Ukweli mchungu: Asilimia kubwa ya Wakristu na Waislamu duniani wanafanya ibada ya sanamu bila kujua kama wanafanya ibada ya sanamu

Tuache sisi tuamini kwa yule tunayemuomba uzima na afya ww endelea kuamini unavyoamini usilazimishe watu kitu kiovu.
 
Reactions: 511
Kama Mungu wako unayemuabuda na kumuomba kila siku anakujibu, tambua huyo ndo MUNGU wa kweli, vinginevyo umepigwa na kitu kizito.

Hapa sijataja dini wala dhehebu, bali nimesema kama unachoabudu hakina majibu kimbia, unaabudu sanamu.
Hakuna Mungu wa aina yeyote ile anayejibu maombi.

Mungu hayupo.
 
Naunga mkono hoja na iwe hivyo kwa jina la Yesu
Kilicho mfanya tb joshua kua tajiri sana namaarufu,mkubwa,akiaminiwa kuponya nakuokoa maisha yawatu ndio kitu sahihi kinacho elezwa mdahuu duniani..siri iliovuja ndio kitu pekee kilicho mfikisha kwenye mafanikio makubwa.
Lakini ona sasa alikua anataja jina la yesu kutoa pepo[emoji848][emoji848] nakuponya wagonjwa..
Amini nguvu kuu yauponyaji ilikua nyuma yake..
Nasasa hatuamini bado..au niuongo wana msingizia[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mtaongea yoote ila ukweli ni kwamba hakuna mungu wala miungu hakuna shetan wala mashetwani ni fix tu kama unashindwa kujipambania kulingana na wakati utegemee hao viumbe utasota saaaana mpaka utapaukaaa mungu ni wewe na shetani ni wewe roho zote mbili unazo mwenyewe ni kuchagua tu uitumie ipi kwa wakati upi
 
NDUGU WW NI SHETANI AU AGENT WAKE AU UNATUMIKA BILA KUJIJUA.OMBA TOBA HARAKA
Shetani mwenyewe hayupo iweje uwe nakazi kwa boss asie kuwepo
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
LIKUD Wewe ndie huna hoja. Ungekuwa na hoja unge mdefend mungu wako na Accumen Mo am defend mungu wake kihoja. Unachofanya hapa ni kumshambulia mungu wake bila kuonyesha uwezo wa huyo mungu wako.
Sawa mkuu upo sahihi kabisa
 
Mimi kama mkristo na Mtumishi wa Mungu nimepata conscious zaidi kwa Uzi huu.
Uko right kwa 100% na uko wrong kwa 100%.
Yaani namaanisha umeandika yasiyo ya ukweli lakini waumini wengi wanaishi kwa namna hii uliyoandika.
Mtu akizini anapata guilt kuwa Mungu amemuona na ana hasira juu yake lakini akiomba apate gari mwishowe anaanza kujiona hana akili , anawaza hilo gari litatoka wapi huku mshahara wake ni laki 4 kwa mwezi.
Wakristo tubadili mtazamo
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
inaonesha hata alicho kilenga mtoa mada wewe hukijui broo.
Kitendo chamfano ule wa ibrahimu ndio mstari wenyewe.
Ficha ujuha dogo.
Unajua maana ya mstari? Unakurupuka tu, mbona yeye aliuleta au yeye ni juha hakuwa anajua wewe ndie mwerevu.
 
Samahani Kidogo Accumen..
Mimi sio Atheist!
ILa nina maswali ya ufahamu..

Ila ningependa kujua Unaamini kabisa Madalyn Murray O'Hair aliyezaliwa miaka ya 1919 kama sikosei ndo mwanzilishi wa Atheists...?

Kama ndyo!
Rumii miaka ya 325-1800 walikuwa wakiwaua Atheist walikuwa wakiua kitu ambacho hakijaanzishwa bado?

Na hata Mtume miaka ya 600s alikuwa akipambana na Makafiri wa kibedui (Atheist) wanaopinga uwepo wa ALLAH..
Alipingana na kitu ambacho hakikuwepo..?

Musa,Yesu, na Mitume wengine wengi walikuwa wakipambana na watu wasioamini Mungu "Atheist" ili kuwafanya waamini Mungu
Kwahyo walikuwa wanawabadili watu gani ili waamini Mungu?..

Natangulisha Shukrani kwako kwa mjadala mzuri..
 
Mwenzako hapo kasema mungu wake ni pesa (mleta mada) ina maana kapuyanga?
Hapana hajapuyanga, Yupo sahihi.

Yani mtu yeyote yuko huru kuabudu chochote hata jiwe kama Mungu wake.

Lakini mtu huyo akianza kudai kwamba imani kwa Mungu wake huyo ndio ina ukweli thabiti kuliko Mungu wa wengine lazima athibitishe hilo.

Maana "Mungu" ni title tu ya kufikirika kutegemea na imani ya mhusika kuhusu nguvu fulani.
 
Huyu Accumen Mo ni mzee wakukurupuka bila facts za uhakika.

Huyu ni sawa na brother K wa kipindi cha futuhi.
 
Hoja nyepesi sana. Sana. Kama unyoya. Mzazi kuna kipindi unaweza omba kitu asikupe sababu anajua si wakati wakw sahihi au anataka ujifunze kitu kwanza. Allah akurambe uso.
 
Reactions: 511
Hajapunga, yuko sahihi. Je utakubali kuwa wewe ndie hauko sahihi kwa kusema mungu hayupu?

Mtu yoyote yuko huru kuabudu chochote hata jiwe. je utakubaliana na mimi kwamba chochote kinchoabudiwa ni mungu kwa huyo anaekiabudu? Kama ndio, Why unasema hakuna mungu.

Mimi nikikwambia haya ninayoyajibu hapa naambiwa na mungu ninaemwabudu (hautaamini), wewe ukitaka nithibitishe. Je utathibitishiwaje kwa kitu unachodai hakipo?

mfano nikisema 13*7=28, utakataa kwa sababu tayari unajua 13*7=91.
kwa kua tayari unajua ( una uhakika kuwa nimekosea) utaniambia nithibitishe. Lakini kama hujui jibu lake na ukataka nithibitishe, na mimi nikathibitisha kuwa ni 28 (japo sio kweli) utabisha au utakubliana na mimi kwamba ni kweli jibu ni 28? (Maana wewe hujui jibu lake)
 
Allah (s.w) ni mjuzi wa kila jambo lililotokea na litakalotokea, hivyo anajua wanaadamu watakaojifanyia wema na kwenda peponi na watakaojifanyia uovu na kwenda motoni.
Rejea Qur'an (11:6), (6:59), (65:12), n.k.
 
suala la kuongoka au kupotea ni la mtu mwenyewe kujichagulia kwani Allah (s.w) amebainisha njia zote, ya uongofu na ya upotofu kisha Allah (s.w) humupeleka huko alikochagua mtu mwenyewe.
Rejea Qur'an (91:7-8), (47:17), (76:1-3), n.k
 
Allah (s.w) ni mjuzi wa kila jambo lililotokea na litakalotokea, hivyo anajua wanaadamu watakaojifanyia wema na kwenda peponi na watakaojifanyia uovu na kwenda motoni.
Rejea Qur'an (11:6), (6:59), (65:12), n.k.
Sasa kama anajua atakayeenda peponi na motoni ya Nini kutuchosha Duniani na kututesa si angetuweka tu huko Tangu tunazaliwa?
 
Yaani hili swala ningekuwa Mtu wa Dini lilukuwa Lineisha Mapema sana, sema watu wa Dini Siku hizi wamejengwa kwenye Misingi mibovu kutukana kutokujenga hoja,kutokuwa wasthimilivu..

Ila jibu la hii hoja kama ni Mtu wa Dini Ni Yakobo 4:3-8

Yakobo 4:3-8

...."Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.

Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.

Au mwadhani ya kwamba maandiko yasema bure? Huyo Roho akaaye ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu?

Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.

Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.".....


Tchaooo Usiku mwema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…