Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Status
Not open for further replies.
Lole Gwasika,
Sasahapo mkuu ndio tunaanza kuto fautiana.
Wakati mwarabu alikuwa na dini yake ya Uislamu, Mzungu naye aliingia na dini yake ya Ukristo. Sehemu walizo kaaa hawa wakolni(wote wazungu,waarabu) waliibadili jumuia hiyo kuingia dini zao.
Inawezekana kabisa resistance ya waarabu kwa ukoloni wa kizungu ilikuwa kutohusiana kwa aina yoyote socially na mikakati ya wazungu.
Hii inajidhihirisha hata pale Zanzibar kwani mkoloni pale alikuwapo lakini maendeleo ya kielimu bado hayakuwa makubwa sana.
Hii inaweza kuwa mada kubwa sana ya utafiti lakini ukweli ni kuwa alipokuwepo mwarabu mkoloni mzungu hakupashughulikia sana kama pale alioishi mwenyewe.
Nimekuapata lakini bado unaichanganya historia yetu.. waarabu walikuja nchini hata kabla ya karne hizo na hawakuja na Uislaam au kueneza Uislaam isipokuwa kufanya biashara. Zipo kumbukumbu nyingi zinazoonyesha walikuja kabla hata ya Uislaam wenyewe. Kwa mfano Persian Na Washiraz walikuja pwani zetu kununua bidhaa kabla hata huyo Sultan wa Oman hajaweka mguu wake pwani ya Mombasa baada ya kukimbia Muscat. Na hata Sultan alipochukua nchi na kuweka kambi yake Zanzibar (in hiding) hakuwa mtawala kama Muingereza alivyokuwa Bara na Kenya.

Na hata Mapinduzi ya Zanzibar mbona huyo Sultan alikimbilia Uingereza na sio kurudi kwao. Utawala wa Sultan Zanzibar ulikuwa ni wa mkimbizi aliyepata hifadhi na kuanza makazi mapya tofauti na hizi historia tunazopewa. Kisha nashindwa kuelewa unapojaribu kulkinganisha nguvu ya Malkia wa Muingereza, Mjarumani au mreno na Sultan wa Oman
Oman of all countries -waliokuwa maskini hata kutuzidi sisi! unaiweka hoja yako ktk misingi ya dini yao na sii kwamba Oman was poor kama sisi wenyewe..I mean mkuu nashindwa hata kukuelewa kabisa kama kweli wewe unafikiria kuwa mkoloni huyo Sultan wa Oman angeweza kuiendeleza Tanzania kama angekuwa Mkristu..
 
Huwezi kujua anavyohisi yatima hadi nawe uwe umepoteza wazazi wako. Ikiwa utajibu kistaarabu tunaweza tukaendelea na mazungumzo lakini ikiwa lugha ndiyo kama hivi kwangu huwa naishiwa na hoja. Napenda mijadala lakini sipendi kuvunjiana heshima. Haya ndiyo mafunzo katika Uislam.

Kwa hiyo asiye yatima hawezi ku-sympathise na yaliyompata yatima? Vile hauwezi kujua yanamsibu mwanamke kama wewe sio mwanamke. Au katika mjadala huu, hauwezi kujua machungu ya muislamu kama wewe si muislamu? Sasa muislamu naye atajuaje machungu ya mkristu kama yeye si mkristu? Kutoa mfano wa yaliyompata mtu mmoja haiwezi kuwa uthibitisho wa ubaguzi wa aina fulani. Hoja yako ingekuwa sahihi kama ungeonyesha kuwa huyo bosi unayemzungumzia alikuwa hahoji vyeti vya wakristu waliomzidi unless unataka kutuambia kuwa aliyemzidi elimu yake ya diploma alikuwa ni muislamu peke yake. Kwa kukimbilia kwenye dini na kutoangalia parameters (kabila, class, jinsia n.k.) nyingine zimenionyesha jinsi ulivyoweka mbele udini. Na hii vile vile natokana na kuchukua simulizi za mtu mmoja ( ambae kwangu mimi ni disgruntled individual) bila kujaribu kuwauliza wengine waliokuwepo wakati huo kama wakina Chief Patrick Kunambi n.k. na kugeuza kama ushahidi tosha wa chuki na unyanyasaji wa mkristu Mwalimu dhidi ya waislamu! Unapoacha kupima simulizi za mtu huyo na ushahidi uliokuwemo kwenye maelezo yake ( wakristu, pamoja na waislamu, kuwemo kwenye harakati za ukombozi na kutotendewa haki baada ya uhuru) na kutaka kulazimisha kuwa bado huo unaouita kuwa ni kutothaminiwa kwa baadhi ya watu, ulifanywa kwa msingi wa dini inaonyesha unakotokea. Na mtu anayefanya hivyo, kwenye kitabu changu, ni mtu muovu ambaye anataka kuchochea hisia za kuonewa kwa upande mmoja ili chuki ijengeke dhidi ya wale wanaowaonea. Na katika kitabu changu vile vile, mtu kama huyo hastahili uvumilivu na anabidi akemewe kwa sauti kubwa. Sasa kama unaona kwa kuambiwa kuwa unachofanya ni hatari na yanaongozwa na udini na chuki dhidi ya wengine basi "so be it". Dini yangu ya kikristu inasisitiza uvumilivu na upendo lakini vile vile inatuambia tukemee uovu tunapouona. Kama unaona nimekutukana una haki ya kuniripoti kwa moderetaz ambao hawatasita kunifungia.

Amandla na karibu J.F.
 
Mambo haya yana uzuri mmoja. Huwezi kujua hatari na shida zake hadi uwe muathirika. Ukiwa hubaguliwi huwezi kujua ukweli wa mambo wala hutoshangaa kujikuta nyie wa dini moja ndio mlohodhi kila kitu. Iwe shirika au idara ya serikali. Meneja mmoja alipata kudai uthibitisho wa elimu ya Muislam kama kweli kasoma kwa kiwango kile jalada lake linavyoonyesha. Yule Muislam aloandikiwa barua ya kuleta vyeti vyake halisi kutoka vyuo vyote alivyosoma ndani na nje ya nchi akashangaa. Hakuamini macho wala akili zake. Akawa anawaza vipi huyu Mkristo mwenye diploma tu haamini vyeti vyangu wakati mimi nimemshinda kwa kisomo katika nyanja zote lakini yeye kanipita kwa mbali kwa cheo hapa shirikani? Wa kushtushwa na elimu ni nani? Ni mimi Muislam kuwa juu ya elimu yote hii nilonayo sikupanda cheo kapanda yeye Mkristo wa diploma au mimi? Basi yule Muislam akamjibu yule mkuu Mkristo barua ya mstari mmoja. Akasema je, hivyo vyeti unavyovitilia shaka umeviona katika jalada langu? Ujumbe ukawa umemfikia kwa haraka sana yule mkuu. Mambo ndiyo haya.

Lakini muhimu tujadili historia ya uhuru wa Tanganyika na mashujaa wake ambao wamefutwa katika historia yab nchi yetu. Hii ndiyo mada kuu na husika katika mjadala huu.

Hapa ndipo tunapotafautiana sana huyu Mkuu Mohammed Said, yeye anaona mambo yoote katika vivuli vya Ukristo au Uislamu.
Je ameona hawa wenzetu wengine mwaziri(wenine waKristo na wengine waIslamu) wenye vyeti vya PhD , vyeti vya kughushi?
Na bado wanapeta.
 
Domokaya, domokaya, domokaya - baada ya kutoa kauli kama hii ni mwenda wazimu tu ataweza kuendelea kujadiliana na wewe, adieus !

Nimecheka saana na hii comment!!
Lakini its an exasperation as a reaction to the extent that some of our fellow Tanzanians will go to make their ill intentions towards unity.
 
Unachosema kina mantiki wala si uongo lakini nasisitiza kuwa hali ya Waislam na sisi Waislam tunavyoijua na mbali na fikra kama hizo. Dini ya Kiislam inahimiza sana ustahamilivu na amani lakini hapo hapo imekataza kudhuluma au kukubali kudhulumiwa. Katika "Mwembechai Killings" mwandishi Prof. Hamza Njozi alieleza jinsi mtandao wa Kanisa unavyofanya kazi katika kuwakandamiza Waislam. Serikali haikutaka kitabu hicho kisomwe na kama Prof. Njozi kasema uongo ajibiwe. Kitabu kikafungiwa ikawa ni kosa la jinai kukutwa na kitabu hicho.

