Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Status
Not open for further replies.
Na kadai Nyerere aliwahi kusema Muhindi asiruhusiwe kuongoza Waislam. Nyerere ambae alikaribia kugombana na wenzie akitetea usawa wa wote, wahindi, wazungu, waafrika. Mada ni uislamu. Msemaji mwongo na wewe, kama wewe sio yeye, pia mwongo mkubwa

Julius Nyerere huyo ambaye wakati wenzake wanasherehekea Iddi Amin kuwafukuza wahindi Uganda yeye aliuita ni ubaguzi wa rangi na dhulma! Julius Nyerere huyo ambaye katika baraza lake la mawaziri hakukosekana mhindi na/au mzungu. Au ni Nyerere mwingine tunayemzungumzia?

Amandla......
 
Ukitaka umuelewe vyema Mwalimu Nyerere inakubidi kwanza usome kitabu na kama unaona shida ya kusoma ipo DVD ilirekodiwa Msikiti wa Mtambani mwezi wa Ramadhani mwaka jana. DVD hii inapatikana Al Hazm Bookshop Msikiti wa Mtoro. Ukipenda msome pia John Sivalon, Bergen, Njozi, Mwaijage, Ghassany nk. kuna mengi ndani ya vitabu hivyo kuhusu Nyerere ambavyo havifahamiki kwa wengi. Mwalimu Nyerere aliwakandamiza sana Waislam na akiwaogopa mno hasa baada ya kuona nguvu yao wakati wa kudai uhuru.

Hivi unajua kuwa hata ile hotuba aliyosoma Umoja wa Mataifa 1955 ile hotuba iliandikwa na Kamati ya TAA chini ya uongozi wa Abdulwahid Sykes 1950? Hili ulikuwa unalijua?

Unajua kuwa Nyerere hakutaka Waislam wawe na Chuo Kikuu na ndiyo maana akaivunja East African Muslim Welfare Society 1968 ambayo ilikuwa katika harakati ya kukijenga? Unajua kuwa njama hiyo aliifanya akishirikiana na Kanisa Katoliki? Insha Allah taratibu tutaeleweshana na huenda iko siku Mungu atatuelekeza katika haki na tutashirikiana katika haki na usawa ili nchi yetu itengemae.
 
Ajabu moja ya historia hii ni kuwa inaumiza wengi na sishangai kuwa lugha yako inakuwa kali kidogo. Lakini ukweli ndiyo huu historia ilitaka kufichwa na mimi Mungu akajaalia nikaiandika. Ikiwa hujakisoma kitabu kisome utakutana na madaktari wote waliokuwa katika siasa: Dr. Joseph Mutahangarwa, Dr Luciano Tsere, Dr Michael Lugazia, Dr Vedasto Kyaruzi. Utamsoma Chief Kunambi, Chief Kidaha Makwaia nk.

Kleist Sykes baba yake Abdulwahid ndiyo alikuwa katibu muasisi wa African Association 1929 na mwanawe akaja kuichukua nafasi hiyo ya ukatibu1950. Haya yalifichwa ikawa historia ya TANU ni Nyerere pekee yake. Hili ndilo lililokuwa likinisikitisha sana. Ikiwa katokea mtu anakasirishwa na ukweli huu hii ni bahati mbaya sana.

Tuendelee kujadiliana kistaarabu bila ya kutumia maneno na lugha isiyokuwa ya kiungwana.
 
Mwalimu Nyerere aliwakandamiza sana Waislam na akiwaogopa mno hasa baada ya kuona nguvu yao wakati wa kudai uhuru.
Basi usiiruke mada kuu hiyo, mada yako hapa ni Waislamu walikandamizwa. Ulitaka kujifanya mada ni wanaharakati za uhuru waliosahaulika kwa ujumla, nikakwambia mongo. Umeshindwa kujificha?

Hivi unajua kuwa hata ile hotuba aliyosoma Umoja wa Mataifa 1955 ile hotuba iliandikwa na Kamati ya TAA chini ya uongozi wa Abdulwahid Sykes 1950? Hili ulikuwa unalijua?
hili linaonyesha vipi kwamba Nyerere alikandamiza Waislamu? Halafu imesemwa kwenye mhadhara wa Mohamed Said kwamba nyaraka haikutaja chanzo cha waandishi au mawazo, wewe umejuaje, umehadithiwa na Skyes?

Ndio hilo umeambiwa na wachangiaji wengine kama F'Mchundo kwamba huwezi kuandika historia kwa kutegemea simulizi za mtu mmoja. Unakaa barazani kwa mzee mwala halua mwacheza bao mwaandika historia ya nchi, mzee mwenyewe kazaliwa na kufia Kariokoo, harakati za Mwanza atazijua? We unajua kwamba kanda ya ziwa wana TANU walipigwa mabomu uchaguzi wa 1958?

Unajua kuwa Nyerere hakutaka Waislam wawe na Chuo Kikuu na ndiyo maana akaivunja East African Muslim Welfare Society 1968 ambayo ilikuwa katika harakati ya kukijenga? Unajua kuwa njama hiyo aliifanya akishirikiana na Kanisa Katoliki?

Unasema kwamba EAMWS ilivunjwa na Nyerere.

Unayatambua maneno haya chini, nani anarekodiwa akiyasema?:

Muhammed Said explains in his book that the Islamic Unity started to collapse after the independence. Abdalla Chaurembo made conflicts with his Sk. because of politics. And because of these internal conflicts among Muslims, there was no Islamic University built only the foundation stone were laid. In 1968, the EAMWS came to an end. Sk. Hassan tried to use his talents and efforts to support this Society. But Tanganyika Muslims were divided in to two different groups. The first group supported any government idea with out questioning if this new thought is Halal or haraam from Islamic point of view, while the second one supported the government only if its idea was Halaal. Because of this condition and conflict, many Sheikhs ... (Muhammed Said. 1998, 368).
Dr. Issa Haji Ziddy, University of Zanzibar, Zanzibar, Tanzania.

Muhammed Said wa kwenye video si huyo aliyerekodiwa na Dr. Haji Ziddy akieleza ukweli wa kuvunjika EAMWS? Kwamba ni tafrani na zogo za wenyewe kwa wenyewe? Leo unataka kutugeuzia kibao sisi wajinga hapa, sio? Mnafik mjaalaana, mwongo habith mkubwa.
 
Ukitaka umuelewe vyema Mwalimu Nyerere inakubidi kwanza usome kitabu na kama unaona shida ya kusoma ipo DVD ilirekodiwa Msikiti wa Mtambani mwezi wa Ramadhani mwaka jana. DVD hii inapatikana Al Hazm Bookshop Msikiti wa Mtoro. Ukipenda msome pia John Sivalon, Bergen, Njozi, Mwaijage, Ghassany nk. kuna mengi ndani ya vitabu hivyo kuhusu Nyerere ambavyo havifahamiki kwa wengi. Mwalimu Nyerere aliwakandamiza sana Waislam na akiwaogopa mno hasa baada ya kuona nguvu yao wakati wa kudai uhuru.

Hivi unajua kuwa hata ile hotuba aliyosoma Umoja wa Mataifa 1955 ile hotuba iliandikwa na Kamati ya TAA chini ya uongozi wa Abdulwahid Sykes 1950? Hili ulikuwa unalijua?

Unajua kuwa Nyerere hakutaka Waislam wawe na Chuo Kikuu na ndiyo maana akaivunja East African Muslim Welfare Society 1968 ambayo ilikuwa katika harakati ya kukijenga? Unajua kuwa njama hiyo aliifanya akishirikiana na Kanisa Katoliki? Insha Allah taratibu tutaeleweshana na huenda iko siku Mungu atatuelekeza katika haki na tutashirikiana katika haki na usawa ili nchi yetu itengemae.
Mohammed Said,
You do not have the monopoly of knowing Julius Nyerere. Wewe peke yako si source ya hulka na tabia za Julius Nyerere kwa hiyo hii ya kutuambia kwamba tusome kitabu chako ndipo tutamjua Julius Nyerere ni kutaka kutusokomezea ideolgy zako na dhana. Nimewasoma wote Sivalon, Bergen, Njozi, Rasheed, Mwaijage(huyu aliwekwa detention kwa kuhusika na njama za kupindua serikali) Wote hao uliowachagua wana theme moja na wewe na kwa hivi nawaweka kundi moja. Bahati nzuri na mimi nilipata bahati ya kumfahamu marehemu Wahid Kleist Sykes. Mwanae Kleist was my school mate and my best friend still up to this day. Nyerere alianza kuandika vitu akiwa Makerere na hata ile hotuba unayodai aliandikiwa na akina Sykes nina hakika 99% Nyerere aliweka mkono wake na mawazo yake pale. Hakuwa mbumbumbu kama unavyotaka watu waamini kwamba alienda UN kusoma kitu kama kasuku. Kama ungefanya utafiki makini ungegundua kwamba kulikuwa na sababu nyingi za Nyerere kuvunja EAMWS na si kwa sababu tu ya harakati za kujenga chuo cha waislamu.
 
