Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
FM: Naogopa hata kukuambia maana ungekuwa umesoma kitabu hayo usingeyaleta hapa ukumbini. Ungesoma jinsi Salum Mpunga na Yusuf Chembera kutoka tawi la TANU Lindi walivyoivunja ngome ya Wamishionari Songea na pembezoni mwake mwaka 1956. Hawa ni watu wa bara tena bara kubwa kabisa. Chembera alikuwa mwanafunzi wa Sheikh Yusuf Badi na sheikh ndiye aliyeandika hotuba ya kupokea uhuru Lindi na hotuba ile ilisomwa na mwanafunzi wake Yusuf Chembera mbele ya DC Mkoloni.
Sema utakavyosema lakini kuitoa TANU mikononi mwa wazee wetu huo ni muhali mkubwa na wenyewe walitaka kabla hawajafa hilo tulijue. CCM ndiyo pata mpatae yaani ya wote jumla jamala. Katika kuasisiwa kwa CCM Nyerere anachukua alama mia kwa mia.
CCM ni yake khasa wala hana mpinzani. Tumsifie kwa hilo.
Je, ungependa kujua ile hotuba ilikuwa na maudhui gani? Endapo utapenda au mwanaukumbi yeyote yule atapenda basi hilo lisemwe na Insha Allah nitatimiza wajibu wangu.