Ukweli kuhusu Wakatoliki kutokuabudu sanamu zilizopo makanisani

Ok!
Hapa ulikuwa una maanisha nini....???


Wewe ni kilaza sana...
Nashukuru mkuu,biblia inazuia mtu kujisifu kwa kuwa na akili hivyo nitanyamaza katika hilo.Wewe kwa kuniita kilaza hakunifanye niwe kilaza.
Sasa turudi darasani ulimwuliza katekista lile swali lako?Leta majibu yake
 
Mimi ni mkatoliki nisiyeunga mkono uwepo wa masanamu kanisani... Na ijumaa kuu huwa sijiangaishi kubusu msalaba. Sisali rozari kwakuwa naamini bikira Maria hawezi kusikia sala zangu...

Ntabakia mkatoliki kwa msimamo wangu.
msimamo wako kama wangu mkuu coz kila nikisoma biblia hili swala na mengine mengi huwa siafiki ila sema tu hakuna dhehebu lililokamilika zaidi ya kuongozwa na Roho Mtakatifu kama wale wakarismatic huwa nawakubali sana ndani ya catholic, hawana mambo ya rozari, misalaba na wateva
 
wakarismatic huwa nawakubali sana ndani ya catholic, hawana mambo ya rozari, misalaba na wateva

Kauli kama hizi ndio zumefanya Majimbo mengine kikundi cha Karismatiki kufutiliwa mbali..

Hakuna vikanisa vyenye taratibu zake tofauti na za Kanisa huku wakijiita Wakatoliki....Hakuna....Wskibainika ni Ex-communication mara moja..

Hata nyie mnaongelea nyuma ya keyboard, ila mkibainika mpo kinyume na mafundisho ya kanisa, ni ex-communication mara moja bila kupoteza muda..

Sifa ya Kanisa Katoliki ni kitokubembeleza....ukibainika ni kufukuzwa ukaanzishe la kwako
 
Niko Parokia ya Mwenye heri Isidori Bakanja, Boko. Hebu njoo nione uwezo wako wa kunizuia.

Maana hata askofu wangu anaujua msimamo wangu na hajawahi kunisema vibaya kama wewe "mtakatifu mbarikiwa"
Isidori bakanja ni raia wa nchi gani ?
 
Unasema haijachakachuliwa halafu Unaondoka 73/72 Unamaana gani?
 
mamlaka gani ya kumex-communicate mtu, nan mwenye mamlaka hayo. kuwafungia karismatic ni wivu wa mapadre tu huo wasioishi maisha ya kiroho wanabaki wakibwabwaja tu na kuona kama wakarismatic wanachukua nafasi zao
 
Unasema haijachakachuliwa halafu Unaondoka 73/72 Unamaana gani?
Maana yake ni kuwa..

Kitabu cha Yeremia na Maombolezo ni kitabu kimoja....Kitabu cha maombolezo huwa kunaitwa kitabu cha Maombolezo ya Yeremia....

Hivyo baadhi ya Biblia huunganisha vitabu hivyo na kuwa kitabu kimoja yaani 72 books...
Na biblia zilizonyingi hutenganisha kitabu cha Yeremia na Maombolezo hivyo kuwa vitabu viwili vinavyoweka jumla ya vitabu 73.,

Sasa nadhani umeelewa
 
mamlaka gani ya kumex-communicate mtu, nan mwenye mamlaka hayo. kuwafungia karismatic ni wivu wa mapadre tu huo wasioishi maisha ya kiroho wanabaki wakibwabwaja tu na kuona kama wakarismatic wanachukua nafasi zao
Kanisa haliendeshwi kama kijiwe cha kahawa...Kumbuka system ya Admin kwa Serikali za kidunia wali-copy kwenye system ya Admin ya Kanisa..

Kuna Canon law na adhabu zake...Sasa wewe peleka upuuzi wako kanisani uone utakachofanywa....


Mtoke muende huko mnskohisi kupo sahihi au mkaanzishe makanisa yenu....Msituharibie kanisa...
 
Roman Catholic si DHEHEBU, ni dini. Madhehebu ni hayo makanisa yenu yaliyojichomoza ndani ya Kanisa Katoliki kwa sababu hii au ile. Wakati Yesu anamkabidhi Petro (Pope Petrus I) kanisa, hakukuwa na Lutheran wala Kakobe sijui nani. Unachopaswa kujiuliza ni mmetokea wapi?

Weka hapa dhehebu lako nikueleze kwa nini kichwa chako kimeandaliwa kubisha zaidi ya kuelewa.
 
nachukia dhehebu...sijataja mtu.. uwege unasoma vizur basi kabla hujajibu.. ila hapa kila mtu ana uhuru wa kueleza yake ya moyoni KAMA NIMEKUKERA AM SOREEE[emoji4] [emoji4] [emoji4]
Wazee wa mipasho, waprotestant waliobobea. Taratibu mtaelewa. Mzee wa upako ni mlokole mwenzenu, juzi hapa amesema unywaji wa pombe sio dhambi, na yeye anakunywa wine kama kawaida. Jambo kama hilo RC walishaliona zamani tu! Tatizo la waprotestant ni tafsiri ya maandiko. Sisi tunasomesha mapadre wetu kiasi cha kutosha, uwezo wao wa kutafsiri ni wa hali ya juu. Lakini kwa waprotestant, kila muumini anajidai anajua kutafsiri, matokeo yake tunawapata watu kama huyu aggyjay ambaye anabeba mstari word to word!
 
Huyo mungu wa dhehebu ulilopo ni noma, mnafundishwa chuki kiasi hicho?
Usilolijua litakusumbua..mbinguni au motoni utaenda peke yako na si na wakatoliki unaowachukia.
Wenyewe tunaoelewa maana ya hizo sanamu wala hatuna shida na mtu. Na pia hatuna shida na dhehebu la mtu. Duniani kuna uhuru wa kuabudu, shikilia yanayokuhusu.
 

moja kati ya sababu zinazofanya kanisa katolik liendelee kuwa la kimwili ndo haya mambo ya ex-communication ambao ni utaratibu wa kidunia wakati kanisa la Kristo liko kiroho, Sijaona kwenye agano jipya Yesu akamuexcommunicate mdhambi/ au mtu aliyekosea kama taratibu za kidunia za kanisa katolik
 
unaujua mwanzo wa kanisa katolik vizuri? au unaongea tu
kanisa la kirumi = kanisa katolik in recent time, kwa sababu lilikuwa kanisa la kiselikari ndio maana likawa na nguvu kudominate majority, ukihitaji zaidi nijulishe tuelimishane vzr mkuu
 
unaujua mwanzo wa kanisa katolik vizuri? au unaongea tu
kanisa la kirumi = kanisa katolik in recent time, kwa sababu lilikuwa kanisa la kiselikari ndio maana likawa na nguvu kudominate majority, ukihitaji zaidi nijulishe tuelimishane vzr mkuu
We naona unajaribu watu kijuu juu ehhh!!!

Babu mzaa nyanya ako wa kule dongobeshi orkesmeti hujui historia yake ila unsifahamu historia ya dunia(catholic).....

Hebu toa vichekesho hapa....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…