sidney" mwana wa Saigon. Nimechelewa kwenye huu mnakasha na nimejipa wiki 2 za muda wangu wa ziada kusoma posts zote. Imethibitika kwa ukweli usio na shaka Sidney you are bigger fish in the small pond. Kwa mimi ninae kufahamu binafsi sishangai kwa nini pamoja weledi wako wa kujenga hoja na vithibitisho vya tafiti za kisayansi unapata majibu ya kejeli, kashfa, dharau na matusi ( wakati mwingine ya nguoni) Huyu ndio Mohamed Said nimjuae anaweza ku interact na watu aina zote kutoka kijiweni kwake pale saigon mpaka katika majukwaa ya kimataifa. Kwake Sidney kuisimulia historia hii ni namna ya kuwa rehemu wazee wake, naam ni jambo la fakhari kuona kwa mtoto kuwa rehemu wazee wake katika namna ili bora kabisa.
Ombi langu wana bodi Mohamed ana hazina kubwa sana ya historia, tutulie tuvune, kubishana kwa hoja ndio uhai wa mnakasha. Matusi na kejeli havijengi bali vina bomoa. Naungana na Mohamed kuelewa hamaki za ndugu zetu wakristo wanapo pewa upande wa pili wa historia, challnege ya Sidney ni kuwa watafiti wengine wa kihistoria wajikite kwenye somo husika na waje na observation zao, uwanja huu ni mpana. Kuishia tu kuitana majina mdini, mgombanishi hakujibu swali husika bali tuna safisha taka ni kuweka chini ya zulia ipo siku zitanuka tu.
Mohamed sijasoma kitabu chote bali nime bahatika kusoma review yake. Kuna mahala Al marhum Dossa Aziz wakiwa na Nyerere kwenye gari maeneo ya palipo jengwa chuo kikuu cha Dar Es Salaam sasa hivi kuna kahistoria hapo kidogo naomba shule tafadhali Sheikh.
Mkuu umenena , lakini wajikanganya katika maoni yako.
Kama umepitia maoni ya wadau wote waliobandika katika mada hii utaona umuhimu wa kujadili mada hii kwa wigo mpana zaidi kuliko ule wa kutetea uislamu.
Kama nada iliwekwa in the first place na "msaigon" mwenzio ikiwa ni changa la macho for narrow Islamic objectives,basi ndio maana unaona mwisho wake unaelekea kusiko tazamiwa na kusiko pendeza.
Kama mada iliwekwa kuutukuza uislamu basi vile vile hapa si mahala pake.
Halikadhalika kama mada iliwekwa kuelezea matatizo ya uislamu na umaskini, na mtanzania mwingine yoyote asivyofaidika na maendeleo , leo miaka 50 baada ya uhuru, basi hapo kuna mjadala.
Hakuna mwenye ujuzi wa kujadili matatizo ya uislamu kama mwislamu mwenyewe.
Asiye mwislamu anapotea muda wake kuchangia katika hili.
Waislamu ndo wanajua fika kwa nini hawa kujisomesha wakati wa mkoloni na vile vile hata kabla ya mkoloni kufika nchini, miaka ya 1600 na kurudi nyuma
Utafiti , kama wa Mohammed Said, usiwe wa kujiridhisha moyo kutafuta mchawi wa matatizo ya kukosa maendeleo yake.
Narrow mindedness ya Maalim Mohammed Said unaiweka wazi tatizo la maeneo yanayokaliwa na waislamu kukosa maendeleo in very simplistic form
Jamaa huyu anaweka mjadala kwa nia ya kuudhibiti ukristo ili uislamu uneemeke kwa sababu yoyote ile. Na vile vile basi anatazamia watu wakae doro na kukubali yale yanayotolewa na kuelezewa as if mipango yote ya kuleta uhuru ilifanyika na kina Sykes na waislamu wengine, na Mwalimu akakaribishwa tu ku-officiate the occassion.
History cannot be so simple and cheap.
Nimeona mkuu MS unamwomba FM alete uchunguzi wa mapambano ya kuleta uhuru kutika sehemu zingine za Mbeya na Arusha, is this an admission that your own research is faulty and inconclusive?
You are not being fair to your selves and the public in general.
Ujinga unatabia moja mbaya, una tabia ya kujitukuza katika mambo ambayo mtu huwa hauji, na bado ukielimishwa unaona kama unadhalilishwa na kutukanwa.
Na ndio maana naona Mwalimu wakati Mwingine alichukua drastic measures za kuwaweka ndani wapinzani wake waelimishwe na kuwekwa katika hali ya kutumika ili waone umuhimu wa umoja.
Kwa sisi tuliopitia miaka hiyo ya Mwalimu tunaelewa hilo, na vijiwe kama vya Saigon tunavifahamu ingawaje tunajua vilianzishwa kutukuza yale wenyewe wasiyoyafahamu.