Ukweli kuhusu Wakatoliki kutokuabudu sanamu zilizopo makanisani

Si ukatoliki Tu,hata usabato nao Una makandokando kibao.
 
Mkuu, katika kipande cha kanuni ya imani, inasema Yesu aliteswa kwa mamlaka ya Mrumi Ponsio Pilato na wala siyo kwa kupitia shinikizo ambalo alilopewa na makuhani na wazee wa Kiyahudi, ambao nao walitaka kumfitinisha na mamlaka yake ya uajiri wake ipale walipodai kuwa Yesu anajifanya kuwa ndiye mfalme wao, wakati wao mfalme wao ni Kaizari! Hivyo anastahili adhabu ya kifo kwa tuhuma za uhaini!

Kuwepo kwa mamlaka ya dola la Rumi katika kanuni hii na kuijumuisha na mamlaka ya kimbingu huenda ndiyo ikawa ndiyo chanzo lkikuu cha Wasabato kuja na "counter attack" dhidi ya Dhehebu Mama la Kikatoliki ndani ya dini ya Kikristo, na pia na mamlaka nzima ya dola ya Rumi.

Nafikiri pengine hiyo ndiyo sehemu ambayo ilimpa ukakasi mwingi Mama Hellen White, kiasi kwamba "fan base" yake haikubaliani na madai au mantiki iliyopo nyuma ya kanuni hii, na hasa ikizingatowa ndiyo tafakari kuu ya kipindi hiki cha Pasaka iliyoletwa na wale wajulikanao kama mababa wa imani waliokutana Rumi kwa wito wa Kaisari Kstaontino (mtaguso), ambao ndio hasa waliitamua siku ya Bwana kama Jumapili na wala siyo Sabato halisi na ya awali kuendana na maandiko matakatifu.
 
Usidhani kanisa katoliki ni mapadre tu na maaskofu na masista.

Kanisa ni pamoja na wewe yaani kila aliyebatizwa na hivyo kila mmoja ana duty ya kulilinda kanisa.

Hivyo mjibu huyo muhubiri usisubiri askofu au padre.
Inaonekana hata yeye mwenyewe hana anachojua,
 
Hakuna mkatoliki aliyesomea biblia, wamesoma canon law tu, wanatumikia taifa la rumi chini ya taasisi yao ya Vatican
Hakuna mkatoliki aliyesomea biblia, wamesoma canon law tu, wanatumikia taifa la rumi chini ya taasisi yao ya Vatican
Huna ulijuwalo, wewe hujui theolojia ni nini.

Wa katoliki wamesoma zaidi ya Biblia mpaka injili inayoitwa Apocrypha ambayo vitabu vyake havimo kwenye Biblia.

Kanisa Katoliki ndio Universal church la mitume.
 
Kwa mjibu wa biblia, siku ya ibada ni ipi?
 
Kanisa la Mungu ni lipi? Kwa hbr ya upotofu, wakati katoliki imepotoka kwa asilimia 95%, Kakobe amepotoka kwa 50% ana nafuu japo wote ni wakosefu.

Punguza u much know. Na utambue fika mimi ni Mkatoliki nisiye sikia kelele zozote zile kutoka kwa wapita njia kama wewe.
 
Wee unaelewaje Kutoka 20 : 4 - 8
Hicho kitabu unatakiwa ukisome ukiwa umetuliza sana akili. Na ukisome na vitabu au vifungu vingine alafu uje kwenye uhalisia pengine utaweza kuelewa zaidi!
Siku ukijua maana halisi ya Sanamu kuwa ni ishara au taswira au hisia au alama au kitu chochote kinachochukua nafasi kwenye mawazo na maisha yetu hakika utajua kuwa sanamu na ibada ya Sanamu inayokatazwa ni ipi.
Fedha ni Sanamu
Simu yako ni Sanamu
Nyumba yako ni Sanamu
Gari lako ni Sanamu
Picha za ni Sanamu
Nguo zako ni Sanamu
Samani zako za ndani zote ni Sanamu!
Tamaa... Dharau... Kiburi... Majivuno... Ufisadi... vyote hivyo ni sanamu
Tamaa, urahibu uliopitiliza wa vitu hivyo na vikakufanya umsahau MUNGU wako hiyo ndo inakua ibada kamili ya masanamu.

Hao wakatoliki mnadai wanaabudu Sanamu si kweli. Katika macho ya imani wanatumia zile ishara kuimarisha imani yao. Ishara ya msalaba! Mapicha yao kanisani vyote vinawaelekeza kuabudu Utatu Mtakatifu.
Kuna watu na makanisa wanathamini fedha na vitu vya anasa na starehe. Hawa ndo mngewafikiria kama waabudio masanamu!
 
Kanisa la Mungu ni lipi? Kwa hbr ya upotofu, wakati katoliki imepotoka kwa asilimia 95%, Kakobe amepotoka kwa 50% ana nafuu japo wote ni wakosefu.
MUNGU ni nani?
Mtu ni nani?
Dini ni nini?
Kanisa ni nini?
Ukatoliki ni nini?
Kupotoka ni nini?
Nani anajua fulani kapotoka fulani yupo sawa?
Naomba majibu
 
Dhehebu ni nyie mliotoka kwenye uasi wa Luther 1517. Kanisa lilikuwa ni moja tu aliloacha Yesu chini ya Petro.
 
Dah! kubabake hii ilikuwa ID yangu ya kwanza kabisa JF badae nikaitelekeza 😀😀😀.
 
Mkuu hakika umeshuka kisawasawa!
 
Hakuna mkatoliki aliyesomea biblia, wamesoma canon law tu, wanatumikia taifa la rumi chini ya taasisi yao ya Vatican
Unaongea utadhani unajua lolote. Cannon law msingi wake ni bibilia. Alafu sisi kila kitu katika ibada msingi wake ni bibilia. Alafu we kiazi kasome historia ya bibilia, hujui kitu unaharisha tu. Jipe muda wa kutafiti sio kuropoka tu kwa akili za kuambiwa
 
Usichokiamini Kinakuchefua vipi.
 
Unawashwa, hakuna dhehebu linaitwa roma kwanza, unatuchefua wewe usie na akili wala lolote ulijualo, sanamu ni zetu, hazikuhusu, na hatuzitoi kamwe. Chukia upasuke au ufe kabisa.
 
Hata wanaoabudu ng'ombe Mungu ameruhusu wawepo?
 

Huo mkutano wa wasabato ulifanyika wapi?
Kanisani au nje ya kanisa?
Maswali uliyoulizwa na kuyajibu ni yapi ndugu
 
Yaani kama unachukia Sanamu ya Yesu alafu unampenda Yesu wewe ni kilaza!
Bora anayetumia Sanamu ya Yesu na akawa na upendo kuliko aliyejichongea masanamu ya kiburi, dharau, chuki, fitina na yakamfanya aabudu fedha, magari, majengo, masengenyo, dharau, umimi na kujikwaza!
Someni Biblia zenu vizuri msiruke ruke kama bisi!
 
Mimi ni mkatoliki nisiyeunga mkono uwepo wa masanamu kanisani... Na ijumaa kuu huwa sijiangaishi kubusu msalaba. Sisali rozari kwakuwa naamini bikira Maria hawezi kusikia sala zangu...

Ntabakia mkatoliki kwa msimamo wangu.
Kukusaidia soma vizuri historia. Ingia pia kwenye hii link usome zaidi:
Watu mnataka mambo ya kiroho myafahamu kwa macho ya kimwili! Si rahisi hivyo! Go read your Bible!

 
Go read the scriptures.
Ile kuchukia tu na kwadharau wengine ni ibada tosha ya masanamu! Mnajichongea masanamu na mnayaabudu bila kujijua!

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…