Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Nimepanda treni ya Kigoma - Dar mwaka 2021, na nilijisemea sitakuja kupanda tena kwa namna treni hii ilivyo na huduma mbovu na za aibu.
Ninatumia usafiri wa ndege Air Tanzania mara kwa mara kwa safari zangu za ndani ya Tanzania. Kuna kipindi hata namba zao za huduma kwa mteja hazipatikani, umekata ticket ya Dar ila unapiga no ya simu ya ofisi ya Dar haipatikani inabidi upige namba ya Arusha au Mwanza wakati wewe ofisi inayopaswa kukuhudumia ni ya Dar.
Nimetumia usafiri wa Tazara mara kadhaa miaka ya nyuma, kote huko huduma ni mbovu kiufupi zipo hoehahe.
Nimekuwa mtumiaji wa mabasi ya mwendokasi tangu yalipoanza na kusema kweli wakati tunakata ticket kielectronic kipindi cha Max Malipo wengi tuliojaaliwa kufika America na Ulaya tulianza kuufananisha mfumo huu wa usafiri na mfumo uliyopo maeneo ya Ulaya na Marekani. Ila alipoingia Jiwe muharibifu aliwaondoa Max Malipo na mwisho kukawa hakuna tofauti kati ya daladala na mabasi ya mwendokasi. Huo ukawa mwisho wangu kupanda magari ya mwendokasi.
Sasa tunaenda kwenye SGR. Walewale TRC wanaoendesha usafiri wa kwenda mwanza na kigoma ndo wanaenda kuendesha SGR. Itachakaa vibaya sana kwa huduma mbovu kabla hata ya miaka 5.
Ifike kipindi tuseme ukweli, serikali zetu Afrika hasa Tanzania haziwezi kufanya biashara. Masuala ya biashara wawaachie tu sekta binafsi ambao wao kutokana na kuwa na akili ya kupata faida kulingana na ubora wa huduma wataweza kuendesha hizi sekta zetu kwa faida na pia kwa kuzingatia ubora wa huduma.
Sekta za huduma za biashara serikali iachane nazo tu, hatuziwezi. Serikali hawajali ubora wa huduma, hawajali maintenance and repair, wao wanajali tu kuingiza pesa na watu kupata mishahara na kupiga.