Ukitaka umuelewe vyema Mwalimu Nyerere inakubidi kwanza usome kitabu na kama unaona shida ya kusoma ipo DVD ilirekodiwa Msikiti wa Mtambani mwezi wa Ramadhani mwaka jana. DVD hii inapatikana Al Hazm Bookshop Msikiti wa Mtoro. Ukipenda msome pia John Sivalon, Bergen, Njozi, Mwaijage, Ghassany nk. kuna mengi ndani ya vitabu hivyo kuhusu Nyerere ambavyo havifahamiki kwa wengi. Mwalimu Nyerere aliwakandamiza sana Waislam na akiwaogopa mno hasa baada ya kuona nguvu yao wakati wa kudai uhuru.

Hivi vitabu vinapatikana msikitini tu? Kwa nini usituambie vimechapishwa na nani na mwaka gani ili tuvitafute wenyewe? Unatuambia tu kuwa Nyerere aliwaogopa waislamu bila kutoa ushahidi wa maana. Simulizi za jirani yako si ushahidi katika akademia. Kukandamizwa kwa Abdul Sykes kama kulikuwepo si ushahidi wa chuki na uoga wa mwalimu dhidi ya waislamu hasa ukizingatia waislamu lukuki aliowakumbatia.

Hivi unajua kuwa hata ile hotuba aliyosoma Umoja wa Mataifa 1955 ile hotuba iliandikwa na Kamati ya TAA chini ya uongozi wa Abdulwahid Sykes 1950? Hili ulikuwa unalijua?

Unataka kutuambia ile hotuba waliifungia kwa miaka mitano wakimngoja Mwalimu aende akaisome N.Y.? Haujatuambia, TAA waliiandika kwa makusudi gani? Na jee baada ya kamati kuandika, waliichapisha? Sasa unataka kutuambia kuwa huyo Mwalimu, msomi wa Edinburg, alipewa hotuba iliyokamilika, akakimbia nayo N.Y bila yeye mwenyewe kujiridhisha kuwa yaliyomo anakubaliana nayo? Viongozi wote wana watu wanaitwa speech writers lakini hata siku moja sijawasikia wakiwacredit kwa kuwaandikia risala. Inawezekana kuwa palikuwa na notes au hata draft ya hotuba lakini ni Mwalimu ndiye aliyeichukua, itia nakshi na kuisoma mbele ya kadamnasi. Ile hotuba ilikuwa yake.

Unajua kuwa Nyerere hakutaka Waislam wawe na Chuo Kikuu na ndiyo maana akaivunja East African Muslim Welfare Society 1968 ambayo ilikuwa katika harakati ya kukijenga? Unajua kuwa njama hiyo aliifanya akishirikiana na Kanisa Katoliki? Insha Allah taratibu tutaeleweshana na huenda iko siku Mungu atatuelekeza katika haki na tutashirikiana katika haki na usawa ili nchi yetu itengemae.

East African Muslim Welfare Society kilianzishwa Mombasa na Sir Sultan Mohamed Shah, aliyekuwa Aga Khan, kiongozi wa waismailia ambao nyinyi hamuwahesabu kama waislamu. E.A.M.W.S. kilihujumiwa na waislamu wenyewe kwa kuogopa kurubuniwa na wahindi. Hata hicho chama walichoanzisha wakina Sykes mwaka 1934 kilikuwa ni katika juhudi za kushindana na waislamu weupe na si kingine. Palikuwa na chuki kubwa ndani ya jumuia ya waislamu dhidi ya wale waliowaona ni weupe ( wahindi na waarabu). Hata pale E.A.M.W.S. ilipohamishia makao makuu yake Dar es Salaam kutoka Mombasa mwaka 1961, na kumfanya Chief Abdallah Fundikira kuwa kiongozi wake bado waislamu weusi ambao wengi walikuwa TANU hawakukibali. Chuo pekee walichokuwa nacho, (The Muslim Academy) kilichokuwa Zanzibar kilifungwa na serikali ya Mapinduzi mwaka 1966! Kote huku Nyerere na wakatoliki walihusika vipi? Pale Chang'ombe pamekuwa na jiwe la msingi la Chuo cha Kiislamu miaka nenda rudi na hatima yake mmekigawa kwa swahiba wenu, Manji. Wakatoliki mote humu wamehusika vipi? Pamoja na yote haya ni mkatoliki Benjamin Mkapa aliyechukua kilichokuwa Chuo cha shirika la umma Tanesco na kuwakabidhi waislamu kiwe Chuo Kikuu chao. Yote haya hauyaoni, bado unakazania kuwa wakatoliki wana kampeni ya kuwahujumu!

Ajabu moja ya historia hii ni kuwa inaumiza wengi na sishangai kuwa lugha yako inakuwa kali kidogo. Lakini ukweli ndiyo huu historia ilitaka kufichwa na mimi Mungu akajaalia nikaiandika. Ikiwa hujakisoma kitabu kisome utakutana na madaktari wote waliokuwa katika siasa: Dr. Joseph Mutahangarwa, Dr Luciano Tsere, Dr Michael Lugazia, Dr Vedasto Kyaruzi. Utamsoma Chief Patrick Kunambi, Chief Kidaha Makwaia nk.

Mimi nilidhani TANU ilikuwa ya waislamu. Hawa wote walikuwa wanafanya nini humo? Au walikuwa ni waislamu waliotumia majina ya kikristu? Na nani anawajuwa hawa? Nao wamesahauliwa kwa sababu walikuwa ni waislamu?

Kleist Sykes baba yake Abdulwahid ndiyo alikuwa katibu muasisi wa African Association 1929 na mwanawe akaja kuichukua nafasi hiyo ya ukatibu1950. Haya yalifichwa ikawa historia ya TANU ni Nyerere pekee yake. Hili ndilo lililokuwa likinisikitisha sana. Ikiwa katokea mtu anakasirishwa na ukweli huu hii ni bahati mbaya sana.

Kwa hiyo wewe tatizo lako ni kuwa jirani yako hakutajwa? Unataka kumfanya sawa na Nyerere? Mbona wengine tuliishawasikia wao, wakina Kambona, Rupia, Bibi Titi, Rashid Kawawa, Mtemvu, Mwapachu na wengine. Lakini wote tunajua kuwa kiongozi wao alikuwa Nyerere. Sasa wewe unataka kutuambia kuwa la hasha, Nyerere alikuwa figure head tu, vichwa na waliokuwa wakiongoza chama ni wakina Sykes na waislamu wenzao! Basi, iko kazi.

Amandla......
 
... Bahati nzuri na mimi nilipata bahati ya kumfahamu marehemu Wahid Kleist Sykes. Mwanae Kleist was my school mate and my best friend still up to this day. Nyerere alianza kuandika vitu akiwa Makerere na hata ile hotuba unayodai aliandikiwa na akina Sykes...
Hao wa kina Sykes wenyewe wamemruka huyo Saidi na uzushi wake.

Sikiliza hapa jinsi mayor Sykes alivyodadavua jinsi Saidi alivyojipendekeza kwa familia yao na udini wake.
 
Hao wa kina Sykes wenyewe wamemruka huyo Saidi na uzushi wake.

Sikiliza hapa jinsi mayor Sykes alivyodadavua jinsi Saidi alivyojipendekeza kwa familia yao na udini wake.

Napenda kumtaka radhi sana Mzee Kleist Sykes kwa ku"insinuate" kuwa ni disgruntled individual. Huyo Mohamed Said anatoa distorted version ya hali ilivyo. Nakushukuru sana Tindikali kwa kutuwekea hiyo video. N
Amandla........
 
Fundi Mchundo, umesikia Sykes alivyosema alimwambia nini Saidi, Saidi unataka kuandika kitabu cha uislamu, au unaandika harakati za ukombozi kwa ujumla, au wasifu wa Bw. Sykes au nini haswa?

Na hilo ndio tatizo nililonalo na huyu Saidi, anaweza kusema chochote anachotaka lakini alipojifanya eti mada yake hapa sio uislamu, hapo ndo nikashtuka na kumwita mwongo. Hicho tu. Asijifanye mwema sana eti tujadili harakati za uhuru, hakuna cha uhuru, mada yake hapa ni uislamu!

Lakini muhimu tujadili historia ya uhuru wa Tanganyika na mashujaa wake ambao wamefutwa katika historia yab nchi yetu. Hii ndiyo mada kuu na husika katika mjadala huu.
 
Je huyu Mohammed Said ndiye MSA(Mohammed Said Abdulla)?

Kama siye then we are dealing with an imposter.
Huyu Jamaa anatumia jina linalo heshimiwa sana la Mohammed Said Abdullah , novelist wa lugha ya kiswahili tuliyemsoma sana miaka ya sekondari.
Uandishi wa huyu Mohammed Said una walakin na hauendani kabisa na Mohammed Said Abdullah tuliyemsoma miaka ya 70.Mahammed Said hafai hata kuwa photocopy ya Mohammed Said Abdullah.

Muhammed Said Abdulla

From Wikipedia, the free encyclopedia

Jump to: navigation, search
For other people named Mohammed Said, see Mohammed Said (disambiguation).
Muhammed Said Abdulla (25 April 1918 - March 1991), was a Swahilinovelist who is often credited as a pioneer of Swahili literature.
He was born in Zanzibar. After working for ten years as an inspector for the Colonial Health Department, Abduall decided to go into journalism; in 1948 he became editor of the newspaper Zanzibari. He later became assistant editor of Al-Falaq, Afrika Kwetu, and Al Mahda. From 1958 to his retirement in 1968 he served as editor of the agricultural magazine Mkulima. 1958 was also the year that his fiction work Mzimu wa Watu wa Kale (Shrine of the Ancestors) won top honors at the Swahili Story-Writing Competition (held by the East African Literature Bureau); in 1960 the work was published as a novel.
This novel marked the first appearance of Bwana Msa, a detective character that features in most of his subsequent works.
[edit] Works

Each subsequent book that Abdullah wrote contained a more complex, sophisticated plot than the one that came before it. The plots of Abduallahs novels usually involve a protagonist who must battle ignorance and superstition in order to resolve the conflict.

The usage of Swahili in his novels is celebrated in East Africa, even to the point that they are used as required reading in schools. A list of these novels includes:
  • Shrine of the Ancestors (Mzimu wa Watu wa Kale), 1960
  • The Well of Giningi (Kisiwa cha Giningi), 1968
  • In the World There Are People (Duniani Kuna Watu), 1973
  • The Secret of the Zero (Siri ya Sifuri), 1974
  • One Wife, Three Husbands (Mke Mmoja Watume Watatu), 1975
  • The Devil's Child Grows Up (Mwana wa Yungi Hulewa), 1976
 
Mimi ni Mohamed Said Salum Abdallah mwandishi wa kitabu The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924-1968) The Untlod Story of the Muslims Struggle Against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London 1998.
 
Hakika mada yangu ni Uislam hilo silikatai wala silionei aibu kwani historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika ni historia ya wazee wetu ambao waliondolewa katika kumbukumbu zote. Nashukuru kuwa leo nimewarudisha katika historia na kuwapa hadhi wanayostahili. Kizazi kijacho Insha Allah kitawasoma na kuwaenzi daima.
 
Mjadala utapendeza ikiwa utakisoma kitabu na kuona kilicho ndani. Vinginevyo tutakuwa tunarudia yale kwa yale.

Ila muhimu ni kuwa baada ya kukiandika kitabu hicho hivi sasa ni moja ya vitabu vya rejea katika African History and Islam katika vyuo vingi duniani.

Katika wasomi waliokisoma na kukifanyia mapitio ni John Iliffe, Jonathan Glassman, James Brendan nk. Mwandishi amepata mialiko mingi ndani na nje ya Tanzania kuzungumzia mada hii ya Uislam na Siasa Tanzania. Amealikwa na kuzungumza University of Ibadan, Nigeria, Kenyatta University, Nairobi na University of Johannesburg, South Africa.

Halikadhalika ametiwa katika program ya Dictionary of African Biographies ya Oxford University Press na Harvard University kama mmoja wa waandishi, ameandika kitabu kingine katika mfumo kama huo ambacho kimechapwa na Oxford University Press Nairobi - The Torch on Kilimanjaro. Chanzo cha hayo yote ni kule kuandika kitabu cha historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika.

Wanaokiogopa kitabu ni wachache sana wengi wamekipenda. Hili si swali la hamaki na kukasirika ni suala la mtu kuwa msomi makini na kukubali hoja pingamizi.

Huo ndiyo usomi.
 
Mohammed said,
Mkuu umeandika kitabu chako ambacho kinazungumzia sana mambo yaliyotokea wakati wa Nyerere (kabla na baada ya Uhuru). Na sidhani kama ni zaidi ya miaka 50 iliyopita kwani kumlaumu Nyerer ni lazima unazungumzia baada ya Uhuru. Sasa wapo Waislaam watanzania wengi sana bado wako hai. Na toka kila mkoa unaweza kupata waislaam ambao watathibitisha madai yako kwa kuelezea experience zao ktk sehemu ulizotaja.. Mara nyingi na vizuri sana, mtu unapoandika documentary kama hii ni unatakiwa kuchukua maelezo ya waathirika ili kuyapa nguvu maelezo yako. Hizi hadithi ya kilitokea hivi na Nyerere alifanya hivi wakati hakuna mtu hata mmoja aliyesimama na kuthibitisha maelezo ya mwandishi ni sawa na mchezo wa sinema.

Mimi Ni Muislaam na sikupitia mambo mengi uloyaandika wala sikuyaona. Pengine yatokana na umri wangu mdogo hivyo sikuweza kupitia mengi uloyapitia wewe au ulosimuliwa na waasisi wa chama. Mimi sii tu nawafahamu kina Sykes, ni marafiki na jamaa zangu wa karibu sana tena naweza sema mjukuu wa AbdulWahid kwa jina hilo hilo ni my best friend. Nilikuwa pia karibu sana na Sheikh Kassim bin Jumaa pamoja na Sheikh Junad pale Mahiwa nikiishi jirani yake.