Mimi baada ya kuona kuwa historia ya uhuru wa Tanganyika imepotoshwa nikaamua kuandika hicho kitabu pamoja na kitabu nimekuwa nikialikwa na Waislam wakiwa na hamu ya kujua historia yao. Hadi leo hakijaandikwa kitabu cha kupinga yale nilosema ndani ya kitabu kile. Ndiyo maana hata hapa unaona nimeliweka jina langu wazi bila kificho kwani naweza kusimama popote na yoyote kwa hoja bila hofu yoyote.

Kwa kumalilza napenda kukushukuru kwa mjadala wako kwa jinsi ulivyoandika kwa ustaarabu. Umenipa faraja na raha. Tuendelee na mazungumzo.

Mohamed Said Salum Abdallah.
 
Lole Gwasika,

Nimekuapata lakini bado unaichanganya historia yetu.. waarabu walikuja nchini hata kabla ya karne hizo na hawakuja na Uislaam au kueneza Uislaam isipokuwa kufanya biashara. Zipo kumbukumbu nyingi zinazoonyesha walikuja kabla hata ya Uislaam wenyewe. Kwa mfano Persian Na Washiraz walikuja pwani zetu kununua bidhaa kabla hata huyo Sultan wa Oman hajaweka mguu wake pwani ya Mombasa baada ya kukimbia Muscat. Na hata Sultan alipochukua nchi na kuweka kambi yake Zanzibar (in hiding) hakuwa mtawala kama Muingereza alivyokuwa Bara na Kenya.
Mkandara Mkuu, sasa we at our bone of contention.
Jinsi gani wewe umuonavyo mwarabu na vile mimi ninavyo mchukulia.
mimi namwaona mwarabu kuwa ni mkoloni vilevile,, wa kuja, na wakutuletea utamaduni wake wakati hapa kwetu tlikuwa na wakwetu.
Pamoja na kuwa hawa waarabu walikuja kwa biashara, walieneza Uislamu katika sehemu zote walizokaa.
Hebu tazama excerpts from Wikipedia,

"Islam was spread mainly through trade activities along the East African coast, not through violent conquest and territorial expansion as was mostly the case in North Africa, but remained an urban littoral phenomenon for a long time. When the violent Portuguese intrusions in the coastal areas occurred in the 16th century, Islam was already well established there and almost all the ruling families had ties of kinship with Arabia, Persia, India and even Southeast Asia owing to their maritime contacts and political connections with the northern and eastern parts of the Indian Ocean. In the end of the 17th century and beginning of the 18th century the coastal Muslims managed to oust the Portuguese with the help of Oman. The Omanis gradually increased their political influence until the end of the 19th century when Europeans arrived at the coast of East Africa.
During the time when Oman dominated the coast politically, the spread of Islam intensified also in the interior of East Africa. Trade contacts with peoples in the interior, especially the Nyamwezi, gained importance and places like Tabora in Nyamwezi territory and Ujiji at Lake Tanganyika became important centers in the ever-increasing trade in slaves and ivory. Many chiefs, even in parts of Uganda, converted to Islam and cooperated with the coastal Muslims. Trade served to spread not only Islam, but also the Swahili language and culture. Before the establishment of German East Africa in the 1880s the influence of the Swahilis was mainly limited to the areas along the caravan routes and around their destinations."

Sasa Mkuu Mkandara unapotofautisha biashara ya waarabu na dini yao hili halikubaliki.Na pengine hii inaweza kuwa na a more sinister motive kuwa hawa jamaa , waarabu, hawakuwa na hisia yoyote ya kumwendeleza mwafika waliyemkuta.Hii inamaanisha nini kama si dharau kuwa mwafika hawezi kuendelea kama wao waarabu.
Nimesema hapo nyuma kuwa si kwamba waarabu hwa kuwa na elimu ya kutosha , walikuwa mabingwa katika kusafiri kwa kusoma nyota na vile vile al-gebra, somo ambalo ni moto hata leo.
Swali kuu la kujiuliza ni kwanini mpaka siku ya leo sehemu ambazo mwarabu alikaa elimu bado duni sana.
Hii ni pamoja na Zanzibar ambako mwarabu alilowea mapema zaidi.
Tukiweza kuyajibu maswali haya pengine tutaweza kupata mwanga wa kwanini waislamu wamekosa elimu kwa ujumla kuliganisha na sehemu nyingine.
Mimi si muislamu lakini tukipata mawazo ya ndugu zetu waislamu itapendeza.
 
Fundi Mchundo,
1. Umesema kwamba wewe ulipokuwa ukisoma (wakati wa mkoloni), ulisoma na Waislaam na Sheikh alikuwa akija kutoa mawaidha.. please naomba unipe jina la shule hiyo au hizo ili nipate kuelimika zaidi.

Mkuu, nilisoma na waislamu na alikuwa anakuja shehe siku moja kwa wiki kuwaelimisha ( sijui tofauti ya kutoa mawaidha na kuelemisha ninachojua walikuwa na darasa lao) wanafunzi wa kiislamu. Hii ilifanyika hata kwa wanafunzi wa madhehebu mengine ya kikristu. Samahani Mkuu, sitaki kukupa jina la shule hiyo au shule hizo. Ni juu yako kuniamini au kutoniamini.

Mkuu wangu tunachozungumzia ni mchango wa Mkoloni ktk kudumaza elimu ya Waislaam, mila na desturi za watu wa Pwani hazihusiani kabisa na kukubaliwa ku register shuleni. Na hakika hadi kufikia Uhuru ni mkoa wa pwani ulikuwa na shule nyingi kuliko mikoa ya bara sasa hatuwezi kusema wazungu walikuwa wajinga kujenga shule zao pwani hali wakijua fika kwamba watu wa pwani hawapendi kusoma..

Hi ni tofauti kidogo na ulichosema mwanzo ambapo ulitupia lawama zote ukoloni. Sasa kama unasema pwani kulikuwa na shule nyingi kuliko bara na hapo hapo unatuambia kuwa wakoloni hawakutaka uwaandikisha watoto wa kiislamu katika shule zao, nani basi alikuwa akisoma kwenye hizo shule zilizokuwa katika hayo maeneo ambako waislamu walikuwa ndiyo sehemu kubwa mno ya jamii? Watoto wote wa kiislamu walijifanya kuslimu na kujiita Moses badala ya Musa? Au wakristu kutoka bara ndio walikuwa wakiandikishwa? Wakina Jakaya waliitwa John walipoandikishwa kwenye shule ya misheni, Bagamoyo?

Sijasema kuwa watu wa pwani hawapendi kusoma bali kuwa msisitizo wao kwenye baadhi ya mila na desturi zao zilikuwa ni kizuizi kwao kuendelea vizuri katika shule zilizokuwa based kwenye mfumo wa magharibi. Kama mtu ali-priotise zaidi shughuli za jando na unyago, ingewawia vigumu sana watoto wao kuendelea na shule. Hii haikuwa kwa watu wa pwani peke yao. Makabila kama ya wamasai nao walikumbwa katika mtego huo. Kuna sehemu Tanganyika na baadae Tanganyika, wazazi walikuwa wakiwahonga walimu ili wafelishe watoto wao! Watu kutoka makabila yaliyokuwa na msimamo tofauti walipeleka watoto wao katika maeneo hayo ili waweze kupasi kirahisi. Wengine walichukuwa majina ya watoto ambao wazazi wao hawakutaka waendelee na shule. Huu ndio ukweli wenyewe, amini usiamini.

All glory ni ya Mwenyezi Mungu hivyo unaponambia kwamba kudumazwa kwa elimu ya waislaam nchini kunatokana na sisi wenyewe kuchagua dhehebu la sunni nashindwa kabisa kukuelewa kwani kiutawala haikutakiwa kuwa hivyo. Utawala wowote wa nchi hautakiwi kushirikisha dini ktk maendleleo ya wananchi wake isipokuwa kiroho..

