Ukweli mchungu: Asilimia kubwa ya Wakristu na Waislamu duniani wanafanya ibada ya sanamu bila kujua kama wanafanya ibada ya sanamu

Ukweli mchungu: Asilimia kubwa ya Wakristu na Waislamu duniani wanafanya ibada ya sanamu bila kujua kama wanafanya ibada ya sanamu

Tuache sisi tuamini kwa yule tunayemuomba uzima na afya ww endelea kuamini unavyoamini usilazimishe watu kitu kiovu.
 
  • Thanks
Reactions: 511
Kama Mungu wako unayemuabuda na kumuomba kila siku anakujibu, tambua huyo ndo MUNGU wa kweli, vinginevyo umepigwa na kitu kizito.

Hapa sijataja dini wala dhehebu, bali nimesema kama unachoabudu hakina majibu kimbia, unaabudu sanamu.
Hakuna Mungu wa aina yeyote ile anayejibu maombi.

Mungu hayupo.
 
Naunga mkono hoja na iwe hivyo kwa jina la Yesu
Kilicho mfanya tb joshua kua tajiri sana namaarufu,mkubwa,akiaminiwa kuponya nakuokoa maisha yawatu ndio kitu sahihi kinacho elezwa mdahuu duniani..siri iliovuja ndio kitu pekee kilicho mfikisha kwenye mafanikio makubwa.
Lakini ona sasa alikua anataja jina la yesu kutoa pepo[emoji848][emoji848] nakuponya wagonjwa..
Amini nguvu kuu yauponyaji ilikua nyuma yake..
Nasasa hatuamini bado..au niuongo wana msingizia[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mtaongea yoote ila ukweli ni kwamba hakuna mungu wala miungu hakuna shetan wala mashetwani ni fix tu kama unashindwa kujipambania kulingana na wakati utegemee hao viumbe utasota saaaana mpaka utapaukaaa mungu ni wewe na shetani ni wewe roho zote mbili unazo mwenyewe ni kuchagua tu uitumie ipi kwa wakati upi
 
NDUGU WW NI SHETANI AU AGENT WAKE AU UNATUMIKA BILA KUJIJUA.OMBA TOBA HARAKA
Shetani mwenyewe hayupo iweje uwe nakazi kwa boss asie kuwepo
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mimi kama mkristo na Mtumishi wa Mungu nimepata conscious zaidi kwa Uzi huu.
Uko right kwa 100% na uko wrong kwa 100%.
Yaani namaanisha umeandika yasiyo ya ukweli lakini waumini wengi wanaishi kwa namna hii uliyoandika.
Mtu akizini anapata guilt kuwa Mungu amemuona na ana hasira juu yake lakini akiomba apate gari mwishowe anaanza kujiona hana akili , anawaza hilo gari litatoka wapi huku mshahara wake ni laki 4 kwa mwezi.
Wakristo tubadili mtazamo
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
inaonesha hata alicho kilenga mtoa mada wewe hukijui broo.
Kitendo chamfano ule wa ibrahimu ndio mstari wenyewe.
Ficha ujuha dogo.
Unajua maana ya mstari? Unakurupuka tu, mbona yeye aliuleta au yeye ni juha hakuwa anajua wewe ndie mwerevu.
 
Duniani kawaida nyie wapumbavu mko wachache sana ,huo ujinga wenu hauingii akili mpaka unakufa hakuna mtu anaweza kukubali huo ujinga wako😅😅
.Pointless huwezi kushawishi mtu

Huyu ndio mwanzilishi wa ujinga huo👇👇ndie mnayemuabudu
View attachment 2933163
Samahani Kidogo Accumen..
Mimi sio Atheist!
ILa nina maswali ya ufahamu..

Ila ningependa kujua Unaamini kabisa Madalyn Murray O'Hair aliyezaliwa miaka ya 1919 kama sikosei ndo mwanzilishi wa Atheists...?

Kama ndyo!
Rumii miaka ya 325-1800 walikuwa wakiwaua Atheist walikuwa wakiua kitu ambacho hakijaanzishwa bado?

Na hata Mtume miaka ya 600s alikuwa akipambana na Makafiri wa kibedui (Atheist) wanaopinga uwepo wa ALLAH..
Alipingana na kitu ambacho hakikuwepo..?

Musa,Yesu, na Mitume wengine wengi walikuwa wakipambana na watu wasioamini Mungu "Atheist" ili kuwafanya waamini Mungu
Kwahyo walikuwa wanawabadili watu gani ili waamini Mungu?..

Natangulisha Shukrani kwako kwa mjadala mzuri..
 
Mwenzako hapo kasema mungu wake ni pesa (mleta mada) ina maana kapuyanga?
Hapana hajapuyanga, Yupo sahihi.

Yani mtu yeyote yuko huru kuabudu chochote hata jiwe kama Mungu wake.

Lakini mtu huyo akianza kudai kwamba imani kwa Mungu wake huyo ndio ina ukweli thabiti kuliko Mungu wa wengine lazima athibitishe hilo.

Maana "Mungu" ni title tu ya kufikirika kutegemea na imani ya mhusika kuhusu nguvu fulani.
 
Samahani Kidogo Accumen..
Mimi sio Atheist!
ILa nina maswali ya ufahamu..

Ila ningependa kujua Unaamini kabisa Madalyn Murray O'Hair aliyezaliwa miaka ya 1919 kama sikosei ndo mwanzilishi wa Atheists...?

Kama ndyo!
Rumii miaka ya 325-1800 walikuwa wakiwaua Atheist walikuwa wakiua kitu ambacho hakijaanzishwa bado?

Na hata Mtume miaka ya 600s alikuwa akipambana na Makafiri wa kibedui (Atheist) wanaopinga uwepo wa ALLAH..
Alipingana na kitu ambacho hakikuwepo..?

Natangulisha Shukrani kwako kwa mjadala mzuri..
Huyu Accumen Mo ni mzee wakukurupuka bila facts za uhakika.

Huyu ni sawa na brother K wa kipindi cha futuhi.
 
Hata wewe msabato unae waponda wakatoliki, kwa mantiki ya uzi huu, wewe pia unafanya ibada ya sanamu.

Kwani ibada ya sanamu nini?

Umewahi kusikia mashabiki wa mpira wanasema " kwenye timu hii golini kuna sanamu?" Je unadhani maana yake huwaga ni nini?

Maana yake ni kwamba kwenye timu hiyo golini kuna kipa ambae hatimizi majukumu yake kama kipa. Kipa kazi yake ni kuokoa mipira yote inayo elekezwa golini kwake. Ila kama kipa huyu hadaki magoli yanafungwa tu haokoi wala nini basi watu watasema golini kuna sanamu.

Ni sawa na wanapo sema "Huyu jamaa ni baba au sanamu la baba?" Wana maanisha ni baba ambae hatimizi majukumu yake.

Vivyo hivyo kwa habari ya ibada ya sanamu.

Ibada ya sanamu ni nini sasa?

Ibada ya sanamu ni ibada yoyote ile ambayo Mungu/muungu anae ombwa hatoi majibu.

Ibrahimu alivyo yaharibu masanamu ya mababu zake alifanya hivyo sio kwa sababu yale walikuwa ni masanamu la hasha ila alifanya hivyo kwa sababu masanamu yale yalikuwa hayatoi majibu ya maombi ndio maana akaenda kuyacharaza mapanga kwa Hasira.

Kama masanamu yale ya miungu ya mababu zake yangekuwa yanatoa majibu basi Ibrahim asinge thubutu hata kunyoosha mkono wake kuyakata. Yani asinge thubutu hata kujifanya kama anajikuna.

Wakristu na waislamu na ibada ya sanamu.

Ukweli ni kwamba Asilimia kubwa ya wakristu na waislamu wengi duniani hufanya ibada za sanamu. Kwa sababu hufanya ibada zisizo na majibu. Sanamu lina masikio lakini halijibu na lina macho lakini halioni. Vivyo hivyo Mungu (wa Wakristu na Waislamu) anasikia maombi yote wanayo muomba watu wake lakini huwaga hajibu na ana ona mambo yote mabaya wanayo tendewa watu wake lakini haintervene. Anayaacha yaendelee kutokea hivyo hivyo licha ya yeye kuwa na uwezo wa kuyazuia yasitokee.

Ndio maana kwa wakristu na waislamu mtu akifanya maombi halafu yakajibiwa majibu hayo huitwa muujiza. Muujiza ni jambo ambalo sio la kawaida. Yesu alipo tembea juu ya maji uliitwa muujiza kwa sababu sio kawaida kwa mtu kutembea juu ya maji.

So maombi yanayo jibiwa na Mungu wa wakristu na waislamu huwaga yanaitwa muujiza kwa sababu sio kawaida Mungu kujibu maombi..

Hata wakristu na waislamu ndani ya nafsi zao huwaga wanajua kabisa kwamba Mungu huwaga hajibu maombi yao. Ndio maana wengi wao huenda kwa waganga kutafuta majibu ya maombi yao.

Wakristu na Waislamu wana amini Mungu anayaona zaidi madhambi yao kuliko maombi yao. Ndio maana mkristu au muislamu akitenda dhambi anakuwa na uhakika kabisa Mungu kamuona na anakuwa na ile kitu inaitwa Guilty conscious kwa sababu anajua Mungu kamuona . Lakini akifanya maombi yake anakuwa hana imani kama Mungu kayasikia na kwamba atamjibu.

Ndio maana hata kwenye Uzi wangu huu wakristu na waislamu watakuja ku comment hapa kwamba Mungu ataniadhibu kwa kuwa ninakufuru ila ningeandika Uzi nikisema nataka nifunge nimuombe Mungu awafanye watu wote duniani waache dhambi basi wakristu na waislamu hao watakuja kunidhihaki hapa kwa sababu wanajua Mungu hatonijibu kwa maana wanajua Mungu huwa hajibu maombi ya watu.

Bahati nzuri vitabu vya dini zote mbili vimeshaweka wazi kabisa kwamba Mungu huwa hajibu maombi ya watu..

Tufanye nini sasa ee rabbi? Vunja masanamu (Vunja connection na Mungu asie jibu maombi yako na anza sasa kumtafuta Mungu mwenye kujibu maombi yako. Acha ibada ya sanamu sasa)
Hoja nyepesi sana. Sana. Kama unyoya. Mzazi kuna kipindi unaweza omba kitu asikupe sababu anajua si wakati wakw sahihi au anataka ujifunze kitu kwanza. Allah akurambe uso.
 
  • Kicheko
Reactions: 511
Hapana hajapuyanga, Yupo sahihi.

Yani mtu yeyote yuko huru kuabudu chochote hata jiwe kama Mungu wake.

Lakini mtu huyo akianza kudai kwamba imani kwa Mungu wake huyo ndio ina ukweli thabiti kuliko Mungu wa wengine lazima athibitishe hilo.

Maana "Mungu" ni title tu ya kufikirika kutegemea na imani ya mhusika kuhusu nguvu fulani.
Hajapunga, yuko sahihi. Je utakubali kuwa wewe ndie hauko sahihi kwa kusema mungu hayupu?

Mtu yoyote yuko huru kuabudu chochote hata jiwe. je utakubaliana na mimi kwamba chochote kinchoabudiwa ni mungu kwa huyo anaekiabudu? Kama ndio, Why unasema hakuna mungu.

Mimi nikikwambia haya ninayoyajibu hapa naambiwa na mungu ninaemwabudu (hautaamini), wewe ukitaka nithibitishe. Je utathibitishiwaje kwa kitu unachodai hakipo?

mfano nikisema 13*7=28, utakataa kwa sababu tayari unajua 13*7=91.
kwa kua tayari unajua ( una uhakika kuwa nimekosea) utaniambia nithibitishe. Lakini kama hujui jibu lake na ukataka nithibitishe, na mimi nikathibitisha kuwa ni 28 (japo sio kweli) utabisha au utakubliana na mimi kwamba ni kweli jibu ni 28? (Maana wewe hujui jibu lake)
 
Allah (s.w) ni mjuzi wa kila jambo lililotokea na litakalotokea, hivyo anajua wanaadamu watakaojifanyia wema na kwenda peponi na watakaojifanyia uovu na kwenda motoni.
Rejea Qur'an (11:6), (6:59), (65:12), n.k.
 
suala la kuongoka au kupotea ni la mtu mwenyewe kujichagulia kwani Allah (s.w) amebainisha njia zote, ya uongofu na ya upotofu kisha Allah (s.w) humupeleka huko alikochagua mtu mwenyewe.
Rejea Qur'an (91:7-8), (47:17), (76:1-3), n.k
 
Allah (s.w) ni mjuzi wa kila jambo lililotokea na litakalotokea, hivyo anajua wanaadamu watakaojifanyia wema na kwenda peponi na watakaojifanyia uovu na kwenda motoni.
Rejea Qur'an (11:6), (6:59), (65:12), n.k.
Sasa kama anajua atakayeenda peponi na motoni ya Nini kutuchosha Duniani na kututesa si angetuweka tu huko Tangu tunazaliwa?
 
Yaani hili swala ningekuwa Mtu wa Dini lilukuwa Lineisha Mapema sana, sema watu wa Dini Siku hizi wamejengwa kwenye Misingi mibovu kutukana kutokujenga hoja,kutokuwa wasthimilivu..

Ila jibu la hii hoja kama ni Mtu wa Dini Ni Yakobo 4:3-8

Yakobo 4:3-8

...."Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.

Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.

Au mwadhani ya kwamba maandiko yasema bure? Huyo Roho akaaye ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu?

Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.

Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.".....


Tchaooo Usiku mwema
 
Back
Top Bottom