Ni katika kukutana na watu kama hawa nilikuja gundua kwamba Waislaam kwa mengi waliyafanya wao wenyewe lakini lawama wakamshushia mwalimu. Kwa mfano, kama alivyosema Fundi Mchundo, waliohujumu jumiya ya waislaam east Africa ni kina Shaban Nassib na hata hii mahakama ya kadhi waliopinga walikuwa Waislaam wenyewe kina Sheikh Kaluta Amri Abeid akiwa waziri wa sheria.

Hakuna swala lolote lililovunga nguvu ya waislaam pasipo mkono wa Muislaam. na hata leo hii mnapotaka na kuweka madai ya OIC au Mahakama ya kadhi wanaoongoza kupinga ni Waislaam ndani ya utawala uliopo, lakini utasikia Vatican hivi ama vile. Ni sawa kabisa na malalamiko makubwa juu ya Uongozi wa Kikwete.. tazama jinsi Watanzania wanavyoandamana kwa shangwe na kumpongeza kisha kesho hao hao watakuja sema Kikwete hafai sii rais mzuri anaongozwa na Vatican yaani ili mradi tu tupate mchawi hali wachawi ni sisi wenyewe.

Mimi ni Muislaam kama wewe na mwanzo nilikuwa nikiamini kama wewe lakini baada ya kukaa na Waislaam na kuwasoma kisha kukaa na viongozi wa dini ambao pia wanajua majungu yaliyomo ndani ya dini yetu nimegundua kwamba HATUFAI. Yaani hatufai kabisa, ni wanafiki kupita maelezo.

Mwisho wa yote haya, la muhimu ni kwamba wewe unataka kufanya nini kuweza kuibadilisha hali hiyo. Ikiwa Nyerere aliwakandamiza Waislaam leo wewe na Waislaam wengine mnafanya nini cha maana ktk jamii ya kiislaam maanake najua hata hizo fedha za Hijjah mnazipigia mahesabu pale Chef Pride. Ni aibu kubwa yaliyotokea mwaka jana yaani hatufai!

Haya huko Bakwata vijana woote wenye msimamo mkali against fraud kina Hassan Chizenga (mshikaji) wanapigwa vita kila siku kukicha. Ni kizuri kipi cha Bakwata ambacho wewe kama Muislaam unaweza kujivunia hata kidogo na kwa nini usiandike kitabu kinachozungumzia Bakwata na ufisadi wa Masheikh dhidi ya Waislaam. Usafi huanza ndani ya nyumba yako mkuu wangu...

Na kibaya zaidi unaonyesha kama unafanya mashindano baina ya waislaam na Wakristu.. sasa kuonyesha kwamba hotuba ya Nyerere UN iliandikwa na Muislaam ndio una maamisha kitu gani?.. Kwani haitokei rais wa nchi kuwa na mwandishi wa hotuba yake? je akiandikiwa hotuba ina maana mwandishi ana akili kuliko rais mwenyewe au ndio utaratibu. Je unajua kwamba hata huyo mwandishi wa Hotuba pia hupangiwa nini cha kuandika?. Acha Udini mkuu wangu hauwezi kukupeleka popote zaidi ya kwamba Kaburini utaingia mwenyewe na hakika utayajibu maswala yanayohusiana na ibada zako sio za Nyerere..
 
Ahsante kwa mawazo yako. Itakuwa bora sana endapo utakisoma kitabu. Baada ya hapo unaweza kutoa hukumu. Tatizo nilionalo katika mjadala huu ni kuwa wengi wanachangia bila ya kuwa na uelewa wa historia ya kudai uhuru wa Tanganyika.

Hii inasababisha wao kutoa maneno tu ya jumla na hili nimeliona hata kwako. Ningependa kukumbusha kama Muislam kuwa Allah katufunza adabu na hili ukizingatia hata katika maingilianao kama haya hujenga tija na mapenzi baina ya watu. Hapana haja ya kushambuliana kwa lugha kali.

Muhimu ni kusoma hoja na kujibu kwa utulivu. Hii huleta raha katika mjadala si kwa wale wanaoshindana bali hata kwa wasomaji wengine. Imam Shaffi kasema yeye anaweza kusimama kwa hoja hata na watu mia yeye akiwa peke yake lakini mjinga mmoja tu yeye huwa
keshashindwa.

Insha Allah tutaendelea kujadiliana na kuheshimiana katika maingiliano yetu hasa zaidi kwa kuwa wewe kama mimi ni Waislam na wasio kuwa Waislam watatuhukumu kwa akhlak zetu.

Hiyo hotuba iliyosomwa na Mwalimu Nyerere mwaka 1955 Umoja wa Mataifa ina kisa kirefu sana na cha kupendeza. Laiti ungekijua kisa chenyewe na watu walioandika na katika mazingira gani hadi ilipomfikia Nyerere 1955 kuna mengi naamini yangepita katika akili yako. Sasa hapo ungekuwa katika hali nzuri sana ya kuchangia. Inasemekana nyaraka hii ile yenyewe ambayo ina mkono wa Abdulwahid Sykes, Sheikh Hassan bin Amir, Hamza Mwapachu, Stephen Mhando imeondolewa katika Tanzania Nationa Archive (TNA) haipatikani.
 
Ningeweza kuacha kujibu hii ila hilo neno "kujipendekeza" ndilo lililonisukuma kufanya maelezo kidogo ili kuuweka vizuri mjadala wetu.

Kwa hakika mimi sina sababu ya kujipendekeza kwa yeyote awaye yule seuze kwake Kleist

Mimi nimezaliwa Mtaa wa Kipata nimemkuta mama yangu Baya bint Mohamed na mama yake Kleist Bi Mwamvua bint Masha wakiwa mashoga. Nimekuwa nikiwaona baba yangu Salum Abdallah na Abdulwahid Sykes wakiwa marafiki urafiki ambao ulianza toka wako watoto wadogo wakiishi mtaa mmoja huo wa Kipata na baba zao wakifanya kazi pamoja Tanganyika Railway katika miaka ya 1920.

Bibi yake Kleist Bi Mluguru bint Mussa na bibi yangu Zena bint Farijala walikuwa vilevile mashoga. Bibi yake Kleist ni bibi yangu. Tukiwa watoto mimi na mdogo wake Kleist, Ebby tulikuwa tukipewa fedha na Bi Mluguru kwenda kununua kaukau ambayo tukiipenda sana.

Sasa hivi ikiwa hii ndiyo historia ya famiia zetu mimi nijipendekeze kwa kina Sykes kwa kutafuta kitu gani?

Mazungumzo ya Kleist na Deus Gunze wa Radio Butiama kutoka Ohio USA yalifanyika baada ya Gunze kufanya mahojiano na mimi. Kisa cha yeye Gunze kuniomba tufanye mahojiano ni kuwa niliandika makala kuhusu Dossa Aziz na nikaeleza masikitiko yangu kwa jinsi alivyosahauliwa katika historia ya kudai uhuru wa Tanganyika. Katika makala ile nilimlaumu Mwalimu Nyerere kwa kuiogopa historia yake mwenyewe.

Hapo ndipo Gunze aliponiomba tufanye hayo mahojiano. Ikiwa umeyasikiliza mahojiano yetu hutopata tabu lau kwa uchache kunielewa.

Inaelekea Gunze aliona kashindwa na hapo ndipo alipofanya mahojiano na Kleist na mimi nimemsikia Kleist. Inawezekana kwa kusukumwa na maswali ya mtego Kleist aliona hapana haja ya kusema kile alichokijua. Kleist kama mwanasiasa alisema yale ambayo yangewapendeza CCM.

Waswahili tuna msemo: Funika kombe mwanaharamu apite.
 
Tatizo nililopata wakati natafuta publisher (mchapaji) wa kitabu changu katika miaka ya 1980 ni kuwa ingawa walikubali kuwa ni kazi nzuri wao walikuwa na uoga wakimuogopa Nyerere. Wote wakanikatalia kukichapa kitabu changu. Ikabidi kitabu kichapwe Uingereza.

Ningefurahi sana kama maduka ya vitabu yangekiuza kitabu hiki lakini ni yale tu yalokuwa chini ya Waislam ndiyo inaelekea wanaokitaka kukiuza.
 
Ahsante kwa mawazo yako. Itakuwa bora sana endapo utakisoma kitabu. Baada ya hapo unaweza kutoa hukumu. Tatizo nilionalo katika mjadala huu ni kuwa wengi wanachangia bila ya kuwa na uelewa wa historia ya kudai uhuru wa Tanganyika.

Hii inasababisha wao kutoa maneno tu ya jumla na hili nimeliona hata kwako. Ningependa kukumbusha kama Muislam kuwa Allah katufunza adabu na hili ukizingatia hata katika maingilianao kama haya hujenga tija na mapenzi baina ya watu. Hapana haja ya kushambuliana kwa lugha kali.

Muhimu ni kusoma hoja na kujibu kwa utulivu. Hii huleta raha katika mjadala si kwa wale wanaoshindana bali hata kwa wasomaji wengine. Imam Shaffi kasema yeye anaweza kusimama kwa hoja hata na watu mia yeye akiwa peke yake lakini mjinga mmoja tu yeye huwa
keshashindwa.

Insha Allah tutaendelea kujadiliana na kuheshimiana katika maingiliano yetu hasa zaidi kwa kuwa wewe kama mimi ni Waislam na wasio kuwa Waislam watatuhukumu kwa akhlak zetu.

Hiyo hotuba iliyosomwa na Mwalimu Nyerere mwaka 1955 Umoja wa Mataifa ina kisa kirefu sana na cha kupendeza. Laiti ungekijua kisa chenyewe na watu walioandika na katika mazingira gani hadi ilipomfikia Nyerere 1955 kuna mengi naamini yangepita katika akili yako. Sasa hapo ungekuwa katika hali nzuri sana ya kuchangia. Inasemekana nyaraka hii ile yenyewe ambayo ina mkono wa Abdulwahid Sykes, Sheikh Hassan bin Amir, Hamza Mwapachu, Stephen Mhando imeondolewa katika Tanzania Nationa Archive (TNA) haipatikani.
Mkuu sielewi kama umeyaelekeza maneno yako kwangu au mtu mwingine lakini hata hivyo nitachukulia kwamba unanambia mimi kwa sababu ndiye mtu wa mwisho kuandika kabla ya majibu haya.

Mkuu Allah katufundisha adabu siikwa mwenye kuipokea ila adabu ni ile unayoitoa wewe. Kama wewe hutakuwa na adabu sijui ulitegemea adabu gani toka kwa wengine kwani kila napokusoma mkuu wangu unawashambulia hawa jamaa kwa lugha ya kupuliza lakini yenye makali ya kukata.

Na siwezi kusema mimi nazungumza kwa lugha kali isipokuwa lugha ya msisitizo ambayo inakutaka wewe uwathamini wengine, uchunge ulimi wako kwamba nao ni binadamu wenye hisia na imani sawa na yako japokuwa hazifanani, kisha walishiriki sawa ktk harakati hizo za uhuru kwa majukumu tofauti hata kama Waislaam ndio walikuwa wengi kwa hesabu ktk uongozi au lolote lile.

Hadi leo hii tunavyozungumza hapa hao CCM bara na Visiwani hawafiki hata Millioni 2, leo huwezi kunambia ati pasipo wao nchi hii isingekuwa huru au hatungeendelea haya ndio matusi ya nguoni ya wana CCM kila siku. Haya ni matusi makubwa kwa wananchi kwani hata siku moja jahazi haliwezi kuwa na nahodha 10 wala pasipo wapiga kasia..Maadam wananchi walikuwepo na waliunga mkono harakati za Uhuru mchango wao unasimama sawa na wale wanaoongoza.

Na Iman Shafi hakuzungumza hivyo kwa kuokoteza hoja isipokuwa alikuwa na maana na hadithi nyuma ya maelezo hayo. Elimu na historia ya Tanzania au Tanganyika haipo kwenye kitabu cha Mohamed Said isipokuwa ni Udini wako ndani ya historia hiyo. Na ndio maana unajibiwa kwa Udini vile vile..

Nimekisoma kitabu chako mkuu wangu na hakika wengi ya watu ulowaita Waislaam hawakufanya hata ibada ya sala zaidi ya kuzaliwa ndani ya Uislaam. Sasa ni kitabu (Kuran) kinatwambia kwamba tofauti baina ya Muislaam na Kafr ni SALA..kama ndivyo hayo mengine jazia mwenyewe...
 
Mohammed Said pamoja na kutokubaliana na wewe juu ya lawama zako kwa Nyerere,at least wewe na wengine have come out of the closet,na kukubali kuwa andiko lako ni ya kimsingi kutetea uislamu.
Huna haja ya kusubiri muda mrefu maana vitatoka vitabu vingi tu kupinga hilo.Hata kwa thread hii na thesis yako nadhani kuna material ya kutosha kurebute propagation zako.
Sasa ukweli utabakia palepale,elimu na maendeleo sehemu nyingi walizokaa waislamu ni duni. Ungeandika kitabu kingine kualleviate hali hiyo. La sivyo rudi kwa ushauri wa Nyerere, jengeni shule za msingi na sekondari maeneo yenu.Halafu watu waache uvivu,walime waache kucheza ngoma zisizo na tija. Maendeleo ni from within, huletewi on a silver platter.
 
Hapana haja ya kutukanana. JM inajisifu kuwa ni "forum of great thinkers." Wengi tumejiunganayo kwa ajili hiyo. Tufanye tu hoja kwa manufaa ya nchi yetu. Kwa hakika watu hawawezi kukubaliana katika kila kitu lakini hili lisiwe sababu ya kuvunjiana heshima.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom