Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Status
Not open for further replies.
Mohamed Said,

..hapa utaona kwamba utendaji wa Malima akiwa waziri wa fedha uliwatibua hata wafadhili wetu na kupelekea kusitisha misaada kwa Tanzania.

..sakata hii mpaka ilipelekea Raisi kuwaita Mabalozi wa nchi za nje na kuwaangukia. kwa nchi tegemezi kama Tz Raisi hawezi kufanya kazi na waziri ambaye wafadhili na nchi marafiki hawamtaki.

..pia ikifika mahali Mabalozi wakaweka pembeni diplomasia na kutamka kwamba fulani[waziri] aondoke, ujue maji yalishawafika shingoni.

African Affairs said:
DONORS EXPRESS SERIOUS CONCERN

Within days of President Mwinyi's announcement the Deputy Treasury Principal Secretary, who had been responsible for signing tax exemption certificates, was removed from office but many observers wondered why responsibility was not being accepted at a higher level.

Donor agencies began to express alarm. An official of the Belgian Agency for Development Cooperation said that tax exemption and revenue collection problems were not caused by one individual. The problem was both institutional and political.

Norwegian Minister for Development Cooperation Kari Nordheim-Larsen said that she viewed the matter extremely seriously and immediately withheld TShs 8.1bn (US$ 15 million) balance of payments support.

The Swedish Ambassador announced the next day (November 17) that Sweden had suspended the release of TShs 7.3bn ($13.5 million) due to the country's mismanagement of revenue collection.

The following day President Mwinyi called representatives of 14 foreign and international donor agencies to State House (Ikulu) and made an appeal to them to continue to disburse approved funds "short of which Tanzanians would suffer and measures taken to adjust the budget would prove futile".

At this meeting, according to the Daily News, the Canadian representative asked why the Minister of Finance did not resign.

Replying to allegations by the representative of Denmark that Tanzania had corrupt leaders, President Mwinyi said that anyone caught evading tax would be dealt with according to the law.

Tanzania faces a budget deficit of TShs 221 billion this year of which the government had hoped that some TShs 168 billion would come from foreign donors.

The Minister of Finance had had a difficult time during the 1994/95 budget debate in Parliament in August. Professor Mbawala (National MP) had said that the Treasury had been weak in collecting taxes because it had concentrated on small traders while leaving big-time businessmen to go scot-free. He accused the Minister of amassing powers and ignoring directives from the cabinet and the President.

At the meeting of the National Assembly in August a private member's motion to re-introduce a leadership code and declaration by leaders of their personal property had received the support of the government and had been passed unanimously.
 
Pasco said:
Joka Kuu, asante kwa hili, naungana na wewe, Marhum Mohamed Aboud, alikuwa ni mcha Mungu wa ukweli, nakumbuka hadu kuhudhuria maziko yake pale nyumbani kwake Upanga na Makaburi ya Kusutu.

Ila pia pamoja na ucha Mungu huo, don't rule out hiyo theory ya "Christian Lobby" if at all, it really existed, kunauwezekano wa Jakaya kujikuta alikuwa akitumiwa bila mwenyewe kujijua, na hivyo kazi ya Aboud ni kupokea kila alicholetewa.

Mathalan kufutwa kwa mahakama ya kadhi, wakati wa mkoloni ilikuwepo na ilioparate smoothly, Kenya ipo, Uganda ipo, lakini kwa Tanzania ni kigugumizi, Sheikh Mkuu yupo na Bakwata yake, Sheikh Yahya alipoanzisha Balukta, kilichomkuta mnakijua, na hatimaye kulazimika kurejea Bakwata, hivyo kuna uwezekano kama ni kweli hiyo lobby ipo, basi inawatumia Waislamu wenyewe bila ya wao kujijua.

Ila pia naomba kumtetea Mwalimu Nyerere katika teuzi zake, hakuangalia dini wala kabila, ila ni mpaka kele za udini tena Ukatoliki zilipopigwa, ndipo akamtuma katibu wake amletere majina, mawaziri wangapi ni Wakristo, na kati yao wangapi ni Wakatoliki, na yeye alishangaa!.

Pasco, Mohamed Said,

..nashukuru kwa kuweka msisitizo kwa kile nilichokisema kuhusu marehemu Mzee Mohamed Aboud, aliyekuwa Controller and Auditor General wakati wa Mwalimu Nyerere na Mzee Mwinyi.

..maandiko ya Mohamed Saidi yanalaumu kila tatizo linalowasibu Waislamu wa nchi hii kwa hiyo "invisible hand" au "Christian Lobby." binafsi sikubaliani na hoja hizo.

..jamani, Tanzania siyo Lebanon!!

..pia ukisikiliza video clips za Mohamed Said utaona kwamba he does not take very well constructive criticim towards Muslims even when it comes frm within their own community.

..binafsi siamini kama mtu akihoji kwanini Bakwata haijaanzisha shule au hospitali zenye viwango basi mtu huyo anakuwa anawasimanga Waislamu.

..kwa maoni yangu Muslims can do much better kwa manufaa yao and Tanzania at large. Bakwata wakianzisha shule nzuri na hospitali nzuri maana yake ni kwamba more Tanzanians[regardless of their belief] watakuwa na access kwa huduma hizo.

..sasa hivi kuna shule ya Waislamu inaitwa Feza Boys. kila mzazi mwenye usongo na elimu ya watoto wake anataka mwanae asome hapo. nimekutana na watoto waliosoma o-level ya seminari, lakini a-level wanagombea kwenda sekondari ya Feza. siri kubwa hapo ni QUALITY of education.

..kwa hiyo hili suala la kusema kuna Waislamu wanatumiwa na "christian lobby" nadhani ni dharau na udhalilishaji wa hali ya juu.

..vilevile pounding over and over on Muslim youths that they are victims in Tanzanian society does not do them any good. at some point there is a risk of this kids buying into that message, and quite trying anything meaningful in their lives. sasa sijui tukifika huko tutakuwa tunamfaidisha nani.

..to cut the story short, nadhani visa vingi vya kihistoria alivyovibainisha Mohamed Saidi ni relevant. nisipokubaliana naye ni CONCLUSIONS anazofanya kutokana na habari hizo za kihistoria. labda anakuwa-carried away na emotions ukizingatia kwamba watu wengi anaowazungumzia ni wazee wake--wajomba,shangazi etc etc.

NB:

..kuna mahali Mohamed Saidi amedai kwamba DSM ya miaka ya 50 ilikuwa ni vigumu kwa mtu wa bara, kama Mwalimu Nyerere, kuanzisha chama na kuwa na wafuasi.

..na mimi kama mtu wa bara napenda kumhakikishia Mohamed Saidi kwamba haikuwa rahisi kwa chama kilichoanzishwa na watu wa Pwani kuungwa mkono na watu wa Bara na bila msaada na ushiriki mkubwa wenyeji wa eneo husika.

..itapendeza sana kama Mohamed Said atawatendea haki wazalendo waliokuwa mikoani/bara ambao walifanya kazi kubwa kukifanya Tanu chama cha kitaifa. itapendeza kama makala na vitabu vyake vitakuwa INCLUSIVE zaidi.

..when you listen to some of his presentations ni kana kwamba watu wa Bara na wasiokuwa Waislamu waliburutwa tu na kupewa uhuru na hiki kikundi cha watu wa Pwani.

..
 
Jokakuu, Mkuu wangu kama ulikuwepo Tanzania wakati wa Mwinyi hiili swala la kuepa ushuru lilikuwa ndio deal kwa viongozi wote nchini na sheria zake zilikuwa lege toka wakati wa Nyerere... Na ikumbukwe tu kwamba ndio kwanza Tanzania tulikuwa tumetoka katika Ujamaa na kuingia Ubepari (1985) hivyo kila kitu kilikuwa kinaingia Tanzania toka nje kiasi kwamba Wadanganyika wakamsifia Mwinyi pasipo kujali gharama ya uingizaji vitu hivi.

Mimi nadhani kabla hujamlaumu Malima ni muhimu kurudi nyuma na kufikiria hali halisi ya Tanzania Baada ya Mwinyi kuvunja Azimio la Arusha mwaka 1992 kule Zanzibar na kilichofuatia baada ya hapo.. kwani sisi Watanzania tunafahamu zaidi kilichotokea kuliko hawa waandishi wa habari ambao wanaweza tunga chochote.

Ukweli unabakia kwamba hadi kufikia wakati Mkapa anaingia madarakani, Tanzania ilikuwa freeport market place..sheria ya kodi na ukusanyaji wake ilikuwa lege vibaya sana. Na vizuri kama tukiipitia kwanza kuona uvunjaji wa sheria hiyo ulikuwa toka wizara moja au nchi nzima ilikosa mtawala shupavu.

Tax exemptions, ndio ilikuwa kazi ya misheni town miaka ya 86 hadi 90 ni kuwapatia watu vibali vya kukwepa kodi na kwenda banki kuu kuchukua madollar bwelele. kwa hiyo maandishi ya huyu mchunguzi hayawezi kuonyesha ukweli zaidi ya sisi wenyewe ndio tulokuwa mitaani tukiwafuata wazee wa chama kutupa barua za msamaha wa kodi kwa wafanyabiashara hali tukiua uchumi wa nchi..Na Mkapa alikuja chukiwa kwa sababu alikuja weka sheria mpya kuthibiti kodi na ukukasanya kwa kuwabana wafanyabiashara waliokuwa wamelimbikiza madeni au kukwepa kodi. Even though he didn't last long kabla naye hajavutwa na tamaa ya FEZA..Ni yale yale ya Mkapa tusema waziri wa fedha (Yona) ndio alikuwa responsible tukimwacha yeye kuwa ni saint..

Nadiriki kusema Utawala wote wa Mwinyi ulikuwa mbaya sana ktk maendeleo ya nchi kuliko hata unavyofikiria na hakika mimi nakubaliana kabisa na maelezo haya hapa uloyanukuu...

- Within days of President Mwinyi's announcement the Deputy Treasury Principal Secretary, who had been responsible for signing tax exemption certificates, was removed from office but many observers wondered why responsibility was not being accepted at a higher level.

Mimi nimeondoka ktk ubishi huu kwa sababu nimeona hakuna maana tena zaidi ya Udini. Jambo kalifanya Kawawa basi ni la Kiislaam kwa sababu tu yeye ni Muislaam dini lakini wanashindwa kuelewa kwamba Kawawa angefanya hivyo hata kama angekuwa Bainani. Ningekubali tu kwamba Kawawa au kina Sykes wangefanya tofauti kama msukumo wa mchango wao kwa Taifa hili ulitokea Msikitini lakini hakuna record hiyo isiipokuwa vikao vya chama ambavyo vilikuwa na wahusika wa dini na madhehebu tofauti - Waislaam kwa Wakristu.
 
Mkandara. Mtazamo huo ndio unaonifanya hata pale tunapotofautiana, nikuheshimu. Hii sumu ya udini inayotaka kuingizwa humu ni mbaya mno na bahati mbaya wako wengi tu ambao wataipokea bila kujiuliza. Nyerere alifanya makosa mengi tu lakini si sahihi na haki kusema kuwa alifanya vyote hivyo kutokana na ukatoliki. Mbona anapofanya mema kama kutaifisha shule zote huo mkono wa wakatoliki hautajwi?

Amandla.....
 
Mkandara,

..asante kwa mchango wako, ukitukumbusha mishen-town enzi za Mzee Ruksa.

..labda niongeze tu kwamba harakati zile zingekuwa za kidini-dini basi zisingefanikiwa, na Mkoloni[kwa kuona mgawanyiko] angepata sababu ya kuzizima kwa mabavu.

..umoja na utaifa ndiyo nguzo kuu za harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.
 
Jokakuu, Mkuu wangu kama ulikuwepo Tanzania wakati wa Mwinyi hiili swala la kuepa ushuru lilikuwa ndio deal kwa viongozi wote nchini na sheria zake zilikuwa lege toka wakati wa Nyerere... Na ikumbukwe tu kwamba ndio kwanza Tanzania tulikuwa tumetoka katika Ujamaa na kuingia Ubepari (1985) hivyo kila kitu kilikuwa kinaingia Tanzania toka nje kiasi kwamba Wadanganyika wakamsifia Mwinyi pasipo kujali gharama ya uingizaji vitu hivi.

Mimi nadhani kabla hujamlaumu Malima ni muhimu kurudi nyuma na kufikiria hali halisi ya Tanzania Baada ya Mwinyi kuvunja Azimio la Arusha mwaka 1992 kule Zanzibar na kilichofuatia baada ya hapo.. kwani sisi Watanzania tunafahamu zaidi kilichotokea kuliko hawa waandishi wa habari ambao wanaweza tunga chochote.

Ukweli unabakia kwamba hadi kufikia wakati Mkapa anaingia madarakani, Tanzania ilikuwa freeport market place..sheria ya kodi na ukusanyaji wake ilikuwa lege vibaya sana. Na vizuri kama tukiipitia kwanza kuona uvunjaji wa sheria hiyo ulikuwa toka wizara moja au nchi nzima ilikosa mtawala shupavu.

Tax exemptions, ndio ilikuwa kazi ya misheni town miaka ya 86 hadi 90 ni kuwapatia watu vibali vya kukwepa kodi na kwenda banki kuu kuchukua madollar bwelele. kwa hiyo maandishi ya huyu mchunguzi hayawezi kuonyesha ukweli zaidi ya sisi wenyewe ndio tulokuwa mitaani tukiwafuata wazee wa chama kutupa barua za msamaha wa kodi kwa wafanyabiashara hali tukiua uchumi wa nchi..Na Mkapa alikuja chukiwa kwa sababu alikuja weka sheria mpya kuthibiti kodi na ukukasanya kwa kuwabana wafanyabiashara waliokuwa wamelimbikiza madeni au kukwepa kodi. Even though he didn't last long kabla naye hajavutwa na tamaa ya FEZA..Ni yale yale ya Mkapa tusema waziri wa fedha (Yona) ndio alikuwa responsible tukimwacha yeye kuwa ni saint..

Nadiriki kusema Utawala wote wa Mwinyi ulikuwa mbaya sana ktk maendeleo ya nchi kuliko hata unavyofikiria na hakika mimi nakubaliana kabisa na maelezo haya hapa uloyanukuu...

- Within days of President Mwinyi's announcement the Deputy Treasury Principal Secretary, who had been responsible for signing tax exemption certificates, was removed from office but many observers wondered why responsibility was not being accepted at a higher level.

Mimi nimeondoka ktk ubishi huu kwa sababu nimeona hakuna maana tena zaidi ya Udini. Jambo kalifanya Kawawa basi ni la Kiislaam kwa sababu tu yeye ni Muislaam dini lakini wanashindwa kuelewa kwamba Kawawa angefanya hivyo hata kama angekuwa Bainani. Ningekubali tu kwamba Kawawa au kina Sykes wangefanya tofauti kama msukumo wa mchango wao kwa Taifa hili ulitokea Msikitini lakini hakuna record hiyo isiipokuwa vikao vya chama ambavyo vilikuwa na wahusika wa dini na madhehebu tofauti - Waislaam kwa Wakristu.

Absolutely Mkuu.
Tuungane katika Utaifa wetu si katika yale yanayotugawa.
Chukua tano!!
 
JK ahsante kwa mchango wako. Nitafurahi sana kama utasoma kitabu nilichoandika kama ikiwa hujasoma. Katika kitabu nimeeleza mengi jinsi TANU ilivyoingia huko bara. Babu yangu mwenyewe Salum Abdallah alikuwa pale Tabora na June 1953 yeye na Sheikh Abubakar Mwilima, George Magembe na baadhi ya walimu wa Tabora School walifanya mkutano wa siri Town School kukusanya fedha za kumpeleka Germano Pacha Makao Makuu ya TAA Dar es Salaam kuhudhuria mkutano wa kuanzishwa kwa TANU. Mpaka kufikia hii mikutano ya siri kuna mengi walifanya kuihujumu serikali ya kikoloni. 1955 Salum Abdallah akachaguliwa kuwa mwenyekiti wa kwanza wa Tanganyika African Railway Union (TRAU) katibu wake akiwa Kassanga Tumbo. Viongozi hawa waliipa TANU nguvu kubwa. Mwaka 1964 Salum Abdallah na viongozi wengine wa vyama vya wafanyakazi wakawekwa kizuizini kwa tuhuma za uongo ati walitaka kuipindua serikali ya Nyerere. Babu yangu alimchukia Nyerere na TANU hadi anaingia kaburini 1974. Salum Abdallah ameacha hazina na kumbukumbu nyingi kuhusu harakati za kudai uhuru toka 1947 alipoongoza mgomo wa kwanza wa wafanyakazi pale Tabora dhidi ya Waingereza. Alipokufa TANU walifika kaburini kwake na kusoma taazia nzuri sana ya kumsifia kuwa alijitolea mali zake na maisha yake kupigania uhuru wa Tanganyika.
 
Fundi Mchundo,
Najua fika kwamba tunatofautiana ktk baadhi ya maswala, lakini nachoweza kusema ni kwamba mimi naweza kutofautisha baina ya DINI na MUUMINI ktk hoja zangu tofauti na wengi wanaoshindwa kuchakachua dini na waumini. Kwa mfano, naweza kuwakashifu waislaam kwa matendo yao (sio Dini) lakini ni vigumu sana baina yenu na huyo Mohammed Said kuwakashifu waumini wa dini zao wenyewe..

Sijaona hoja hata moja ya Said akiwakashifu Waislaam jina kwa mapungufu yao na kila walilotenda ni kwa jina la dini badala ya Uzalendo kwa nchi yao, na wala sijakuoneni nyie mkiwakashifu Wakristu jina (Sio Dini ) dini kwa maovu yao na pengine kukubali kwamba uhalifu wao unatokana na nafsi zao sio swala la dini.. Kila mmoja wenu anajaribu ku defend position ya mtu wake (dini moja) pasipo kujiuliza kwamba huyu mtu hana mahusiano na dini yangu isipokuwa kwa ubatizo wake tu ambao hamfanyi kuwa mkristu/Muislaam kamili.
 
Mkuu wangu hizo harakati alofanya baba yako alizifanya kwa Uzalendo wake yeye kama Mtanzania na sio Muislaam. Hata mimi nakumbuka vizuri Mwalimu alipokuwa akija Ukerewe, nyumbani kwetu ndio ilikuwa safehouse yake na wajuimbe alokuwa akiongozana nao.. Nakumbuka Bibi Titi alifikia nyumbani pia tena marehemu mzee wangu akimpisha Nyerere Kitanda chake. Sasa siwezi kudai hapa kwamba marehemu baba yangu aliyafanya hayo kwa sababu alikuwa Muislaam au mchango wake umetokana na Uislaam.. Na kwa nini nisiseme ni kwa sababu ya rangi au kabila lake ila tu nichague moja nalo ni dini..
 
Fundi Mchundo,
Najua fika kwamba tunatofautiana ktk baadhi ya maswala, lakini nachoweza kusema ni kwamba mimi naweza kutofautisha baina ya DINI na MUUMINI ktk hoja zangu tofauti na wengi wanaoshindwa kuchakachua dini na waumini. Kwa mfano, naweza kuwakashifu waislaam kwa matendo yao (sio Dini) lakini ni vigumu sana baina yenu na huyo Mohammed Said kuwakashifu waumini wa dini zao wenyewe..

Sijaona hoja hata moja ya Said akiwakashifu Waislaam jina kwa mapungufu yao na kila walilotenda ni kwa jina la dini badala ya Uzalendo kwa nchi yao, na wala sijakuoneni nyie mkiwakashifu Wakristu jina (Sio Dini ) dini kwa maovu yao na pengine kukubali kwamba uhalifu wao unatokana na nafsi zao sio swala la dini.. Kila mmoja wenu anajaribu ku defend position ya mtu wake (dini moja) pasipo kujiuliza kwamba huyu mtu hana mahusiano na dini yangu isipokuwa kwa ubatizo wake tu ambao hamfanyi kuwa mkristu/Muislaam kamili.

Mkandara. Mwanzoni wa mjadala huu niliwataja wakina Oscar Kambona, John Chipaka, Michael Kamaliza kuwa walitaka kumpindua Nyerere. Nimesema wazi kuwa Julius Nyerere, mkristu mwenzangu alikuwa na matatizo yake. Mmoja wa mijadala yangu ya mwanzo ilikuwa wenye kuhoji utendaji wa Waziri wetu wa Mambo ya Ndani, ambaye ni mkristu. Nimemtetea Rostam Aziz ( si katika thread hii ) dhidi ya Mengi, mkristu mwenzangu n.k. Kunitaka mimi niwakashifu wakristu katika mjadala unaohusu kile kinachodaiwa ni kutotendewa haki kwa waasisi wa kiislamu naona hakuna mantik. Mtazamo wangu ni kuwa wote hao tunaowaita waasisi waliungana kizalendo bila kujali dini kupambana na mkoloni ambaye alikuwa ni muingereza , mkristu. Lakini siwezi kudai kuwa wakina Sykes, Nyerere na wenzao walipambana na ukristu wa muingereza badala ya ukoloni wake. Wakina Mohamed wanataka kutuambia kuwa mapambano hayo yalikuwa dhidi ya ukristu ( wakisahau kuwa mtawala wetu alikuwa manglikani na sio mkatoliki) na yalifanywa na kuongozwa kwa kiasi kikubwa na waislamu! Hii hainiingii kichwani hata siku moja.

Wakati Mohamed Said anataka kutuambia kuwa Kighoma Malima ( muislamu mwenziwe) alikuwa mtu shupavu wakristu wengi humu hawasiti kuwatupia madonge wakina Benjamin Mkapa, Edward Lowassa, Lawrence Masha n.k. Sijasikia mtu akitamba kuwa wakina Julius Nyerere, Vedasto Kyaruzi, John Rupia, Stephen Mhando , Oscar Kambona kuwa walifanya walichofanya kwa sababu tu ya ukristu wao! Wenzetu hawasiti kudai hivyo kwa waasisi wetu wa kiislamu. Na pale maovu yakifanywa na mkristu kuuunganisha moja kwa moja na imani yake! Hapo ndipo tunapotofautiana.

Amandla......

Amandla..........
 
Fundi Mchundo,
Mkuu nadhani unakosea unapozungumzia kukosoa uongozi wa mtu kama kiongozi wa Taifa (Uzalendo) na kujadili maswala ya mtu huyo huyo kuuhusiana na imani ya dini. Ulivyofanya nyuma inawezwa sana na watu wote hapa JF na pengine hata huyo Mohammed Said leo hii anampinga Kikwete au Karume (Uzalendo) hali akiwa mwanachama wa CCM na Muislaam.. Lakini huyu huyu Said inapokuja issue za dini kuwahusu watu hao hao hawezi kuchukua nafasi ile ile ya kuwapinga hao watu kwa sababu sasa swala limeondoka ktk utu wao na kuingia ktk imani ya dini.

Na mara nyingi nimewasoma wengi hapa kwamba inapofikia swala linazungumziwa kwa dini za wahusika tunashindwa kujizuia na kukubali ukweli wa matukio. Kwa mfano Tanzania chini ya Uongozi wa Nyerere aliifunga jumuiya ya Waislaam wa afrika mashariki lakini sii kwa sababu yeye ni mkristu isipokuwa kutokana na shinikizo la Waislaam wenyewe ndani ya CCM kutopenda uhusika wao..

Mimi sijui sababu haswa lakini nachofahamu ni kwamba Waislaam masheikh na sub dhehebu la Sufi ndio wali play big role kuua Jumuiya hiyo sijui kama ilikuwa kutokana na capitalist Orientation ya EAMWS (sisi tukiwa wajamaa) au kwa sababu kilimilikiwa na Wahindi (Agha Khan) which fall under racism, au pengine ilitokana na dhehebu lao Shiite -Ismailia - (Udini ndani ya dini) kuwa ndio wamiliki. Lakini ukweli utabakia kwamba walioipinga EAMWS walikuwa watu weusi, wazalendo na Waislaam wanachama wa TANU.

Sasa nikisoma utetezi wenu kwa mwalimu hauweki ukweli wa kilichotokea isipokuwa mnabishana pasipo hata nyie wenyewe kuwa na hoja yenye kumpa majibu Said isipokuwa kwa kutetea mwalimu na Ukristu ulivyoweza kuwanufaisha waislaam nje ya sababu za kufungwa kwa jumuiya hiyo. Hakuna mwenye kutoa prove ya kwamba haikuwa hivyo isipokuwa mnatafuta taarifa zilizowahi kuandikwa nje ya mada husika kumtetea mwalimu kama Mkristu, na Waislaam kuendelea kumlaumu Nyerere kwa sababu ni mkristu hali (ukweli) ushahidi mzima unaonyesha wazi kwamba Waislaam wenyewe walihusika sana kuvunja nguvu zao wenyewe toka wakati wa Nyerere hadi leo hii tunapojadiliana hapa. Na kinachovunja nguvu hizi ni kuchanganya imani ya dini na siasa.. mtu unapoanza kuyatazama matendo na matukio kwa rangi zake (Udini) basi sii rahisi kuubali ukweli isipokuwa utatafuta mchawi.

Mkuu wangu nimekusoma sana na nimeweza kuona jinsi Uadilifu wako ulivyo ktk dini yako lakini mara nyingi umeshindwa kutenganisha Dini kama imani na watu waumini wa dini hizi inapofikia swala likahusishwa na dini. I have always saidi kwamba Mwinyi ndiye aliyemuua Sheikh Kassim Bin Jumaa na nitaendelea kuamini hivyo pamoja na kwamba hao wenye Udini wanasema ni Mrema. Ni Mwinyi na waislaam waliokuwa madarakani CCM ndio walipinga kuundwa kwa Balukta kuivunja Bakwata na sio Mrema na mwisho kabisa Order ya kumweka ndani Sheikh Kassim bin Jumaa ilitolewa na rais mwenyewe sio Mrema.

Wakati Mohamed Said anataka kutuambia kuwa Kighoma Malima ( muislamu mwenziwe) alikuwa mtu shupavu wakristu wengi humu hawasiti kuwatupia madonge wakina Benjamin Mkapa, Edward Lowassa, Lawrence Masha n.k. Sijasikia mtu akitamba kuwa wakina Julius Nyerere, Vedasto Kyaruzi, John Rupia, Stephen Mhando , Oscar Kambona kuwa walifanya walichofanya kwa sababu tu ya ukristu wao! Wenzetu hawasiti kudai hivyo kwa waasisi wetu wa kiislamu. Na pale maovu yakifanywa na mkristu kuuunganisha moja kwa moja na imani yake! Hapo ndipo tunapotofautiana.
Haswaa ndipo naposema kwa nini nanyi mnajibu kama wao wanavyotaka kusikia?..
 
Sina ugomvi na hayo ila lililonishangaza ni pale nilipokuja kugundua kuwa historia ya TANU inaogopwa kwa kuwa wengi wa walipigania uhuru wa nchi hii walikuwa Waislam na kwa ajili hiyo zikafanyika njama za kuifuta historia hiyo. Iweje leo CCM iandike historia ya TANU isimtaje Abdulwahid Sykes, Tatu bint Mzee, Iddi Faizi Mafongo, Mshume Kiyate na wazalendo wengi sana na ukisema historia imekosewa watu wakasirike?
 
16 Solid years spent in education in the motherland TANZANIA,yet leo hii napewa somo la historia na Jamii Forum-no wonder our education system is the butt of all jokes
 
Mohamed Said,
Mkuu unaweza kunionyesha Historia ya TANU kama ilivyoandikwa na hao unaowalaumu. Kwani mara zote historia huandikwa na wana historia sasa ilikuwaje hao wazee wetu hao unaowaita Waislaam walishindwa hata kuandika ukweli ili kizazi hiki kipate ukweli unaodai. Kwa nini tunaulaumu utawala wa Nyerere hali kuandika kitabu cha historia ni utashi wa mtu yeyote na Nyerere asingeweza kumzuia baba yako au hao ulowataja wasiandike ukweli wa historia ya TANU.
 
Mkandara ahsante kwa mchango wako. Inaelekea imekupita pale nilipoeleza kuwa historia ya TANU iliandikwa na marehemu Abdulwahid Sykes na Dr Kleruu miaka ya mwanzo ya uhuru. Nyerere hakuipenda kama mnavyopata tabu nyinyi hivi leo kuamini kuwa hivi nisemavyo ndivyo ilivyokuwa. Ikiwa utapenda kuupata mkasa mzima Insha Allah nitauweka ukumbini kwa faida yetu sote. Hata pale nilipoandika kwa mara ya kwanza 1987 habari za marehemu Abdulwahid Sykes, Ally Sykes na baba yao Kleist Sykes, Saadan Abdu Kandoro, Salum Abdallah, Bilali Rehani Waikela akina Dharura bint Abdulrahman na wengineo katika kupambana na ukoloni gazeti lililochapa makala hiyo (Africa Events, London, March/April 1987) lilikusanywa lote na makachero na ni machache tu yaliyoweza kupenya na kuuzika mitaani Dar es Salaam. Yako mengi katika sakata hii kama kuibiwa kwa mswada wa Abdulwahid Sykes, memorandum ya mwaka 1950 ambayo ndiyo iliyotengeneza hotuba ya TANU Umoja wa Mataifa iliyosomwa na Nyerere na mengi. Hii ndiyo faida ya mijadala kama hii. Tunaelezana mengi yenye faida katika kuiweka sawa historia ya nchi yetu achilia mbali kuwa huenda baadhi yetu wanapata tabu kuamini.
 
Son of Alaska ahsante kwa mchango wako. Oxford University Press, Nairobi walikuwa na mradi wa kufundisha Kiingereza shule za msingi lakini wakati huo huo katika kusoma lugha watoto wasome na historia ya nchi zao. Nchi zote za Afrika ya Mashariki waandishi walichangia jumla ya vitabu 15 (titles) zikieleza historia za nchi zao na mashujaa waliopigania uhuru. Tanzania hatukuweza kuandika hata kitabu kimoja. Oxford wakaniomba niandike kitabu cha Mwalimu Nyerere ili nasi tuwemo katika mradi ule. Niliwapelekea mswada ambao kwa kweli nilipokwenda Nairobi kuwaona walisifia sana ile kazi na kitabu kikachapwa. Kitabu "Torch on Kilimanjaro" kinamueleza Mwalimu Nyerere katika miaka ya 1950 wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika kwa lugha ya kitoto kiasi kuwa mtoto wa miaka 10 - 12 hivi anaweza kumwelewa Nyerere na hapo hapo akawa kajifunza Kiingereza. Kitabu kilizinduliwa Kempinsky kwa dhifa kubwa sana na maofisa wote wa Wizara ya Elimu walialikwa na walikuwapo na wote walipewa nakala ya kitabu. Oxford walinipandisha jukwaani na nikaeleza maudhui ya kitabu. Huu sasa ni mwaka wa tano kitabu kimepigwa "conspiracy of silence." Wenye nchi yao hawakukipenda ingawa wataalamu wa Oxford walisema ni kitabu kizuri sana kwa kusomeshea historia ya Mwalimu Nyerere na wazalendo wenzake waliopigania uhuru pamoja. Oxford walipeka barua kwa Waziri wa Elimu Mama Sitta na wakampelekea nakala nyingine ili kipite mchakato kipate ithibati kisomeshwe katika shule za Tanzania. Barua haikujibiwa hadi leo. Hii ndiyo hali ya nchi yetu. Hapa ndipo tulipofika.
 
Dr. Said,

Nimeangalia clips zote hapo juu, nimefurahi kwamba kuna watu wanaweka historia yetu wazi. Mimi mwenyewe nina mizizi "Misheni Kota" na kwa hiyo hizi habari hazikuwa mpya kwangu, kwa sababu nimepata mapokeo kutoka kwa watu kama kina Mzee Chaurembo waliokuwepo tangu enzi za Kitchwele Street, Mwembetogwa na hata kurudi nyuma kwenye habari za viazi vya kinyasini. Kwa hiyo najua harakati za waasisi waliomkaribisha Nyerere mjini na kumpa itifaki kwamba mjini Dar wakubwa hawavai kaptura.

Nimesikitishwa na uchache wa wanafunzi na jamii nzima kuhudhuria katika mjadala wako, na hata hao wachache sikuona kama walikuwa na mwamko mkubwa kuwa interactive. Nashukuru umekuja hapa labda tutaweza kuwa interactive zaidi.

Nina maswali kwako, inaonekana kama kuna msuguano kati ya dhana ya "Muslim brotherhood" na concept ya utaifa, hususan kama taifa si la kiislamu. Ulitaja mtafaruku wa Nyerere kuzuia kushamiri kwa East African Muslim Welfare Society (niwie radhi kama sikulipatia jina barabara). Huoni kwamba Nyerere alitaka kushamiri na kujitegemea kwa uislamu Tanzania bila kutegemea watu wa nje, hususan Aga Khan ?

Hii dhana ya Muslim brotherhood inayokuwa na allegiance kwenye uislamu zaidi ya utaifa itaweza vipi kurandana na dhana ya utaifa ?

Na pia, unaposema kwamba TAA ilijaa waislamu waliomkaribisha Nyerere, watetezi wa Nyerere wakikwambia yeye hakuwaona kama waislamu bali aliwaona kama waafrika wenzake, na ni waislamu wanaokazania udini leo ndio wenye matatizo ya udini kwa kukazania kuangalia dini za watu wale badala ya kuangalia mambo ya kisiasa yaliyowaunganisha, pamoja na uafrika wao uliowafanya wakandamizwe pamoja, utasemaje ?
 
Mkuu Kiranga,dhana kwamba ujanja woote wapatikana mjini ni potofu.Na unaingia katika mtego ambao si rahisi kujinasua. Kuvaa au kutovaa kaptura si dalili ya ustaarabu,ni tamaduni tu zilivyolutwa kama ambavyosi rahisi mwarabu kuvaa vazi hili. Na je vipi ndege mjanja wa mjini akashindwa kujiendeleza kielimu?
Mimi nimeuliza swali hili mara kadhaa hapa bila kupata jibu.
Tukipata jibu la swali hili pengine na mjadala huu wa udini utapata jawabu.

Nakubaliana na wewe kabisaa katika suala lako la pili,naningeliweka dhahiri wazee wetu walipigaia ukombozi wa mwafrika au dini zao?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom