Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Status
Not open for further replies.
Kumbe Mkuu haukujua kuwa huko walikotokea wakina Dr. William Mwanjisi, Mzee John Mwakangale, Mzee Japhet Kirilo aliyesimamia kidete kesi ya mgogoro wa adhi wa wameru. Na wengine waliotoka nje ya mikoa unayoijua wewe ni wakina Mzee Joseph Kimalando kutoka Moshi ambaye amehusika katika harakati za kupinga ukoloni toka miaka ya 1930s akiwa ameajiriwa kwenye shirika la reli Tanganyika, mhehe Julius Mwasanyaji, mhindi Amir Jamal kutoka Morogoro, Frank Humplick na dada zake Mary na Regina ambao nyimbo zao ndizo zilitumika kuhamasisha wana TANU. Hata huko Tanga kwenye waislamu wengi, mchango wa Stephen Mhando na mdogo wake Peter Mhando katika kuhamasisha wabondei hauwezi kudharauliwa! ( kutoka " Nyerere and Africa: End of an era cha Godfrey Mwakikagile"). Na hawa ni sehemu ndogo tu ya waliohusika katika mapambano hayo. Ukweli nikuwa sehemu za pwani bila kuungwa mkono na sehemu nyingine za Tanganyika zisingefua dafu mbele ya mkoloni. Wote walihusika, tofauti na unavyotaka kutuaminisha.

Amandla.........

FM: Pole sana ndugu yangu. Mwakikagile amenakili kazi yangu. Ungesoma kitabu changu ungestaajabu na kusema mbona hii kama inatoka kitabu cha Mohamed Said? Ndiyo maana nikikusisitizia kuwa soma kwanza kitabu ndipo utakuwa katika hali nzuri ya kufanya majadiliano. Mwakikagile si wa kwanza kufanya hivyo watu wengi sana wanatumia kazi zangu kama zao na mimi ninafuata mila ya Kiislam kuwa elimu na taalamu haviuzwi kwa hiyo hata mtu akichukua kazi yangu akaitumia huwa kwangu si kitu hata kama hakunitaja.
 
FM: Pole sana ndugu yangu. Mwakikagile amenakili kazi yangu. Ungesoma kitabu changu ungestaajabu na kusema mbona hii kama inatoka kitabu cha Mohamed Said? Ndiyo maana nikikusisitizia kuwa soma kwanza kitabu ndipo utakuwa katika hali nzuri ya kufanya majadiliano. Mwakikagile si wa kwanza kufanya hivyo watu wengi sana wanatumia kazi zangu kama zao na mimi ninafuata mila ya Kiislam kuwa elimu na taalamu haviuzwi kwa hiyo hata mtu akichukua kazi yangu akaitumia huwa kwangu si kitu hata kama hakunitaja.

Cha msingi hapa ni je anayosema ni uongo? Kuwa hao wote hawakuhusika katika jitihada za kugombea uhuru? Kama Mwakikagile amenakili kazi yako na yote alioyaandika yamo kwenye kitabu chako basi huu si ushahidi tosha kuwa hata wewe unajua kuwa walihusika wengi katika kudai uhuru na sio waislamu au wakina Sykes au wazee wako peke yako? Kama ukweli huu unaujua na umeuandika kwenye kitabu chako kwa nini basi kwenye mihadhara yako hausemi hivyo bali unashikilia kuwa ni waislamu PEKE YAO ndio waliohusika katika mpambano huo na wakristu walibebwa tu? Na kama Mwakikagile amenakili kazi yako bila kukutaja kwa nini basi usimpleke kwa Pilato maana plagiarism ni kosa kubwa sana!! Lakini kama amekunukuu na kukutaja, hiyo ni kawaida katika uandishi kama wewe mwenyewe jinsi ulivyonukuu kazi za wengine. Mimi nimekuambia tangu mwanzo kuwa maandishi yako yanakushitaki maana humo humo una-refute haya unayoyasema hadharani kwa wale ambao ni wavivu wa kufikiri.

Amandla.......
 
Mkuu umenena , lakini wajikanganya katika maoni yako.
Kama umepitia maoni ya wadau wote waliobandika katika mada hii utaona umuhimu wa kujadili mada hii kwa wigo mpana zaidi kuliko ule wa kutetea uislamu.
Kama nada iliwekwa in the first place na "msaigon" mwenzio ikiwa ni changa la macho for narrow Islamic objectives,basi ndio maana unaona mwisho wake unaelekea kusiko tazamiwa na kusiko pendeza.
Kama mada iliwekwa kuutukuza uislamu basi vile vile hapa si mahala pake.
Halikadhalika kama mada iliwekwa kuelezea matatizo ya uislamu na umaskini, na mtanzania mwingine yoyote asivyofaidika na maendeleo , leo miaka 50 baada ya uhuru, basi hapo kuna mjadala.
Hakuna mwenye ujuzi wa kujadili matatizo ya uislamu kama mwislamu mwenyewe.
Asiye mwislamu anapotea muda wake kuchangia katika hili.
Waislamu ndo wanajua fika kwa nini hawa kujisomesha wakati wa mkoloni na vile vile hata kabla ya mkoloni kufika nchini, miaka ya 1600 na kurudi nyuma
Utafiti , kama wa Mohammed Said, usiwe wa kujiridhisha moyo kutafuta mchawi wa matatizo ya kukosa maendeleo yake.
Narrow mindedness ya Maalim Mohammed Said unaiweka wazi tatizo la maeneo yanayokaliwa na waislamu kukosa maendeleo in very simplistic form
Jamaa huyu anaweka mjadala kwa nia ya kuudhibiti ukristo ili uislamu uneemeke kwa sababu yoyote ile. Na vile vile basi anatazamia watu wakae doro na kukubali yale yanayotolewa na kuelezewa as if mipango yote ya kuleta uhuru ilifanyika na kina Sykes na waislamu wengine, na Mwalimu akakaribishwa tu ku-officiate the occassion.
History cannot be so simple and cheap.
Nimeona mkuu MS unamwomba FM alete uchunguzi wa mapambano ya kuleta uhuru kutika sehemu zingine za Mbeya na Arusha, is this an admission that your own research is faulty and inconclusive?
You are not being fair to your selves and the public in general.

Ujinga unatabia moja mbaya, una tabia ya kujitukuza katika mambo ambayo mtu huwa hauji, na bado ukielimishwa unaona kama unadhalilishwa na kutukanwa.
Na ndio maana naona Mwalimu wakati Mwingine alichukua drastic measures za kuwaweka ndani wapinzani wake waelimishwe na kuwekwa katika hali ya kutumika ili waone umuhimu wa umoja.
Kwa sisi tuliopitia miaka hiyo ya Mwalimu tunaelewa hilo, na vijiwe kama vya Saigon tunavifahamu ingawaje tunajua vilianzishwa kutukuza yale wenyewe wasiyoyafahamu.

Mkuu Lole,

Calm down, punguza ukali wa maneno ungeweza kufikisha ujumbe wako vizuri tu bila ya maneno "narrow mindness ya maalim Mohamed Said" na ujumbe ungefika. Hapa tuna elimishana hatushindani nani fundi wa kuvurumisha maneno yasiyo na tija kwenye mnakasha.

Back to the mada, kitabu cha Mohamed Said kinaweka historia iliyo potoshwa sawa, hilo la "kuudhibiti" ukristo na kuufanya uislamu ushamiri unamuonea tu. Mohamed Said is on the record hapa akisema nia sio kuwazuia vijana wa kikristo wasisome au kuendelea huko ni kuwaonea na wala sio mafunzo ya uislamu. Ninacho kiona hapa Mh Lole unakijitahidi kwa makusudi kupotosha ili Mohamed Said aonekana mtu mbaya.

Mkuu tujadiliane kwa heshima na tupingane bila kupigana naamini thats not too much to ask!
 
Kumbe Mohamed Said almaarufu kwa jina "Sidney"? Na memba mwingine wa Saigon jina lake ni "Eddie"! Nashindwa kuelewa kwa nini hawa wanaopinga udhalimu wa wakristu hawachelei kuchukua majina ya "kikristu". Kwa nini wasiige mfano wa Mobutu Sese Seko Nkuku Ngbendu wa Za Banga?

Amandla......


Fundi, shukran kwa mchango wako.

Sio hayo tu bali pia hata hicho kitabu cha Mohamed Said kimeandikwa kwa lugha ya madhalimu "wakikristu" how about that?

Wapi pame semwa kila kitu kuhusu ukristo ni "udhalimu" na hakifai? kuweka sawa historia ya wazee wetu ndio imekuwa nongwa mpaka wachukizwa na majina tu?, tupo kwenye ulimwengu na sayansi na teknolojia tunatumia pc's, internet, nk ambavyo mainly ni mavumbuzi ya "wakristu" sasa ndugu yangu wataka tusitumie haya kwa sababu tu ya kuwasema vibaya wakristo?

Tujikite kwenye mada watu wanatusoma hizi cosmetics za majina zisi kusumbue mkuu wangu ni vionjo tu.
 
Ha ha ha!!
Mkuu umenikumbusha miaka hiyoooo!
Wakati ule baada ya kuanzia mwaka 1968 kuendelea hadi miaka ya 1970's mapigano katika vita vya Vietnam kati ya Vietnam Kaskazini na Kusini vilipambamoto.Vietnam Kusini pamoja na kusaidiwa na Marekani na nguvu kubwa sana ya kijeshi ilizidiwa vibaya na wapiganaji wa misituni wa kikomunisti wa Vietnam ya Kaskazini wakisaidiwa na Uchina.
Jiji la Siagon likawa under siege hadi mwishoni mwa vita hivyo na kwa muda mrefu tu.
"Saigon" ya Dar es salaam iliundwa na vijana wengi tu wa kihuni kutoka sehemu mbali mbali za Kariakoo na kuzunguka.Ilisemekana vijana wengi kati ya hao walikuwa wavuta bangi na kupigana ovyo mitaani na vikundi vinavyo pingana.
Kwa hiyo ukiingia eneo la "Saigon" Kariakoo, basi unaingia sehemu ya umwamba, vurugu na tafrani.
Mimi nalifahamu hilo kwa vile hata sehemu za Temeke,Toroli,Chang'ombe lilikuwepo kundi la "Black September" lenyewe kama Saigon ilikuwa fujo tu hasa katika matamasha ya kitaifa(kama miziki) na mipira uwanja wa Taifa kuingia bure kwa kuruka ukuta.
Alipokuja Lwambo Lwanzo Makiadi 1971, kundi hili lilifanya fujo kubwa kwa kuingia kwa kuruka ukuta Uwanja wa Taifa, hili nalikumbuka maana nilikuwepo.

Mada ni " Ukweli kuhusu waasisi wa TANU" uki taka habari za "wahuni" na wavuta bangi" wa Saigon hilo lina jadilika lakini sio hapa fungua thread nyingine tuta changia huko.

Turudi kwenye mada tafadhali.
 
FM: Ahsante kwa mchango wako. Kama nilivyosema hapo nyuma kuwa hata kama mtu atanakili kazi yangu mimi huwa sijali. Huchukua hiyo kazi na kuiweka katika maktaba yangu. Elimu katika Uislam ni kitu cha bure, hakiuzwi. Sasa nitajifedhehesha kama nitampeleka mtu mahakamani kwa kuwa ati tu kanakili kazi yangu. Ulosema nimeyaelewa na nakushukuru sana kwa michango yako. Nakuwekea taazia niliyoandika ya Frank Humplink ambayo mtu kainakili na kuifanya yake. (Taazia hii ilichapwa kwa mara ya kwanza na The East African (Magazine). Ukiingia katika website yao utaikuta. Kuna vitabu viwili mna maneno yangu verbatim na mimi kila nikisoma hufurahi na kusema huyu bwana basi hata kubadili maneno kidogo hakutaka? Wala hainishughulishi kama yeye aliyeninakili kadai fedha kwa mchapaji au vipi.) Mzee Humplink alikuwa rafiki yangu sana na nimechota mengi kutoka kwake. Hebu soma hii:


Singer who angered the colonialists

Article Summary
by:murugu Original Author: joseph murugu
PicExportError
Summary rating: 5 stars (3 Ratings)
PicExportError
Visits : 194
PicExportError
words:900
PicExportError

More About : singer who angered the colonialists

FEW PEOPLE ARE AWARE OF THE PASSing away of Frank Humplick, the gifted singer, guitarist and composer of many melodies that though
recorded more than 50 years ago, still never fail to entertain the
present generation and stir memories of yesteryears for those who lived
through those times. Frank Humplick, died in Lushoto on Saturday
August 25, 2007. Frank Humplick was born on April 3, 1927, on his
father's farm in Moshi. Frank, as he was popularly known, was baptised
Franz Yosef Humplick. His father was a Swiss civil engineer and his
mother was a Chagga. His father, Yosef Humplick, was among the
engineers who built the Tanga-Arusha railway line at the turn of the
20th century. Frank's death passed unnoticed outside Lushoto
despite his being a giant among East African musicians of his time. One
has only to visit the record library of the Radio Tanzania Dar es
Salaam or the Kenya Broadcasting Corporation to realise how prolific a
composer Frank was. The musician was a household name in East
Africa competing with others of his time like Salum Abdallah, Mwenda
Jean Bosco, Eduardo Massengo, Fadhili William, Fundi Konde, John Mwale
and Daudi Kabaka among others. Unlike the deaths of his peers,
which made national news, Humplick's passing was announced in a small
column in one of the national dailies. Those who have listened to
Humplick's music will agree that it is timeless. Each composition is
unique and carries that unique Humplick signature in the melody and
guitar work. Listening to his songs, the flavour is still the same as
it was when he first entertained his fans. He was backed on the vocals
by his two sisters - Techla Clara and Maria Regina - and the Jambo Boys
Band of Nairobi. His most memorable composition is Harusi, which
he recorded with his sisters in the 1950s and which has become a
wedding anthem in East Africa. This song was later recorded in Sweden
by the late Patrick Balisidja of Tanzania and the Archimedes, a Swedish
band in the late 1970s. Harusi and other composition by Humplick were
later recorded by the Harrison brothers of Them Mushrooms now known as
Uyoga. The band introduced his music to the present generation.
The recordings by such young musicians such as Them Mushrooms and
Balisidja gave Humplick's music a new lease of life and a touch of
modernity. Growing up in Moshi and attending Majengo Middle School in
the early 1960s as a young boy, I used to see young Humplick riding his
motorbike with a guitar strapped to the back seat. Our school gate
overlooked his parent's house across the road. The house still
stands. Humplick was a popular figure even with children,
particularly because of his song Kwenye kabati kuna nyoka (There is a
snake in the cupboard) which was very popular for its satire depicting
the musician as a schoolteacher teaching English to students who found
it difficult to grasp the real meaning of English vocabulary. After
several sessions, he started narrating to me his life after being
discharged from the King's African Rifles at the end of World War Two
in 1945. Sykes said that, in his opinion, the most appropriate person
for me to talk to about that period was his friend and business partner
of many years, Peter Colmore. SYKES THEN CALLED COLMORE in
Nairobi and it was arranged that I travel to Nairobi to talk to him. I
interviewed Colmore at his Muthaiga residence and had the chance to see
his photo archive comprising photos of musicians whose songs he had
produced. But Mzee Humplick would later tell me that
his favourite songs were the ones which he recorded with his sisters
such as Harusi, Wanipenda Juu Kwa Juu, Ponda Mali Hujafa and
others. Indeed listening to his music, many people's favourites
are are precisely those songs he sang with his sisters. Nevertheless,
he recorded very memorable work with renowned guitarists Fundi Konde,
Fadhili William and Eduardo Massengo at the peak of his carrier.
Back in Dar es Salaam, I asked Sykes about Humplick. He showed me an
old photograph of himself Humplick and Peter Colmore taken in Moshi in
the early 1950s.This was the last time I saw my friend Frank
Humplick.Not many people, even his contemporaries were aware of his
whereabouts since he bowed out from the stage. Humplick lived a
dignified, comfortable and quiet life in Lushoto. However, he was an
important personality in the township community and in the local
church. This is the reason why his funeral was well attended. An
album containing the same 25 songs that I bought in Mombasa was cut in
the US. Ambassador Mohamed Maharage Juma (Tanzania's envoy to
Democratic Republic of Congo) who shares my taste in music since our
schooldays, saw the album in New York at the residence of the late
Ambassador Tatu Nuru, a contemporary of Humplick. When I asked
Humplick about this, he said he was not aware of the album just as he
was oblivious of the fact that his audio cassettes were selling like
hot cake in Kenya.
Published: January 09, 2008

 
FM: Mimi siyo Eddie. Wala sijaandika katika kitabu changu neno lolote la kutunisha kwa kuwa najua si mafunzo ya Kiislam kutukana dini au yeyote yule. Mimi ni mwanachama mwanzilishi wa Saigon Sports Club 1967 na nikicheza mpira katika club hiyo kwa kipindi kirefu tukianzia club yetu ya zamani Everton. Nina kumbukumbu nzuri sana za wenzangu ambao wengine wameshatangulia mbele ya haki kama Jumanne "Tarzan" Hassan au Masimenti, Mrisho "Wanted", Ghalib "Guy" Hamza, Abdallah "George Young" Fadhili...kwa wakati ule wa utoto tukipenda kujiita majina ya stars wa Ulaya katika senema au vilabu vya mpira. Hapakuwa na zaidi ya hilo. Mimi nilikuwa Mohamed "Eusobio" Said halafu nilipoingia sekondari nikachukua "Sidney" kutoka kwa Sidney Poitier. Hii ndiyo ilikuwa Dar es Salaam ya miaka hiyo. Hilo la kuwa Saigon ilikuwa club ya wahuni mimi nalisikia kwako hii leo. Najivuna kuwa mimi nilikua na kuwajua hao wote nlowataja. Saigon hadi leo ni club yenye heshima na tuna wapenzi na marafki wengi sana na wengine wamejiunga na club miaka mingi baada ya sisi kuwa watu wazima na hata huo mpira hatuuwezi kamwe. Na hao waliojiunga wala si watoto wa Kariakoo bali ni watu kutoka bara. Wote hao wanajinasibu na club yetu hadi hii leo.
 
LG: Kuomba wengine waandike kuhusu TANU kwengineko ni kutaka historia ikamilike. Kazi yangu lazima iwe na makosa wala hilo halina shaka. Kazi ya binadamu yoyote yule haiwezi kukamilika. Ilo na ukamilifu ni kalamu ya Allah (SW) peke yake. Ndiyo maana unaona hapa ukumbini mnanitoa makosa.
 
LG: Kuomba wengine waandike kuhusu TANU kwengineko ni kutaka historia ikamilike. Kazi yangu lazima iwe na makosa wala hilo halina shaka. Kazi ya binadamu yoyote yule haiwezi kukamilika. Ilo na ukamilifu ni kalamu ya Allah (SW) peke yake. Ndiyo maana unaona hapa ukumbini mnanitoa makosa.

Mkuu MS ieleweke wazi kuwa mimi sikupingi kwa maana ya kupinga Uislamu la hasha! Ninachopinga ni kuinarrrow down historia ya nchi hii katika macho ya kufumba na kufumbua , na in black and white kuwa kati ni ya Uislamu na Ukristo.
Uliyo yaeleza katika mada zako ni ya kweli kabisa ila tunapotofautiana ni katika interpretation ya mambo haya.
Tumesikia mengi ya "wa kuja", "mvaa kaptura", "watu wa kutoka shamba" nk.
Tupende tusipende kama nilivyosema awali kama hatuna kitu kati yetu cha kujivunia as a common historical acheivement, then we might as well agree to go different worlds kulingana na maono ya kila mtu.
Hili halipendezi kwa mustakabali wa nchi hii na kile tunachotarajia siku za usoni.
Na kuna wadau wanaoona kuwa Utaifa ni kitu cha kishamba sana, watu wa mjini hili haliwahusu.
Ndio hapo presha inapanda na presha inashuka!!
Na ndio maana vile vile nimekataa kuzijibu hoja hizo as being too low to contemplate.

Hata hivyo pamoja na hadithi nzuri unazotuletea ,kama nilivyosema hapo nyuma, interpretation yake lazima iwe positive , na isiwe divisive.
Kama kuna matatizo tufanye nini kama Taifa ili sehemu zilizo nyuma kimaendeleo ziendelee na kufaidika na uhuru wa nchi hii.

Sitasahau kuwa miaka karibu 20 iliyopita wananchi wa mikoa ya kusini walichoshwa na ahadi za serikali za kujenga barabara ya kwenda Lindi na Mtwara.
Wakati huo Waziri Mkuu alikuwa Edward Sokoine.
Wananchi kupitia wabunge wao walileta azimio la kujenga wenyewe barabara hiyo!
Wazo lile liliwagusa watu wengi sana na hisia za kujenga nchi yetu na hasa hii barabara ilishika kipaumbele.
Sokoine alikataa wazo hilo na kuahidi kuwa mipango ya utekelezaji wa barabara ile utafanyika tu na serikali.
Kweli leo, tunasahau kuwa ahadi hiyo imetekelezwa na ujenzi unakaribia kukamilika.

Sasa Mkuu Mohammed Said nimetoa mfano huu ili kuonyesha jinsi mtu ukiwa pro-active unavyoweza kuigusa jamii na kuchangia maendeleo pale yanapokosekana.
Na pale unapochangia kujenga shule au barabara unamchangia Mtanzania kwanza, na hatuweki suala la udini hapo.
Mimi nimekutuhumu mara kadhaa Mkuu Mohammed Said kuwa mada yako ni divisive kwa vile ukitoa lawama ambazo sana sana ni za kuhisi tu, zaidi ya nusu ya waTanzania hawataafikiana nawe.
Ndipo nikakuuliza wewe na wale supportes wako tufanye nini sasa?
 
Mkuu Lole,

Calm down, punguza ukali wa maneno ungeweza kufikisha ujumbe wako vizuri tu bila ya maneno "narrow mindness ya maalim Mohamed Said" na ujumbe ungefika. Hapa tuna elimishana hatushindani nani fundi wa kuvurumisha maneno yasiyo na tija kwenye mnakasha.

Back to the mada, kitabu cha Mohamed Said kinaweka historia iliyo potoshwa sawa, hilo la "kuudhibiti" ukristo na kuufanya uislamu ushamiri unamuonea tu. Mohamed Said is on the record hapa akisema nia sio kuwazuia vijana wa kikristo wasisome au kuendelea huko ni kuwaonea na wala sio mafunzo ya uislamu. Ninacho kiona hapa Mh Lole unakijitahidi kwa makusudi kupotosha ili Mohamed Said aonekana mtu mbaya.

Mkuu tujadiliane kwa heshima na tupingane bila kupigana naamini thats not too much to ask!

Mkuu nafikiri hii mada umeiingilia katikati, jaribu kupitia post zote na utaona mlolongo wa ubishano uliopo. Inabidi nikuwekee some allegations zinazokera kutoka kwa mwenzetu MS ili uweze kuona nini kunaendelea vichwani mwa watu wakiendelea na mada hii,

Post no 345 Mohammed Said
EAMWS ilimtisha Nyerere kwa kuwa nguvu yake na ya Kanisa ilikuwa itadumu mindhali Waislam hawana elimu. Ikishakuwa Waislam wataelimika na ujanja waliokuwanao kiasi cha kuweza kumtoa Muingereza nchini yeye na Kanisa lake watakuwa na wakati mgumu. Aga Khan na EAMWS walikuwa tayari wanajenga shule kila mkoa na wilaya na mpango wa chuo kikuu ulikuwa ushakamilika. Viongozi wa mipango hii alikuwa Aga Khan, Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Aziz Khaki na Tewa Said Tewa. Ikabidi hawa wote awafanye maadui zake. Kisa hiki nimekieleza kwa kirefu katika kitabu. Siku zote ninapoalikwa katika hadhara na nikaombwa kuzungumza juhudu za Waislam katika kujiendeleza katika elimu nikifika hapa watu wengi hulia. Kwa ufupi Nyerere akaunda Bakwata na kuivunja EAMWS. Mufti Sheikh Hassan bin Amir akakamatwa kwa tuhuma ati alikuwa anafanya mipango ya kupindua serikali. Taasisi za Kikristo hazikuguswa ziko na nguvu hadi sasa. Historia ya Waislam nayo ikawa ni mwiko kuelezwa kokote. Hadi sasa.

Nadhani maelezo haya yanajibu kwa nini Waislam tumeshindwa kujiendeleza katika elimu.



Haya mkuu ni maandiko yasiyo na ukweli wa kudhibitika ya ndugu yetu huyu.

Post no 797 ya Lole Gwakisa
Mkuu Mohammed Said, I have said again and again that it is the Islamic communities that RESISTED formal education , sometimes refering to it as kafir education!
Lets refer to John Illife pg 445 in his book A modern history of Tanganyika,

" In 1948 literacy among children between six and fifteen yrs old varied from 21% in Tanga Province to5 % in Central Province. Whereas in 1956 some 90% of Chagga children were at school, the proportion among the neighbouring Meru three years later and among the Arusha only 34%. SOME MUSLIM REGIONS STILL RESISTED EUROPEAN SCHOOLING, BUT MOST OTHER BACKWARD AREAS STROVE TO CATCH UP WITH MORE FORTUNATE NEIGHBOURS WHO THEMSELVES STROVE, GENERALLY TO STAY AHEAD. SO SMALL TRIBES WITH EARLY MISSION EXPERIENCE GENERALLY KEPT THEIR EDUCATIONAL LEAD OVER LARGER TRIBES-WITH IMPORTANT POLITICAL REPERCUSSIONS."

Mohammed Said ili upate kueleweka na wananchi wote wa Tanzania na si waislamu tu, fanya utafiti wako pan territorial na utapata kuelewa wengine tunachokiongelea.
Ushindani wa elimu haukuanza wakati wa Sykes tu , bali hata kabla.

Sasa Mkuu Eddie tumwamini yupi kati ya Illife aliyefanya utafiti zamani sana tokea 1940's au historia ya "kisasa" ya mwenzetu Mohammed Said.
Kuna walio mwita anaandika uongo , pitia post zote, kuita utafiti wa MS kuwa narrow minded ni haswa beffiting maana yeye anaquote yale tu yanayowatukuza babu zake(babu zake waislamu kuwa exact) na si vinginevyo.

Mbaya zaidi ni kujaribu kuweka matatizo ya kukosa maendeleo mengi tu sehemu nyingi nchini kuwa ni tatizo la Mwalimu, kama Mkristo na Christian lobby yake.
It is infuriating I am sorry.
 
MAY i ask,hivyo where is the member GAME THEORY?????? going by his past postings,it is impossible for him to stay in the sidelines-800 plus postings na huyu mmanyema GT hajatokea-something is cleary not right somewhere
 
SOA: Kwa hisani yako naomba unifahamishe maana ya GT nini tafadhali.
 
LG: Mimi sina tatizo na John Illiffe au mtafiti yoyote yule. Hapo nyuma nimesema kuwa kwangu mie ni muhali kuegemea historia ya wazee wangu ije aindikwe na wageni kutoka Uingereza na Marekani. Mimi nimetafiti na kuandika historia kama nilivyoelezwa na wenyewe waliopindua gurudumu la historia. Juu ya hilo sina ugomvi na historia hizo nyingine na zisomeshwe kama inavyofanyika sasa lakini nilikataalo ni sisi kukatazwa kuwaenzi wazee wetu na kuhifadhi historia yao. Illife amenishambulia sana katika Cambridge Journal of Africa History (sikumbuki citation yake) baada ya kutoka kitabu changu na kumtaja mle lakini nimekubali criticism zake kwani kila mtu ana haki ya kueleza anachokiona sawa. Wapo watu kama wewe watamuona Illife yuko sahihi na wako wengine wataniona mimi niko sahihi.
 
LG: La kufanya kwanza serikali ikubali lipo tatizo. Hili swali limeulizwa mara nyingi na nimelijibu.
 
SOA: Kwa hisani yako naomba unifahamishe maana ya GT nini tafadhali.

huyu ni member hapa Jamii Forum,yeye posting kama hizi huvaa njuga na kusumbua sana watu,kama unavyofanya wewe,he is a knowledge able person.I am surprised hajatokea,i hope ni mzima wa buheri
 
SOA: Kwa hisani yako naomba unifahamishe maana ya GT nini tafadhali.

Kaka GT ni mwana-jf mmoja anajulikana kama GAME THEORY.Hata mimi naamini angejitumbukiza katika mjadala huu basi mambo yangekuwa matamu zaidi.Nimejifunza mengi sana katika mjadala huu,kubwa zaidi ni uwezo wenu wa kukosoana huku mkivumiliana,nasikitika mnaelekea kukubaliana japo kwa kutokukubaliana.Mjadala huu umenikumbusha JF ileeeeeeeeeee
 
Che K: Ahsante kwa mchango wako na nimefurahi kama umefaidika na mjadala.
 
SOA: Ala! kumbe mambo ni mema basi. Si nimesema mwalimu wangu Maalim Haruna (Mungu amrehemu) alinifunza vyema adabu za majadiliano? Ndizo hizo nazitumia leo. Kwanza ni kumheshimu yule ufanyae mnakasha na pili ikiwa yeye ni mshari hana lugha njema ujibidiishe kumtuliza kwa maneno mazuri. Kubwa alikuwa anasisitiza usomi makini. Ulijue somo ulizungumzalo.
 
Wanaukumbi: Nadhani mmepata kusikia kitabu Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru. Nilikuwekeeni pitio nililoandika kuhusu kitabu hicho humu ukumbini. Sasa kitabu kipo nchini kinauzwa Al Hazm Bookshop Msikiti wa Mtoro bei ni Shs: 45,000.00. Kitabu kimebadili historia nzima ya Zanzibar. Pitio limechapwa vilevile na Raia Mwema la 15 September na An-nuur la 14 na 17 September.
 
lk pont bado hujaigusa, said anasema licha ya waislam kuwa mstari wa mbele ktk harakati za kudai uhuru. lkn baada ya uhuru wazee hao walitengwa kabisa hii ndio point unatakiwa pia uitete

FM: Kuna tofauti ya kufanya rejea na kunakili la kwanza inakubalika la pili ni wizi (jinai) kwa sheria hizi za Kilimwengu. Mimi siwezi kunakili kazi ya mtu mwingine. Nadhani sababu unaijua.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom