Sijakupinga sehemu nyingine yeyote isipokuwa pale uliposema wakoloni sio sababu ya waislaam kukosa elimu isipokuwa wao wenyewe ndio hawakwenda shule. Na nikasema haya sii maneno ya kweli kwani mimi mwenyewe nilikuwa victim wa mfumo wa mkoloni..nikaishia hapo hadi wewe uliporudi na kupinga maelezo yangu kuwa hayana merit.
Mkuu sote ni binadamu, huteleza au hufanya makosa ktk kujieleza wakati hukumaanisha hivyo au ulivyofundishwa ndio imepelekea kuamini hayo. JF ni uwanja wa kukosoana, kufahamisha na hakika mimi nimekosolewa sana humu na kukubali kwamba info nilizokuwa nazo hazikuwa sahihi na nikajifunza. Uzuri wa JF kwa kila anayekupinga humwaga ukweli hivyo hata wale tusiojua ukweli huokoteza...
I agree with you totaly Mkuu Mkandara on this ingawaje naomba nisieleweke kuwa natetea wakoloni(wa ulaya) dhidi ya wakoloni(wa uearabuni).
Nilicho kuwa napinga haswa presentation ya Mohammed Said na wenziwe ni kuweka lawama za wao kutoendelea kielimu na maendeleao kwa ujumla kwa Mwalimu na Tanu yake.Mohammed Said na wenziwe wakaenda mabli zaidi kwa kuchijukulia credit ya ukombozi wa Tanganyika na kwamba Mwalimu alikaribishwa tu katika harakati hizo.
Generally that is the gist of my rebuttal to Mohammed Said and co.
Msimamo wangu ulikuwa kupinga mawazo ya Mohammed Said kuyaona matukio ya nchi hii katika miwani ya uislamu, na kwa kuona kuwa waislamu kiujumla walionewa hasa kielimu.
Sasa hapo ndio tukaanza kutofautiana.
My argument
1
Kufika kwa wakoloni(Waarabu na Wazungu pia)
Wakoloni hawa aliyejijengea umaarufu wa kufika kwanza ni mwarabu(1100AD hadi 1800's AD)
Najua waarabu vilevile wna elimu nzuri tu kama algebra etc, pamoja na ubaharia kwa kutumia nyota.
Pamoja na kufika mapema nchi hii na kuweka makao, kulowea, sehemu walizo kaa hawakuziendeleza kielimu.Mantiki ya elimu pengine niseme ni ile elim dunia.Elimu ya kuendeleza mtu kupambana na mazimgira yake.
Na nikatoa mifano ya sehemu walizokaa, yaani Zanzibar,Pangani,Kilwa,Lindi, Msasani huko sehemu za Tabora na Ujiji.
Mimi siwalaumu kwa kulowea , nawalaumu kwa kutoleta elimu kama nilivoianisha hapo juu.
Hii ni pamoja na ukweli kuwa kwa sehemu walizokaa waarabu walioa sana mama zetu na kujiwekea uhalali wa kuishi ndani ya nchi yetu, hili silipingi hata kidogo.
Mkoloni mzungu yeye alikuja mwishoni mwa miaka ya 1800, baada ya scramble for Africa kuanza. Mkoloni mzungu alikuja na mtazamo tofauti.Yye aliona Tanganyika kama vile sisi leo tuonavyo plot au shamba ulilopewa na halmashauri ya Jiji.
Hakuona watu waliomo katika nchi hii kama watu, bali source of cheap and enforceable labour.
Mkoloni mzungu alipingwa sana na wote waliokuwepo, pamoja na ukweli kuwa huko Zanzibar Mkoloni na Mwarabu waliingia ligi moja ya kuheshimiana.
Mkoloni mzungu alichagua sehemu zake za kuishi,sehemu alizoona zinalingana na matakwa yake na biashara zake.Sas ili kuendeleza utawala wake alianzisha
shule ambazo kimsingi ilikuwa kufundisha waafrika kumwendeshea biashara au utawala wake.
Sasahapo mkuu ndio tunaanza kuto fautiana.
Wakati mwarabu alikuwa na dini yake ya Uislamu, Mzungu naye aliingia na dini yake ya Ukristo. Sehemu walizo kaaa hawa wakolni(wote wazungu,waarabu) waliibadili jumuia hiyo kuingia dini zao.
Inawezekana kabisa resistance ya waarabu kwa ukoloni wa kizungu ilikuwa kutohusiana kwa aina yoyote socially na mikakati ya wazungu.
Hii inajidhihirisha hata pale Zanzibar kwani mkoloni pale alikuwapo lakini maendeleo ya kielimu bado hayakuwa makubwa sana.
Hii inaweza kuwa mada kubwa sana ya utafiti lakini ukweli ni kuwa alipokuwepo mwarabu mkoloni mzungu hakupashughulikia sana kama pale alioishi mwenyewe.
2
Ukombozi wa Tanganyika na TANU
Kiujumla waafrika waliupinga sana tawala zote zilizokuja.Tawala za kiarabu hata hivyo zilijiIdentify sana na wenyeji na kujichanganya nao baada ya muda katika sehemu walizolowea.
Historia za kupinga ukoloni wa kizungu ,za kina Mkwawa namashujaa wengine zinaonyesha wazi kupingwa kutawaliwa.
Mapambano ya enzi hizi zilikuwa za waafrika na utamaduni wao na uwezo wao dhidi ya wazungu , utamaduni wao na uwezo wao.
Nidhahiri uwezo wetu ulishindwa kuhimili uwezo wazungu.
Uanzishwaji wa TANU ulikuwa hitimisho la kuwaelewa wazungu, utamaduni wao na uwezo wao.
Pamoja na shule, vita kuu zote mbili na maendeleo ya kupata mwanga wa elimu hivi vyote vilimpa mwaafrika silaha yakuweza kupambana na mkoloni mzungu kwa kutumia itikadi yake mwenyewe.Na hapo ndio kina Mwalimu Nyerere na wenziwe wanaingia.
Mifumao ya elimu aliyo wekwa na mkoloni mzungu hata Nyere aliikuta, hakuiasisi.
Yeye Nyere alifaidika na mfumo huo wa elimu ya Mkoloni na baada ya Uhuru alijitahidi sana katika sekta ya elimu kusambaza leimu ili iwe kwa wananchi woote.
Sasa mkuu Mkandara frame work ya upinzani wangu kwa Mohammed Said and co. ni kumlaumu Nyerere kwa kutoendeleza elimu kwa WAISLAMU TU, wakati si kweli.
Mfano uliojitole wewe mwenyewe Mkuu Mkandara , ni mfano tosha kuelezea kuwa elimu ya Mkoloni mzungu ilichagua pale yeye tu(mkoloni mzungu) alipoona pana returns kwake, utawala wake na biashara zake.
Kwa bahati nzuri mimi nilikuwepo Mlimani mwaka 1978 wakati Mwalimu alikuja kuonana na wanafunzi.
Profesa Che Mponda alimuuliza swali hili
" Mwalimu tulipoonana kule Marekani uliniambia turudi nyumbani na kuiendeleza nchi yetu ya Tanzani.
Mimi nikaja na nikapata kazi hapa UDSM,Lakini hapa kuna ukabila mkubwa sana.Mkuu wa Faculty kabila moja na wakuu wa departments kabila hilo hilo sasa sisitunakereka, Utasemaje juu ya hilo."
Mwalimu akacheeka na kile kikohozi chake , lakini akajibu kwa umakini mkubwa.
Yeye ailopiata nchi hii nilikuwa na wasomi wachache sana, daktari mmoja au wawili pale muhimbili na engineer mmoja tu.
Aliendelea kuwa wakoloni(wazungu) wali jenga shule sehemu tatu kuu, Kilimanjaro,West Lake na Mbeya. Na sehemu hizo ndio unapata wasomi ingalau walioweza kuwa makarani wa kwanza.Na alisema ana makarani wengi sana toka sehemu hizo kwa vile ndio walianza kupelekewa shule na wakoloni.
Na lisema kuwa huwa inapotokea nafasi ya kazi, anaPOletewa recommendations za watu wan ofaa anakuta wa kwanza aliyesoma ni wakabila la mchagga , wa pili ni mchagga na watatu ni mchagga, wote waliosoma sana.
Na ndiyo maana akaamua kutaifisha mfumo wa elimu ili uwe wa wote, wananchi wote.
Mwalimu aliongeza kuwa sehemu kama za Tabora na Mwanza kuna kundi kubwa sana la watu, lakini ambao hwana shule kabisa na hawakujiendeleza.Akaongeza kuwa sehemu za kwao Mara wakoloni waliwachukua watu wa huko kwenda jeshini tu, nako wakijenga shule chache sana.
Na ndio maana akasema leo una kina Mwita ,Chacha na Marwa wengi jeshini lakini hawana elimu ya kutosha .Hii ni kwa vile hata jeshini makabila yaliyosomeshwa na mkoloni yalikuwa yakiongoza huko.Baada ya uasi wa 1964 Mwalimu aliongeza kusema akawapandisha vyeo wote hawa Mwita ,Marwa na Chacha ambao kimsingi bado hawajasoma.
Mwalimu altioa ushauri ambao naukumbuka hata leo.JENGENI SHULE ZA MSINGI KWA WINGI KATIKA MAENEO YENU.
Mkuu Mkandara nimeandika sana lakini nafikiri kwa sasa niishie hapo.