Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Status
Not open for further replies.
FM: Angalia hii hapa chini upate picha ya harakati za siasa miaka ile ya 1950s mwishoni:

Kufichuka kwa msimamo wa Nyerere wa kutaka TANU iingie kaatika kura tatu kulishtua uongozi wa Tanga. Majadiliano makali yalifuata uongozi wa Tanga ukionyesha upinzani wao kwa msimamo wa Nyerere. Baada ya majadiliano ya muda mrefu Nyerere alifanikiwa kuwashawishi wote wawili, Hamisi Heri na Mwalimu Kihere ambao ndiyo walikuwa wapinzani wakubwa wa msimamo wa Nyerere na uchaguzi wa kura tatu. Nyerere aliutahadharisha uongozi wa Tanga kuwa agenda ya kura tatu itakapokuja anatabiri kupata upinzani mkali kutoka katika majimbo. Huko Tanga kwenyewe, TANU ilikuwa ikikabiliwa na upinzani mkali kutoka UTP na serikali. Matawi kadhaa yalikuwa yamepigwa marufuku. [1] UTP ilikuwa na nguvu Tanga kwa sababu wanachama wake wengi walikuwa wakimiliki mashamba ya mkonge katika jimbo hilo. Kwa ajili hii chama kilikuwa kinaelemewa na mashambulizi kutoka wa wapinzani. Wakati huo Tanga ilikuwa imetoa viongozi wenye uwezo lakini wote walikuwa wamehamishiwa makao makuu mjini Dar es Salaam. Wapangaji mikakati wazuri kama Peter Mhando alikuwa amehamishiwa Dar es Salaam na kutoka hapo alipelekwa Tabora ambako si muda mrefu akafa. Elias Kissenge vilevile alihamishiwa makao makuu kushika nafasi ya Katibu Mkuu wa TANU baada ya Oscar Kambona aliyekuwa ameshika nafasi hiyo kwenda Uingereza kwa ajili ya masomo. Uongozi wa TANU Tanga hata baada ya kujadili mbinu waliyopanga na huku Nyerere akielekeza mikakati ambayo Mwalimu Kihere na Abdallah Rashid Sembe wataitekeleza Tabora, bado uongozi ule ulikuwa na wasiwasi wa mafanikio ya mpango huo. Kwa ajili ya wasiwasi huu, viongozi wa TANU wa Tanga walimuomba Nyerere wawe pamoja ili ifanywe "tawaswil" waombe msaada wa Allah awape ushindi dhidi yaa vitimbi vya Waingereza.

Maili tatu kutoka Tanga kipo kijiji cha Mnyanjani ambako kulikuwako na tawi la TANU lililokuwa na nguvu sana likiongozwa na Mmaka Omari kama mwenyekiti na Akida Boramimi bin Dai akiwa katibu. Mmaka alikuwa kijana aliyekuwa akiendesha mgahawa pale kijijini na Akida bin Dai alikuwa mwashi. Akida aliongoza tawi la vijana wa TANU ambalo baadae lilikuja kujulikana kama Tanga Volunteer Corps (TVC). TVC ilikuwa sawasawa na Bantu Group, ambayo wakati huo ilikuwa imekwishaanzishwa huko Dar es Salaam na Tabora. Vikundi hivi mbali na kufanya shughuli za propaganda na kuhamasisha wananchi halikadhalika viliifanyia TANU ujasusi. Nyerere na Kissenge walichukuliwa hadi Mnyanjani na "tawaswil" ikasomwa. Waliohudhuria kisomo hicho walikuwa Abdallah Rashid Sembe, Sheikh Dhikr bin Said, Mzee Zonga, Hemed Anzwan, Salehe Kibwana aliyekuwa mshairi maarufu, Akida Boramimi bin Dai na Mmaka Omari. Aliyechaguliwa kusoma Quran Tukufu alikuwa mjomba wa Mwalimu Kihere, Sheikh Ali Kombora.
 
Humo humo kuna wakina PETER MHANDO, ELIAS Kissenge. Sasa kusomewa "tawaswil" wakina Nyerere kunageuza mapambano yote kuwa ya kiislamu? Unazungumzia matawi ya TANU katika maeneo yenye waislamu wengi tu na ku-ignore matawi kama ya Arusha na Mbeya ambako wakristu ndio walikuwa wengi! Hii cherry picking yako ndio tunayoipinga!

Amandla.....
.
 
MOHAMED SAID,umesikika,wenye kukaa na madras yao haya,wenye kukaa na kanisa haya.all in all hii dot.com generation haina dini,wala hataki kujua historia,what they know ni live by the day with the present na let fate take care of the future-hapa with all due respect unampigia mbuzi mluzi.
 
LG: Hapana hiyo si nukuu kutoka Qur'an hayo ni maneno ya mwalimu wangu alikuwa akinifundisha adabu ya mazungumzo na umuhimu wa kuheshimiana. Alikuwa akienda mbali kidogo akisema ikiwa unayejadilinae ni katika kundi ambalo wako juu kwa hali na mali huyo hupelekea kuchukuliwa na hali yake na utaiona ile dharau kwako. Sasa Maalim Haruna akisema hali kama hiyo ikidhihiri wajibu ni kuwa mtulivu na kufanya juhudi umtulize yeye ili mjadala ustawi. Vinginevyo mtaishia kutoleana maneno yasiyokuwa na tija. Maalim Haruna akisisitiza kuwa katika mnakasha usimwangalie mpinzani wako yeye ni mmoja bali ipeleke akili yako kwa wale wanaosikiliza kwa kuwa hao ni wengi na ndiyo watakaotoa hukumu. Alilkuwa akisema kuwa silaha ni elimu nzuri na ujuzi wa somo unalozungumza. Wakati mwingine alikuwa akisema sisi ni umma bora basi tudhihirishe hilo katika matendo na kauli njema. Maalim Haruna hakuwahi kuingia darasani elimu yote hii alonifunza mimi kasomeshwa na masheikh zake Msasani, Dar es Salaam.
 
SOA: Ahsante kwa nasaa zako. Mimi sioni hivyo. Kwa hakika wapo kama hao unaosema na wako waliolelewa. Sasa kwa kuwa sisi ni umma bora tuna dhima ya kunasihiana asaa kheri huenda faida ikapatikana. Naamini nguvu zangu hazijenda patupu. Ninapata feedback nzuri sana kuhusu huu mjadala hata mie nashangaa. Hili ndilo linalinipa nguvu ya kuendelea na mjadala.
 
FM: Ahsante kwa mchango wako. Ingekuwa bora sana laiti angepatikana mtu wa kuandika habari za huko. Nimemshauri kijana mmoja anafundisha historia katika moja ya vyuo vikuu vyetu awape wanafunzi wake assignment wakati wa likizo waandike vitu kama hivyo ulivyosema ili tujue Mbeya na Arusha mambo yalikuwaje.
 
Mkuu wewe saizi yako vijana wa madrasaa na primary kubishana nao.
My allegations still stand, period.
Nashukuru kwamba umeelewa ya kuwa mimi si saizi yako katika huu mjadala.Nikitaka kupata hoja za maana basi nitafute wenzangu wa madrasa tujadiliane.

Kama unavyoonekana kwenye picha Lole umechoka sana kwenye hii mada,umeishiwa hoja mpaka unatoa majibu ya kukufedhehesha kiasi hiki.Yaani maelezo yote kwenye hii post umeishia kutoa jibu kama hilo.Ungekuwa uko katika madrasa yangu ningekuchapa mikwaju ya mpera sawa sawa.Kuanzia sasa hizi barghashia,kofia na vilemba tunavyovaa utakuwa umeelewa kuwa vinaficha hekima nyingi chini yake.

Kwa hapa kwenye jukwaa kwa kweli huna jipya,marudio ya hoja zako za umoja wa kitaifa bila kutoa namna umoja huo utakavyofikiwa huku waislamu wakidhulumiwa,hii ni kupoteza muda tu wa wanaJF.Ndio maana nikasema wewe ni wa kupigwa mikwaju ya mpera,baada ya hapo utaweza kujua tofauti kati ya umoja na dhulma ni ipi.
 
Mohamed Said Salum Popo "Sidney" mwana wa Saigon. Nimechelewa kwenye huu mnakasha na nimejipa wiki 2 za muda wangu wa ziada kusoma posts zote. Imethibitika kwa ukweli usio na shaka Sidney you are bigger fish in the small pond. Kwa mimi ninae kufahamu binafsi sishangai kwa nini pamoja weledi wako wa kujenga hoja na vithibitisho vya tafiti za kisayansi unapata majibu ya kejeli, kashfa, dharau na matusi ( wakati mwingine ya nguoni) Huyu ndio Mohamed Said nimjuae anaweza ku interact na watu aina zote kutoka kijiweni kwake pale saigon mpaka katika majukwaa ya kimataifa. Kwake Sidney kuisimulia historia hii ni namna ya kuwa rehemu wazee wake, naam ni jambo la fakhari kuona kwa mtoto kuwa rehemu wazee wake katika namna ili bora kabisa.

Ombi langu wana bodi Mohamed ana hazina kubwa sana ya historia, tutulie tuvune, kubishana kwa hoja ndio uhai wa mnakasha. Matusi na kejeli havijengi bali vina bomoa. Naungana na Mohamed kuelewa hamaki za ndugu zetu wakristo wanapo pewa upande wa pili wa historia, challnege ya Sidney ni kuwa watafiti wengine wa kihistoria wajikite kwenye somo husika na waje na observation zao, uwanja huu ni mpana. Kuishia tu kuitana majina mdini, mgombanishi hakujibu swali husika bali tuna safisha taka ni kuweka chini ya zulia ipo siku zitanuka tu.

Mohamed sijasoma kitabu chote bali nime bahatika kusoma review yake. Kuna mahala Al marhum Dossa Aziz wakiwa na Nyerere kwenye gari maeneo ya palipo jengwa chuo kikuu cha Dar Es Salaam sasa hivi kuna kahistoria hapo kidogo naomba shule tafadhali Sheikh.
 
Haya madudu yapelekwe jukwaa la kidini. yanaleta kichefuchefu

Small: Ni bahati mbaya umepata hisia kama hizo lakini huu ni mjadala wa kisomi na kuna manufaa mengi ndani yake hata kama wachangiaji hatukubaliani katika muono na mawazo. Hii si kitu ndiyo dalili za ukomavu wa elimu. Nakuwekea hapa chini utangulizi wa kitabu changu ambacho ndiyo chanzo cha yote haya. Nakuomba usome na unifahamishe unajisikiaje baada ya kusoma utangulizi huo:

Utangulizi

Kazi hii ni matokeo ya mambo niliyoyapata kuyafahamu mimi mwenyewe kutokana na masimulizi niliyopokea kutoka kwa watu wengi, kuhusu mambo yalitokea Dar es Salaam. Nikiwa nimezaliwa Dar es Salaam ambako ndipo kulipokuwa na chimbuko la harakati za kupinga ukoloni Tanganyika, kama Tanzania ilivyokuwa ikijulikana wakati huo, nina kumbukumbu nyingi za watu mashuhuri na matukio yaliyotokea. Kauli za watu waliyoyaona mambo kwa macho yao wenyewe yakitendeka zilikuza maarifa yangu. Nilipokuwa mwanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mahali ambapo utafiti wa kitabu hiki ulipoanza, niligundua kuwa mambo yaliyokuwa yakifundishwa kuhusu harakati za kudai uhuru wa Tanganyika hayakulingana na ukweli kama niliyokuwa nikiujua. Kidogo kidogo nikatambua kuwa kulikuwa na jaribio la makusudi kabisa la kufifilisha kazi kubwa iliyofanywa na baadhi ya wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika.

Nikiwa kijana mdogo, baba yangu Said Salum Abdallah alikuwa akinisimulia habari za ushujaa wa babu yake, Samitungo Mwekapopo. Samitungo alivuka mpaka toka Belgian Congo na kuingia Tanganyika kupitia sehemu ya kaskazini ya ziwa Tanganyika katika miaka ya mwishoni 1800. Wakati huo Tanganyika ilikuwa chini ya utawala wa Wajerumani. Wajerumani walikuwa wamewashinda Waarabu chini ya Abushir bin Salim bin Harith katika ukanda wa pwani na machifu kama Mkwawa waliokuwa wakitawala bara. Samitungo alipata kupigana na chui, akamuua na yeye akanusurika kuuwawa. Hata hivyo yule chui alimtia kilema cha maisha. Babu yangu Salum Abdallah Popo alizaliwa Shirati huko Musoma ambako baba yake Samitungo alikuwa askari katika Boma la Wajerumani. Nasikia kuwa boma hilo lingalipo hadi leo. Babu yangu alikuwa mtu jasiri kama baba yake. Ingawa vitabu vya historia havimtaji, lakini babu yangu yeye ndiye aliyeongoza mgomo wa kwanza wa Tanganyika mwaka 1947 dhidi ya Waingereza katika majimbo ya kati ya Tanganyika. Babu yangu alikuwa mmoja wa wazalendo wa kwanza wakati wa ukoloni kuanzisha harakati za vyama vya wafanyakazi. Vilevile alikuwa kati ya watu wa mwanzo kuiunga mkono Tanganyika African National Union (TANU), chama cha kizalendo kilichopigania na kunyakua uhuru kutoka kwa Waingereza mwaka 1961.

Babu yangu alipendelea kuitwa kwa jina lake la utani "Kapipi," ambapo neno la Kimanyema lililokuwa na maana "mweusi." Baadaye alipostaafu kazi na akiwa na mtu wa kujiweza kidogo na akiishi Tabora, wale waliokuwa karibu naye walimwita kwa jina la utani Gulamsojo, likimaanisha "bwana." Lakini jina hili hawakuthubutu kulitamka mbele yake kwa sababu babu yangu alijulikana kuwa hakuwa mtu wa maskahara hasa kwa yale mambo yasiyompendeza.

TAA ilipofanya mkutano wa siri katika shule moja pale Tabora ili kuchangisha fedha kumwezesha katibu wa TAA Jimbo la Magharibi Germano Pacha kusafiri Dar es Salaam kuhudhuria mkutano mkuu wa kuanzishwa TANU Julai mwaka 1954 mchango, mkubwa kupita yote ilikuwa shilingi ishirini. Fedha hizi alitoa babu yangu. Mkutano huu ulihudhuriwa na watu maarufu wa Tabora pamoja na baadhi ya waalimu kama Abubakar Mwilima, Harub Said na George Magembe. Hawa walikuja kuwa watu muhimu sana wakati wa harakati za kudai uhuru. Hata hivyo, babu yangu alitupana mkono na Julius Nyerere kama wengi walivyofanya, na alitiwa kizuizini na serikali mara baada ya uhuru chini ya Preventive Detention Act ya mwaka 1962.

Mara nyingi nilipodadisi baadhi ya mambo katika historia ya TANU jibu nililopata kutoka kwa waalimu wangu na wanafunzi wenzangu lilikuwa, ni lete ushahidi wakoí Nilipomtaja baba yangu kuwa ndiyo shahidi wangu, wenzangu walinifanya kichekeso na kuniona mpumbavu. Baba yangu alizaliwa Tabora lakini aliishi maisha yake yote ya utoto na ujana wake Dar es Salaam. Kupitia kwake nilijifunza mambo mengi kuhusu mji wenyewe na kuhusu maisha yake ya utoto akiwa na rafiki zake, marehemu Abdulwahid Sykes na mdogo wake Ally. Waliingizwa shule pamoja katika Al Jamiatul Islamiyya Muslim School na baadae katika shule ya serikali. Baba yangu alinieleza jinsi Abdulwahid na Ally walivyopenda kujinasibu na asili yao ya Kizulu na baba yangu na kaka yake mkubwa Humud walijinasibu kuwa wao ni Wakongomani. Jina jingine la baba yangu mkubwa lilikuwa Popo - jina la babu yake, Samitungo Mwakapopo. Hili lilikuwa ndiyo jina ambalo kwalo alijulikana mjini Dar es Salaam katika miaka ya 1950, ambako aliishi, akafanya kazi na kufia hapo.

Babu yangu Salum Abdallah na Kleist Sykes walikuwa majirani katika miaka ya 1930 nyumba zao zikitazamana katika Mtaa wa Kipata (sasa Kleist Sykes0, na wote wakiwa wameajiriwa na Tanganyika Railways. Babu yangu akifanya kazi katika karakana ya kuyeyusha chuma. Lango kuu la kuingia loko shedi kama sehemu hiyo ilivyokuwa ikijulikana ilikuwa limeelekea katika mtaa ambao sasa unajulikana kama Mtaa wa Nkrumah. Hii ndiyo ilikuwa karana kuu ambayo treni na mabehewa yake yalikuwa yakifanyiwa matengenezo na vipuli kutengenezwa hapo. Kazi yake ilikuwa ngumu inayohitaji kufanyika katika hali ya joto la juu kabisa kutoka katika moto ambao ulihitajika ili kukunja chuma kwa moto mkali. Hii ilikuwa kazi ngumu iliyohitaji nguvu na afya nzuri, kazi hasa iliyomfaa babu yangu kwa tambo lake kubwa la Kimanyema. Kleist alikuwa amesoma katika shule ya Wajerumani. Kwa ajili hii basi alikuwa na kazi isiyokuwa na sulubu, wakati ule akiajiriwa kama karani wa mahesabu. Kleist na Salum Abdallah, baba yangu alinifahamisha, hawakuwa kwa hakika watu waliopendana sana. Wazulu wanafahamika kwa sifa ya shari kama walivyo Wamanyema. Lakini watoto wa Kleist na Salum Abdallah Popo, walikuja kujenga urafiki ambao ulidumu miaka mingi.

Wakati nakua, nilikuja kujua kuhusu watu hawa na mambo yaliyotokea Dar es Salaam hata kabla sijazaliwa mwaka wa 1952. Baba yangu, ndugu zake na watu wengine wa Dar es Salaam walikuwa ndiyo walikuwa walimu wangu kwa yote niliyojifunza kuhusu mji wenyewe na historia yake.

Wakati huo mjini Dar es walikuwako Wazulu wanne maarufu kutoka Afrika ya Kusini; Kleist Sykes, (jina lake lingine lilikuwa Abdallah) mwanzoni akijulikana kama Kleist Plantan, hili jina la Plantan alilipata kutoka kwa Afande Plantan, mlezi wa Kleist baada ya kifo cha baba yake Sykes Mbuwane. (Affande lilikuwa ni cheo katika jeshi la Waturuki. Huenda liliingizwa ndani ya majeshi ya Wajerumani wakati wa vita Kuu ya Kwanza ya Dunia wakati Uturuki na Ujerumani zilipokuwa washirika katika vita hivyo). Kwa kweli jina la Kizulu la Affande Plantan lilikuwa Shangaan. Hili jina lilitokana na kijiji katika Inhambane Msumbiji, walikotoka Sykes Mbuwane na Affande Plantan. Wajerumani waliwaajiri Wazulu 400 kutoka Msumbiji kama mamluki na kujanao Tanganyika ili wapigane na Abushiri na Chifu Mkwawa. Pamoja na Kleist katika mji wa wa Dar es Salaam walikuwepo ndugu wa mbali watatu, Mwalimu Thomas Plantan, (hilo jina Mwalimu alipewa kwa sababu alikuwa Mwalimu wa shule), Schneider Abdillah Plantan na Ramadhani Mashado Plantan. Hawa Wazulu waliweza kutambulika kwa urahisi kutokana na majina yao ya Kikristo ingawa wao wenyewe walikuwa Waislam. Majina hayo yalikuwa na mchanganyiko wa majina ya Kijerumani, Kireno na Kiingereza; kama vilevile Kleist na Schneider ni majina ya Kijerumani; Mashado ambalo ni jina la Kireno na Thomas ni la Kiingereza. Wote hao, Kleist, Mwalimu Thomas, Schneider na Mashado baadaye walifanya kazi kubwa katika kupiga vita ukoloni na katika kuupeleka mbele Uislamu, kabla na baada ya uhuru. Bahati mbaya majina haya ya Kiislamu ya wazalendo hawa hayakujitokeza sana ba badala yake walijulikana zaidi kwa majina yao ya Kizungu waliyoyarithi kutoka Wajerumani kupitia wazee wao wa Kizulu.

Vilevile kulikuwa na idadi kubwa kidogo ya Wamanyema mashuhuri, kama vilevile Mzee bin Sudi (ambaye alikuwa ndiyo kiongozi wa Wamanyema mjini Dar es Salaam), Sheikh Hussein Juma msomi mahiri, Nassoro Kiruka aliyekuwa mtu tajiri mwenye majumba ya kupangisha na mtu wa kujipendekeza sana kwa Waingereza; na Iddi Tosiri ambaye pamoja na Kleist na Waislam wengine walijenga Al Jamiatul Islamiyya Muslim School katika miaka ya katikati ya 1930, shule ambayo baba yangu na wengi wa marika yake walipata elimu yao ya dini na ya dunia. Halikadhalika alikuwepo Erika Fiah, Mganda maarufu aliyeamua kulowea Tanganyika baada ya vita Vikuu vya Kwanza. Hawa ëwagenií ikiwa tunaweza kuwaita hivyo, waliacha athari kubwa katika siasa mjini Dar es Salaam.

Nilipokua napata makamo nilikuja kuwajua watu hawa na juu ya matukio yaliyotokea mjini Dar es Salaam hata kabla sijazaliwa katika mwaka 1952. Baba yangu, ndugu na jamaa na watu wa Dar es Salaam walikuwa ndiyo walionioeleza kila kitu nilichokujakukifahamu kuhusu mji na historia yake.

Ninakumbuka siku moja miaka mingi iliyopita, nilikuwa ninatazama picha ya waasisi wa TANU. Wakati huo ilikuwani desturi wakati wa kuadhimisha kuanzishwa kwa TANU mnamo Julai 7, 1954, inapofika tarehe hiyo kila mwaka ilikuwa ni sikukuu. Ilikuwa kawaida kuchapisha katika magazeti ya serikali na chama, picha ya pamoja ya wale waasisi kumi na saba iliyopigwa mbele ya ofisi ya TAA. Mmoja wa baba zangu, Abdallah Mohamed aliyefahamiana na Abdulwahid kwa miaka mingi alitazama picha ya Abdulwahid kisha akasema, "Huyu ndiye mtu aliyeanzisha TANU na angekuwa rais wa nchi hii, kama angetaka."

Vilevile vilevile baba yangu aliniambia, mara yake ya kwanza kumuona Julius Nyerere ilikuwa mwaka 1952 nyumbani kwa Abdulwahid. Wote wawili baba yangu, na marehemu Abduwahid walikuwa vijana umri wao miaka ishirini na nane. Baba yangu alikuwa mbali na siasa. Kitu kimoja tu kilichomuunganisha na marehemu Abdulwahid ilikuwa ni utanashati na kwa enzi zile wao ndiyo walikuwa vijana waungwana wa mjini. Walichanganya utamaduni wa Kiswahili na ule wa Ulaya na sehemu nyingine za dunia. Walisikiliza muziki wa Edmund Ross, Victor Silvester, Nat King Cole, Luis Amstrong, Alma Cogan, Bing Crosby na wanamuziki wengine. Wakati mwingine waliwasikiliza waimbaji wa Kiarabu, Um Kulthum, Mohammed Abdulwahab, Farid Atrash, Abdul Halim Hafidh, Feruz na Sabah. Santuri za baba yangu za muziki wa jazz zimedumu kwa muda mrefu zaidi ya miaka ya arobaini.

Familia yangu ilifahamiana na Dome Budohi, mmoja wa wanaharakati kutoka Kenya. Wakati ule wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika alikuwa akiishi Dar es Salaam. Budohi alikuwa mmoja wa wazalendo walioasisi TANU na kadi yake ya uanachama ni nambari sita aliyopewa Julai 1954. Mwaka 1955 alikamatwa na serikali ya kikoloni kwa tuhuma ya kuwa mmoja wa askari wa Mau Mau harakati za wazalendo takriban wengi wao wakulima wadogo waliokuwa wakipigana na ukoloni wa Waingereza nchini Kenya. Ninazo kumbukumbu nyingi za utoto nikimtembelea Budohi ndani ya selo yake Kituo Cha Kati cha Polisi. Hivi sasa jengo hilo ni Makao Makuu ya Shirika la Reli la Tanzania. Wakati huo mimi nilikuwa mtoto, si zaidi ya miaka minne hivi. Jambo la kwanza ninalokumbuka kuhusu Budohi ni kuwa kila mara tulipokwenda kumtembelea tulimkuta anasoma gazeti. Baadae Budohi alihamishiwa Kenya na aliwekwa kizuizini katika kisiwa cha Lamu. Alipofunguliwa toka kizuizini mwaka wa 1963 miezi michache kabla ya uhuru wa Kenya, Budohi alikwenda Uganda na akaajiriwa na gazeti la "Uganda Argus." Hivi sasa ninaelewa kwa nini siku zile kila mara nilikuwa namkuta amezama ndani ya gazeti kila tulipokwenda kumtembelea pale rumande mjini Dar es Salaam.

Niliweza kwa msaada wa rafiki yake Maxwell aliyelowea Tanganyika, kumpata Budohi mjini Nairobi mwaka 1972. Nilimtembelea mjini Nairobi wakati huo alikuwa akiishi Ruiru maili chache kutoka Nairobi mjini. Budohi alikuwa ametundika picha ya Nat King Cole sebuleni kwake. Mwaka 1974 nilimtembelea tena, safari hii katika nyumba yake ya Ngei Estate. Budohi alikuja kuwa mtu wa kwanza kabisa kunipa habari kuhusu historia ya harakati za Tanganyika dhidi ya ukoloni wa Waingereza. Hata hivyo wakati ule nilikuwa bado sijapata hamu wala kuwa na hamu ya kuandika kitabu kuhusu uhuru wa Tanganyika.

Katika hali kama hii vipi mimi nisijione kuwa ni sehemu ya historia hiyo? Katika hali kama hii vipi nitamudu kukaa kimya wakati historia ya uongo ndiyo inayoenziwa na ile ya kweli inafichwa? Nilipoanza kupitia vitabu na maandiko mengine juu ya somo hili, nilistaajabu kuona kuwa hakuna hata mmoja kati ya watu mashuhuri niliowajua ambao walihusika na harakati za uhuru walikuwa wametajwa katika vitabu hivyo. Nilipigwa na butwaa nipogundua kuwa hata Abdulwahid Sykes, shujaa ambae baba yangu akimtaja sana katika siasa za Tanganyika hakuwa ametajwa popote.
 
Ndugu yangu Eddie ahsante sana kwa msaada wako na kwa kunipamba. Insha Allah nitakieleza kisa cha Dossa, Nyerere na mpango wa kujenga Chuo Kikuu. Wako wapi waliotaka kupanda ngazi kuu? Siwaoni.
 
Nashukuru kwamba umeelewa ya kuwa mimi si saizi yako katika huu mjadala.Nikitaka kupata hoja za maana basi nitafute wenzangu wa madrasa tujadiliane.

Kama unavyoonekana kwenye picha Lole umechoka sana kwenye hii mada,umeishiwa hoja mpaka unatoa majibu ya kukufedhehesha kiasi hiki.Yaani maelezo yote kwenye hii post umeishia kutoa jibu kama hilo.Ungekuwa uko katika madrasa yangu ningekuchapa mikwaju ya mpera sawa sawa.Kuanzia sasa hizi barghashia,kofia na vilemba tunavyovaa utakuwa umeelewa kuwa vinaficha hekima nyingi chini yake.

Kwa hapa kwenye jukwaa kwa kweli huna jipya,marudio ya hoja zako za umoja wa kitaifa bila kutoa namna umoja huo utakavyofikiwa huku waislamu wakidhulumiwa,hii ni kupoteza muda tu wa wanaJF.Ndio maana nikasema wewe ni wa kupigwa mikwaju ya mpera,baada ya hapo utaweza kujua tofauti kati ya umoja na dhulma ni ipi.
Safu kabisa mkuu ukiisha kubishana na kushinda mabishano yako na vijana wa madrassa na primary, na ukishinda chagua mji.
Mimi nakupa Saadani , Pangani au Lindi ngome yenu toka miaka ya 1700.
Huko ndo stahili yako
 
LG: Hapana hiyo si nukuu kutoka Qur'an hayo ni maneno ya mwalimu wangu alikuwa akinifundisha adabu ya mazungumzo na umuhimu wa kuheshimiana. Alikuwa akienda mbali kidogo akisema ikiwa unayejadilinae ni katika kundi ambalo wako juu kwa hali na mali huyo hupelekea kuchukuliwa na hali yake na utaiona ile dharau kwako. Sasa Maalim Haruna akisema hali kama hiyo ikidhihiri wajibu ni kuwa mtulivu na kufanya juhudi umtulize yeye ili mjadala ustawi. Vinginevyo mtaishia kutoleana maneno yasiyokuwa na tija. Maalim Haruna akisisitiza kuwa katika mnakasha usimwangalie mpinzani wako yeye ni mmoja bali ipeleke akili yako kwa wale wanaosikiliza kwa kuwa hao ni wengi na ndiyo watakaotoa hukumu. Alilkuwa akisema kuwa silaha ni elimu nzuri na ujuzi wa somo unalozungumza. Wakati mwingine alikuwa akisema sisi ni umma bora basi tudhihirishe hilo katika matendo na kauli njema. Maalim Haruna hakuwahi kuingia darasani elimu yote hii alonifunza mimi kasomeshwa na masheikh zake Msasani, Dar es Salaam.

Mkuu, mwalimu wangu wa darasa la pili, yeye alinielimisha kuwa maisha ni pamambano.
Everything is a challenge, and go and deal with it with a mentality to WIN.
Losing should not be an option, thats where we differ Maalim.
Mimi ni mpambanaji, na ikija challenge in whatever way 1st option ni ku overcome the challenge na sio ku submit. Kama ninyi na kundi lako hamtaona umihimu wa kushirikiana na waTanzania wengine maisha ni mbele kwa mbele, we face other challenges , and to win them over.
 
Mohamed Said Salum Popo "Sidney" mwana wa Saigon. Nimechelewa kwenye huu mnakasha na nimejipa wiki 2 za muda wangu wa ziada kusoma posts zote. Imethibitika kwa ukweli usio na shaka Sidney you are bigger fish in the small pond. Kwa mimi ninae kufahamu binafsi sishangai kwa nini pamoja weledi wako wa kujenga hoja na vithibitisho vya tafiti za kisayansi unapata majibu ya kejeli, kashfa, dharau na matusi ( wakati mwingine ya nguoni) Huyu ndio Mohamed Said nimjuae anaweza ku interact na watu aina zote kutoka kijiweni kwake pale saigon mpaka katika majukwaa ya kimataifa. Kwake Sidney kuisimulia historia hii ni namna ya kuwa rehemu wazee wake, naam ni jambo la fakhari kuona kwa mtoto kuwa rehemu wazee wake katika namna ili bora kabisa.

Ombi langu wana bodi Mohamed ana hazina kubwa sana ya historia, tutulie tuvune, kubishana kwa hoja ndio uhai wa mnakasha. Matusi na kejeli havijengi bali vina bomoa. Naungana na Mohamed kuelewa hamaki za ndugu zetu wakristo wanapo pewa upande wa pili wa historia, challnege ya Sidney ni kuwa watafiti wengine wa kihistoria wajikite kwenye somo husika na waje na observation zao, uwanja huu ni mpana. Kuishia tu kuitana majina mdini, mgombanishi hakujibu swali husika bali tuna safisha taka ni kuweka chini ya zulia ipo siku zitanuka tu.

Mohamed sijasoma kitabu chote bali nime bahatika kusoma review yake. Kuna mahala Al marhum Dossa Aziz wakiwa na Nyerere kwenye gari maeneo ya palipo jengwa chuo kikuu cha Dar Es Salaam sasa hivi kuna kahistoria hapo kidogo naomba shule tafadhali Sheikh.

Mkuu umenena , lakini wajikanganya katika maoni yako.
Kama umepitia maoni ya wadau wote waliobandika katika mada hii utaona umuhimu wa kujadili mada hii kwa wigo mpana zaidi kuliko ule wa kutetea uislamu.
Kama nada iliwekwa in the first place na "msaigon" mwenzio ikiwa ni changa la macho for narrow Islamic objectives,basi ndio maana unaona mwisho wake unaelekea kusiko tazamiwa na kusiko pendeza.
Kama mada iliwekwa kuutukuza uislamu basi vile vile hapa si mahala pake.
Halikadhalika kama mada iliwekwa kuelezea matatizo ya uislamu na umaskini, na mtanzania mwingine yoyote asivyofaidika na maendeleo , leo miaka 50 baada ya uhuru, basi hapo kuna mjadala.
Hakuna mwenye ujuzi wa kujadili matatizo ya uislamu kama mwislamu mwenyewe.
Asiye mwislamu anapotea muda wake kuchangia katika hili.
Waislamu ndo wanajua fika kwa nini hawa kujisomesha wakati wa mkoloni na vile vile hata kabla ya mkoloni kufika nchini, miaka ya 1600 na kurudi nyuma
Utafiti , kama wa Mohammed Said, usiwe wa kujiridhisha moyo kutafuta mchawi wa matatizo ya kukosa maendeleo yake.
Narrow mindedness ya Maalim Mohammed Said unaiweka wazi tatizo la maeneo yanayokaliwa na waislamu kukosa maendeleo in very simplistic form
Jamaa huyu anaweka mjadala kwa nia ya kuudhibiti ukristo ili uislamu uneemeke kwa sababu yoyote ile. Na vile vile basi anatazamia watu wakae doro na kukubali yale yanayotolewa na kuelezewa as if mipango yote ya kuleta uhuru ilifanyika na kina Sykes na waislamu wengine, na Mwalimu akakaribishwa tu ku-officiate the occassion.
History cannot be so simple and cheap.
Nimeona mkuu MS unamwomba FM alete uchunguzi wa mapambano ya kuleta uhuru kutika sehemu zingine za Mbeya na Arusha, is this an admission that your own research is faulty and inconclusive?
You are not being fair to your selves and the public in general.

Ujinga unatabia moja mbaya, una tabia ya kujitukuza katika mambo ambayo mtu huwa hauji, na bado ukielimishwa unaona kama unadhalilishwa na kutukanwa.
Na ndio maana naona Mwalimu wakati Mwingine alichukua drastic measures za kuwaweka ndani wapinzani wake waelimishwe na kuwekwa katika hali ya kutumika ili waone umuhimu wa umoja.
Kwa sisi tuliopitia miaka hiyo ya Mwalimu tunaelewa hilo, na vijiwe kama vya Saigon tunavifahamu ingawaje tunajua vilianzishwa kutukuza yale wenyewe wasiyoyafahamu.
 
Mkuu Mohammed Sais, I have said again and again that it is the Islamic communities that RESISTED formal education , sometimes refering to it as kafir education!
Lets refer to John Illife pg 445 in his book A modern history of Tanganyika,

" In 1948 literacy among children between six and fifteen yrs old varied from 21% in Tanga Province to5 % in Central Province. Whereas in 1956 some 90% of Chagga children were at school, the proportion among the neighbouring Meru three years later and among the Arusha only 34%. SOME MUSLIM REGIONS STILL RESISTED EUROPEAN SCHOOLING, BUT MOST OTHER BACKWARD AREAS STROVE TO CATCH UP WITH MORE FORTUNATE NEIGHBOURS WHO THEMSELVES STROVE, GENERALLY TO STAY AHEAD. SO SMALL TRIBES WITH EARLY MISSION EXPERIENCE GENERALLY KEPT THEIR EDUCATIONAL LEAD OVER LARGER TRIBES-WITH IMPORTANT POLITICAL REPERCUSSIONS."

Mohammed Said ili upate kueleweka na wananchi wote wa Tanzania na si waislamu tu, fanya utafiti wako pan territorial na utapata kuelewa wengine tunachokiongelea.
Ushindani wa elimu haukuanza wakati wa Sykes tu , bali hata kabla.
Mimi mwenyewe mjomba wangu, kaka yake mama yangu amefia na kuzikwa Ngudu,Mwanza 1957, kabla ya uhuru akifanya kazi cooperatives , katika juhudi za kuongezea ujuzi na kuongeza ushuindani huko Rungwe Cooperative Union.
Historia ya ushindani haitaishia wal haikuanzia hapa sehemu za pwani.
 
Kumbe Mohamed Said almaarufu kwa jina "Sidney"? Na memba mwingine wa Saigon jina lake ni "Eddie"! Nashindwa kuelewa kwa nini hawa wanaopinga udhalimu wa wakristu hawachelei kuchukua majina ya "kikristu". Kwa nini wasiige mfano wa Mobutu Sese Seko Nkuku Ngbendu wa Za Banga?

Amandla......
 
FM: Ahsante kwa mchango wako. Ingekuwa bora sana laiti angepatikana mtu wa kuandika habari za huko. Nimemshauri kijana mmoja anafundisha historia katika moja ya vyuo vikuu vyetu awape wanafunzi wake assignment wakati wa likizo waandike vitu kama hivyo ulivyosema ili tujue Mbeya na Arusha mambo yalikuwaje.

Kumbe Mkuu haukujua kuwa huko walikotokea wakina Dr. William Mwanjisi, Mzee John Mwakangale, Mzee Japhet Kirilo aliyesimamia kidete kesi ya mgogoro wa adhi wa wameru. Na wengine waliotoka nje ya mikoa unayoijua wewe ni wakina Mzee Joseph Kimalando kutoka Moshi ambaye amehusika katika harakati za kupinga ukoloni toka miaka ya 1930s akiwa ameajiriwa kwenye shirika la reli Tanganyika, mhehe Julius Mwasanyaji, mhindi Amir Jamal kutoka Morogoro, Frank Humplick na dada zake Mary na Regina ambao nyimbo zao ndizo zilitumika kuhamasisha wana TANU. Hata huko Tanga kwenye waislamu wengi, mchango wa Stephen Mhando na mdogo wake Peter Mhando katika kuhamasisha wabondei hauwezi kudharauliwa! ( kutoka " Nyerere and Africa: End of an era cha Godfrey Mwakikagile"). Na hawa ni sehemu ndogo tu ya waliohusika katika mapambano hayo. Ukweli nikuwa sehemu za pwani bila kuungwa mkono na sehemu nyingine za Tanganyika zisingefua dafu mbele ya mkoloni. Wote walihusika, tofauti na unavyotaka kutuaminisha.

Amandla.........
 
Kumbe Mohamed Said almaarufu kwa jina "Sidney"? Na memba mwingine wa Saigon jina lake ni "Eddie"! Nashindwa kuelewa kwa nini hawa wanaopinga udhalimu wa wakristu hawachelei kuchukua majina ya "kikristu". Kwa nini wasiige mfano wa Mobutu Sese Seko Nkuku Ngbendu wa Za Banga?

Amandla......

Ha ha ha!!
Mkuu umenikumbusha miaka hiyoooo!
Wakati ule baada ya kuanzia mwaka 1968 kuendelea hadi miaka ya 1970's mapigano katika vita vya Vietnam kati ya Vietnam Kaskazini na Kusini vilipambamoto.Vietnam Kusini pamoja na kusaidiwa na Marekani na nguvu kubwa sana ya kijeshi ilizidiwa vibaya na wapiganaji wa misituni wa kikomunisti wa Vietnam ya Kaskazini wakisaidiwa na Uchina.
Jiji la Siagon likawa under siege hadi mwishoni mwa vita hivyo na kwa muda mrefu tu.
"Saigon" ya Dar es salaam iliundwa na vijana wengi tu wa kihuni kutoka sehemu mbali mbali za Kariakoo na kuzunguka.Ilisemekana vijana wengi kati ya hao walikuwa wavuta bangi na kupigana ovyo mitaani na vikundi vinavyo pingana.
Kwa hiyo ukiingia eneo la "Saigon" Kariakoo, basi unaingia sehemu ya umwamba, vurugu na tafrani.
Mimi nalifahamu hilo kwa vile hata sehemu za Temeke,Toroli,Chang'ombe lilikuwepo kundi la "Black September" lenyewe kama Saigon ilikuwa fujo tu hasa katika matamasha ya kitaifa(kama miziki) na mipira uwanja wa Taifa kuingia bure kwa kuruka ukuta.
Alipokuja Lwambo Lwanzo Makiadi 1971, kundi hili lilifanya fujo kubwa kwa kuingia kwa kuruka ukuta Uwanja wa Taifa, hili nalikumbuka maana nilikuwepo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom