Ukweli mchungu: Kombe la Mapinduzi ni mashindano ya kutoa fursa kwa wachezaji wanaochipukia

Ukweli mchungu: Kombe la Mapinduzi ni mashindano ya kutoa fursa kwa wachezaji wanaochipukia

Jaribu kufatilia hata kipindi cha Nabi, wachezaji wanaocheza kwenye hili kombe ni watoto + wa majaribio + wasiopata namba. Ila nakumbuka kuna mechi ilikuwa dhidi ya Azam, Nabi akawapandisha kwenye boti wachezaji waliokuwa mapumziko wakila bata ili waje kuongeza nguvu ila hatimaye wakatolewa kwa penati. Gamondi kabakia na msimamo wake tokea awali hadi hatua ya robo kuwa kikosi chake ni kile kile. Mchezaji wa first eleven alikuwa ni Mzize na Lomalisa pekee na Lomalisa alitolewa.
Jana watu walitegemea kumuona Maxi, Pacome, Yao n.k Gamond akasema huu ni uhuni, siwezi kurisk kuweka hawa watu wakati nina kombe la ligi na nashiriki hatua ya makundi klabu bingwa.
 
Ukweli mtupu!
Ila kuna litimu wanachezesha wachezaji wana mvi kila eneo.
Kapombe, Ngoma, Kanoute, Phiri, Onana, Baleke na Saido wote hawa ni kikosi cha kwanza cha Simba.

Ni sawa na 70% ya kikosi cha kwanza, while Yanga wana 20% to 30% ya kikosi cha kwanza kushiriki michuano hii.
 
Hii haibadilishi ukweli kwamba yanga wametolewa,hizi ni hadithi tu za sizitaki mbichi zile.
 
😂😂😂😂😂

We kubali umetolewa
Kukimbilia ulikua unachezesha majaribio sjui haina uhalisia kwa kweli

Kama mliona haina maana hizi nyuzi za kujielezea hazikua na maana kwa kweli😂😂😂

Twafahamu imeuma kutolewa
Tangu mwanzo nilipendekeza wapelekwe vijana wa U20 Kwenye mapinduzi nashukuru uongozi wa yanga ulifuata maoni .
Okra anatakiwa akawapige chenga Al ahly na belouzidad na kuwafunga halafu unampandisha boti akacheze na watoza ushuru wa unguja au apr timu isiyoshiriki mashindano yoyoye ya kimataifa .
Binafsi nilitaka yanga afungwe.
Kucheza mapinduzi ni kupoteza muda .
 
Simba angemfunga yanga Hata 1-0 kelele zingekuwa nyingi kuliko 🖐🏿 wasingeangalia wachezaji 14 wa kikosi cha kwanza hawakuwepo .
Hata 1976 simba alimfunga yanga 6 baada ya yanga kufukuza timu yote ya first eleven ambayo ilienda kuunda pan African lakini 1968 yanga alimfunga simba wote wakiwa kamili Kama ilivyokuwa 2023.
 
Japo sijui kama hii ndio ilikuwa dhamira ya viongozi wa Yanga na kocha wa timu hiyo, ila ukweli ni kuwa kwa kocha makini na viongozi makini wa timu za ligu kuu, mashindano haya ni fursa ya kuona vipaji na uwezo wa wachezaji chipukizi pamoja na wale wa kikosi cha pili. Kutumia proffesinal players kwa mashindano kama haya huku una michezo ya kimataifa na ligi kuu, sio tu ni ku-risk, bali ni matumizi mabovu ya resources na kuwanyima fursa wachezaji chipukizi.

Huu ndio ukweli kwa wale wanaoona mbali na wenye malengo ya kuchukua vikombe vyenye kuheshimisha timu na hata nchi kwa ujumla. Hivyo, kama huu ndio ulikuwa mpango wa timu ya Yanga, basi wamefanya jambo sahihi na kwa hizi mechi walizocheza, kocha atakuwa teyari amejua ni mchezaji yupi wa kumpandisha na yupi bado.

The end justifies the means.

Habari ndio hio.le wa
THAT'S FACT...simba na yanga huwa siriaz na hili kombe pale wanapoona hawana posibility ya kushinda ligi au FA,so mwafulani hana jinsi lazma apambane ili ajiokotee hili kopo la mapinduzi ili mbumbumbu wapate kutulia
 
Ila APR wanacheza kwa kujiamini aisee tuache masihara.niliona Lomalisa akigandisha mpira mguuni kumbe vijama vinamchora tu[emoji23][emoji23]
 
Japo sijui kama hii ndio ilikuwa dhamira ya viongozi wa Yanga na kocha wa timu hiyo, ila ukweli ni kuwa kwa kocha makini na viongozi makini wa timu za ligu kuu, mashindano haya ni fursa ya kuona vipaji na uwezo wa wachezaji chipukizi pamoja na wale wa kikosi cha pili. Kutumia proffesinal players kwa mashindano kama haya huku una michezo ya kimataifa na ligi kuu, sio tu ni ku-risk, bali ni matumizi mabovu ya resources na kuwanyima fursa wachezaji chipukizi.

Huu ndio ukweli kwa wale wanaoona mbali na wenye malengo ya kuchukua vikombe vyenye kuheshimisha timu na hata nchi kwa ujumla. Hivyo, kama huu ndio ulikuwa mpango wa timu ya Yanga, basi wamefanya jambo sahihi na kwa hizi mechi walizocheza, kocha atakuwa teyari amejua ni mchezaji yupi wa kumpandisha na yupi bado.

The end justifies the means.

Habari ndio hio.
Bado hamjasema
 
Hii isitumike kama excuse, yaani ukipigwa ni umepigwa tuu
 
Back
Top Bottom