Hapa haunitendei haki. Hakuna mahali ambapo nimesema kuwa kuCHAGUA kwenu dhehebu la Sunni kumesababisha kudumazwa kwa elimu ya waislamu. Nitasemaje hivyo wakati nimetoka kukupinga kwa kupeleka lawama zote upande mmoja, hususan ukoloni? Naamini kuwa imani ilikuwa ni MOJAWAPO ya sababu zilizochangia kudumaa kwa hiyo elimu kwa sehemu kubwa ya waislamu ( waismailia kwa mfano hawamo humu). Naamini kuwa kuna waislamu ambao walikataa kuwapeleka watoto katika shule za kimisheni kwa kuogopa kuwa wataslimishwa. Vile vile naamini kuwa kuna baadhi ya shule za wamisheni ziliweka vikwazo kwa waislamu kusoma ili kujaribu kuwabadilisha dini. Lakini si waislamu wote walioogopa kuwapeleka watoto wao katika shule za kimisheni na sio shule zote za wamisheni ziliweka vikwazo hivyo. Na ninajua sana kuwa wewe ni msunni maana si mara ya kwanza mimi na wewe kujadiliana masuala haya.

Kama umewahi kunisoma mimi huko nyuma nimekuwa mpinzani mkubwa wa swalka la AFYA na ELIMU kuachiwa vyombo binafsi kuendesha kwa sababu naamini kwamba hizi ni haki za kila binadamu na ni jukumu la mtawala kuhakikisha vitu hivyo anavipata mwananchi wake. Na ndio maana hata tunapopima maendeleo ya nchi ktk elimu au afya huwa tunalaumu utawala uliopo na sio mashirika binafsi. Tunatazama nguvu ya seriukali iliyotenga kupambana na adui hawa na sio kuwaachia missionaries ku deal la shida zetu za kidunia.

Kwa hiyo, Mkuu, unataka serikali wapige marufuku vyombo binafsi kushiriki katika utoaji wa elimu na huduma za afya? Ni kosa kweli kwa serikali kuachia masuala haya kwa vyombo binafsi peke yao. Lakini sidhani kama itakuwa busara kutoshirikiana nao pale wanapoweza. Serikali inatakiwa ku-regulate na kuhakikisha kuwa wananchi wote wanakuwa na haki ya kutobaguliwa kwa misingi ya rangi, dini, ulemavu au jinsia katika shule zote nchini. Serikali haina uwezo na ujuzi wa kutoa huduma zote hizi peke yake. Wamisheni na watu wa madhehebu mengine (waismailia, mabohora na wahindu) waliongezea tu pale palipokuwa na upungufu. Sidhani kama kuna nchi duniani ambako huduma za afya na elmu zinatolewa na serikali peke yake.

Kwa hiyo naweza kusema kwamba Waislaam wanapolalamikia swala hili ni kutokana na kwamba serikali yetu imesahau wajibu wake na kuiga baadhi ya tamaduni au ibada za dini fulani kufanya sheria kwa watu wote..Yes, ktk dunia ya leo ni kilema kikubwa kwa waumini wa sunni kutokuwa organised kwa ajili ya maendeleo yao kama walivyo Wakristu au Wahindi kina Agha Khan lakini pia kukubali kuwa na Organisation kama hizi kunawapa nguvu hawa viongozi kuwa MIUNGU WATU.

Wanakuwa wakiabudiwa jambo ambalo mfuasi wa Sunni hawezi kulikubali kiimani hata siku moja. Na ndio maana kina Shaban Nasibu wakatuletea Bakwata wakifikiria wanaweza kuwaongoza Waislaam kwa kupitia nguvu za watu ikashindikana. sasa wamekuja na mpya ya kutumia Kadhi ambayo pia imeleta utata na kufikia waislaam wa Tanzania kuanza kuwa na makundi ndani ya sunni. Mwezi unaandama ati wamsubiri Kahi mkuu aseme.... hapo ndipo mtu kama mimi sintakubaliana naye na sababu ninazo.

Sijasema kuwa hierarchical systems za wakristu, washia n.k. ni bora. Tunajua matatizo yanayowakumba wakatoliki hasa katika nchi za magharibi kutokana na uongozi wao kufumbia macho vitendo viovu vinavyofanywa na baadhi ya mapadiri. Tunajua wote kilio cha mabohora kuhusu madai ya michango kila akija kiongozi wao.Yote haya ni mapungufu. Lakini pamoja na haya, mshikamano huu unawapa nguvu za pekee kushughulikia matatizo ya kidunia yanayowasibu waumini wao. Mimi nilitoa mfano wa system hizi kujenga hoja kuwa si sahihi pale baadhi ya wasunni wanapotaka kujilinganisha na wakatoliki. Nadhani kuwa pale Bakwata itakapokuwa na nguvu sawa na vyombo kama hivyo vya wakristu na washia basi wasunni watakuwa wamepoteza kitu muhimu kinachowatofautisha na wengine. Hiki ni imani yao kuwa hakuna mtu anayetakiwa kuwatenganisha kati yao na Mungu wao. Kadhi hata siku moja kwa wasunni hawezi kuwa kama Kadinali kwa wakatoliki.

Yote haya yanatokana na kujaribu ku introduce mila na culture za madhehebu mengine ambayo kiimani hayakubaliki ndani ya sunni. na kama unakumbuka Mstaafu Alhajj Mwinyi alichukua kofi la kerbu alipozungumza ujinga. Hii ndio dini ya Sunni na kusema kweli malalamiko yao yooote ni kutokana nakwamba Sunni ni dini na hawana ushiriki ktk ibada zao na maswala ya kidunia. Ni kazi ya serikali kufuatilia mabo ya kidunia na dini inajihusisha na maswala ya dini tu kila mmoja wetu akiwa na nafasi sawa mbele ya Mwenyezi Mungu.

Sawa kabisa. Lakini hii isiwazuie wale wasio wasunni kujifanyia mambo yao jinsi wanavyoelekezwa na imani yao ili mradi hawaingilii haki za wasunni. Wasunni wanapaswa kutafuta njia mbadala ambayo haitabadilisha imani yao.


Amandla......
 
Unachosema kina mantiki wala si uongo lakini nasisitiza kuwa hali ya Waislam na sisi Waislam tunavyoijua na mbali na fikra kama hizo. Dini ya Kiislam inahimiza sana ustahamilivu na amani lakini hapo hapo imekataza kudhuluma au kukubali kudhulumiwa. Katika "Mwembechai Killings" mwandishi Prof. Hamza Njozi alieleza jinsi mtandao wa Kanisa unavyofanya kazi katika kuwakandamiza Waislam. Serikali haikutaka kitabu hicho kisomwe na kama Prof. Njozi kasema uongo ajibiwe. Kitabu kikafungiwa ikawa ni kosa la jinai kukutwa na kitabu hicho.

Mimi baada ya kuona kuwa historia ya uhuru wa Tanganyika imepotoshwa nikaamua kuandika hicho kitabu pamoja na kitabu nimekuwa nikialikwa na Waislam wakiwa na hamu ya kujua historia yao. Hadi leo hakijaandikwa kitabu cha kupinga yale nilosema ndani ya kitabu kile. Ndiyo maana hata hapa unaona nimeliweka jina langu wazi bila kificho kwani naweza kusimama popote na yoyote kwa hoja bila hofu yoyote.

Kwa kumalilza napenda kukushukuru kwa mjadala wako kwa jinsi ulivyoandika kwa ustaarabu. Umenipa faraja na raha. Tuendelee na mazungumzo.

Mohamed Said Salum Abdallah.

Mkuu, hapa sijui unamzunguzia nani lakini kama ni mimi nashukuru kwa kunielewa. Kama sio, nakushukuru pia kwa kukubali kuendelea na mjadala.

Amandla.....
 
jokaKuu,
Umesema jambo la maana sana. Watanzania tuache uvivu wa kusoma vitabu na tujitume kuandika vitabu. Wakati Mwalimu anaingia mamlakani kulikuwa na ombwe la elimu, usomi, utafiti, kila kitu. Lakini inaonekana kuna wanaomlaumu Mwalimu eti alijaribu kupotosha historia ya uhuru wa Tanganyika. Hapana. Huyu huyu Mwalimu tulimtegemea atuundie serikali, atujengee shule, hospitali, na pia atuandikie historia yetu? Saa ngapi? Ni kweli historia ya kwanza ya harakati za Tanganyika iliandikwa na wazungu. Lakini sasa tumesoma, utafiti tunauweza, sources zipo, tujitahidi tuandike na kujazia au kusahihisha pale Mohammed Said alipokosea. Utafiti hauna kikomo na historia si moribund. Juzi nimeshangaa kusoma mahali jinsi mabaharia wa Massachussetts walivyomsaidia Jemadari Washington. Historia hii haifundishwi shuleni hapa Marekani, lakini ukifanya utafiti kidogo utaipata.

Mkuu, siku zote historia inaandikwa na aliye na nguvu. Huko marekani ni hivi karibuni tu ndiyo mchango wa watu weusi na wengine katika historia ya marekani umeanza kuwekwa wazi na kuthaminiwa. Ni hivi karibuni tu ndiyo extent ya dhuluma iliyofanywa na watu weupe dhidi ya wamarekani wa asili imeanza kuthaminiwa. Karibu dunia nzima, historia inaangaliwa upya ili kuupa uzito unaostahili mchango wa wanawake. Lakini katika yote haya, mchango wa yule anayewadhulumu wenzie hautupwi jalalani. Vitendo vya mtu mmoja au wawili wa kikundi fulani si ushahidi tosha kuwa ali/walikuwa wanawakilisha kikundi chote. Kwa hali hiyo kuchukuwa vitendo vya Julius Nyerere na Benjamin Mkapa kama ushahidi wa mkono wa wakatoliki katika hujma dhidi ya waislamu si haki na ni hatari maana hawa hawajawahi kuwa wawakilishi wa wakatoliki. Vile vile kuchukua vitendo vya Ali Hassan Mwinyi na Jakaya Kiwete kama ushahidi wa mkono wa waislamu katika hujma dhidi ya wakristu si sahihi na ni hatari pia. Ndio maana kwangu mimi watu wanaofanya hivi hawastahili kuitwa historians bali wachochezi. Kama Mohamed Said angeandika kuhusu mchango wa waislamu katika harakati za kugombea uhuru, ningemshukuru sana. Lakini pale anapodai kuwa kusahauliwa huko ni ushahidi wa namna ukristu ulivyowa-oppress waislamu, hapo tutatofautiana kwa nguvu. Mimi nimesoma katika shule za kikristu na ninaenda kanisani kila mara na hata siku moja sijawahi kufundishwa kuwa niwachukie waislamu kwa sababu ni inferior kwetu. Kuwa tuko tofauti kiimani na kuwa wataenda motoni pamoja na wale wote wasio wakristu hiyo nimefundishwa (kama vile ninvyoamini rafiki zangu waislamu wanavyoamini kuwa mwisho wangu ni jehanam). Lakini kuwa ni inferior, na niwanyime haki na niwapendelee wakristu wenzangu, hapana, hapana, hapana. Sasa hao wakina Nyerere, Mkapa na wengine walikuwa indocrinated wapi kama sio huko kwenye shule na sehemu za ibada zao?

Amandla........
 
Mkuu, siku zote historia inaandikwa na aliye na nguvu. Huko marekani ni hivi karibuni tu ndiyo mchango wa watu weusi na wengine katika historia ya marekani umeanza kuwekwa wazi na kuthaminiwa. Ni hivi karibuni tu ndiyo extent ya dhuluma iliyofanywa na watu weupe dhidi ya wamarekani wa asili imeanza kuthaminiwa. Karibu dunia nzima, historia inaangaliwa upya ili kuupa uzito unaostahili mchango wa wanawake. Lakini katika yote haya, mchango wa yule anayewadhulumu wenzie hautupwi jalalani. Vitendo vya mtu mmoja au wawili wa kikundi fulani si ushahidi tosha kuwa ali/walikuwa wanawakilisha kikundi chote. Kwa hali hiyo kuchukuwa vitendo vya Julius Nyerere na Benjamin Mkapa kama ushahidi wa mkono wa wakatoliki katika hujma dhidi ya waislamu si haki na ni hatari maana hawa hawajawahi kuwa wawakilishi wa wakatoliki. Vile vile kuchukua vitendo vya Ali Hassan Mwinyi na Jakaya Kiwete kama ushahidi wa mkono wa waislamu katika hujma dhidi ya wakristu si sahihi na ni hatari pia. Ndio maana kwangu mimi watu wanaofanya hivi hawastahili kuitwa historians bali wachochezi. Kama Mohamed Said angeandika kuhusu mchango wa waislamu katika harakati za kugombea uhuru, ningemshukuru sana. Lakini pale anapodai kuwa kusahauliwa huko ni ushahidi wa namna ukristu ulivyowa-oppress waislamu, hapo tutatofautiana kwa nguvu.

Amandla........


Mkuu Fundi Mchundo umemaliza yote kama hitimisho, ingawaje mjadala huu ni mzito sana na si mwepesi kama mtoa mada wa awali, ndugu Mohammed Said na Al Saidy walivyouleta.
Nimefaidika sana na michngo yote mimi binafsi ingawaje nimejifunza kuwa wengine wanajadili mambo mazito kama haya kutokana na hisia za kidini na mwelekeo wao kidini.
Pale unapoanza kulaumu wengine bila kuwa na facts zilizosimama basi hata adui yako unakuwa humjui,sana sana unongea na kuvuli cha matatizo yako.Hivyo basi kuweka sawa matatizo yaliyojitokeza katika jamii ni wazi kuwa mtoa mada akitaka kupata msaada wa jamii hiyo hiyo kutatua matatizo, inabidi mada ikae katika muundo wa ukweli na unaeleweka na jamii hiyo hiyo.
Kulazimisha kuweka mambo sawa bila ukweli kuheshimiwa ni sawa na kuanzisha fujo ambaya mwisho wake hata mtoa mada hana uhakika kama anaweza kuudhibiti.
Zaidi ya yote kuli dhalilisha jina la Nyerere leo hii bila kuweka ukweli bayana ni kujitengenezea uadui tu na wale wanaoufahamu vyema ukweli huo.
Hii haimanishi kuwa sehemu walizo kaa waislamu ziko nyuma ,la hasha , lakini kubadilisha hali hiyo inabidi kuanza from basic principles, kama Mwalimu alivyosema ,lazima tuanze na kujenga shule za msingi zaidi na watoto lazima waende shule..
 
Mkuu, nilisoma na waislamu na alikuwa anakuja shehe siku moja kwa wiki kuwaelimisha ( sijui tofauti ya kutoa mawaidha na kuelemisha ninachojua walikuwa na darasa lao) wanafunzi wa kiislamu. Hii ilifanyika hata kwa wanafunzi wa madhehebu mengine ya kikristu. Samahani Mkuu, sitaki kukupa jina la shule hiyo au shule hizo. Ni juu yako kuniamini au kutoniamini.
Fundi Mchundo,
Kwa hili nitakusaidia kwa sababu experience yako inafanana kidogo na yangu. Mimi nilisoma Nyasho Middle School (Musoma) 1960-1963 na pale walikuwepo waislamu, wakatoliki, wasabato, na wamennonite. Kila ijumaa Waislamu walikuwa na darasa lao maalumu la dini na alikuja Sheikh pale kuwasomesha. Sisi wengine kwa sababu tulikuwa tunasali jumamosi/jumapili hatukulazimika kuletewa mapasta pale lakini headmistress wetu alitangaza kuwa kama kuna yeyote anayetaka aletewe kiongozi wa dini ijumaa wakati wenzetu waislamu wanasalishwa ilikuwa ruksa. Sisi wengine tuliamua kutumia muda huo kucheza mpira. Si unajua tena ujana. Na hii ilikuwa shule ya serikali.
 
Fundi Mchundo,

..hata mimi wakati nipo shuleni tulikuwa na vipindi vya dini na waalimu kutoka madhehebu mbalimbali walikuwa wanakuja kufundisha.

..kitu nilichokiona ni kwamba waalimu Wakatoliki ndiyo walikuwa hawakosi kuja kutoa mafundisho kwa waumini wao.

..sisi wengine kwa utukutu tulikuwa tunaenda kupiga soga kwenye darasa lilolokuwa dedicated kwa Waislamu kwasababu wao kwa muda mrefu sana walikuwa hawana waalimu wa dini yao.

..nadhani tukielewa mfumo wa utawala, na uongozi, wa Wakatoliki, na jinsi ulivyo mkongwe, tunaweza kupata majibu ya maswali yetu mengi kwamba kwanini linapokuja suala la huduma za kijamii[shule,zahanati,...] madhehebu haya yawaacha wenzao kwa mbali sana.

..umeelezea vizuri sana tatizo la mfumo wa uongozi ktk madhehebu ya Kiislamu. kutokuwepo kwa mamlaka ya aina yoyote ile inayoratibu masuala ya kiimani na kijamii ktk madhehebu ya Kiislamu ni moja ya chanzo kinachodumaza maendeleo yao.

..binafsi nasikitishwa sana na Waislamu wanaofanya kila juhudi kuipinga Bakwata. naamini chombo hiki kinapaswa kuungwa mkono zaidi na Waislamu bila kujali mazingira yaliyopelekea kuanzishwa kwake. Muslims should work to save Bakwata now.

..siamini kwamba kuna mikoa ambayo serikali zetu imeamua kuitenga kwa makusudi. wanaodai kwamba kuna mikoa ya kaskazini inapendelewa waitaje mikoa hiyo, na waeleze serikali imefanya nini cha maana ktk mikoa hiyo.

..mkoa kama Kilimanjaro ukiungalia ni mdogo sana kuweza kudai kwamba ndiyo umetafuna hazina yote ya taifa mpaka kupelekea Tanzania nzima kudumaa kimaendeleo. lakini vilevile lazima u-appreciate bahati iliyokuwa nayo mkoa huo kwa kuwa kitovu cha zao la kahawa. miundo mbinu mingi iliyoko Kilimanjaro iliachwa na mkoloni, tofauti na maeneo mengine ambapo mkoloni hakuacha kitu chochote kile.

..pia kuna maeneo kama ya kusini ambako wakoloni waliyatawala kikatili, na kuyafanya maeneo rasmi ya kusomba manamba kwenda kufanya kazi kwenye plantations. mkoloni hakuanzisha zao lolote lile la biashara ktk maeneo hayo kwasababu hakutaka kabisa wananchi wa maeneo hayo wainuke kiuchumi.

..serikali ilijaribu kusaidia mikoa ya kusini kupitia ile experiment ya operation vijiji. tatizo ni kwamba the experiment failed so badly kiasi kwamba ikawaongezea matatizo juu ya yale waliyokuwa nayo. wananchi wa kusini wameathirika zaidi kutokana na kuanguka kwa zao la korosho, na si kutokana na wananchi wa kaskazini kupendelewa kuliko wao.

..binafsi naamini kuna factors nyingi sana za kuangaliwa kuliko ku-focus kwenye Waislamu vs Wakristo.

NB:

..maeneo ambayo wananchi wake wanajiona wameonewa na serikali ndiyo hayo hayo yanaongoza katika kuipa ushindi wa kishindo CCM.
 
Fundi Mchundo,
Mkuuu sii vizuri kubishana ili mradi tunabishana, haina radha hata kidogo.
Ni wewe ulosema ulipokuwa ukisoma shule (wakati wa mkoloni), waislaam nao walikuwa na darasa lao. Na binafsi sijawahi kusikia wala kusoma na mtu aliyepitia shule hiyo wakati wa mfumo wa mkoloni. Itakuwa vizuri sana kama utanielemisha ili nami kesho naweza kutumia mfano huu. Hatubishani, Nipo hapa kujifunza na kuandika ninayoyajua mimi. Kama wewe una taarifa tofauti ni vizuri kuiandika tofauti hiyo ili tuweka vitu sawa.

Pili, Muda wote nimewalaumu wakoloni kwa sababu kuna mchanganyiko wa lawama hapa. Yaani Mohammed Said akiwalaumu Wazungu, Nyerere na wakristu kwa kuwaangusha Waislaam, Na kina Lole Gasika wakitumia mfano huo huo kuonyesha kwamba ni waarabu wakoloni hao ndio sababu ya Waislaam kuwa chini kielemu. Yaani sote tunatafuta mchawi wa kidini kwa kujibu hoja iliyoandikwa na sii kutafuta ukweli wa kile kilichotokea.

Sasa umeuliza swala la Pwani kuwa na shule nyingi kuliko bara lakini Waislaam wengi hawakuwa na elimu.. jambo ambalo wewe halikuingii akilini..Nadhani mkuu wangu hukuisoma hoja hii kwa makini zaidi. Kwani kama Pwani ndio ilikuwa na shule nyingi zaidi ya bara yet waislaam hawakupa elimu (fact) basi kuna sababu ya hao waislaam kutopata elimu hiyo na ndio madai ya kina Mohammed Said yanapokuja kwamba Waislaam walibaguliwa. Ubaguzi siku zote hutokea pale mtu anapoanzisha kitu in your face na hakuruhusu wewe kujoin, tofauti na mtu kwenda jenga kitu mbali na wewe kisha ukadai unabaguliwa hali huna acceess ya kufika huko.

Kwa hiyo kifupi ni kwamba maadam Waislam wengi waliishi Pwani na shule nyingi zilikuwepo Pwani lakini kati ya wakazi wa Pwani waislaam waliachwa nyuma. basi bila shaka Mkoloni alikuwa na mbinu za kuwazuia waislaam na sii watu wa pwani kuingia shule, na kumbuka tu kwamba hao watu wa Pwani walikuwa na mila na jadi sawa pasipo kujali dini zao. Mimi nazungumzia hoja ya waislaam kukosa elimu na sio watu wa Pwani kwa ujumla, wakristu wengi waliosoma wakati wa mkoloni walisoma pwani vile vile kuliko bara..

Swala la imani ya Sunni,
Mkuu wangu sikukulaumu isipokuwa nilikuwa nakujulisha ugumu wa wafuasi wa Sunni kuunda jumuiya inayowawezesha ktk maswala ya Kidunia. Ndipo niliposema kwamba Sunni wanaheshimu dini kama ni chombo cha kiroho na inapofikia maswala ya utawala hawa sunni wanatakiwa kuwaheshimu viongozi wao wa nchi kwa kuwa ndio wanatakiwa kutimiza mahitaji ya wananchi wote na sii swala la viongozi wa dini tena. Nafikiri hapa tulikuwa tumekwenda kuzungumzia wakati wa Nyerere hadi kufikia leo na jinsi gani waislaam hasa Sunni wamekuwa nyuma kielimu. Ni mawili, dini (kitabu) kichukue majukumu yote au dini ibakie ktk maswala ya imani na sii jumuiya kuchukua dhamana ya waislaam wote.

Sasa usipoelewa muundo wa dhehebu hili ni vigumu sana kukubali kwamba Nyerere alidumaza elimu yao kulingana na mtazamo wao. Na bahati mbaya watu kama Mohammed said wenyewe wameshindwa kuelewa sababu zinazotoka ndani ya mfumo wa dini au dhehebu lao kuwa ndio sababu ya kudumaa kwa elimu kutokana na kwamba mfumo wa kitaifa ulihitaji vyombo vya kidini kuwawezesha wananchi wake.

Mimi kama Mkandara siku zote nimewabishia kina Mohammed kwa sababu nilisoma pia wakati wa Nyerere na kuziona tofauti baina ya Mkoloni na Nyerere baada ya kutangaza Azimio la Arusha. waislaam waliokuiwa wakibaguliwa kuingia shule walipewa nafasi ya kujiunga na shule yoyote ile Tanzania hata zile za Kikristu ambazo ilikuwa ni ndoto kwa Muislaam kujiandikisha acha mbali kujiunga.. Sisi wengine tulokuwa tukitumia majina ya Bandia tulirudia majina yetu na hakika tumepata elimu hadi vyuoni pasipo kubaguliwa kutokana na iomani yetu ya dini..

Nachoamini mimi, kama kuna Muislaam aliyebaguliwa wakati wa Nyerere basi ubaguzi huo ulitokana na walimu wenyewe kwani mamlaka ya kuandikishwa bado yalikuwa mikononi mwa watu na ilichukua muda mrefu sana kuweza kuweka system nzima ikubalike kwa wote. na sidhani kama iliwezekana hadi leo hii bado tunao ubaguzi mkubwa ndani ya Elimu ingawa sii mkubwa kiasi cha kushtua watu. lakini bado watanzania wanatazama Watanzania wengine kwa rangi za za dini

Na mwisho, umetoa hoja ya Sunni watafute njia ya wao kujiendeleza.. Hapa mkuu wangu unataka sunni watoke njew ya imani yao ya dini kwa sababu serikali yetu imechukua mfumo wa dini na madhehebu mengine. Swala la ELIMU ni haki ya kila raia ni jukumu la serikali iliyopo madarakani kuwapa wananchi wake na huo ndio msimamo wa sunni kama dini.

Kama serikali haiwezi basi kubalini kwamba Sunni wanaonewa kielimu na kwamba Tanzania sio nchi isiyokuwa na dini ila ni nchi inayochukua baadhi ya taratibu za dini fulani kukuwawezesha wao. At the same time ikiwa kweli serikali yetu haiwezi kuwapa wananchi wake elimu na kwamba ni swala la jumuiya hizo, mbona ni hiyo hiyo serikali inayokataa swala la OIC wakidai kwamba ni kueneza Uislaam nchini hali kuna vyombo vya kikanisa na Ismailia hao kina Agha Khan vinaingia nchini kuwaendeleza watu wao.

Mengine nitarudi baadaye..Lole Gwasika, mkuu wangu Utawala wa Waarabu haukuhusika kabisa na kuelea kwa Uislaam Tanzania. Hizo habari ulizo quote zimeandikwa na wale waliotaka tuamini kwamba Sultan wa Oman ndiye aliyeuleta Uislaam Tanzania wakati sivyo kabisa kwa sababu waulize hao watu kama wanaweza kuestablish link between Sultan huyo na kina Mirambo.

Between all merchant from Persian to Sultan waliokuja coast ya East Africa na hata huyo Sultan - non of them was of - SUNNI. Ukweli ni kwamba Hata Sultan alipokuja Mombasa, Lamu na hata kutinga Unguja, waliwakuta wakazi wake tayari ni waislaam wakiishi na ubaguzi ulokuwepo ulikuwa ni wa rangi na makabila sio dini. Na ndio maaana ilikuwa rahisi kwao (sultan) ku mingle na society, hii ndio faida aloipata Sultan na sio yeye kutuletea..
 
Fundi Mchundo,
Mkuuu sii vizuri kubishana ili mradi tunabishana, haina radha hata kidogo.
Ni wewe ulosema ulipokuwa ukisoma shule (wakati wa mkoloni), waislaam nao walikuwa na darasa lao. Na binafsi sijawahi kusikia wala kusoma na mtu aliyepitia shule hiyo wakati wa mfumo wa mkoloni. Itakuwa vizuri sana kama utanielemisha ili nami kesho naweza kutumia mfano huu. Hatubishani, Nipo hapa kujifunza na kuandika ninayoyajua mimi. Kama wewe una taarifa tofauti ni vizuri kuiandika tofauti hiyo ili tuweka vitu sawa.

Hatubishani. Sababu ya mimi kukataa kutaja shule niliyosoma bila shaka unaweza kukisia. Lakini soma bandiko la Jasusi ambae alikuwa na experience kama ya kwangu na shule ameitaja na mwaka alipokuwa hapo. Nadhani mfano aliotoa unatosha kukusaidia. JokaKuu nae ana experience hiyo hiyo.

Sasa umeuliza swala la Pwani kuwa na shule nyingi kuliko bara lakini Waislaam wengi hawakuwa na elimu.. jambo ambalo wewe halikuingii akilini..Nadhani mkuu wangu hukuisoma hoja hii kwa makini zaidi. Kwani kama Pwani ndio ilikuwa na shule nyingi zaidi ya bara yet waislaam hawakupa elimu (fact) basi kuna sababu ya hao waislaam kutopata elimu hiyo na ndio madai ya kina Mohammed Said yanapokuja kwamba Waislaam walibaguliwa. Ubaguzi siku zote hutokea pale mtu anapoanzisha kitu in your face na hakuruhusu wewe kujoin, tofauti na mtu kwenda jenga kitu mbali na wewe kisha ukadai unabaguliwa hali huna acceess ya kufika huko.

Mkuu, jibu ambalo wakina Mohamed Said wanalipata ni kutokana na kukataa kujiangalia wenyewe mapungufu yao na kulaumu mwingine. Ni rahisi zaidi kukimbilia kwenye kubaguliwa kuliko kuangalia wewe mwenyewe unachangiaje katika matatizo yako. Mfano hai ni ndugu zetu wamarekani weusi. Kama kweli ilikuwa ni ubaguzi wa wamisheni ndio uliowazuia watu wa pwani kusoma ni nini kilichowazuia na kinachowazuia kuchangamkia hiyo elimu miaka hamsini baada ya wakoloni kuondoka? Au Mkuu unataka kutuambia mpaka leo waislamu wanabaguliwa kuandikishwa kwenye shule za msingi Kilwa, Mkuranga, Bagamoyo na kwengine? Au wakina Jakaya waliosoma shule za Bagamoyo walislimu kabla ya kukubaliwa? Mimi naamini kuwa pamoja na ukweli kuwa palikuwa na ubaguzi katika baadhi ya shule lakini cha msingi zaidi ni tamaduni za watu wengi wa pwani. Kama ilivyokuwa kwa makabila mengine bara ambayo hayakuona umuhimu wa elimu ya kizungu.

Na mwisho, umetoa hoja ya Sunni watafute njia ya wao kujiendeleza.. Hapa mkuu wangu unataka sunni watoke njew ya imani yao ya dini kwa sababu serikali yetu imechukua mfumo wa dini na madhehebu mengine. Swala la ELIMU ni haki ya kila raia ni jukumu la serikali iliyopo madarakani kuwapa wananchi wake na huo ndio msimamo wa sunni kama dini.

Kama serikali haiwezi basi kubalini kwamba Sunni wanaonewa kielimu na kwamba Tanzania sio nchi isiyokuwa na dini ila ni nchi inayochukua baadhi ya taratibu za dini fulani kukuwawezesha wao. At the same time ikiwa kweli serikali yetu haiwezi kuwapa wananchi wake elimu na kwamba ni swala la jumuiya hizo, mbona ni hiyo hiyo serikali inayokataa swala la OIC wakidai kwamba ni kueneza Uislaam nchini hali kuna vyombo vya kikanisa na Ismailia hao kina Agha Khan vinaingia nchini kuwaendeleza watu wao.

Ni nchi chache sana ambazo serikali pekee ndiyo inayoruhusiwa kutoa elimu kwa wananchi wake. Labda Cuba na nchi za mashariki ya kati peke yake. Lakini katika nchi nyingi serikali ( kuu na za mitaa) zinashirikiana na vyombo binafsi ( vya imani, vya kujitolea, vya kibiashara n.k.) kutoa elimu hiyo. Jukumu kubwa la serikali ni kuweka viwango vya elimu na kuhakikisha kuwa elimu haitolewi kibaguzi. Nchini ufaransa, kwenye "projects" ambako wanaishi waislamu wengi, kanisa linashirikiana na serikali kutoa elimu na waislamu wengi wanawapeleka watoto wao kusoma kwenye shule za misheni kutokana na ubora wa elimu inayotolewa huko. Naamini vile vile ukienda Saint Anthony Mbagala utakuta vijana wa kiislamu wengi tu kama ambavyo utawakuta wakristu Al Muntazir. Hivi ndivyo inavyotakiwa.

Ninaposema wasunni ni lazima watafute njia mbadala itakayokidhi mahitaji ya imani yao si kuwabagua bali kuwapa changamoto. Kama kwenye msikiti kuna madrassa ambayo yanatoa elimu kwa nini yasitumike kuwasaidia waumini wake kupata elimu dunia? Nasikia baadhi ya misikiti imefanya hivi. Kwa nini mashehe wasihubiri na kuwahimiza waumini katika misikiti yao kutafuta elimu? Ingawa mimi naona uoga wa serikali kuhusu OIC hauna mantik lakini vile vile kuamini kuwa kujiunga kwenye OIC kutatua matatizo yote ya waisunni ni ndoto. OIC itasaidia lakini ni wasunni wenyewe watakaojikwamua. Hao mnaodhani wanasaidiwa na mashirika ya nje wanachangia sana maendeleo yao. Nenda kwenye makanisa ukaone sadaka zinavyochangwa kujenga chekechea pamoja na makanisa. Nenda kwa waismailia uone wanavyochangia mfuko wa Aga Khan. Nenda kwa mabohora uone wanavyochangia maendeleo yao wenyewe. Ni mara chache sana makanisa kutegemea misaada kutoka nje peke yake. Tofauti kubwa na wasunni ni kuwa viongozi wa haya madhehebu wanahimiza na wanasikilizwa kwenye masuala si ya maendeleo ya kiroho peke yake bali hata yale ya duniani. Kitu gani kinachowazuia wasunni kufanya hivyo badala ya kungojea mtu kutoka nje (awe serikali au OIC)kuwatoa kwenye umasikini wa elimu dunia? Kwa vile tunaishi katika nchi yenye mchanganyiko wa imani wasunni hawawezi kuwazuia wale wa madhehebu nyingine kujisaidia pale wanapoona serikali ina upungufu. Hata hivyo kwa vile shule za serikali ni nyingi kuliko za vyombo binafsi basi wasunni wangefanya jitihada za ziada kuhakikisha kuwa wanazitumia kikamilifu. Isiwe kilio kikubwa ni watu kutokwenda shule na kama wakienda kukatiza masomo mapema kama ilivyo kwenye sehemu nyingi za mikoa ya pwani. Wakiendelea hivyo, wataendelea kubaki nyuma katika elimu dunia.

Amandla....
 
Fundi Mchundo,
Hitimisho lako ni muruwa kabisa. Mimi nina swali moja tu ambalo ningependa Mohammed Said asaidie kulijibu. Mwaka kesho Tanzania inasherehekea miaka 50 tangu tuwe watu huru. Ningependa kusikia kutoka kwa Mohammed Said au wengine wenye maoni kama yake ni hatua gani ambazo angependekeza zichukuliwe na serikali ya Tanzania ili kufungua mianya sawa ya maendeleo katika elimu kwa ndugu zetu Waislamu? Je, kuanzishwe mpango maalumu wa kutenga nafasi kwa watoto wa Kiislamu , kama walivyofanya Wamarekani na affirmative action kuhusu Wamarekani weusi, na hatua hizi zisimamiwe na nani? Wizara ya elimu, serikali za mitaa au jumuiya ya Waislamu?
 
Ufunguo wa tatizo hilo umetolewa kwa serikali mara nyingi na kupitia njia nyingi za kificho na dhahiri lakini tatizo kubwa ni kuwa hao hao wanaotuhumiwa ndiyo wanaotegemewa kulifanyia kazi tatizo hili. Pamekosekana uadilifu na ushujaa wa kukubali kuwa tatizo lipo. Ukweli ni kuwa ndani ya serikali kuna mtandao wa Wakatoliki uliojikita na kusimikwa na Mwalimu Nyerere toka uhuru. Ngome hii ina nguvu sana na ni moja ya sababu hii leo inaogopwa hata kusomeshwa historia ya kweli ya kudai uhuru. Kuna hofu kuwa Waislam wataijiuliza uhuru huu tuliwapigania Wakatoliki?

Marehemu Prof. Malima alieleza alichokikuta Wizara ya Elimu wakati alipokuwa waziri katika wizara hiyo na alipoitahadharisha serikali dhulma aliyoikuta hapo dhidi ya vijana wa Kiislam katika elimu sote tunajua kilichomkuta.
 
Amandla uniwie radhi lakini inaelekea hujui historia ya Waislam nini walifanya baada ya kuupigania uhuru na kumweka Mwalimu Nyerere kwenye kiti. Hapa itakuwa tabu kueleza kuwa chanzo cha ugomvi baina ya Nyerere na Waislam ni pale walipoanza juhudu za kujenga shule na kuanza mipango ya kuanzisha Chuo Kikuu. Nakushauri usome kitabu "The Life and Times of Abdulwahid Sykes" Part Three ya kitabu kina anuani: "Conspiracy Against Islam" hapo ndipo utakapopambana na ukweli uliwaweka Waislam katika hali hii tuliokuwa nayo leo takriban miaka hamsini baada ya uhuru.

Mie mara kwa mara ninapojadiliana na marafiki zangu Wakristo kuhusu mambo haya huwasihi sana kwa kuwaambia wasinipuuze wakidhani wanazungumza na mtu mkorofi mwenye chuki na Ukristo. Huwaeleza kuwa nina mengi sana ninayoyajua ambayo wao wamefichwa hawayafahamu.

Mfano mdogo tu ni huu wa Waislam ambao walitoa mchango mkubwa sana katika uhuru wa Tanganyika lakini hata majina yao hayapo katika historia ya nchi yetu. Naamini Amandla hujapata kumsikia Mshume Kiyate, Sheikh Hassan bin Amir, Iddi Faiz Mafongo, Tatu bint Mzee, Asha Ngoma, Hawa bint Maftah nk. Historia za wazalendo hawa ni za kutukuka. Inatustaajabisha sana kuwa kwa wengine zinaudhi.

Kwa hakika wale ambao waliacha bongo zao wazi mwishowe wamenambia kwa kwa hakika hawawakujua mashujaa hawa na wala hawakufahamu kuwa nchi yetu inaendeshwa katika hali ya kibaguzi kama hivi.

Insha Allah tutaendelea kuelezana kila nafasi itakapojitokeza.
 
Ufunguo wa tatizo hilo umetolewa kwa serikali mara nyingi na kupitia njia nyingi za kificho na dhahiri lakini tatizo kubwa ni kuwa hao hao wanaotuhumiwa ndiyo wanaotegemewa kulifanyia kazi tatizo hili. Pamekosekana uadilifu na ushujaa wa kukubali kuwa tatizo lipo. Ukweli ni kuwa ndani ya serikali kuna mtandao wa Wakatoliki uliojikita na kusimikwa na Mwalimu Nyerere toka uhuru. Ngome hii ina nguvu sana na ni moja ya sababu hii leo inaogopwa hata kusomeshwa historia ya kweli ya kudai uhuru. Kuna hofu kuwa Waislam wataijiuliza uhuru huu tuliwapigania Wakatoliki?

Marehemu Prof. Malima alieleza alichokikuta Wizara ya Elimu wakati alipokuwa waziri katika wizara hiyo na alipoitahadharisha serikali dhulma aliyoikuta hapo dhidi ya vijana wa Kiislam katika elimu sote tunajua kilichomkuta.

Maneno kama haya ndiyo yanayofanya nikuite mchochezi. Hebu tuangalie jinsi hao wakatoliki, Julius Nyerere na Benjamin Mkapa walivyosaidia kudumaza maendeleo ya waislamu hususan katika elimu. Huyo Julius Nyerere aliyetarishwa na cabal ya wakatoliki kitu cha kwanza alichofanya ni kunyang'anya kanisa hilo shule zake zote na kuzifanya za serikali yake ambapo kila raia alikuwa na haki ya kuhudhuria. Huyo huyo kwa chuki aliyekuwa nayo dhidi ya waislamu akaondoa karo katika elimu ili hao waislamu ambao wengi wao hawakuwa na uwezo mkubwa wa fedha wasiweze kujiandikisha kusoma. Huyo huyo, Julius aliyekuwa akiabudu katika kanisa la Mtakatifu Petro bila kukosa, baada ya kusukwa vyema na wakatoliki, akaachia ngazi ya uwaziri mkuu wa nchi akampisha Rashidi (ambaye wote tunajua aliishaslim zamani na kuitwa Robert) ashike usukani kwa mwaka mzima. Huyo huyo, Julius, akifuata maagizo kutoka Vatican akamtolea nje swahiba wake Oscar Kambona, Michael Kamaliza, John Chipaka, Eliya Chipaka, William Chacha, Grey Mattaka na Alfred Mulinga ili tu amshikishe adabu bibi Titi Mohamed! Na wakati akifanya yote haya, msaidizi wake mkuu alikuwa Rashidi ( ambaye wote tunajua aliisha batizwa kuitwa Robert)! Kwa kuona kuwa mambo yao hayakufanikiwa, wakatoliki wakampika kisawasawa Benjamin William Mkapa ili aje ahakikishe kuwa sisi wote tunakuwa wakatoliki na waislamu hawaoni ndani katika elimu. Huyu Benjamin hakuwaangusha maana akaenda akachukua chuo kilichojengwa kwa pesa ya umma, akakikabidhi kwa waislamu wajenge chuo chao kikuu. Yote haya akitekeleza waraka wa kuwadumaza wa wakatoliki wa kuwadumaza waislamu kielimu. Na huyo huyo Benjamin akawarubuni waislamu wauze eneo lao walilokuwa nalo miaka nenda rudi pale Chang'ombe kwa mwenzao. Akimalizia kazi aliyoianza Julius wa kuwalazimisha kula pesa walizopewa kujengea chuo chao! Na kadhalika, na kadhalika.

Unamzungumzia Kighoma Malima kama vile alikuwa martyr. Huyo mheshimiwa alikuwa waziri wakati wa serikali ya Ali Hassan Mwinyi, sio ya Julius au Benjamin. Huyo mheshimiwa alipandishwa cheo kutoka wizara ya elimu akakabidhiwa ya fedha. Wote tunajua kilichoendelea katika wizara ile. Huyu mheshimiwa ingekuwa nchi nyingine asingeachishwa kazi tu bali angefunguliwa mashtaka ya grand corruption. Leo unataka kumgeuza martyr kwa sababu tu alikuwa mdini mwenzako? Kama unajua ukweli mwengine basi tuambie. Tuambie yale mapesa alitoa wapi na nini kilichomuua ughaibuni! Au unataka kutuambia walitumwa assassins kutoka Vatican kuchukua roho yake? Tuelimishe basi. Utuambie vile vile nini alichokikuta wizara ya elimu. Na alifanya nini kukabili hali mbaya ya unyanyasaji na uonevu alioukuta. Na kwa nini mabadiliko hayo hadi hivi sasa hayajamsaidia muislamu. Au nako wakatoliki wametia kauzibe? Kwa vipi?

Mkuu, mimi naamini kuwa maneno yako ni ya hatari sana maana yanachofanya ni kujenga chuki kwa sehemu ya jamii bila kuwa na ushahidi kamili. Ni kama vile wapuuzi wamarekani ambao hadi sasa wanaamini kuwa rais wao si raia na si mkristu kutokana na chuki yao dhidi ya waislamu na watu weusi. Watu kama nyinyi sina uvulimu nanyi.

Amandla......
 
Amandla uniwie radhi lakini inaelekea hujui historia ya Waislam nini walifanya baada ya kuupigania uhuru na kumweka Mwalimu Nyerere kwenye kiti. Hapa itakuwa tabu kueleza kuwa chanzo cha ugomvi baina ya Nyerere na Waislam ni pale walipoanza juhudu za kujenga shule na kuanza mipango ya kuanzisha Chuo Kikuu. Nakushauri usome kitabu "The Life and Times of Abdulwahid Sykes" Part Three ya kitabu kina anuani: "Conspiracy Against Islam" hapo ndipo utakapopambana na ukweli uliwaweka Waislam katika hali hii tuliokuwa nayo leo takriban miaka hamsini baada ya uhuru.

Mie mara kwa mara ninapojadiliana na marafiki zangu Wakristo kuhusu mambo haya huwasihi sana kwa kuwaambia wasinipuuze wakidhani wanazungumza na mtu mkorofi mwenye chuki na Ukristo. Huwaeleza kuwa nina mengi sana ninayoyajua ambayo wao wamefichwa hawayafahamu.

Mfano mdogo tu ni huu wa Waislam ambao walitoa mchango mkubwa sana katika uhuru wa Tanganyika lakini hata majina yao hayapo katika historia ya nchi yetu. Naamini Amandla hujapata kumsikia Mshume Kiyate, Sheikh Hassan bin Amir, Iddi Faiz Mafongo, Tatu bint Mzee, Asha Ngoma, Hawa bint Maftah nk. Historia za wazalendo hawa ni za kutukuka. Inatustaajabisha sana kuwa kwa wengine zinaudhi.

Kwa hakika wale ambao waliacha bongo zao wazi mwishowe wamenambia kwa kwa hakika hawawakujua mashujaa hawa na wala hawakufahamu kuwa nchi yetu inaendeshwa katika hali ya kibaguzi kama hivi.

Insha Allah tutaendelea kuelezana kila nafasi itakapojitokeza.

Samahani lakini mimi naitwa Fundi Mchundo na sio Amandla.

Hauwezi ku-base arguments zako kuhusu kubaguliwa na kutotendewa haki waislamu kutokana na simulizi za mtu mmoja tu. Wakina Sykes tunawajua sana. Mchango wao katika kupigania uhuru wa nchi hii unajulikana mno kuliko unavyoweza kuamini. Wewe umewaona hao waislamu, je ni wangapi wanawajua wakina Kyaruzi na Pombeah? Wakina Sykes si angalau waliachiwa wafanye biashara wakati wa ujamaa na kupewa ubalozi.

Mimi naamini kabisa kuwa waliochangia mapambano ya uhuru ni wengi kuliko hao uliowataja maana tofauti na unavyotaka kutulazimisha tukubali mapambano hayo hayakufanyika Dar es Salaam na pwani peke yake. Hata huko bara kuna watu walijitolea mhanga lakini leo tumewasahau. Historia yeyote haiwezi kuwakumbuka wote ambao kwa namna moja au nyingine walishiriki katika mapambano dhidi ya dhulma. Kwa vile umetutajia hao tuliowasahau basi itakuwa bora utuambie kila mmoja mchango wake ulikuwa nini. Na sisi tutakutajia wakristu na watu wa bara ambao nao walijitolea mhanga. Kusema kuwa waislamu ndiyo waliomweka Nyerere kwenye kiti cha uongozi ni ku-distort historia. Wakina Rupia na hao niliowataja walishiriki kikamilifu katika kumpa nafasi ya uongozi.Mtu unaweza ku-argue kuwa bila mchango wa wakina JOHN Rupia, Nyerere asingeweza New York kutetea haja yetu ya kupata uhuru. Na kama asingeenda, huo uhuru ungebakia ndoto. Sasa leo unataka wakina Rupia waseme wao ndio walioleta uhuru Tanganyika? Hivi wangapi ( acha tuliokulia Dar es Salaam) wanaojua mchango wa wakina Rupia? Au napo tuseme kuna kampeni dhidi ya waanglikana? Au mkatoliki mwenzie, Chief Patrick Kunambi?


Mkuu, tofauti na unavyodhani, naijua sana historia ya nchi yangu na nchi nyingine. Sitaki kuona kilichotokea nchi nyingine kitokee kwetu kutokana na kutaka kutugawa kwa misingi ya dini. Kusema kuwa una marafiki wakristu na kuwa hauna chuki nao hakutoshi. Ni vitendo vyako ndivyo vinavyodhiirisha mapenzi yako si kwa wenzio tu bali kwa ukweli.

Amandla......
 
Lakini muhimu tujadili historia ya uhuru wa Tanganyika na mashujaa wake ambao wamefutwa katika historia yab nchi yetu. Hii ndiyo mada kuu na husika katika mjadala huu.
Mkubwa, hapa husemi ukweli. Na asiyesema ukweli hapa mimi humwita mwongo.

Msemaji kwenye mhadhara huu anaongelea waislamu walivyokandamizwa, walivyofichwa kutoka kwenye historia ya harakati za uhuru, kutotambuliwa na kubaguliwa na Wakatoliki, Nyerere, Kanisa na Wakristo. Ndio maudhui ya msingi ya msemaji, na nimesikiliza sehemu zote kumi na moja za mhadhara.

Msemaji katukana BAKWATA, msemaji kadai kwa vile Waislamu waliwaondoa waingereza basi Wakristo hawatafua dafu moto ukiwashwa, moto ambao waislam walimwambia Nyerere kwamba hawezi kuuzima, kadai kisa cha Bibi Titi kugombana na Nyerere ni uislamu, kadai mkutano wa TANU Tabora lengo lake kukandamiza waislam, na mengine lukuki ya kidini.

Na kadai Nyerere aliwahi kusema Muhindi asiruhusiwe kuongoza Waislam. Nyerere ambae alikaribia kugombana na wenzie akitetea usawa wa wote, wahindi, wazungu, waafrika. Mada ni uislamu. Msemaji mwongo na wewe, kama wewe sio yeye, pia mwongo mkubwa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom