Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
FM: Ahsante mkuu wangu na tuendelee na mjadala.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
FM: Angalia hii hapa chini upate picha ya harakati za siasa miaka ile ya 1950s mwishoni:
Kufichuka kwa msimamo wa Nyerere wa kutaka TANU iingie kaatika kura tatu kulishtua uongozi wa Tanga. Majadiliano makali yalifuata uongozi wa Tanga ukionyesha upinzani wao kwa msimamo wa Nyerere. Baada ya majadiliano ya muda mrefu Nyerere alifanikiwa kuwashawishi wote wawili, Hamisi Heri na Mwalimu Kihere ambao ndiyo walikuwa wapinzani wakubwa wa msimamo wa Nyerere na uchaguzi wa kura tatu. Nyerere aliutahadharisha uongozi wa Tanga kuwa agenda ya kura tatu itakapokuja anatabiri kupata upinzani mkali kutoka katika majimbo. Huko Tanga kwenyewe, TANU ilikuwa ikikabiliwa na upinzani mkali kutoka UTP na serikali. Matawi kadhaa yalikuwa yamepigwa marufuku. [1] UTP ilikuwa na nguvu Tanga kwa sababu wanachama wake wengi walikuwa wakimiliki mashamba ya mkonge katika jimbo hilo. Kwa ajili hii chama kilikuwa kinaelemewa na mashambulizi kutoka wa wapinzani. Wakati huo Tanga ilikuwa imetoa viongozi wenye uwezo lakini wote walikuwa wamehamishiwa makao makuu mjini Dar es Salaam. Wapangaji mikakati wazuri kama Peter Mhando alikuwa amehamishiwa Dar es Salaam na kutoka hapo alipelekwa Tabora ambako si muda mrefu akafa. Elias Kissenge vilevile alihamishiwa makao makuu kushika nafasi ya Katibu Mkuu wa TANU baada ya Oscar Kambona aliyekuwa ameshika nafasi hiyo kwenda Uingereza kwa ajili ya masomo. Uongozi wa TANU Tanga hata baada ya kujadili mbinu waliyopanga na huku Nyerere akielekeza mikakati ambayo Mwalimu Kihere na Abdallah Rashid Sembe wataitekeleza Tabora, bado uongozi ule ulikuwa na wasiwasi wa mafanikio ya mpango huo. Kwa ajili ya wasiwasi huu, viongozi wa TANU wa Tanga walimuomba Nyerere wawe pamoja ili ifanywe "tawaswil" waombe msaada wa Allah awape ushindi dhidi yaa vitimbi vya Waingereza.
Maili tatu kutoka Tanga kipo kijiji cha Mnyanjani ambako kulikuwako na tawi la TANU lililokuwa na nguvu sana likiongozwa na Mmaka Omari kama mwenyekiti na Akida Boramimi bin Dai akiwa katibu. Mmaka alikuwa kijana aliyekuwa akiendesha mgahawa pale kijijini na Akida bin Dai alikuwa mwashi. Akida aliongoza tawi la vijana wa TANU ambalo baadae lilikuja kujulikana kama Tanga Volunteer Corps (TVC). TVC ilikuwa sawasawa na Bantu Group, ambayo wakati huo ilikuwa imekwishaanzishwa huko Dar es Salaam na Tabora. Vikundi hivi mbali na kufanya shughuli za propaganda na kuhamasisha wananchi halikadhalika viliifanyia TANU ujasusi. Nyerere na Kissenge walichukuliwa hadi Mnyanjani na "tawaswil" ikasomwa. Waliohudhuria kisomo hicho walikuwa Abdallah Rashid Sembe, Sheikh Dhikr bin Said, Mzee Zonga, Hemed Anzwan, Salehe Kibwana aliyekuwa mshairi maarufu, Akida Boramimi bin Dai na Mmaka Omari. Aliyechaguliwa kusoma Quran Tukufu alikuwa mjomba wa Mwalimu Kihere, Sheikh Ali Kombora.
Nashukuru kwamba umeelewa ya kuwa mimi si saizi yako katika huu mjadala.Nikitaka kupata hoja za maana basi nitafute wenzangu wa madrasa tujadiliane.Mkuu wewe saizi yako vijana wa madrasaa na primary kubishana nao.
My allegations still stand, period.
Haya madudu yapelekwe jukwaa la kidini. yanaleta kichefuchefu
Safu kabisa mkuu ukiisha kubishana na kushinda mabishano yako na vijana wa madrassa na primary, na ukishinda chagua mji.Nashukuru kwamba umeelewa ya kuwa mimi si saizi yako katika huu mjadala.Nikitaka kupata hoja za maana basi nitafute wenzangu wa madrasa tujadiliane.
Kama unavyoonekana kwenye picha Lole umechoka sana kwenye hii mada,umeishiwa hoja mpaka unatoa majibu ya kukufedhehesha kiasi hiki.Yaani maelezo yote kwenye hii post umeishia kutoa jibu kama hilo.Ungekuwa uko katika madrasa yangu ningekuchapa mikwaju ya mpera sawa sawa.Kuanzia sasa hizi barghashia,kofia na vilemba tunavyovaa utakuwa umeelewa kuwa vinaficha hekima nyingi chini yake.
Kwa hapa kwenye jukwaa kwa kweli huna jipya,marudio ya hoja zako za umoja wa kitaifa bila kutoa namna umoja huo utakavyofikiwa huku waislamu wakidhulumiwa,hii ni kupoteza muda tu wa wanaJF.Ndio maana nikasema wewe ni wa kupigwa mikwaju ya mpera,baada ya hapo utaweza kujua tofauti kati ya umoja na dhulma ni ipi.
LG: Hapana hiyo si nukuu kutoka Qur'an hayo ni maneno ya mwalimu wangu alikuwa akinifundisha adabu ya mazungumzo na umuhimu wa kuheshimiana. Alikuwa akienda mbali kidogo akisema ikiwa unayejadilinae ni katika kundi ambalo wako juu kwa hali na mali huyo hupelekea kuchukuliwa na hali yake na utaiona ile dharau kwako. Sasa Maalim Haruna akisema hali kama hiyo ikidhihiri wajibu ni kuwa mtulivu na kufanya juhudi umtulize yeye ili mjadala ustawi. Vinginevyo mtaishia kutoleana maneno yasiyokuwa na tija. Maalim Haruna akisisitiza kuwa katika mnakasha usimwangalie mpinzani wako yeye ni mmoja bali ipeleke akili yako kwa wale wanaosikiliza kwa kuwa hao ni wengi na ndiyo watakaotoa hukumu. Alilkuwa akisema kuwa silaha ni elimu nzuri na ujuzi wa somo unalozungumza. Wakati mwingine alikuwa akisema sisi ni umma bora basi tudhihirishe hilo katika matendo na kauli njema. Maalim Haruna hakuwahi kuingia darasani elimu yote hii alonifunza mimi kasomeshwa na masheikh zake Msasani, Dar es Salaam.
Mohamed Said Salum Popo "Sidney" mwana wa Saigon. Nimechelewa kwenye huu mnakasha na nimejipa wiki 2 za muda wangu wa ziada kusoma posts zote. Imethibitika kwa ukweli usio na shaka Sidney you are bigger fish in the small pond. Kwa mimi ninae kufahamu binafsi sishangai kwa nini pamoja weledi wako wa kujenga hoja na vithibitisho vya tafiti za kisayansi unapata majibu ya kejeli, kashfa, dharau na matusi ( wakati mwingine ya nguoni) Huyu ndio Mohamed Said nimjuae anaweza ku interact na watu aina zote kutoka kijiweni kwake pale saigon mpaka katika majukwaa ya kimataifa. Kwake Sidney kuisimulia historia hii ni namna ya kuwa rehemu wazee wake, naam ni jambo la fakhari kuona kwa mtoto kuwa rehemu wazee wake katika namna ili bora kabisa.
Ombi langu wana bodi Mohamed ana hazina kubwa sana ya historia, tutulie tuvune, kubishana kwa hoja ndio uhai wa mnakasha. Matusi na kejeli havijengi bali vina bomoa. Naungana na Mohamed kuelewa hamaki za ndugu zetu wakristo wanapo pewa upande wa pili wa historia, challnege ya Sidney ni kuwa watafiti wengine wa kihistoria wajikite kwenye somo husika na waje na observation zao, uwanja huu ni mpana. Kuishia tu kuitana majina mdini, mgombanishi hakujibu swali husika bali tuna safisha taka ni kuweka chini ya zulia ipo siku zitanuka tu.
Mohamed sijasoma kitabu chote bali nime bahatika kusoma review yake. Kuna mahala Al marhum Dossa Aziz wakiwa na Nyerere kwenye gari maeneo ya palipo jengwa chuo kikuu cha Dar Es Salaam sasa hivi kuna kahistoria hapo kidogo naomba shule tafadhali Sheikh.
FM: Ahsante kwa mchango wako. Ingekuwa bora sana laiti angepatikana mtu wa kuandika habari za huko. Nimemshauri kijana mmoja anafundisha historia katika moja ya vyuo vikuu vyetu awape wanafunzi wake assignment wakati wa likizo waandike vitu kama hivyo ulivyosema ili tujue Mbeya na Arusha mambo yalikuwaje.
Kumbe Mohamed Said almaarufu kwa jina "Sidney"? Na memba mwingine wa Saigon jina lake ni "Eddie"! Nashindwa kuelewa kwa nini hawa wanaopinga udhalimu wa wakristu hawachelei kuchukua majina ya "kikristu". Kwa nini wasiige mfano wa Mobutu Sese Seko Nkuku Ngbendu wa Za Banga?
Amandla......