Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Status
Not open for further replies.
FM: Naogopa hata kukuambia maana ungekuwa umesoma kitabu hayo usingeyaleta hapa ukumbini. Ungesoma jinsi Salum Mpunga na Yusuf Chembera kutoka tawi la TANU Lindi walivyoivunja ngome ya Wamishionari Songea na pembezoni mwake mwaka 1956. Hawa ni watu wa bara tena bara kubwa kabisa. Chembera alikuwa mwanafunzi wa Sheikh Yusuf Badi na sheikh ndiye aliyeandika hotuba ya kupokea uhuru Lindi na hotuba ile ilisomwa na mwanafunzi wake Yusuf Chembera mbele ya DC Mkoloni.

Sema utakavyosema lakini kuitoa TANU mikononi mwa wazee wetu huo ni muhali mkubwa na wenyewe walitaka kabla hawajafa hilo tulijue. CCM ndiyo pata mpatae yaani ya wote jumla jamala. Katika kuasisiwa kwa CCM Nyerere anachukua alama mia kwa mia.

CCM ni yake khasa wala hana mpinzani. Tumsifie kwa hilo.

Je, ungependa kujua ile hotuba ilikuwa na maudhui gani? Endapo utapenda au mwanaukumbi yeyote yule atapenda basi hilo lisemwe na Insha Allah nitatimiza wajibu wangu.
 
Kuna watu wanaoamini kwamba Waislamu walikandamizwa na Nyerere na kanisa la Kikatoliki na wanaendelea kukandamizwa na Wakristo. Wanaamini pia kwamba ni Waislamu waliokuwa mbele katika ukombozi wa nchi yetu kutoka kwa wakoloni. Hata majina ya Wakristo yanayojulikana nchi nzima na kuthibitisha kwamba Wakristo pia walikuwa miongoni wa viongozi waliokuwa mbele katika ukombozi wa nchi yetu hayatoshi na hayateweza kuwaridhisha ndugu zetu wanao amini kwamba ni Waislamu waliokuwa viongozi katika ukombozi wa Tanganyika.

Wataendelea kuamini hivyo. Ushahidi unao onyesha kwamba huo siyo ukweli, hata unapotoka kwa Waislamu wenzao, hauwezi kubadili mawazo yao.
Kileleni ndio kwanza unaingia.Jaribu kuwa kama wenzako ambao wengine walitumia hata 2 weeks kusoma michango iliyopita kuepuka kuwa kituko katika huu mjadala.
Ikiwa huwezi kuanza shinani angalau kuanzia pg40 hivi utaelewa kiasi.Ukianza kileleni kama hivi utasumbuana na wana ukumbi bure.
 
K: Muhammad Ali katika kitabu chake "The Greatest My Own Story" anasema baada ya kurudi ulingoni baada ya kufungiwa kwa ajili ya kukataa kupigana na Viet Cong anasema moyo wake ulibadilika sana katika mapambano. Alikuwa hawezi kupigana kama zamani kwa kuwa nafsi yake ilikuwa imejaa huruma. Akiona kama mpinzani anajitahidi sana amshinde kitu ambacho kwa wakati wake Ali kilikuwa hakiwezekani, Ali alikuwa akimtazama mwamuzi kama kumpa ishara alimalize pambano.

Kuna mambo Nyerere aliwafanyia wazee wetu ambayo yaliwasikitisha kupita kiasi. La kwanza ni kule kuvunja Baraza la Wazee mwaka 1963. Kisha akawatia kizuizini baadhi ya masheikh na kumkamata Sheikh Hassan bin Ameir na kumrejesha Unguja na kumpiga marufuku asikanyage Bara maisha yake yote. Kisha akaivunja EAMWS, Daawat Islamiyya, Jamitual Islamiyya na nyingezo.

Wazee wetu hawakufanya kitu walirudi majumbani kwao wakasubiri. Sasa ilipokujaandikwa historia ya TANU na wakaisoma wakajiuliza hii historia ya TANU au historia ya Nyerere?

Wazee wetu ni watu makini sana si kama mnavyowafikiria.

Hawakupata tabu kupata jibu.

Kila niliyekwenda kumhoji na kumweleza kuwa ninaandika historia yao sikuondoka ila nilisomewa dua ndefu.
 
Asante, Mkuu kwa kuweka wazi hili. Nasikia Kambano alifanya kazi pasipo mshahara wa uhakika maana TANU ilikuwa hoi bin taaban kifedha wakati ule. Wakina MS hawataki kukubali kuwa bila watu wa bara kuunga mkono TANU huo uhuru wala usingepatikana. Na TANU ingekuwa identified kama ya waswahili basi watu wa bara wangeisusia. Ni jitihada kubwa na uzalendo wa hali ya juu wa viongozi wa wakati ule ndio uliofanya watanganyika waweke pembeni masuala ya ukabila na dini na kuungana WOTE kudai uhuru ambao leo tunajivunia. Kwangu mimi ni matusi makubwa kujaribu kuugeuza uzalendo wao na kuufanya udini.

Amandla......

Kambona alifanya kazi bila mshahara wa uhakika.Hapo umefurahi.Kwanini hukutoa pongezi zaidi ya hizo ulipoambiwa mzee Mshume Kiyate alitoa shilingi mia 2 alipokutana na Julius Nyerere akielekea sokoni Kariakoo kwa miguu na akamlalamikia kuwa hakuwa na hata senti mfukoni!.Huu ndio aina ya ubaguzi munaoufanya na kulazimisha uwe ndio historia ya nchi.
Yawezekana Kambona hakufanya hivyo kwa uzalendo bali kwa kuwa hakuwa na sehemu nono tu ya kukimbilia.Mwenye uzalendo ni yule aliyetoa pesa kumsaidia mtu aliyeonekana kuwa ni mpigania uhuru.Pesa hiyo iliweza kujenga nyumba ndogo kariakoo enzi hizo.
 
Kileleni: Naomba nikuulize kwanza, je umeshasoma kitabu changu? Hapo ndipo kilipo chanzo cha mjadala. Vinginevyo kwa hisani yako soma niliyoeleza ukumbini kuhusu nafasi ya Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika. Wakristo kwa hakika walikuwapo lakini Waislam ndiyo walioongoza mapambano na command post 1950 hadi 1954 ilikuwa kwanza nyumbani kwa marehemu Abdulwahid Sykes Mtaa wa Aggrey/Sikukuu na post ndogo TAA Makao Makuu, New Street (sasa Lumumba), alipokuja Nyerere na kuanzishwa kwa TANU chumba cha mapambano kikahamia TAA Makao Makuu 1954 hadi 1961.

Kukupa picha tu ndiyo maana baada ya uhuru na baada ya Abdu Sykes kufariki pakazuka mvutano ndani ya TANU kutaka kujua nyaraka za TAA/TANU nani mmiliki wake halali? Ukoo wa akina Sykes au ni za chama (TANU)? Hiki ni kisa kinataka wasaa kukieleza. Ally Sykes alikataa kukabidhi nyara zile kwa uongozi wa juu wa TANU akidai zile nyaraka zote ni mali ya marehemu kaka yake, Abdulwahid Sykes.

Nini kilifanyika hapo kwa marehemu Abdu na nini kilifanyika Makao Makuu ya TAA nini ilikuwa kazi ya Baraza la Wazee chini ya mwenyekiti wake Sheikh Suleiman Takadir (1955 hadi 1958) na baada yake chini ya uenyekiti wa Iddi Tulio (1958 hadi 1963) yote nimeyamwaga hapa ukumbini.

Sasa wewe kazi yako ni kusoma kisha Insha Allah tutajadili. Hii ni historia ambayo kwetu ni azizi sana hatutokubali yeyote yule atunyang'anye.
 
FM: Kubwa ninaloona katika ukumbi huu (mimi ni mgeni) ni kuwa inaelekea wachangiaji wengi hawakusomeshwa adabu ya ilm. Sisi tulipokuwa wadogo hatukupelekwa chekechea kwanza tulipelekwa madras. Cha kwanza tulichofunzwa kabla ya yote ni adabu. Kisha ikafuatia kusoma, kisha ikafuati "hifidh" kusoma kitu na kukinasisha katika ubongo kiasi kuwa unaweza kumsomea mtu kurasa mbili, tatu, nne na kuendelea kwa "ghibu" yaani kusoma kutoka kichwani. Sasa ukija shule na Chuo Kikuu hupati tabu ya kunasa masomo na kufanya "reference na cross reference'' kwa wepesi kabisa. Mafunzo yote hayo yanakutoa uchovu katika kusoma. Kuna mushkeli umebishana na mwenzako akatoa rejea kusema hebu pitia kitabu fulani sula hili lilishapata "fatwa" hurudi kwake kesho bila kuwa umesoma kitabu hicho kusadikisha. Hii ni adabu ya ilm kuwa unathamini yale unayoelekezwa katika mjadala. Na walimu wakitia mkazo hapo kwa kuwa wakituambia kuwa ilm haisimami inakua kila uchao sasa wewe ukiwa mvivu wa kusoma au mkaidi tu utafika wakati utakuwa kama yule ambaye hakusoma.

Tatizo hili nimeliona kwako.
 
Wakati umefika wa Serikali kuomba radhi kuhusiana na historia iliyopotoshwa.Katika kufanya hivyo historia iliyoandikwa na Kivukoni ichomwe moto hadharani siku ya sherehe za uhuru,watu waone kwenye runinga,na historia mpya chini ya jopo ambalo Mohammed Said atakuwa mjumbe iandikwe upya.

La sivyo ?

Wewe unataka niseme nini kwa suali hilo.Jibu lipo kwenye Qur'an pale Mungu aliposema:
.... .Hakika Mungu hawaongozi (njia ya kheri) watu madhalimu."(5:51)
Maridhiano penye kutokuelewana ni jambo muhimu kinyume cha hivyo ni hasara yenye kujitokeza katika namna ambayo binadamu hajui ilivyoanzia.Ukitaka ushahidi soma kutokana na matukio yanayoendelea katika dunia hivi sasa.
 
FM: Tusivutane katika hili hapana haja ya sisi kubebeshana mlima. Tusonge mbele na mjadala tuna mengi ya kujadili.
 
MALARIA SUGU: Hakuna msikiti ambao TANU ilinyanyapaliwa. Sheikh Hassan bin Ameir aliyekuwa Mufti wa Tanganyika yeye kadi za TANU akitembea nazo kote alikodarsisha iwe Dar es Salaam au majimboni (kama mikoa ilivyokuwa ikifahamika wakati ule). Sheikh Hassan bin Ameir akiwakatia watu kadi za TANU ndani ya misikiti khasa. Vilevile Sheikh Mtoro Rehani nae akifanya hivyo hivyo kule Kigoma kama alivyokuwa akifanya Sheikh Hassan bin Ameir. Madrasa zote, zawiyya zote, misikiti yote ilikuwa nyuma ya TANU pamoja na wanafunzi, waumini wa kawaida na muridi wote. Hii ndiyo siri ya kushindwa kwa AMNUT na hata Congress na UTP.

Katika uchaguzi mmoja kule Bagamoyo Sheikh Mohamed Ramiyya aliitisha maulid kubwa siku chache kabla ya kupiga kura kisha akapanda katika membar usiku wa manane maulid imekolea na kasida za Quadiriyya zinawaka moto. Sheikh kavaa juba lake la ukhalifa. Akasema, "Ataempigia Mtemvu kura basi ajue..." Siwezi hata kuyasema hayo maneno. Mungu awasamehe hawa wazee wetu. Waliyafanya hayo yote si kwa kibr ila kwa kutaka mkoloni aondoke nchini kwetu tuwe huru tujitawale wenyewe.
 
FM: Unaongea kuhusu Kambona kufanya kazi bila mshahara...Juma Selemani (Juma Mlevi), Rashid Sisso, Bantu Group wengi tu walifanya kazi kwa kujitolea tena nyingine za hatari. Unawajua walinzi wa Nyerere wakati wa harakati nani akiwalipa?

Unazungumzia kufanya kazi bila mshahara. Unawajua waliokuwa wakimlipa Nyerere mshahara? Abdu Sykes biashara yake ya Petrol Station ilifilisika. Dossa kafa masikini. Unajua gari ya kwanza TANU kuwa nayo wakati wa kupigania uhuru alitoa Dossa? Unajua mchango wa Mshume Kiyate?

Waswahili huwa hatutoi kisha tukahadithia.
 
Endelea kutupa historia ya kweli ya Tanganyika ili ukweli ubainike.
 
......................Sema utakavyosema lakini kuitoa TANU mikononi mwa wazee wetu huo ni muhali mkubwa na wenyewe walitaka kabla hawajafa hilo tulijue. CCM ndiyo pata mpatae yaani ya wote jumla jamala. Katika kuasisiwa kwa CCM Nyerere anachukua alama mia kwa mia.

CCM ni yake khasa wala hana mpinzani. Tumsifie kwa hilo. ................

Duuuhh sasa..............this is funny
 
FM: Unaongea kuhusu Kambona kufanya kazi bila mshahara...Juma Selemani (Juma Mlevi), Rashid Sisso, Bantu Group wengi tu walifanya kazi kwa kujitolea tena nyingine za hatari. Unawajua walinzi wa Nyerere wakati wa harakati nani akiwalipa?

Unazungumzia kufanya kazi bila mshahara. Unawajua waliokuwa wakimlipa Nyerere mshahara? Abdu Sykes biashara yake ya Petrol Station ilifilisika. Dossa kafa masikini. Unajua gari ya kwanza TANU kuwa nayo wakati wa kupigania uhuru alitoa Dossa? Unajua mchango wa Mshume Kiyate?

Waswahili huwa hatutoi kisha tukahadithia.

Naam, ni wengi tu lakini haiondoi ukweli kuwa Oscar Kambona MKRISTU alifanya kazi bila mshahara. Mbona hata wakina Pombeah walikuwa wakimchukua Mwalimu kwa pikipiki bure? Mbona wakina John Rupia nao walichangia chama kama walivyofanya wakina Sykes? Na huko bara bila shaka kuna wengi zaidi ambao nao walijitolea kama walivyojitolea watu wa pwani. Kuwa kuna waislamu walijtole, hilo hatukatai. Tunachokupinga ni msimamo wako wa kutaka kutuambia kuwa ni waislamu PEKE YAO ndio waliojitolea.

Amandla.........
 
Ogah: Ingekuwa bora laiti ungesema kitu. Au wewe waonaje? Au ungesema kwa Kiswahli hiki ni kichekesho ingekuwaje? Mimi si mjuzi wa Kiingereza nionee huruma.
 
BM: Karibu ndugu yangu. Amesema Sheikh Muhammad Ayubu, "Elimu ni kama amana mwenyewe akijaitaka sharti umpe amana yake." Tuna wajibu wa kusomesha kile ambacho wenzetu hawakijui. Kukubali au kukataa somo hiyo ni juu yao lakini sisi tutakuwa hatuna dhima.
 
Ogah: Ingekuwa bora laiti ungesema kitu. Au wewe waonaje? Au ungesema kwa Kiswahli hiki ni kichekesho ingekuwaje? Mimi si mjuzi wa Kiingereza nionee huruma.

Usiwaghilibu wachangiaji mkuu, huko nyuma umetoa mada nyingi tu kwa kiingereza, tena kigumu.
 
Wakati umefika wa Serikali kuomba radhi kuhusiana na historia iliyopotoshwa.Katika kufanya hivyo historia iliyoandikwa na Kivukoni ichomwe moto hadharani siku ya sherehe za uhuru,watu waone kwenye runinga,na historia mpya chini ya jopo ambalo Mohammed Said atakuwa mjumbe iandikwe upya.

Wewe unataka niseme nini kwa suali hilo.Jibu lipo kwenye Qur'an pale Mungu aliposema:
.... .Hakika Mungu hawaongozi (njia ya kheri) watu madhalimu."(5:51)
Maridhiano penye kutokuelewana ni jambo muhimu kinyume cha hivyo ni hasara yenye kujitokeza katika namna ambayo binadamu hajui ilivyoanzia.Ukitaka ushahidi soma kutokana na matukio yanayoendelea katika dunia hivi sasa.

Naona sasa njadala unelekezwa kibla
 
FM: Kubwa ninaloona katika ukumbi huu (mimi ni mgeni) ni kuwa inaelekea wachangiaji wengi hawakusomeshwa adabu ya ilm. Sisi tulipokuwa wadogo hatukupelekwa chekechea kwanza tulipelekwa madras. Cha kwanza tulichofunzwa kabla ya yote ni adabu. Kisha ikafuatia kusoma, kisha ikafuati "hifidh" kusoma kitu na kukinasisha katika ubongo kiasi kuwa unaweza kumsomea mtu kurasa mbili, tatu, nne na kuendelea kwa "ghibu" yaani kusoma kutoka kichwani. Sasa ukija shule na Chuo Kikuu hupati tabu ya kunasa masomo na kufanya "reference na cross reference'' kwa wepesi kabisa. Mafunzo yote hayo yanakutoa uchovu katika kusoma. Kuna mushkeli umebishana na mwenzako akatoa rejea kusema hebu pitia kitabu fulani sula hili lilishapata "fatwa" hurudi kwake kesho bila kuwa umesoma kitabu hicho kusadikisha. Hii ni adabu ya ilm kuwa unathamini yale unayoelekezwa katika mjadala. Na walimu wakitia mkazo hapo kwa kuwa wakituambia kuwa ilm haisimami inakua kila uchao sasa wewe ukiwa mvivu wa kusoma au mkaidi tu utafika wakati utakuwa kama yule ambaye hakusoma.

Tatizo hili nimeliona kwako.

Mkuu unakosea sana.
Katika shule tulizosomeshwa sisi tulifundishwa kuwa kupindisha ukweli ni sawa sawa na kusema UONGO.
Na OUNGO NI TABIA YA SHETANI, NI DHAMBI KUBWA.
UONGO hutenganisha watu
UONGO huleta matafaruku katika jamii kati ya mtu na mtu
Hii ndio tofauti kubwa Maalim
 
nO, USINIDANGANYE MZEE. MIMI NAIJUA TZ, NAJUA WATZ WALIVYO, NAWAAJUA WAKIRISTO WLIVYO. KILA MAKAL ILIOANDIKWA NDANI YA MAGAZETI HUJIBIWA. KWA MFANO UKIANDIKA MAKALA NDANI YA MWANAHALISI, RAI, MWANANCHI, AU GAZETI LOLOTE LINALOSOMWA HUJIBIWA NA WAHUSIKA. KWA MFANO SWALA LA MAHAKAMA YA KADHI MAKALA NYINGI ZINAZOTOLEWA NA WASIALM HUJIBIWA. MIMI NI MMOJA NINAEADIKA MAKAL HIZO KWA BAHATI TOLEO LINALOFUATA HUJIBIWA TENA KWA KISHINDO. LKN PIA BAADHI YA MAKAL ZA MAPINDUZI YA ZANZIBAR YALIVYOPOTOSHWA HUJIBIWA TENA . UKITOA LINAL;OFUATA HUJIBIWA. LKN KWA MAKAL ZA HARAKATI ZA UHURU TANGANYIKA HASA ZINAZOTOLEWA NA MOHAMMED SAID HAZIJIBIWI. HAKUNA ALIETAYARI KUZIJIBU. JEE TUSEME WANAZIOGOPA? WANAONA HAZINA MAANA.
KAMA HAZINA MAANA KWANINI MAKALA YA MAPINDUZI YA ZNZ ZIONEKANE ZINAMAANA? LKN HIZI ZINAZOMGUSA BABA WA TAIFA ZISIONEKANE HAZINA MAANA. UNATWAMBIA SISI WATZ TUNAISHI DUNIA YA TATU? mimi hapo sidanganyiki mzee

Mkuu Malaria Sugu, watu vile vile tunaifahamu Tanganyika ,Tanzania hadi Bongo!
Kama kwenye magazeti unayoaandikia unapata feedback hafifu basi hapa JF utapata ile reaction first hand, and from the horses mouth.
Maalim Mohammed Said ameshindwa kuwa convince wana JF hapa na sasa ni karibu mwezi anaendelea kupewa vipande vyake,sembuse gazeti linalotoka once in 24 hrs.
Kama hoja hiii ni upele, basi imepata mkunaji.
Kwa kusema unawafahamu wakristo inaelekea uelewa wako ni very shallow na hata audience yako katika magazeti haina intellectual input.
Soma post zilizopo katika thread hii na utaamua mwenyewe ukweli upi na hadithi ni zipi,
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom