Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Status
Not open for further replies.
FM: Nimesoma fikra zako sidhani kama unataka nikujibu. Ikiwa utataka jibu nifahamishe na Insha Allah nitafanya hivyo.

Akina Sykes ni ndugu zangu na ninawependa sana. Ngoja nikupe kisa kimoja Ebby Abdulwahid Sykes tumepishana siku moja katika kuzaliwa kwetu. Kitanda alicholala mama yake Ebby akazaliwa Ebby akaja mama yangu siku ya pili akanizaa mimi.

Akina mama wakitoka kwa Bwana Abdu Stanley Street kumuona mzazi mama yake Ebby kisha wanakuja kwetu Kipata kumuona mama yangu. Kwa hiyo toka utoto mimi na Ebby mchezo wetu mmoja. Ni ndugu yangu khasa.

Juu ya hayo kitabu changu ukenda kwenye name index ndiyo itakupa picha ni biography ngapi ndogo ndogo ziko mle.

Lakini kubwa ni kumrehemu baba yangu Abdulwahid Kleist Sykes. Alipofikisha miaka 20 baada ya kifo chake nilimuandikia kumbukumbu katika Africa Events (London) September 1988 "Abdulwahid K Sykes (1924 - 1968) The Founder of a Political Movement"

Hii ndiyo makala iliyomliza Ahmed Rashad Ali rafiki yake Abdu Sykes ambae kwenye mazungumzo Abdu aliyofanya na Jomo Kenyatta Nairobi 1950 walikuwa wote.

Mwakilishi wa Library of Congress Tanzania aliifanyia cutting makala ile na iko katika catalogue hapo Washington DC.
 
FM: Mufti Sheikh Hassan bin Ameir alisema kuwa kisa cha ugomvi wake na Nyerere ni yeye kutaka kujenga Chuo Kikuu chini ya EAMWS. Sheikh Hassan bin Ameir hawezi kusema uongo. Wale ambao ni Waislam waliohusika katika fitna ile baadhi yao walikwenda Zanzibar kumwangukia sheikh na kutaka awasamehe. Hii khabari ni maarufu kwa Waislam wote wala haihitaji kuuliza kwingi.
 
LG: Hilo silikatai. Ninachosema ni kuwa historia iliwadharau wazee wetu na sisi tumeamua kuwarudishia heshima yao.
 
WANAUKUMBI: Nimeulizwa swali vipi Nyerere ampe medali Zuberi Mmanga Mwinshehe Mtemvu na yeye alitoka TANU? Niltoa jibu mashine ikakorofisha jibu limepotea. Sasa naeleza mambo yalivyokuwa kabla ya mtafaruku wa 1958 kupelekea wana TANU maarufu kama Ramadhani Mashado Plantan, Saleh Muhsin, Said Chamwenyewe, Zuberi Mtemvu na wengineo kujitoa TANU wengine kuanzisha Congress na wengine AMNUT.

Muhali mkubwa sana mimi kuona historia hii ya wazee wangu inapotoshwa na mimi nikae kimya. Kwa hili sina stahamala na yeyote.

Wataniwia radhi.

Nakubaliana nawe bwana Mohamed Said kuwa si vema hata kidogo kuvumilia historia ikipotoshwa. Na ninakushukuru kwa maelezo marefu na mazuri uliyotoa. Lakini katika yote, hujatuthibitishia kuwa dhulma hii waliyofanyiwa hawa waasisi inatokana na uislamu wao. Picha ninayopata hapa na hata kwenye kitabu chako ni ya watu walioshirikiana hapo awali kupigania uhuru, lakini wakaja kutofautiana kiitikadi hata wegine wakahama vyama na kuanzisha vingine, halafu wale waliopata utawala baada ya uhuru wakaamua 'kuwapuuza' ama kwa lugha ya siku hizi 'kuwapotezea' wale waliokuwa washirika wao awali. Haya yanatokea mara nyingi katika siasa, mimi pia nayapinga sana. Mtu kupingana nawe si sababu ya kufuta mazuri aliyoyafanya. Lakini ndugu yangu unaponichanganya ni pale unapodai ati hawa walitendewa haya ati kwa kuwa waislamu! Hili naendelea kusema si kweli hadi utakapoleta ushahidi dhahiri. Ni hoja ya kishabiki zaidi, ya kibaguzi, lakini kikubwa zaidi ni ya hatari maana inataka kujenga uadui kwa misingi ya kiimani, hasa kati ya waislamu na wakristo. Kama historia ilipotoshwa na kufuta mchango wa watu wengine walioshiriki kwa kuwa tu wametofautiana na watawala katika mitazamo ya kisiasa ni jambo la kukemewa na kurekebishwa. Lakini hata hili la kwako la kudai kuwa kupotoshwa huko kwa historia kulifanywa kwa visa vya chuki dhidi ya uislamu ilhali hakuna ushahidi wowote kuthibitisha, nalo pia ni la kukemewa sana na liachwe haraka.
 
Swadakta mkuu, couldnt have put it better!
 
FM: Mufti Sheikh Hassan bin Ameir alisema kuwa kisa cha ugomvi wake na Nyerere ni yeye kutaka kujenga Chuo Kikuu chini ya EAMWS. Sheikh Hassan bin Ameir hawezi kusema uongo. Wale ambao ni Waislam waliohusika katika fitna ile baadhi yao walikwenda Zanzibar kumwangukia sheikh na kutaka awasamehe. Hii khabari ni maarufu kwa Waislam wote wala haihitaji kuuliza kwingi.

Kwa nini asiweze kusema uongo? Ni kama vile unavyosema, hii habari nilisimuliwa na babu yangu au Abdulwahid kwa hiyo lazima mniamini! Katika akademia statements kama hizi hazina mshiko! EAMWS imekuwa ikipingwa hata kabla huo mpango wa kujenga Chuo Kikuu kutokea! Sasa unataka kutuambia kuwa kwa sababu hiyo habari ni maarufu kwa waislamu basi ndio kweli? Sisi tunachotaka ni hard facts, kuwa ni Nyerere ndiye aliyekuwa akiipinga EAMWS na sio wakina Abeid na Rashid.

Amandla.....
 
MALARIA SUGU: Baba yangu akiijua sana historia ya Dar es Salaam. Tukitembea njiani akikutana na mtu basi atanambia huyu mdogo wake Dossa unajua alikuwa na dada yake akiitwa fulani huyu alikuja olewa na fulani nk. tunakwenda njiani gumzo linanoga. Tena ajabu hakuna utakaemtaja yeye akawa hamjui. Hivi nami nikaja jua mengi sana kuhusu mji wa Dar es Salaam na historia yake.

Sikiza kihoja hiki: Mwaka 1988 nikamshauri Bwana Ally Sykes nikamwambia tumfanyie Bwana Abdu kumbukumbu katika magazeti tununue nafasi mimi nitaandika kitu. Wakati ule bado kitabu chake sijamaliza. Mwaka 1988 marehenu Abdu alikuwa anatimiza miaka 20 toka kufariki. Basi nikaandika kumbukumbu na kuipeleka Daily News na Uhuru. Katika kumbukumbu ile nimesema Abdu ndiyo muasisi wa TANU na kadi yake no. 3. Kadi No. 1 Julius Kambarage Nyerere, No. 2 Ally Kleist Sykes na Kadi No. 3 Abdulwahid Kleist Sykes. Kisha nikasherehesha na mengi alofanya katika jamii kama kuwa katika Aga Khan Education Committee, Baraza la Kiswahili nk. Daily News alikuwako Reginald Mhango yeye akifahamiana na Kleist (mtoto wa Abdu Sykes) walisoma wote Aga Khan School. Reginald Mhango akampigia simu Kleist usiku akitaka radhi kuwa hatoweza kutoa ile kumbukumbu ya baba yake hadi apate idhini kutoka ngazi za juu. Kleist akauliza kwanini iwe hivyo? Jibu alotowa Mhango ni kuwa, "Historia ya baba yako inagusa historia ya Tanzania kwa hiyo sitoweza kuitoa mpaka nipate idhini."

Siku ya pili ile kumbukumbu kwa bahati nzuri ilitoka katika Daily News na katika gazeti la Uhuru lakini yale yote maneno muhimu katika historia ya Abdu Sykes na mchango wake katika TAA hadi TANU yalifutwa. Ikawa ile kumbukumbu ni sawa na kumbukumbu ya mtu yoyote yule.

Mimi nikawa najiuliza hivi kinachoogopwa khasa ni nini?

Mpaka hapa mzee wangu nimesoma na nimekuelewa kabisa unavyojisikia, na nasema ni sahihi kabisa kujisikia hivyo kibinadamu. Lakini sijaona popote ushahidi kuwa dini ndiyo iliyotumika kuzuia hizo kumbukumbu nzuri ulizokusudia kuandikwa kwenye makala hiyo ya gazeti. Umeeleza tukio pengine la kweli kabisa, lakini sababu unazotoa za tukio hilo ndizo zinazonitia shaka, na ninaamini kwa dhati kuwa si za kweli. Mtafaruku baina ya waasisi hao wa TANU na watawala waliokuwepo enzi zao (ambao kabla walikuwa washirika wao katika mapambano), mtafaruku huo si wa kidini, narudia, hakuna ushahidi wowote wa kuhusisha mtafaruku huo na chuki dhidi ya uislamu. Hilo nakuomba sana urekebishe.
 
FM: Nimesoma fikra zako sidhani kama unataka nikujibu. Ikiwa utataka jibu nifahamishe na Insha Allah nitafanya hivyo.

Akina Sykes ni ndugu zangu na ninawependa sana. Ngoja nikupe kisa kimoja Ebby Abdulwahid Sykes tumepishana siku moja katika kuzaliwa kwetu. Kitanda alicholala mama yake Ebby akazaliwa Ebby akaja mama yangu siku ya pili akanizaa mimi.

Akina mama wakitoka kwa Bwana Abdu Stanley Street kumuona mzazi mama yake Ebby kisha wanakuja kwetu Kipata kumuona mama yangu. Kwa hiyo toka utoto mimi na Ebby mchezo wetu mmoja. Ni ndugu yangu khasa.

Juu ya hayo kitabu changu ukenda kwenye name index ndiyo itakupa picha ni biography ngapi ndogo ndogo ziko mle.

Lakini kubwa ni kumrehemu baba yangu Abdulwahid Kleist Sykes. Alipofikisha miaka 20 baada ya kifo chake nilimuandikia kumbukumbu katika Africa Events (London) September 1988 "Abdulwahid K Sykes (1924 - 1968) The Founder of a Political Movement"

Hii ndiyo makala iliyomliza Ahmed Rashad Ali rafiki yake Abdu Sykes ambae kwenye mazungumzo Abdu aliyofanya na Jomo Kenyatta Nairobi 1950 walikuwa wote.

Mwakilishi wa Library of Congress Tanzania aliifanyia cutting makala ile na iko katika catalogue hapo Washington DC.

Hizo zote hapo juu ni hadithi na hazijibu swali nililokuuliza. Kuwa Eddy ni ndugu yako haichangii lolote katika mjadala huu. Au kwamba Ahmed Rashad alilia! Ni hadithi nzuri lakini kwangu hazina tija. Lenye tija kwangu mimi ni hiyo heading ya article uliyoandika kumuenzi huyo unayedai kuwa ni baba yako. Kumuita THE Founder ni kurudia makosa yale yale unayowashutumu watu wa Kivukoni kufanya. Hakuna mahali ambapo panasema kuwa Abdulwahid Sykes PEKE YAKE ndiye aliyenzisha "Political Movement" yeyote. Kila mahali alishirikiana na wenzie!

Amandla......
 
Mkuu Lole inaonekana maudhui muhimu sana ya mada hii umeisahau, naomba nikukumbushe. Kwanza nashkuru sana kama umeanza kukubali kuwa hiyo historia inayoitoa Mohamed Said ina ukweli ndani yake.

Kinachopotoshwa ni kuwa Historia ya nchi hii imeandikwa tofauti na alivyoiandika Mohamed Said na katika kupotoshwa huku ndiko kunapozua maswali mengi ya msingi ambayo Mohamed Said anajaribu kuyafafanunua.

Cha muhimu zaidi kama hukubaliani na Historia aliyoandika Mohamed Said unatakiwa uje na ushahidi wa kumkosoa na ueleze wewe Historia yako unavyoifahamu.

Naomba kila tunapochangia tusisahau maudhui muhimu ya mada hii kuwa Historia ya nchi yetu iliyoandikwa na inayofundishwa mashuleni imepotoshwa na kuna watu muhimu sana katika Historia ya nchii hii wamesahauliwa.

Tuendelee kujadiliana ili kupata elimu na faida kwa watu wote.

Hilo nakubaliana nawe al Saidy. Nisichokubali ni dai la bwana Mohamed Said kuwa hao waliosahauliwa katika historia ati wamefanyiwa hivyo kwa kuwa ni waislamu. Hilo silikubali hadi uje ushahidi unaotosheleza, na kikubwa ni kuwa wapo wakristo na wengine wenye dini za jadi ambao nao pia walitengwa katika historia au kupewa majina ya wasaliti, maadui wa ujamaa nk. Kwa hiyo hili la kuelezea tofauti hii kwa msingi wa udini ndiyo upotoshaji wa dhahiri ambao unapaswa kukemewa kwa nguvu zote.
 
FM:"Hadithi" hazikusaidii wewe ukiwa unadhani kuwa humu ukumbini mimi nazungumza na wewe peke yako. La hasha si hivyo mimi nazungumza na watu wengi sana na hizo "hadithi" wao zinawafaa na wananiandikia na kunambia nizidi kama wasemavyo wenyewe "kutoa darsa." Hilo la kwanza la pili nasoma katikati ya mistari naona hamaki, dharau na kudhani labda mimi najipendekeza natafuta umaarufu hayo yote nimejibu kuwa mimi ni maarufu sihitaji kutafuta chochote kwa mtu sasa hapo ndipo ninapoeleza nimetokea wapi.

Kuna waliojinadi wao ni "wanasayansi" nami jibu mimetoa.

Nimekusihi sana usome kitabu jibu lako kwangu ukanambia ukumbi huu siyo wa "biashara." Mimi nina shida gani hata nije nitafute fedha hapa! Majibu ya fedhuli. Ungesoma kitabu ugelikuta kisa cha Chief Kidaha Makwaia na Abdulwahid Sykes. Mipango 1950 ilikuwa ni kumfanya Chief Kidaha President wa TAA kisha inaundwa TANU Kidaha anaongoza harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika. Hapa Abdu yuko peke yake? Labda nikufahamishe kuwa nilikutana na Chief Kidaha 1967 mwanae nikisomanae darasa moja.

Hivi hujui kwa nini Ahmed Rashad Ali alilia? Kwa nini huchukui tabu ya kudodosa? Ahmed Rashad Ali alikuwa Cairo akifanya kazi na Radio Free Africa. Abdulwahid alikuwa na Rashad pale Cairo, Abdu alikuwa anaelekea Ulaya ...Nyerere kaja katika mkutano wa All Africa Conference ulioitishwa na Gamal Abdel Nasser. Hapo palipitika mazungumzo kati ya Nyerere na Abdu...sina haja ya kuendelea...

Anasema Ahmed Rashad Ali, "Hujapata kumuona mtu karim kama Abdu...ungeyajua alomfanyia Nyerere machozi yangekutoka. Katika mazishi ya Abdu mimi nimekula sinia moja na Nyerere kwenye jamvi..." Mzee Rashad akifika hapo anamkumbuka rafiki yake machozi yanamwagika. "Leo Abdu hatajwi katika historia ya nchi hii na Nyerere kakaa kimya..." Mzee Rashad hakuwa anaweza kuendelea. Hii ikijirudia mara zote nikiwa kwake akinihadithia yale ya ndani katika kugombea uhuru wa Tanganyika.

HL mimi nawazungumzia wazee wangu mara elfu narudia kauli hii na wewe eleza habari za wazee wako. La kama huna historia hiyo ni bahati mbaya ndiyo majaaliwa yako.

HK uliza uelezwe. Ndipo utakapojuwa kwani kuuliza si ujinga. Sisi ukituchukulia historia hii ya ukombozi wa Tanganyika kutoka ukoloni unakuwa umetukata kichwa na ukikatwa kichwa mtu hana uhai.
 
Mkuu, Mohamed Said, naendelea kukubali wewe ni mwanazuoni mwenye kipaji cha oratorial, wewe ni orator, hadithi hii pia ni hadithi nzuri, endelea kutupigia hadithi, kama nilivyosema, mimi ni mpenzi wa hadithi, simulizi, tungo, nahau, mithali na tamathali za semi.

Paper hii uliyoiwasilisha Univesity of Nairobi, itafutie upenyo uiwasilishe UDSM, uone utakaposimama, uzuri wa wasomi ni uwezo wa kufanya critique analysis, uwasilishaji mada bila analysis nao pia ni simulizi vile vile.
Simulizi nzuri.
Maelezo hayo ya Pasco aliyatoa alipokuwa akimjibu Mohammed Said kuhusiana na paper aliyoiwasilisha Kenyatta University.
Baadhi ya vipande vilivyokuwemo humo na kumvutia Pasco ni kama ifuatavyo:
..What followed on Easter Monday was unprecedented in the history of Tanzania. After the
arrests of the imams the previous day at the Central Police, Muslims from all corners of
Dares Salaam assembled at the Mtoro Mosque to discuss their next step. Muslims were informed
that Sheikh Kassim bin Juma who was in Arusha enroute to Nairobi for medical treatment was
also arrested on orders of Augustine Mrema the Minister of Home Affairs
...Muslims totalling 70 were remanded at Ukonga Prison. They were denied food from home and medical attention. It was only after 11 Muslims fell seriously sick that the Ministry of Home Affairs allowed them medical attention.
....After his arrests Sheikh Kassim was detained at a military camp in Monduli, a few miles from Arusha town and was later flown back to Dar es Salaam under heavy escort. Sheikh Kassim was to reveal to his close confidants that his captors were under instructions to torture him. At the military camp in Monduli he was to witness many horrifying scenes. While in remand he was put under solitary confinement and denied medical attention.
...When the police raided the house of Sheikh Salum Rajab leader of the Ansar to search for bombs, they also arrested the three boys. All attempts by lawyers to ask the court to release them from remand pleading their innocence as victims of circumstances and for their tender age were refused.

Mtu mwenye kufurahishwa wakati waislamu wakitendewa kama hivyo, hawezi kufurahi pia wakitajwa kwa wema kama waasisi waliopigania uhuru wa Tanganyika.
 
FM:"Hadithi" hazikusaidii wewe ukiwa unadhani kuwa humu ukumbini mimi nazungumza na wewe peke yako. La hasha si hivyo mimi nazungumza na watu wengi sana na hizo "hadithi" wao zinawafaa na wananiandikia na kunambia nizidi kama wasemavyo wenyewe "kutoa darsa." Hilo la kwanza la pili nasoma katikati ya mistari naona hamaki, dharau na kudhani labda mimi najipendekeza natafuta umaarufu hayo yote nimejibu kuwa mimi ni maarufu sihitaji kutafuta chochote kwa mtu sasa hapo ndipo ninapoeleza nimetokea wapi.

Kuna waliojinadi wao ni "wanasayansi" nami jibu mimetoa.

Nimekusihi sana usome kitabu jibu lako kwangu ukanambia ukumbi huu siyo wa "biashara." Mimi nina shida gani hata nije nitafute fedha hapa! Majibu ya fedhuli. Ungesoma kitabu ugelikuta kisa cha Chief Kidaha Makwaia na Abdulwahid Sykes. Mipango 1950 ilikuwa ni kumfanya Chief Kidaha President wa TAA kisha inaundwa TANU Kidaha anaongoza harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika. Hapa Abdu yuko peke yake? Labda nikufahamishe kuwa nilikutana na Chief Kidaha 1967 mwanae nikisomanae darasa moja.

Hivi hujui kwa nini Ahmed Rashad Ali alilia? Kwa nini huchukui tabu ya kudodosa? Ahmed Rashad Ali alikuwa Cairo akifanya kazi na Radio Free Africa. Abdulwahid alikuwa na Rashad pale Cairo, Abdu alikuwa anaelekea Ulaya ...Nyerere kaja katika mkutano wa All Africa Conference ulioitishwa na Gamal Abdel Nasser. Hapo palipitika mazungumzo kati ya Nyerere na Abdu...sina haja ya kuendelea...

Anasema Ahmed Rashad Ali, "Hujapata kumuona mtu karim kama Abdu...ungeyajua alomfanyia Nyerere machozi yangekutoka. Katika mazishi ya Abdu mimi nimekula sinia moja na Nyerere kwenye jamvi..." Mzee Rashad akifika hapo anamkumbuka rafiki yake machozi yanamwagika. "Leo Abdu hatajwi katika historia ya nchi hii na Nyerere kakaa kimya..." Mzee Rashad hakuwa anaweza kuendelea. Hii ikijirudia mara zote nikiwa kwake akinihadithia yale ya ndani katika kugombea uhuru wa Tanganyika.

HL mimi nawazungumzia wazee wangu mara elfu narudia kauli hii na wewe eleza habari za wazee wako. La kama huna historia hiyo ni bahati mbaya ndiyo majaaliwa yako.

HK uliza uelezwe. Mimi

Sina sababu yoyote ya kupinga haya maelezo. Tatizo langu ni conclusion yako katika maandiko yako mengi kuwa kusahaliwa/kupuuzwa/kuondolewa katika historia rasmi kwa data hizi kunatokana na chuki dhidi ya uislamu. Hili ndilo hujatupatia ushahidi wake. Yalitokea kama ulivyosimulia, sawa nakubali, na nasema kama kweli watu walitendwa hivyo basi ni vibaya. Lakini sababu ya kutendwa hivyo unayotaja wewe ina utata, haina ushahidi, na inachochea chuki ambazo ninaamini haikuwapo wakati haya yanatokea. Wazee hawa waliudhika kuhusu hali hiyo, hilo ninaamini, lakini siamini kuwa hata wao walisema kuwa wamefanyiwa hayo sababu ya dini yao au hilo umeongeza wewe? Mbona wengine wenye dini hiyo aliendelea nao mwalimu hadi kifo chake, na tena siku chache kabla ya kifo chake akaagiza rafiki yake Rashidi Kawawa asimamie kukamilisha ujenzi wa msikiti aliouahidi kwa waislamu wa kijiji chake Nyerere cha Butiama? Na mbona hata wakristo wenzie aliwatenda hayo hayo? Nafurahi umemtaja chifu Kidaha Makwaia (Paul David majina yake ya kikristo), na unajua kuwa hata huyu alikuja kutengwa tu kama wenzie, akaishia kuwa katekista kanisani na masikini tu.

Narudia, hakuna yeyote kati ya wazee wako hao aliyefanyiwa dhulma kutokana na dini yake.
 
K: Umemtaja Kawawa. Nakutafadhalisha hebu soma hili pitio la kitabu chake Simba wa Vita labda itakusaidia kumjua vyema na kisha tutaendelea na mjadala. Hii niliweka hapa siku za mwanzo za mjadala lakini kwa faida ya wanaukumbi naiweka tena. Msome Simba wa Vita:

MAPITIO YA KITABU SIMBA WA VITA KATIKA HISTORIA YA TANZANIA RASHIDI MFAUME KAWAWA

Na Mohamed Said

Kwa mara ya kwanza Tanzania ilishuhudia kuandikwa kwa historia ya mmoja wa viongozi wakuu wake kupitia kitabu "Simba wa Vita Katika Historia ya Tanzania Rashidi Mfaume Kawawa" kilichoandikwa na Dk. John M. J. Magotti. Sidhani kama katika historia ya Tanzania kuna kumbukumbu ya kuandikwa kwa kitabu kinachohusu maisha ya kingozi yoyote achilia mbali kufanyika kwa sherehe ya kukizindua kitabu hicho Ikulu ikiongozwa na rais mwenyewe. Kwa hakika sherehe ilifana sana na tukakisubiri kwa hamu kitabu madukani ili tupate kunufaika na kumbukumbu za Mzee Kawawa.

Msomaji anaweza kukisoma kitabu chote chenye kurasa 127 kwa muda wa saa moja akawa kakimaliza chote na atakapokiweka chini akawa hakubakia na chochote cha maana katika fikra yake. Kwa nini iwe msomaji asibaki na kumbukumbu yoyote ya kiongozi mkubwa kama Mzee Kawawa mtu aliyeshuhudia kwa macho yake mwenyewe harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika na si hivyo tu yeye mwenyewe ni mmoja wa wale waliopigania uhuru wa Tanganyika na kushika nyadhifa kubwa za uongozi chini ya Mwalimu Julius Nyerere. Kwa kawaida vitabu vya maisha ya viongozi hasa wapigania uhuru huwa vina mambo mengi sana ambayo kwa muda mrefu huwa siri, hayafahamiki hadi hapo kitabu kitakapoandikwa ama kwa mkono wake kiongozi mwenyewe au kuandikwa na muandishi. Mifano ipo mingi. Kitabu kama "Mahatma Gandhi" klichoandikwa na Robert Payne au "Long Walk to Freedom" alichoandika Nelson Mandela mwenyewe au "Seeds of Freedom" alichoandika Bildad Kaggia hakika unapomaliza kusoma vitabu hivi lazima urudi nyuma kufungua kurasa hapa na pale kuzisoma upya zile sehemu zinasosisimua.

Huwezi kupata haya katika kitabu cha Mzee Kawawa. Huwezi kuyapata haya kwa kuwa mwandishi hakuandika kitu. Hakuandika kitu si kama Mzee Kawawa hana historia ya kusisimua na kuwa hana mengi ambayo wengi hawayajui katika maisha yake, nadhani mwandishi hakuwezakuja na jipya labda kwa sababu hakufanya utafiti wa kutosha kuweza kuandika kitabu kinachomuhusu simba wa vita aneunguruma. Kuna msemo wa Kiswahili usemao "Aungurumapo simba mcheza ni nani?" Kwa hakika simba wa vita hakuungurma kabisa katika kitabu hiki. Sijui lawama zielekezwe wapi.

Mimi simjui Mzee Rashidi Kawawa kwa kiwango cha kusema naweza kunyanyua kalamu na kufanya pitio la kitabu kilichoandikwa kuhusu yeye. Nathubutu kuandika kuhusu kitabu chake kutokana na kumjua kwangu mimi nikiwa kama mwandishi na mtafiti ambae katika kutafiti kwangu nimekutana na jina la Mzee Kawawa hapa na pale katika nyaraka zilizo katika hifadhi ya ukoo wa akina Sykes. Nitatumia uzoefu wangu huu kueleza yale niliyoyaona katika nyaraka hizi na ninayojua kuhusu Mzee Kawawa na kufanya tathmini kwa yale niliyoyasoma katika kitabu cha Magotti.

Miaka kama ishirini iliyopita nikiwa kijana mdogo nilipata hamu ya kuandika historia ya kudai uhuru wa Tanganyika. Sikuona mtu wa kumuendea isipokuwa Ally Sykes. Nilipomueleza kuwa nia yangu ni kuandika kitabu kuhusu marehemu kaka yake Abdulwahid Sykes (1924- 1968) Ally Sykes alinambia kuwa atanipa nyaraka zake zote nizipitie kisha ndiyo nakaenae chini kwa mahojiano ya ana kwa ana. Katika nyaraka alizonikabidhi ndani yake nilikuta barua ya mkono aliyoandika Rashid Kawawa mwaka 1952 kutoka Bukoba akimletea Ally Sykes aliekuwa Dar es Salaam. Barua hii ya Mzee Kawawa kwa Ally Sykes ilikuwa ikimfahamisha Ally Sykes hali ya siasa Kanda ya Ziwa. Hii barua hadi leo ipo katika nyaraka za akina Sykes. Nilipokaa na Ally Sykes kutaka maelezo ya barua ile aliyoandikiwa na Kawawa, Ally Sykes alinipa kisa hiki:

"Mwaka 1951 nilichaguliwa kuwa katibu mkuu wa Tanganyika African Government Servants Association (TAGSA). Chama hiki kiliundwa mwaka wa 1927 kwa lengo la kuendeleza maelewano mazuri baina ya serikali ya Malkia na sisi watumishi Waafrika. Rashid Kawawa alikuwa mwana kamati. Mimi nilichaguliwa pamoja na Thomas Marealle kama rais wa TAGSA. Katiba ya TAGSA iliamuru uchaguzi wa kila mwaka, na mimin nilirudishwa madarakani kama katibu mara nne hadi Oktoba, 1954 nilipojiuzulu baada ya kuhamishwa kwenda Korogwe kama adhabu kwa kuwa miongoni mwa wale wanachama 17 waliounda TANU. Watu kadhaa walishika urais. Stephen Mhando na Dr Wilbard Mwanjisi wote hao waliwahi kuchaguliwa kuwa marais wa TAGSA. Miongoni mwa wanachama watendaji wa TAGSA walikuwa Dr Michael Lugazia na Rashid Kawawa ambao alichaguliwa kuwa katibu baada ya mimi kujiuzulu. Kupitia TAGSA, Kawawa alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Tanganyika Federation of Labour (TFL).

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa ulipokuja kuzuru Tanganyika Agosti, 1951 kwa mara ya tatu, vyama vyote viwili, TAA na TAGSA, viliwakilisha malalamiko kwa ujumbe huo. TAGSA iliwakilisha malalamiko yake kuhusu ubaguzi katika utumishi serikalini kwa mujibu wa kupanga mishahara kufuatana na rangi ya ngozi. Mshahara wa Mwafrika ulikuwa wa chini zaidi kuliko ule aliokuwa akipokea Mzungu au Muasia kwa kazi hiyo hiyo. Kwa mfano Mwandishi wa hati mkato Mzungu alikuwa akipata mshahara mkubwa kuliko Mwafrika aliyekuwa na shahada au digrii kutoka chuo Kikuu cha Makerere. TAGSA vilevile tulilalamika kuhusu kuajiri makarani wa kutoka India na hali walikuwepo Waafrika kutoka Afrika ya Mashariki na Nyasaland ambao wangeweza kujaza nafasi hizo kwa urahisi.

Vyama vyetu hivi viwili TAA na TAGSA viliwakilisha malalamiko haya tukifahamu fika kwamba Uingereza ilikuwa ikiitawala Tanganyika chini ya vifungu nambari 76 na 77 vya Umoja wa Mataifa ambavyo viliwekwa ili kuendeleza maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ya nchi zilizokuwa chini ya udhamini. Kama mdhamini Uingereza ilitakiwa kuhimiza na kuheshimu haki za binadamu na uhuru wa kwa wote bila kubagua kwa misingi yajinsia, lugha au dini. Lakini Uingereza ilikuwa ikipuuza vifungu hivi bila aibu. TAGSA tuliwakilisha malalamiko haya ili Umoja wa Mataifa ujue matatizo halisi ya ukoloni nchini Tanganyika.

Mimi nikiwa katibu wa TAGSA nilifuatilia serikalini masuala yaliyoainishwa ndani ya malalamiko yetu. Suala lililokuwa likituhangaisha sana wakati ule ilikuwa uajiri wa Wahindi kutoka India, jambo ambalo niliieleza serikali halikuwa na faida, maadam kulikuwako na Waafrika ndani ya nchi ambao wangeweza kujaza nafasi zile. Jambo hili lilikuwa likisababisha manugíuniko makubwa miongoni mwa Waafrika. Hakuna majibu maridhawa yaliyopatikana kutoka kwa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa. Barua tulizoandika serikalini juu ya masuala hayo zilipuzwa na Chief Secretary, Bruce Hutt. Katika kufuatilia malalamiko haya, Niliandika barua moja kali sana na kwa mara ya kwanza bila kutafuna maneno niliuliza uhalali wa Waingereza kututawala Waafrika wa Tanganyika. Nillimwambia Katibu Mkuu kuwa kwa kuwa serikali imeshindwa kupata ufumbuzi kwa matatizo ya Waafrika, Uingereza lazima ijitoe Tanganyika na Umoja wa Mataifa utawale Tanganyika. Barua hiyo ilimkasirisha Katibu Mkuu na siku chache baadaye nilipokea barua kutoka serikalini iliyokuwa imejaa vitisho, dharau, stihizai na makemeo. Nikajibiwa kuwa hakuwa na suala la Umoja wa Mataifa kutekeleza utawala wa moja kwa moja Tanganyika.

Dkt Mwanjisi alikuwa amegusa suala nyeti sana kwa kuzungumzia matatizo ya ubaguzi wa rangi uliokuwa ukitukabili Waafrika wa . Kawawa, kama mjumbe wa kamati, akaniandikia barua akanitahadharisha nisichapishe ile hotuba ya Dkt Mwanjisi katika jarida la TAGSA bila idhini ya kamati ya utendaji. Kufuatia majibishano haya kati ya TAGSA na serikali, Dkt Mwanjisi kama alivyofanyiwa Dk Kyaruzi kabla yake, akahamishwa kutoka hospitali ya Sewa Haji mjini Dar es Salaam hadi Kingolwira Prison Hospital karibu na Morogoro. Kawawa na yeye akapewa uhamisho kwenda Bukoba na mimi nikapewa uhamisho kwenda Mtwara. Dk Mwanjisi na Kawawa walikubali uhamisho wao na wakaondoka Dar es Salaam. Mimi nilikataa uhamisho na nikabakia Dar es Salaam kupinga uhamisho wangu."

Alipokuwa Bukoba ndipo Kawawa akamwandikia Ally Sykes barua ile ya mwaka 1952 akimweleza hali ya siasa kama alivyoikuta Kanda ya Ziwa. Huyu ndiye Kawawa niliyemjua mimi kupitia nyaraka na mahojiano na Ally Sykes. Kwa kweli inasikitisha kuwa Dk Magotti hakupata fursa ya kuziangalia nyaraka hizi muhimu sana katika siyo historia ya Kawawa bali katika historia ya kuundwa kwa TANU na kudai uhuru wa Tanganyika. Endapo angepata nafasi ya kuziona hizi nyaraka zingempelekea katika kuwajua wazalendo wengine waliotajwa mle ndani kama Dk. Kyaruzi, Dk. Wilbard Mwanjisi ambao Kawawa alikuwanao katika harakati za TAGSA. Katika majina hayo angeweza kudodosa mengi kutoka kwa Mzee Kawawa na hivyo kuandika yale ambayo hayafahamiki kwa wengi. Hii imgekifanya kitabu kiwe cha maana.

Mathalan Kawawa angeeleza mtafaruku kati ya Mwalimu Nyerere na Dk. Mwanjisi nini chanzo chake na nini ikajakuwa matokeo yake. Halikadhalika angempa fursa Mzee Kawawa kumuhadithia mchango wa Dk. Michael Lugazia katika kuasisi kwa TANU hasa kipindi kile cha 1953 wakati TAA ilipokuwa inatayarisha rasimu ya katiba ya TANU. Kwa ufupi ni kuwa Dk Lugazi alikuwa akijaribu kuamsha ari ya TAA Bukoba ari iliyokufa kutokana na kufungwa kwa kiongozi wa TAA Bukoba Ali Migeyo. Kisa cha Ali Migeyo ni moja ya visa vinavyosikitisha sana katika historia ya Tanganyika kwani aliwekwa kizuizini na Mwalimu Nyerere kama alivyofungwa na Waingereza. Haiwezekani kuwa Kawawa asiwe na habari na kile kilichopelekea mpigania uhuru hodari kama Ali Migeyo aishie jela tena wakati nchi ikiwa huru. Migeyo alifungwa na wakoloni kwa kuwahamasisha Watanganyika kudai uhuru labda Mzee Kawawa angeulizwa angeeleza ni nini kilitokea wakaamua kumfunga Migeyo kama walivyomfunga Waingereza.

Kitabu kimegusia kazi alofanya Kawawa kama mtumishi wa serikali ya kikoloni katika kambi za raia wa Kenya walioshukukiwa kuwa ni Mau Mau. Katika hawa wafungwa walikuwawepo wananchama wa TANU ingawa hawa walikuwa Wakenya. Maarufu katika hawa alikuwa Dome Okochi Budohi (ambae kadi yake ya TANU ilikuwa na 6) na Patrick Aoko. Budohi alicheza senema pamoja na Kawawa iliyoitwa "Wageni Wema." Kawawa na Budohi walikuwa wakifahamiana vizuri sana kwa sababu wote walikuwa wasanii. Budohi alikuwa mmojawapo katika bendi ya vijana wa mjini iliyojulikana kama Skylarks. Bendi hii baadaye ilibadilisha jina na kuitwa Blackbirds. Matangazo ya radio yalipoanza Tanganyika, Blackbirds midundo ya Blackbirds ilikuwa haikosekani kusikika radioni katika Sauti ya Dar es Salaam. Kawawa kama walivyo vijama wote wa Dar es Salaam wa wakati ule alikuwa mmoja wa wapenzi wa bendi hii na alikuwa hakosekani Ukumbi wa Arnatouglo bendi hii ikitumbuiza katika ile miaka ya 1950. Ilikuwa katika ule upigaji muziki wa Budohi ndipo alipoungana na Kawawa katika kutengenezwa kwa senama hiyo ya "Wageni Wema" ambayo mwandishi kaitaja lakini aliishia hapo tu.

Budohi na Aoko ni kati ya wafungwa wa Mau Mau waliokuwa Handeni ambako Kawawa alikuwa na jukumu la kuwaangalia. Budohi ndiyo alikuwa mtu wa kati baina ya TAA na KAU na kuanzia hali ya hatari ilipotangazwa Kenya mwaka 1952 Budohi na Aoko wakawa katika jicho kali la makachero. Makachero hawa Waafrika wanafahamika na wengine walikuja kufanya kazi hiyohiyo katika Tanganyika huru. Hiki ndicho kipindi ambacho Kaimu Rais wa TAA na Katibu wa TAA Abdulwahid Sykes alipokutana na Kenyatta Nairobi. Wakati Wakenya hawa wanafungwa Tanganyika, viongozi wa KAU akina Bildad Kaggia, Jomo Kenyatta, Kun'gu Karumba, Achieng Oneko, Paul Ngei na Fred Kubai walikuwa wamekamatwa Kenya. Kawawa ni mmoja kati ya viongozi hawa na ingependeza sana kama kupitia kwake tungeelezwa jinsi KAU na TAA ilivyokuwa ikishirikiana kwani haiwezekani kuwa Budohi na Kawawa uswahiba wao ukaishia kwenye kucheza senema tu.

Wanaharakati wote walishtushwa na kutiwa mbaroni kwa Budohi na Aoko. Haiwezekani kuwa iwe Mzee Kawawa kasahau matukio haya muhimu. Budohi na Aoko walikuwa wamefungwa minyororo walipokuwa katika selo pale Kituo cha Kati cha Polisi kwa sasa jumba hilo liko kituo cha mabasi kinachojulikana kama "station." Waliwekwa pale kwa miezi sita muda wote wakiwa na minyororo miguuni. Waliwekwa pale kwa miezi sita wakihojiwa kabla hawajapelekwa Handeni walipomkuta Kawawa. Hivi ndivyo vitu ambavyo kwa hakika vingeongeza ladha ya kitabu cha Mzee Kawawa endapo mwandishi angechukua muda kutafiti na kuzungumza na watu waliokuwa katika harakati wakati ule ambao bado wa hai kama Ally Sykes na mdogo wake Balozi Abbas Sykes na wengine wengi ambao walikuwepo wakati ule kama Mzee Chipaka.

Katika migomo ya wakati wa kudai uhuru hakuna mgomo uliofanikiwa na kuvuta hisia za wananchi kama mgomo wa reli wa mwaka 1960 uliodumu kwa siku 82. Ukiachia kutajwa tu kama sehemu ya historia undani wake na jinsi mipango yake ilivyokwenda na nafasi ya viongozi wa Tanganyika Railway African Union (TRAU) walivyopata misaada kutoka nchi za Mashariki hivi havijawekwa wazi. Si treni, meli wala mabasi ya railway yaliyotembea kwa mieizi mitatu. Mipango ya mgomo huu ilifanyika Tabora ambako ndiko palikuwa na karakana kuu ya reli na hapo ndipo palipokuwa makao makuu ya viongozi wa TRAU, Salum Abdallah mwenyekiti na Kassanga Tumbo katibu. Kawawa ana mengi katika kadhia hii kwa kuwa yeye wakati ule ndiye alikuwa Katibu Mkuu wa TFL. Inasemekana mgomo huu miezi michache kabla Tanganyika haijapata uhuru ndiyo ilikuwa kama zinduo kwa Mwalimu Nyerere kutambua kuwa hakuwa peke yake na sauti kwa wananchi. Walikuwapo viongozi wengine pembeni yake ambao nao wakipiga wananchi wanacheza. Ilimdhihirikia kuwa huko mbeleni wanakokwenda ipo siku atapambana na viongozi hawa. Hivyo ndivyo ilivyotokea.

Inasemekana Mwalimu Nyerere akimtumia Kawawa alianza mipango kabambe ya kujitayarisha hilo lisitokee. Hii ilikuwa nukta muhimu sana kwani haukupita muda baada ya uhuru kupatikana mwaka wa 1961 viongozi hawa wa vyama vya wafanyakazi wakajikuta wamewekwa kizuizini. Wasomaji wangependa kujua Kawawa alijihisi vipi wakati viongozi wenzake wa vyama vya wafanyakazi aliofanya nao kazi wakati wa kudai uhuru wakishirikiana na TANU kama Victor Mkello, Paul Pamba, Abdallah Mwamba, Hassan Khupe, Salum Abdallah na wengine wengi walipokamatwa mwaka wa 1964 na kuwekwa kizuizini kwa amri ya Mwalimu Nyerere. Maelezo ya Mzee Kawawa katika mambo haya yangetia mwanga katika yale mengi yasiyofahamika katika historia ya Tanzania.

Waislam wangependa sana kujua hisia za Kawawa kama muumini alihisi vipi wakati makachero walipomvamia mzalendo aliyepigania uhuru wa Tanganyika Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Amir usiku wa manane na kumrudisha Zanzibar na kuwekewa masharti kuwa hana ruhusa kurejea Tanzania Bara. Nilitegemea kusoma sakata zima la kukamatwa kwa Sheikh Hassan bin Amir na kuvunjwa kwa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) jumuia ya Waislam iliyokuwa ikipanga kujenga Chuo Kikuu Dar es Salaam.

Nilitegemea halikadhalika kusoma mchango wa Mzee Kawawa katika kuunda Bakwata. Mengi yamesemwa kuhusu hujuma hii kwa Waislam moja wapo ni kuwa EAMWS ilivunjwa kwa shinikizo la Kanisa Katoliki likimtumia Mwalimu Nyerere. Hili si jambo la siri tena tafiti mbalimbali zimefanywa na vitabu kuandikwa na waandishi kutoka nje ya Tanzania kuhusu tatizo hili la kujitokeza udini mapema baada ya uhuru kupatikana. Kwa kuwa Kawawa alikuwa pamoja na Mwalimu Nyerere na alishiriki katika kuunda Bakwata wananchi hasa Waislam wangenufaika kusoma hisia zake wakati maamuzi hayo yanapitishwa na serikali. Kwa hakika kuna maamuzi mengi sana ambayo Kawawa alishiriki yaliwaumiza sana Waislam katika juhudi zao za kujitafutia elimu. Waislam wangependa sana kujua ni kipi kilikuwa kinamsukuma kufanya vile.

Kwa yeyote atakaepata bahati ya kusoma kitabu cha maisha ya Mzee Kawawa ni wazi hatakuta jipya ambalo hakuwa akilijua kabla. Kwa ajili hii basi mlango bado uko wazi kwa watafiti wengine kuandika kitabu kuhusu Rashidi Mfaume Kawawa kwani maisha ya Mzee Kawawa bado hayajaandikwa. Hata hivyo tumpongeze mwandishi kwa kazi hii kwani ni baada ya yeye kutuandikia kitabu ndipo nasi tumepata nguvu ya kunyanyua kalamu zetu na kusema.

3rd January 2010
 
AMI: Nacheka peke yangu wallahi. Nilipomwambia kuwa hao wasomi alionitishanao wa UDSM wawili wamenakili paper yangu moja na kuifanya yao word to word na kitabu kimechapwa na REDET. Hajasema kitu. Nilidhani atakuja mtu kusema walimu wa UDSM wananakili "hadthi" za Mohamed Said.

Hilo kama halitoshi wanawakataza wanafunzi kufanya rejea kutoka kitabu changu. Sikujua kama hawa watu dhalili kiasi hiki. Ajabu ya Rahman.

Wao wameandika historia ya TANU wazee wetu wamewatoa na hatujakataza wanetu kusoma vitabu hivyo. Kila uchao miaka nenda miaka rudi ndiyo historia wanayosomeshwa sisi kimya. Leo tunawapa ukweli wanapiga vita kitabu.

Ama kweli haki imeingia na batili ni yenye kutoweka.
 
Tufike mahali
Tufike mahali tukubali kwamba MTanzania yeyote ni ndugu yangu
Tufike mahali tukubali kujenga umoja, na kulikuwepo na dhamira ya makusudi ya kuvunja mishikamano ya kiasili kama dini, kabila, rangi
Tufike mahali tukubali kuwa katika kujenga umoja haki za vikundi, jamii nyingi tu zilivunjwa
Tufike mahali tukubali kuwa tupende tusipende waTanzania wote licha ya rangi, dini, kabila ni ndugu
Tufike mahali tukubali kuwa waTanzania waIslamu na waTanzania waKristo na waTanzania waHindu na waTanzania wasio na dini ni ndugu
Tufike mahili tukubali kuwa utengano ni udhaifu baina ya waTanzania wote na mshikamano ni nguvu
Tufike mahali tukubali kuwa nguvu ya waTanzania wote ndio nguvu ya maendeleo
Tufike mahali tusikubali kutenganishwa katika tofauti za imani zetu
Tufike mahali tusiyakweze yale yanayo leta mtafariku katika jamii yetu
Tufike mahali tusipuuze yale yanayotutenganisha kama waTanzania
Tufike mahali tukubali kuwa sisi ni waTanzania tunaweza
Tufike mahali tukubali kuwa sisi waTanzania, YES WE CAN.
Unfortunately sometimes dreams can be elusive!
 
LG: Mngekuwa mnayajua hayo msingetuwekea vikao Ikulu Nyerere na Maaskofu kutuhujumu. Mngekuwa mnayajua hayo msingeigeuza Wizara ya Elimu Jimbo la Kanisa Katoliki. Mngekuwa mnayajua hayo Kanisa Katoliki lisingekuwa na Kamati ya Majeshi.

Nyerere kaja Dar es Salaam mgeni mno akijuana na wale tu alokuwanao Makerere. Kapokelewa na marehemu Abdulwahid Sykes akalala nyumbani kwake na kuondokea hapo kwenna Musoma kufunga ndoa na Mama Maria. Karudi Dar es Salaam wamishonari wamemlazimisha aache kazi. Kakaa nyumbabi kwa Abdulwahid Mtaa wa Stanley (sasa Aggrey). Abdu kamfahamisha kwa Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, wazee wa mji na vijana wote waliokuwa kwenye harakati.

Ijaza aliyowalipa ni Sheikh Hassan bin Ameir kumtumia makachero kumkamata usiku wa manane kumrudisha Unguja na kuvifungia vyama vyote vya Kiislam ha Abdulwahid kumfuta kwenye historia. Mfano mzuri wa hili ni kama vile Rais Kikwete kuwatuma makachero wakamkamate Kadinali Pengo.

Sisi hatujambagua yeyote yule historia hii niliyoandika shahidi. Kama una ushahidi wa Waislam kuweka vikao vya kuwahujumu Wakristo ulete ushahidi hapa ukumbini.

Sisi ni watu wa subra tuchunguzeni mtatufahamu. Juu ya matusi na kejeli sikupatapo kurejesha kejeli kwa kejeli au tusi kwa tusi.

Tuendelee na mjadala.

Ila kaeni mkijua huwezi kuikomoa ardhi kwa kuikanyaga, Maalim Haruna akituambia.
 
FM:"Hadithi" hazikusaidii wewe ukiwa unadhani kuwa humu ukumbini mimi nazungumza na wewe peke yako. La hasha si hivyo mimi nazungumza na watu wengi sana na hizo "hadithi" wao zinawafaa na wananiandikia na kunambia nizidi kama wasemavyo wenyewe "kutoa darsa." Hilo la kwanza la pili nasoma katikati ya mistari naona hamaki, dharau na kudhani labda mimi najipendekeza natafuta umaarufu hayo yote nimejibu kuwa mimi ni maarufu sihitaji kutafuta chochote kwa mtu sasa hapo ndipo ninapoeleza nimetokea wapi.
Najua kuwa hapa wanasoma wengi ndio maana nasema kuwa "simulizi" zako hazina mshiko kwa maana haujazifanyia utafiti wa kutosha na hii inafanya conclusions zako ziwe na walakin. Unachukua maneno ya upande mmoja na kutaka sote tuamini kuwa ndivyo ilivyokuwa kwa sababu tu ya uhusiano wako nao kijamii au kidini. Kwa mfano kuna mahali ulidai kuwa waliokuwa nyuma ya mgogoro wa ardhi ya wameru walikuwa waislamu wakina Kandoro na Sykes bile kumtaja mkristu Japhet Kirilo. Nilipokuuliza na kukwambia kuwa, hapana, mtu aliyeenda New York kusimamia kesi ya mgogro huo alikuwa Kirilo na ni yeye ndiye aliyezunguka nchi nzima pamoja na hao uliowataja, ukasema kuwa ulienda Arusha kumtafuta Kirilo ukiongozana na Abduu na kunitajia mpaka gari mlilopanda kwenda kule lakini hamkumkuta maana alikuwa ameenda Nairobi. Mtafiti mahairi anayetaka ukweli angerudi tena au hata kumtafuta Mzee Kirilo kwa simu! Umetusimulia hotuba ya Kighoma Malima halafu ukadai kuwa ndiye yeye aliyeleta taratibu ya kutumia namba katika mitihani ya darasa la saba ili kuzuia ubaladhuli wa wakristu. Ulipopingwa na kuelezwa kuwa wengi tu wamefanya mitihani hiyo KABLA ya Kighoma Malima kuwa waziri, umekaa kimya. Nilitumaini ungetuambia kama wewe katika mtihanio wako wa darasa la saba (au nane) uliandika jina lako na sio namba na kwa sababu hiyo wakristu waovu walikufelisha! Umetoa statistics zikionyesha uwiano wa dini katika bunge letu na kudai kuwa zinaonyesha kuwawabunge wakatoliki ni 75% ya bunge. Nilipochukuwa statistics zako na kukuonyesha kuwa tofauti na unavyosema, zinaonyesha kuwa wislamu ni majority katika hilo bunge , umekaa kimya! Na mifano kama hii iko mingi. Unapobanwa unachukuwa kurasa nzima hata kama haiendani na kilichoulizwa na kuibandika hapa. Au unatupa hadithi ambayo unatuambia ulisimuliwa peke yako. Hadithi hizo ni nzuri na zinafurahisha lakini hazitoshi.

Mwenye dharau ni wewe, Mkuu. Umezoea kusifiwa na watu kupokea kila unachosema kama vile wewe ni malaika fulani. Unapopingwa unadai kuwa ati unadharauliwa na lugha ya kukejeliwa. Wewe kama umewahi kufanya presentation katika midahalo ya kimataifa ambayo ni diverse na sio ya waislamu wenzako, ungetambua kuwa vigorous criticism ni course for par! Ukiweka kitu hadharani ni lazima atatokeza mtu kupinga na kudai uthibitisha na kuonyesha mapungufu yake. Ni kama vile wewe unavyochambua historia iliyoandikwa na watu wa Kivukoni basi na wewe vile vile kitabu chako kitachambuliwa. Ndivyo ilivyo. Wewe unaonyesha dharau kubwa kwa kutufanya kama watoto wadogo ambao umekuja kutufungulia macho!

Mimi naona kwa mtu ambae anajifanya kuwa ni mnyenyekevu suala la umaarufu umeliweka mbele mno. Kuwa wewe ni mtoto wa mjini, kuwa wewe ni ndugu wa watu maarufu, kuwa wewe unakaribishwa na vyuo vikuu vikubwa vikubwa ( nilikuhoji kuhusu hili na mpaka sasa haujanijibu) n.k. n.k. Yote hayo hayana maana hapa. Hapa tunaangalia hizo video zako na maandishi ayako unayoyaweka na tunayajibu ipasavyo. Mimi nimekulia Dar es Salaam na mbona sikujui? Au umaarufu wako ni kwa wenzako wenye dini yako tu?

Umezoea kusifiwa na hao wanaokuomba uwapedarasa bila kupingwa au kuambiwa u-substantiate allegations zako.

Kuna waliojinadi wao ni "wanasayansi" nami jibu mimetoa.

Nimekusihi sana usome kitabu jibu lako kwangu ukanambia ukumbi huu siyo wa "biashara." Mimi nina shida gani hata nije nitafute fedha hapa! Majibu ya fedhuli. Ungesoma kitabu ugelikuta kisa cha Chief Kidaha Makwaia na Abdulwahid Sykes. Mipango 1950 ilikuwa ni kumfanya Chief Kidaha President wa TAA kisha inaundwa TANU Kidaha anaongoza harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika. Hapa Abdu yuko peke yake? Labda nikufahamishe kuwa nilikutana na Chief Kidaha 1967 mwanae nikisomanae darasa moja.
Mimi sijui kama una shida ya pesa au la. lakini hii kusisitiza kuwa hauwezi kujadiliana na mtu hadi huyo mtu asome kitabu chako kunanitia wasiwasi. Unataka kuniambia kuwa unapoenda kwenye hizo kongamano za kimataifa, haumjibu mtu mpaka akuhakikishie kuwa amesoma kitabu chako? Si mara nyingi unajibiwa kwa yale unayowaelezea? Kitabu chako si msahafu kiasi kuwa bila kukisoma basi mtu hauwezi kujua ukweli wa historia yetu. Ni kitabu kimoja tu katika vingi.

Wewe ( sio mimi ) ndiye uliyemuita Sykes THE Founder of Political Movements. Au haujui maana yakutumia neno "THE"? Kama ulijua kuwa alikuwepo mwingine, hata mmoja tu usingetumia neno hilo. Huu ni uthibitisho mwingine wa upotoshaji wa makusudi unaoufanya. Kama ulijua kuwa Chief Kidaha Makwaia alihusika pia katika kuanzisha TANU ( kitu ambacho si kweli, maana hawakuwa peke yao hawa) kwa nini basi ulimuita Sykes THE FOUNDER ... kama vile alikuwa peke yake barabarani akielekea Damascus?

Hivi hujui kwa nini Ahmed Rashad Ali alilia? Kwa nini huchukui tabu ya kudodosa? Ahmed Rashad Ali alikuwa Cairo akifanya kazi na Radio Free Africa. Abdulwahid alikuwa na Rashad pale Cairo, Abdu alikuwa anaelekea Ulaya ...Nyerere kaja katika mkutano wa All Africa Conference ulioitishwa na Gamal Abdel Nasser. Hapo palipitika mazungumzo kati ya Nyerere na Abdu...sina haja ya kuendelea...

Anasema Ahmed Rashad Ali, "Hujapata kumuona mtu karim kama Abdu...ungeyajua alomfanyia Nyerere machozi yangekutoka. Katika mazishi ya Abdu mimi nimekula sinia moja na Nyerere kwenye jamvi..." Mzee Rashad akifika hapo anamkumbuka rafiki yake machozi yanamwagika. "Leo Abdu hatajwi katika historia ya nchi hii na Nyerere kakaa kimya..." Mzee Rashad hakuwa anaweza kuendelea. Hii ikijirudia mara zote nikiwa kwake akinihadithia yale ya ndani katika kugombea uhuru wa Tanganyika
Kumbe aliliia akimkumbuka rafiki yake kipenzi! Hivi mlitaka Nyerere afanye nini? Yeye hakuandika kile kitabu mnachodai kuwa kimedharau Sykes. Sijawahi kumsikia Nyerere hata siku moja akikipigia debe kitabu hicho. Mzee Rashad kama mtu mwiingine yeyote alikuwa na haki ya kufanya ulichofanya wewe, kusahihisha mapungufu hayo kwa kuandika kitabu. Kulia kwake hakusaidii kitu bali kuandika kwake kungetusaidia wote.

Hivi wewe ambae umechukua jukumu la kutuandikia masahihisho hayo, kitabu chako kimepigwa marufuku? Umewahi kutiwa ndani kutokana na maandishi yako?

HL mimi nawazungumzia wazee wangu mara elfu narudia kauli hii na wewe eleza habari za wazee wako. La kama huna historia hiyo ni bahati mbaya ndiyo majaaliwa yako.
Hakuna mtu anayekukataza kuwaenzi wazee wako kwa kandika waliyokusimulia. Tatizo ni pale unapotaka kutulazimisha kuwa simulizi zao ni ukweli wetu sote. Hii haikubalik hata kidogo. Ndiyo maana umeambiwa kuwa ulichoandika hakiendani na title ya kitabu chako.

Amandla........
 
AMI: Nacheka peke yangu wallahi. Nilipomwambia kuwa hao wasomi alionitishanao wa UDSM wawili wamenakili paper yangu moja na kuifanya yao word to word na kitabu kimechapwa na REDET. Hajasema kitu. Nilidhani atakuja mtu kusema walimu wa UDSM wananakili "hadthi" za Mohamed Said.

Hilo kama halitoshi wanawakataza wanafunzi kufanya rejea kutoka kitabu changu. Sikujua kama hawa watu dhalili kiasi hiki. Ajabu ya Rahman.

Wao wameandika historia ya TANU wazee wetu wamewatoa na hatujakataza wanetu kusoma vitabu hivyo. Kila uchao miaka nenda miaka rudi ndiyo historia wanayosomeshwa sisi kimya. Leo tunawapa ukweli wanapiga vita kitabu.

Ama kweli haki imeingia na batili ni yenye kutoweka.

Cha msingi hapa ni je anayosema ni uongo? Kuwa hao wote hawakuhusika katika jitihada za kugombea uhuru? Kama Mwakikagile amenakili kazi yako na yote alioyaandika yamo kwenye kitabu chako basi huu si ushahidi tosha kuwa hata wewe unajua kuwa walihusika wengi katika kudai uhuru na sio waislamu au wakina Sykes au wazee wako peke yako? Kama ukweli huu unaujua na umeuandika kwenye kitabu chako kwa nini basi kwenye mihadhara yako hausemi hivyo bali unashikilia kuwa ni waislamu PEKE YAO ndio waliohusika katika mpambano huo na wakristu walibebwa tu? Na kama Mwakikagile amenakili kazi yako bila kukutaja kwa nini basi usimpleke kwa Pilato maana plagiarism ni kosa kubwa sana!! Lakini kama amekunukuu na kukutaja, hiyo ni kawaida katika uandishi kama wewe mwenyewe jinsi ulivyonukuu kazi za wengine. Mimi nimekuambia tangu mwanzo kuwa maandishi yako yanakushitaki maana humo humo una-refute haya unayoyasema hadharani kwa wale ambao ni wavivu wa kufikiri.

Amandla.......
Mtu mzima kuwa muongo wala haipendezi. Unasema sikukujibu na hii hapo juu nilikuwa namjibu nan na ninii? Si nilikuuliza kama kweli wakina Mwakagile wamenukuu paper zako verbati basi wanachosema ni kweli hata kama waliupata ukweli huo kwa njia ya udanganyifu? Na kama ni kweli basi hayo maneno yao ( ambayo unasema ni ya kwako) yanapinga hoja yako kuwa ni waislamu peke yao wakiongozwa na wakina Sykes ndio waliokuwa vinara katika kugombea uhuru wa nchi yetu. Tofauti na unavyotaka tuamini, ni wewe unaekacha kujibu maswali!

Amandla......

Najua kuwa hapa wanasoma wengi ndio maana nasema kuwa "simulizi" zako hazina mshiko kwa maana haujazifanyia utafiti wa kutosha na hii inafanya conclusions zako ziwe na walakin. Unachukua maneno ya upande mmoja na kutaka sote tuamini kuwa ndivyo ilivyokuwa kwa sababu tu ya uhusiano wako nao kijamii au kidini. Kwa mfano kuna mahali ulidai kuwa waliokuwa nyuma ya mgogoro wa ardhi ya wameru walikuwa waislamu wakina Kandoro na Sykes bile kumtaja mkristu Japhet Kirilo. Nilipokuuliza na kukwambia kuwa, hapana, mtu aliyeenda New York kusimamia kesi ya mgogro huo alikuwa Kirilo na ni yeye ndiye aliyezunguka nchi nzima pamoja na hao uliowataja, ukasema kuwa ulienda Arusha kumtafuta Kirilo ukiongozana na Abduu na kunitajia mpaka gari mlilopanda kwenda kule lakini hamkumkuta maana alikuwa ameenda Nairobi. Mtafiti mahairi anayetaka ukweli angerudi tena au hata kumtafuta Mzee Kirilo kwa simu! Umetusimulia hotuba ya Kighoma Malima halafu ukadai kuwa ndiye yeye aliyeleta taratibu ya kutumia namba katika mitihani ya darasa la saba ili kuzuia ubaladhuli wa wakristu. Ulipopingwa na kuelezwa kuwa wengi tu wamefanya mitihani hiyo KABLA ya Kighoma Malima kuwa waziri, umekaa kimya. Nilitumaini ungetuambia kama wewe katika mtihanio wako wa darasa la saba (au nane) uliandika jina lako na sio namba na kwa sababu hiyo wakristu waovu walikufelisha! Umetoa statistics zikionyesha uwiano wa dini katika bunge letu na kudai kuwa zinaonyesha kuwawabunge wakatoliki ni 75% ya bunge. Nilipochukuwa statistics zako na kukuonyesha kuwa tofauti na unavyosema, zinaonyesha kuwa wislamu ni majority katika hilo bunge , umekaa kimya! Na mifano kama hii iko mingi. Unapobanwa unachukuwa kurasa nzima hata kama haiendani na kilichoulizwa na kuibandika hapa. Au unatupa hadithi ambayo unatuambia ulisimuliwa peke yako. Hadithi hizo ni nzuri na zinafurahisha lakini hazitoshi.

Mwenye dharau ni wewe, Mkuu. Umezoea kusifiwa na watu kupokea kila unachosema kama vile wewe ni malaika fulani. Unapopingwa unadai kuwa ati unadharauliwa na lugha ya kukejeliwa. Wewe kama umewahi kufanya presentation katika midahalo ya kimataifa ambayo ni diverse na sio ya waislamu wenzako, ungetambua kuwa vigorous criticism ni course for par! Ukiweka kitu hadharani ni lazima atatokeza mtu kupinga na kudai uthibitisha na kuonyesha mapungufu yake. Ni kama vile wewe unavyochambua historia iliyoandikwa na watu wa Kivukoni basi na wewe vile vile kitabu chako kitachambuliwa. Ndivyo ilivyo. Wewe unaonyesha dharau kubwa kwa kutufanya kama watoto wadogo ambao umekuja kutufungulia macho!

Mimi naona kwa mtu ambae anajifanya kuwa ni mnyenyekevu suala la umaarufu umeliweka mbele mno. Kuwa wewe ni mtoto wa mjini, kuwa wewe ni ndugu wa watu maarufu, kuwa wewe unakaribishwa na vyuo vikuu vikubwa vikubwa ( nilikuhoji kuhusu hili na mpaka sasa haujanijibu) n.k. n.k. Yote hayo hayana maana hapa. Hapa tunaangalia hizo video zako na maandishi ayako unayoyaweka na tunayajibu ipasavyo. Mimi nimekulia Dar es Salaam na mbona sikujui? Au umaarufu wako ni kwa wenzako wenye dini yako tu?

Umezoea kusifiwa na hao wanaokuomba uwapedarasa bila kupingwa au kuambiwa u-substantiate allegations zako.

Mimi sijui kama una shida ya pesa au la. lakini hii kusisitiza kuwa hauwezi kujadiliana na mtu hadi huyo mtu asome kitabu chako kunanitia wasiwasi. Unataka kuniambia kuwa unapoenda kwenye hizo kongamano za kimataifa, haumjibu mtu mpaka akuhakikishie kuwa amesoma kitabu chako? Si mara nyingi unajibiwa kwa yale unayowaelezea? Kitabu chako si msahafu kiasi kuwa bila kukisoma basi mtu hauwezi kujua ukweli wa historia yetu. Ni kitabu kimoja tu katika vingi.

Wewe ( sio mimi ) ndiye uliyemuita Sykes THE Founder of Political Movements. Au haujui maana yakutumia neno "THE"? Kama ulijua kuwa alikuwepo mwingine, hata mmoja tu usingetumia neno hilo. Huu ni uthibitisho mwingine wa upotoshaji wa makusudi unaoufanya. Kama ulijua kuwa Chief Kidaha Makwaia alihusika pia katika kuanzisha TANU ( kitu ambacho si kweli, maana hawakuwa peke yao hawa) kwa nini basi ulimuita Sykes THE FOUNDER ... kama vile alikuwa peke yake barabarani akielekea Damascus?

Kumbe aliliia akimkumbuka rafiki yake kipenzi! Hivi mlitaka Nyerere afanye nini? Yeye hakuandika kile kitabu mnachodai kuwa kimedharau Sykes. Sijawahi kumsikia Nyerere hata siku moja akikipigia debe kitabu hicho. Mzee Rashad kama mtu mwiingine yeyote alikuwa na haki ya kufanya ulichofanya wewe, kusahihisha mapungufu hayo kwa kuandika kitabu. Kulia kwake hakusaidii kitu bali kuandika kwake kungetusaidia wote.

Hivi wewe ambae umechukua jukumu la kutuandikia masahihisho hayo, kitabu chako kimepigwa marufuku? Umewahi kutiwa ndani kutokana na maandishi yako?

Hakuna mtu anayekukataza kuwaenzi wazee wako kwa kandika waliyokusimulia. Tatizo ni pale unapotaka kutulazimisha kuwa simulizi zao ni ukweli wetu sote. Hii haikubalik hata kidogo. Ndiyo maana umeambiwa kuwa ulichoandika hakiendani na title ya kitabu chako.

Amandla........

Mkuu Fundi Mchundo , hayo ni makombora ya uhakika kabisa.
Ningekua Mohammed Said ningeandika kitabu kingine cha kujisahihisa.
Sasa hebu tukae chonjo, tungojee hadithi nyingine ya Mohammed Said, nusu page ya "alisema hivi", "akamjibu hivi", "inaaminika hivi" nk
Asije sema tunamdharau, tumeshazoea modus operandi yake muungwana huyu, endelea.
 
FM: Kwanza. hilo la title ni kweli yaliyomo ndani hayafanani sana na anuani na ntakupa sababu. Mwalimu wangu Maalim Haruna akisema, "Kila binadamu umuonae katika mgongo wa ardhi jua ana kitu kinamtisha hata akiwa na nguvu kiasi gani. Mimi nilkuwa kwa muda mrefu natafuta kitu kinachomtia hofu Nyerere. Nikakipata. Kwanza hakuwa anapenda kunasibishwa na waasisi waliomtangulia katika kupigania uhuru wa Tanganyika. Pili alikuwa akiuhofia sana Uislam. Ushahidi nimetoa ukumbini jinsi alivyowapa Kivukoni kazi ya kuandika historia ya TANU na ikaandikwa kwa sampuli ya kumpendeza yeye. Nilipoandika ile makala katika Africa Events (March/April 1988) magazeti yakakusanywa na kuchomwa moto. Hapo ndipo nilipojua kinachomtisha na ndiyo nikatoa anuani hii kwa kitabu changu: The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Utold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika.

Swali ulouliza wewe nilishaulizwa sana lakini sikuwa natoa jibu. Nilikuwa nasubiri mtu kama wewe ndiyo nilitoe maana kwako wewe jibu lina maana kuliko kwengineko.

Pili: Kuhusu kuwa mimi sielewi maana ya "definite article" nakuibia siri. Cambridge English Language Oral Examination - Merit Pass (1st Class).

Tatu: Kusisitiza usome kitabu ni kukurahisishia kazi kwani ni dhahir kuwa endapo ungelichukua tabu ya kusoma kitabu changu kuna maswali usingeliuliza hivyo tungeokoa muda. Huwezi kujadili kitu usichokifahamu.

Nne: Hili la Japhet Kirilo usiongelileta kama ungesoma kitabu. Kamati ya Meru Land Case ilikuwa - Abbas Sykes, Abdu Kandoro na Japhet Kirilo. Fedha za Kirilo za safari alizituma Ally Sykes (Mweka Hazina wa TAA) kwa Money Order kwenda USA River bahati mbaya hapo hapakuwa na Posta hivyo Kirilo hakuzipata fedha zile. Kamati ilitembea takriban nchi nzima. Serikali ilimnyima Kirilo pasi ya kusafiri ikabidi Abdu Sykes Rais wa TAA aingilie kati na pasi ikatolewa.

Tano: Hili la umaarufu hujibu mimi maarufu toka azal pale ninaposhutumiwa kuwa natafuta umaarufu. Wala sishangai kuwa hunijui. Mtu hata akiwa maarufu vipi si wote watamfahamu. Lakini sasa bado tu hunijui?

Sita: Kujuana na watu maarufu siyo ujanja wangu ni kutokana na kuzaliwa katika jamii hiyo na kwa wakati ule na sehemu ile vinginevyo ningelikuwa kama mtu mwingine yeyote.

Saba: Hilo la kujifanya mnyenyekevu hilo kwa watu wengine kusema.

Nane: Hizo takwimu za Waislam Bungeni sijaziona tafadhali nitumie tena.

Tisa: Simlazimishi mtu kuamini nisemayo hata kama nitataka uwezo huo sina.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom