Hatuhitaji kutumia nguvu kubwa kueleza ubaya wa Magufuli, kwa sababu yeye mwenyewe alifanya kazi kubwa na ya wazi kuonesha hayo.
Sisi tunafanya marejeo tu.
Tatizo tuna uelewa tofauti. Sasa unategemea mimi nifikiri sawa na mtu ambaye hajui uhuru wake, hajui haki za binadamu, hajui sheria, hajui historia, hajasoma, hajui Kiingereza kupanua wigo wa mawazo, hajasafiri kufika hata Kenya?
Watanzania wengi ndio wapo katika kundi hilo, wajinga, wanaridhika kirahisi, wanaongozwa na woga, wanataka mbabe fulani na kuona ubabe ndiyo uongozi mzuri, hawataki kutetea uhuru wao.
Sasa watu hao wakimpenda mtu kwa ujinga wao, wingi wao ndio unafanya waliposimama pawe sawa?
Unaweka hoja kwamba wingi ndiyo kuwa sawa, nchi yenye wajinga wengi wajinga wengi wanaweza kupenda kitu kibaya kinachowaumiza wao wenyewe.
Magufuli kanunua ndege za dola milioni 726, katika nchi ambayo haina hata business plan ya kuendesha biashara ya ndege.
Halafu tunaambiwa kilimo ndiyo uti wa mgongo wa Tanzania, na bajeti ya kilimo cha umwagiliaji ni dola za Marekani milioni 16, hiyo bei ya nyumba moja tu hapo Malibu.
Yani tuendelee kulima kwa kutegemea mvua za kudra wakati hela zote hizo tunanunulia ndege!
Tena ndege zenyewe zinaishia kukamatwa huko nje kwa madeni. No staregic planning at all.
Wewe unamuona huyo mtu anajua priorities za nchi?
Tanzania announced an order for a 787-8 Dreamliner, a 767-300 Freighter, and two 737 MAX jets at the 2021 Dubai Airshow.
www.tanzaniainvest.com