'Tarehe 27 Aprili, 1985 Julius Kambarage Nyerere, sasa akijulikana kama Baba wa Taifa, katika sherehe kubwa katika viwanja vya Ikulu, alitoa jumla ya medali 3979 kwa Watanzania waliochangia katika maendeleo ya taifa. Kati ya wale ambao walipewa medali hizo alikuwa Sheikh Abdallah Iddi Chaurembo. Wazalendo waliotajwa ndani ya kitabu hiki ambao walipigania uhuru wa Tanganyika, hakuna hata mmoja wao aliyekuwa katika orodha ile ya heshima. Baada ya siku chache kupita, Nyerere kama mtu aliyegutuka alimualika Dossa Aziz Ikulu. Dossa Aziz, wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika alikuwa mtu maarufu, mwenye nafasi, na kujiweza sana. Sasa Dossa baada ya miaka kupita hakuwa akifahamika tena na ule umaarufu na utajiri wake ulikuwa umetoweka. Alikuwa akiishi maisha ya kawaida kijijini Mlandizi, maili chache nje ya Dar es Salaam. Katika sherehe ya faragha Nyerere alimtunukia medali Dossa Aziz, rafiki yake wa zamani.'[/SIZE][/FONT]
SIZE][/FONT]
Mkuu Mohamed Said, nadhani ukosoaji wa kimantic kwenye upande wa data. Nafanyia kajiresearch kadogo hii hesebu ya 3,979 waliopatiwa nishani na Nyerere, Mwislamu alikuwa ni mmoja tuu!. No research, no right to speak, and no right to critisize. Kwa vile wewe umefanya research, umekuja na jina la Muislamu mmoja tuu kati yao, nakufanyia kaji counter reseach ili nipate right to speak and to criticise.
Ika kwa kutumia just comon sense, Watunukiwa hao 3,979 walipewa nishani katika makundi matatu
1. Nishani ya Utumishi wa Muda Mrefu
2. Nishani ya Utumishi Uliotukuka
3. Nishani ya Utumishi Uliotukuka na Tabia Njema.
Waliopewa nishani hizi, wengi wao ni watumishi wa umma. Kundi la Kwanza, ni watumishi wote wa umma waliokuwepo serikali siku tunapata uhuru, na bado walikuwepo kwenye utumishi wa umma mpaka hiyo 1985 walipata ile nishani ya kwanza ya Utumishi wa muda mrefu. Sitaki kuamini eti Waislamu wote waliokuwepo serikali, walibaguliwa, wakapewa Wakristu tuu, wala sitaki kuamini, ni Wakristu tuu ndio waliokuwepo serikalini na kuendelea kuwepo mpaka mwaka huo 1985!.
Waliopewa Nishani ya Utumishi uliotukuka ni watumishi wote wa umma, walikuwa serikali tangu 1961 mpaka 1985 ambao walifikia ngazi ya Uofisa. Na wale waliopatiwa Nishani ya Utumishi Uliotukuka na Tabia Njema, ni wale wote ambao walikuwa Maofisa wa Juu, ma loyalist to Nyerere.
Hizi hazikuwa nishani za Mashujaa wa Taifa, Wapigania Uhuru, Wanachama waaminifu wa TANU, au Watanzania wa kawaida, hizi zilikuwa nishani kwa watumishi wa umma, wakiwemo wanajeshi wetu wa majeshi ya ulinzi na usalama. Siamini kuto huko hakukuwa na waislamu. Nalifanyia kazi hizi, nipo nikurudie Mkuu Mohamed Said, na ikitokea ikawa kweli, Muslamu alikuwa mmoja tuu, kati ya hawa 3,979, nakuhakikishia Mzimu wa Nyerere, utaamka kutoka kaburini pale Mwitongo, na utawaomba msamaha Waislamu kwa such an omission!.