Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Nafurahi kwamba nawe Pasco umeingia kuwasaidia wenzio.Tunahitaji nguvu mpya ili tendelee kwa sababu wenzako wameshindwa sana kutoa hoja za kutetea nukta zao.Kwa upande mwengine wameonesha udhaifu ambao kama wangeufanya mbele ya mashabiki wao basi wangepigiwa kelele Kaa chini!,au kocha angeambiwa Toa huyoo!..
Ami, mjadala huu ni bahari ya kina kirefu, ila kwa maneno haya "lakini kwa nyinyi hamna jipya na mimi sasa naingia kwa kishindo kuwaumbua ili wana ukumbi wawaone ujinga wenu katika huu mjadala.Kwa kweli sasa nina hasira kwa ujinga wenu", nadhani utaishia kuzama bure, maana waonekana kama mvuvi kinda unaingia kwa kishindo bahari kuu kushindana na wazoefu!, eti uje kuwaumbua? haya tunakusubiria tuone hizo hasira zako, karibu!.
Angalia mfano:
Fundi Mchundo na Lole mara nyingi wamemshutumu Mohammed kwamba katika utafiti wake amekuwa akikwepa kutaja majina ya wapigania uhuru ambao ni wakristo.Katika kutaka kuthibitisha hilo Fundi Mchundo akaleta ushahidi wa majina ya wakristo kama yalivyotajwa na Mwakikagile.Maskini hakujua kuwa uandishi wa Mwakikagile ni nakili ya Mohammed.
Kuthibitisha hilo ni kulitaja jina la William Mwanjisi badala ya Wilbard Mwanjisi.Hili William baada ya Mohammed kupata malalamiko kwa ndugu wa Wilbard alikuwa tayari amelirekebisha katika toleo lake la Kiswahili.
Hapa kuna vitu viwili kwanza ndugu zako wamepwaya na hoja yao kuwa Wakristo hawajatajwa.Isingekuwa busara kutajwa kwa zaidi ya walichofanya kinyume na wenzao waislamu.Jengine ni kuwa kwa kutokuleta kinyume chake baada ya kuzindushwa hivyo ni kuwa wamekubali kuwa hawana hiyo historia iliyo madhubuti ya kutetea hoja zao.Ndugu wa Wilbard hawakukanusha au hawakutaka zaidi ya alivyotajwa mhusika kinyume na nyinyi na Nyerere wenu munaotaka kuhodhi hata vya wenzenu.Walichotaka ni usahihi wa jina tu.
Pamoja na wewe kuingia kwenye huu mjadala sina hofu na wewe hata kidogo, kwani kwa dharau zako za kuiita paper ya Mohammed Said kwenye hadhara ya Kenyatta University kuwa ni hadithi nzuri tu unayopenda kuisikiliza, na wala si presentation mbele ya wasomi,najua utaangukia huko huko walikoishia wenzako.
Tunakusubiri !.