PART TWO...................
Nitajitaidi angalau kwa leo ni post Sehemu hii ya pili tu kwani kwa sasa niko na majukumu ya ofisi mengi!
Tuendelee!!!
.
.
Huu ndio ulikuwa Mwanzo wa ukaribu wangu na Malaika huyu wa duniani. Kwa Semester ile tulimalizia discussion na maandalizi ya UE kwa pamoja, alinisaidia sana pamoja na classmate wenzangu ku cover pale nilipo miss. Nashukuru Mungu Sikupata Supp, japo ufaulu wangu ulikuwa wa kawaida sana.
Nikiwa Likizo baada ya semester ya kwanza, katika moja na mbili na mama, alinipa simulizi moja ambayo sikuwa naifahamu kumuhusu baba. Mama alisema, wakati tukiwa wadogo, kuna Mnyarwanda mmoja alikuja kama mkimbizi, alimkaribisha pale nyumbani kwa mikono miwili kama mdogo wake, mama aliendelea kusema binti yule alipata ujauzito na baadae mtoto wa kike ambaye baba yake hakuwa anafahamika. Mama alisema baada ya miaka mitatu alikuja kugundua baba wa mtoto yule wa kike alikuwa ni baba yetu mzazi. Mama akasema alichukua hatua ya kumfukuza binti yule (Dada Nshime) bila kumhusisha baba. Mama aliongeza kwa kusema mpaka baba anafariki hakuwai kumsamehe wala kutuambia sisi watoto wake kuhusu jambo hili. "Johannes mna dada yenu huko duniani" alijisemea mama!
Semester ya Pili ilianza kwa mixed feelings. Kwanza nilikuwa sijui namna ya kubehave nikiwa na Herrieth, mara zote tukiwa kwenye discussions, nilijitaidi kuwa perfectionist na problem solver, niliamini hii ndio njia pekee ya kuendelea kuwa karibu yake. Pili bado nilikuwa nina kipengele cha mkopo na pesa ya kujikimu kimaisha.
Herrieth alinifanya niiipende shule, nililazimika kusoma sana ili niwe brighter kuliko yeye, assignment nyingi nilikuwa nafanya mimi ili nimfurahishe, na namshukuru Mungu njia zangu zilikuwa zina fanya kazi na kutoa matokeo.
Baada ya Tests za kwanza, matokeo yetu kwa pamoja yalikuwa mazuri sana, Herrieth alifurahi kweli na sifa zote kuhusu ufaulu wake nilipewa mimi. Taratibu nilianza kuona udhaifu wa Herrieth na nguvu (strength) zangu ni zipi. Niliona mimi najiweza sana Darasani na nina uwezo mkubwa wa kufundisha, discussions za usiku ziliongezeka na mara kadhaa, tulifanyia discussion Hall 3, alipokuwa anakaa Herrieth na wenzake.
Siku moja Jumapili, mida ya mchana, Herieth alinipigia simu akiomba aje kunitembelea Ghetoni kwangu Msewe. Hakuna siku moyo wangu ulivuja damu kama siku hii. Kwanza sikuwepo msewe, nilikuwa nimeenda TAIFA na wadau kuangalia mechi ya Simba, pili Gheto langu lilikuwa ni baya sana, nilikuwa nina godoro moja tu la 3*6 tena la inch 4, wenyewe wana liita godoro la kunyoosha mbavu, sina mziki ghetoni, wala chochote chenye thamani. Mashuka yalikuwa ni machafu halafu ndani hamna feni, niliogopa Herrieth angekuja kwenye hali hiyo , ndoto yoyote niliyokuwa nayo juu yake ingeyeyuka.
Nilimsihi Herrieth tufanye wakati mwingine, alinijibu kwamba yuko Msewe kwa rafiki yake wa kike, hivyo ingekuwa ni rahisi kwake kwa siku hiyo. Kwa haraka sana Nilitafakari cha kufanya, nilimuomba anipe lisaa limoja nirudi ghetoni (nilimdanganya niko jirani), wakati niko njiani narudi nilijaribu kuazima godoro kwa wadau (majirani zangu) bila mafanikio, hivyo nikasema moyoni liwalo na liwe.
Saa kumi alasiri nilifika ghetoni, kwa haraka sana nikajaribu kufanya usafi kwa kadri nilivyoweza, kuna Mdau(jirani) mmoja wa CONAS alikuwa anaenda chuo, nikajaribu kumuomba mashuka, mwamba akakubali kwa ahadi ya kufuliwa kabla ya kuyarudisha. Ile tu nimemaliza kutandika mashuka, kudeki chumba na kuondoa nguo zote chafu nje, Herrieth akanipigia simu kwamba hatoweza kuja tena amepata dharula na amelazimika kurudi chuo. Kwa kweli nilipata mixed feelings, kwanza nilighazabika kwa kuwa nimetoka taifa na kuacha mechi muhimu halafu kilichonirudisha hakipo. Lakini pia nilifarijika baada ya kukwepa aibu kubwa ya mwaka.
Siku moja usiku, mida ya saa tano baada ya evening Prep, mwamba niliamua kuwasindikiza wakina Herrieth mpaka Hall 3, tuliongea mambo mengi ikiwa ni pamoja na historia ya maisha yetu, Herrieth alitueleza kwamba yeye alizaliwa 1995, hivyo mimi nilikuwa mkubwa kwake kwa miaka mitatu, pia alisema hajawahi kumfahamu Baba yake tangu amezaliwa, na mama yake amekuwa akimwambia Baba yake alifariki wakati wa vita nchin Rwanda.
Baada ya kuwafikisha Hall 3, Herieth na rafiki zake waliniaga na kuondoka, lakini Herrieth alisita, akarudi nyuma na aliniambia "Johannes wait a minute let me put my bag, I have something for you," Nilikaa pale nje kama kwa dakika 20 hivi namsubiri, then nikaona ameshuka na rasket ndogo kaweka mgongoni, nikajiuliza leo sijui napewa nini? " Lets go Johannes, today i want to sleep at your place" Moyo wangu ulilia Paa!!!! Yani sikujua cha kujibu, nilibaki namwangalia tu kwa wasiwasi mkubwa sana. Ndugu msomaji, napenda uamini kwamba huyu binti alikuwa ni mzuri sana, mrefu, natural hair tena ndefu, alikuwa ana shingo ndefu na ngozi yake ilikuwa very soft mpaka unaogopa kuiangalia.
Nikasema moyoni, hivi haya yanayotokea ni ndoto au ni ukweli, maana huu ni usiku. "Johannes, is everything okay? I’m sorry if I crossed any boundaries" nilipayuka "no no no Herrieth, I'm truly amazed—I never expected such an angel to place her trust in someone as poor as me" nilimjibu kwa unyonge sana Herrieth huku nikikumbuka hali ya chumba changu kilivyo kichafu, hakuna feni, mashuka nilirudisha kwa mdau wa CONAS, vumbi la chumbani, yote kwa yote nikasema Liwalo na liwe.
Tulielekea mpaka kituo cha Kontena kusubiria bodaboda, kwani kwa usiku ule tusingeweza kutembea. Baada ya muda boda alifika tukaelewana bei (elfu 3) mpaka Msewe, tulipanda Mshikaki, Boda mbele, Herrieth Katikati mimi kwa nyuma nimembambia Herrieth kwa mara kwanza kwenye bodabdoa
Nilifungua chumba changu kwa unyonge mkubwa sana, taa ikawashwa, uso wa aibu ulikuwa umenivaa kwani gheto lile lilikuwa ni baya mno. Halikuwa hadhi ya Herieth, magheto kama yale yaliwafaa mafukara sambuli yetu. Herieth alimwagika machozi kwa uchungu, nami sikuweza kumzuia, nilimuacha alie kwani nilijua kilichomliza. Hali yangu ya maisha ilikuwa ni mbaya sana, na hayo yote yalionekana kwenye reflection ya chumba changu.
"Johannes, you have the most beautiful soul I've ever encountered—so humble, loving, caring, and always smiling. It’s hard to believe that someone like you is living this kind of life?" Yalikuwa ni maneno ya uchungu kutoka kwa mrembo Herieth, huku akizidi kuangua kilio kanakwamba kafiwa na mzazi. Baada ya muda alinyamaza nami nikapata ujasiri wa kumueleza Herieth ukweli.
Nimwambia Herieth, historia ya maisha yangu, nilimueleza kuhusu hali ngumu ya mama yangu na ndugu zangu, nilimwambia chochote unachonipa huwa namtumia mdogo wangu wa kike anayesoma, niliweleza kwa kawaida nakula mara moja tu kwa siku, na siku nyingine navusha bila kula, nakumbuka simulizi ile kwa Herieth ilimuumiza sana, alijisikia mnyonge sana huku akinilaumu kwa nini sikumwambia siku zote hizo.
Sikuwa na maneno mazuri ya kumueleza Herieth, tayari alikuwa amesha choka sana, alikuwa mnyonge. Taratibu nilimuweka kwenye kigodoro changu kidogo na kumlaza, nilisita kufanya chochote kwake kwani alikuwa yuko na hali ya huzuni sana. Baada ya kimya kirefu kama nusu saa hivi, Herieth alianza kutoa nguo zake, akabaki na nguo za ndani tu! Bila kuongea chochote, huku natetemeka, nilitoa trouser yangu ya kitambaa na T-Shirt nilibaki na boxer tu! "What do you think you`re doing?" Nilishtushwa na swali, tena kwa ukali kutoka kwa Herieth, "Its hell in here, thats why i had to remove my clothes," aliendelea kuhamaki na kujitetea. Mwamba nikaona huu ni ujinga, yani tunda limenguka lenyewe nishindwe kulila? Nilimwambia " Herieth, you are the most beautiful person I have ever encountered in this lifetime" huku nikimsogelea kwenye godoro "Your eyes are calling out to me, and your waist is longing for my touch" huku nikitasamu niliendelea kushusha verse na kumtuliza mtoto "Herieth, from the moment I first laid eyes on you, my life transformed completely. You redefined beauty in a woman for me, and being with you feels like everything is at its highest stakes"
Usiku ule ulikuwa mrefu, mzuri sana kwetu sote, mrembo Herieth alinipa penzi ambalo sikuwahi kupata, mixer pigo za kinyarwanda na kihaya. Herieth uzuri wake nili-udhihirisha hadi kwenye tendo la ndoa, hakuwa mvivu pamoja na ubovu wa chumba, udogo wa godoro, au joto la mule ndani. Mtoto aligugumia tendo mwanzo mwisho, Penzi lile lilikuwa ni tamu zaidi ya asali, sikuwa kwenye maisha yangu kuwa na ndoto za kulala na mwanamke wa levels zile, kwangu ulikuwa ni muujiza, ilikuwa ni ndoto iliyotimia.
Penzi letu lilizidi kumea, karibu kila mtu darasani kwetu alifahamu kuhusu sisi, tuliongozana kila sehemu pamoja na Mungu akatusaidia tukamaliza salama Mwaka wa Pili wa Shule ya Uhandisi pale Chuo kikuu cha DSM.
2017 tukiwa tunaingia mwa wa nne, mwaka wa mwisho wa Shule yetu ya Uhandisi, Mimi na Harieth tulikuwa tumepanga Chumba na Sebule, Changanyikeni. Maisha kipindi hiki yalianza kuwa mazuri kwani Mwaka wa TATU nilirudishiwa Mkopo wangu. Herieth nilimpenda sana, sidhani kama kuna mwanaume hata mmoja aliyewahi kumpenda mwanamke kiasi kile.
Nilimtambulisha Herieth kwa mama na ndugu zangu, huku nikimwambia mama kwamba huyo ndiye mke wangu mtarajiwa. Herieth alipata ujauzito Semester ya mwisho ya mwaka wa nne. Nilimwambia Herieth, ujauzito huo asiutoe, na mara baada ya chuo nitaongozana naye kwenda Rwanda kumtolea possa.
Siku moja Herieth akiwa na mazungumzo ya simu na mama yake, alimpa simu mama yake anisalimie, Mama Mkwe alikuwa anajua kihaya vizuri, tulisalimiana na kutaniana sana, baadae nilimuuliza mama Mkwe, Kihaya umejifunzia wapi?, akanijibu kwamba aliwahi kuishi mkoa wa Kagera miaka ya 90, nikamuuliza uliishi Kagera sehemu gani, akasema Muleba, Kijiji cha Bisheke. "Now she caught my attention". Baada ya hapo moyo wangu ulisita sana kuendelea kumuhoji maswali mengi kwani nilihisi namfahamu huyo Mama Herieth ambaye ni Mama Mkwe mtarajiwa.
Mimba ya Herieth ikiwa na miezi 6, niliendelea kumdodosa Mama Herieth hasa nikitaka kujua aliwahi kuishi "Bisheke" kwa nani? Siku moja nilimuuliza Herieth hivi jina la mama yako ni nani? "Nshimeimana" alinijibu mara moja. Niliendelea kusita.
Kesho yake nilimuomba Herieth kuongea na mama yake, siku hiyo Mama yake Herieth alinieleza kwamba aliwahi kuishi Muleba, Bisheke, nyumbani kwa familia ya Rwebangira na ndipo alipo mpata Mtoto wake Herieth! Nilichoka aiseee..............
Kwa lugha rahisi, Herieth alikuwa ni dada yangu wa damu.
Kwa leo naomba niishie hapa, Je! Ni nini kitaendelea kuhusu kisa hiki cha kweli kwenye amisha yangu? Ungana nami siku ya Kesho!