Ukweli mchungu kuhusu KINANA

Ukweli mchungu kuhusu KINANA

Au mimi sijaelewa!kwamba ametumikia Jeshi kwa miaka 20,amestaafu/kuacha Jeshi 1972..wakati sisi Uhuru tumepata 1961!Ina maana Kinana alikuwa Jeshini tangu enzi za King African Rifles (K.A.R)?....."Ukisikia 'Tuuuuuuu' jua Tembo kakoswa,Usiulize nani huyoo..We jua tu Kinana kapita"
 
Mleta uzi, umefulia...kinana ni jangili...anaua tembo wetu.arudishwe kwao somalia maana si raia wa Tanzania. Ewe mleta uzi povu jingiii kwa kumtetea jangili..shame on you....kikwete ataendelea kuchange makatibu kila mara, plus mawaziri wake wenye vyeti vya kughushi.ccm nI chama dhaifu.


Huo uaskari jeshi wake na hiyo strategic planning yake aliyosomea ndiyo anayoitumia kuangamiza tembo wetu huko mbugani!!
 
Ama kweli Kinana ni mtu makini,yaani kwa miaka yote hiyo akiwa mtendaji wa Chama na Serikali amekuwa akituulia Tembo wetu na kuvuna Maliasili yetu bila hata kutiliwa shaka.
 
Ama kweli Kinana ni mtu makini,yaani kwa miaka yote hiyo akiwa mtendaji wa Chama na Serikali amekuwa akituulia Tembo wetu na kuvuna Maliasili yetu bila hata kutiliwa shaka.

mti wenye matunda ndio urushiwao mawe
 
Ni wakati wa kuangalia mambo aliyofanya kinana before amekuwa ni mtu wa mikakati,makini ,mwenye huruma kwa watu na sasa kamudu kuwaunganisha watu wa chama chake na kurejesha umoja na mshikamno ambao uliyumba wakati wa mkama.
 
Aisee. Kutokana na uwezomhuo wa kinana, ndo maana chadema wanaweweseka na kutafuta kila mbinu chafu kumchafua

wanamchafuaje? kusema meli zake zimepeleka pembe za ndovu kwa kudanganya ni renewable plastics? Je si magari ya Jeshi yamekuwa yakitumika kusafirisha wanyama walio hai na mazao ya wanyama hao?

Unakumbuka lile gari la Jeshi lilikamatwa likisafirsha kule ARUSHA japokwa lilikamatwa baada ya kupinduka? Juu namba za jeshi na chni namba za kiraia? si ndo hujuma za hawa askari unaowaita majemedari?

sasa kusema wanahusika na ujangili ni mbinu za kuwachafua au ni kusema kweli?
 
Hii thread ni makala ya Absalomu Kibanda ambayo ilishaprove kinyume na maudhui yake. Kwa muda aliokaa Kinana na cheo hicho sijaona lolote la maana mpaka sasa alilofanya zaidi ya Mukama. Kama ni kuzomewa wote wamezomewa na kama ni kuhonga wapinzani uchwara ili wajiunge na kununua kadi Kinana vivyo hivyo na mengine.... Nami na nasema ni mpuuzi tu anayeeendelea kuamini maudhui ya makala hii ya zamani, kwa wakati huu tulio nao.
 
Mleta uzi, umefulia...kinana ni jangili...anaua tembo wetu.arudishwe kwao somalia maana si raia wa Tanzania. Ewe mleta uzi povu jingiii kwa kumtetea jangili..shame on you....kikwete ataendelea kuchange makatibu kila mara, plus mawaziri wake wenye vyeti vya kughushi.ccm nI chama dhaifu.
Wengine wanaua watu hamsemi na wanaendele kupanga mauaji lakini husemi mpaka wanapanga kumuua yulema mama ila uko kimya,badala yake unaishia kutunga uongo tu.
 
Kinana ni mtendaji makini zaidi ya makatibu wakuu wote wa vyama njaa akina slaa na utendaji wake unajulikana ndiyo maana chadema wanahaha na mambo ya meno ya tembo hivi ukiwa na basi ukapakia abilia akiwa na bangi kwenye begi lake ile bangi ikikamatwa wewe mwenye gari unahusika vipi? Mbona kuna viongozi wa upinzani ni wachafu wauaji lakini mnawasifia kila siku mfano mbowe alihusika na mauaji ya chacha wangwe na legia mtema na amezaa na esta matika lakini munamuna mungu wenu kwa sababu ya ujinga na uelewa wenu unao lingana na kuku wa kienyeji! Pole sana kinana atawanyosha mwaka huu hadi mkome.
 
Uzoefu wake katika siasa za kiraia unaanzia mwaka 1972 wakati alipostaafu jeshi akiwa Kanali baada ya kulitumikia kwa miaka 20 ndiyo ambao amekuwa akiutumia kama silaha kubwa ya kukijua chama chake na pengine kumfanya awe mmoja kati ya watu wachache ambao wamepata kuwafanyia kazi marais wote wane wa Tanzania.

Aisee.....kumbe aliingia jeshini 1952?
 
mleta uzi kafungua macho yangu sikuwahi kusoma makala hii,hili nalo ni la kutafakali tena,yawezekana hata yanayoendelea bungeni ni mpango maalum wa kumchafua ila kama mtu ni msafi ni msafi tu.
 
Mleta uzi, umefulia...kinana ni jangili...anaua tembo wetu.arudishwe kwao somalia maana si raia wa Tanzania. Ewe mleta uzi povu jingiii kwa kumtetea jangili..shame on you....kikwete ataendelea kuchange makatibu kila mara, plus mawaziri wake wenye vyeti vya kughushi.ccm nI chama dhaifu.
Mmeshindwa kuthibitisha madai yenu sasa mnakuja na issue ya uraia. Inacyoelekea hata maana na aina ya uraia hujui
 
Au mimi sijaelewa!kwamba ametumikia Jeshi kwa miaka 20,amestaafu/kuacha Jeshi 1972..wakati sisi Uhuru tumepata 1961!Ina maana Kinana alikuwa Jeshini tangu enzi za King African Rifles (K.A.R)?....."Ukisikia 'Tuuuuuuu' jua Tembo kakoswa,Usiulize nani huyoo..We jua tu Kinana kapita"

Mkuu barafu hii ni makala ya hovyo aliyoandika Kibanda ina makosa mengi, hapo kwenye red ndo ujue hii makala haikuandikwa tu hivihivi kulikuwa na kitu nyuma yake ndo maana imejaa upotoshaji. Cha kushangaza historia yake inaonesha kazaliwa mwaka 1951 (i humbly stand to be collected) kwa hiyo aliingia jeshini akiwa na umri wa mwaka mmoja. Hapo ndo ujue kumbe huyu waliyemng'oa meno na kumtoboa jicho walianza kumtumia siku nyingi. Alipohama kambi ndo yamemkuta yaliyomkuta. MAGAMBA HAWANA KITU WAMEISHA NI SUALA LA MUDA TU tutawatupa nje.
 
Ni mtu asiyejali au mpuuzi asiyezijua vyema siasa za Tanzania anayeweza akasimama na kuudharau uteuzi uliofanywa na Rais Kikwete ambaye baada ya kushindwa mara kadhaa hatimaye amefanikiwa kumshawishi, mmoja wa wanasiasa makini na wakongwe, mtumishi wa umma wa muda mrefu, mwanadiplomasia na Kanali Mstaafu wa Jeshi, Abdulrahaman Kinana kuwa Katibu Mkuu wa CCM.

Kwa muktadha huo na kwa kuzingatia nafasi kuu ya utendaji aliyopewa, nitazungumzia kwa sehemu tu wasifu wa Kinana, mtu ambaye naamini anapaswa kuangaliwa kwa jicho la karibu na wakati mwingine kudhibitiwa ili kasi yake ya kukijenga chama alichopewa dhamana ya kukinusuru isije ikasababisha kuyumba kama si mauti ya kisiasa kwa baadhi ya vyama vya upinzani.

Ni wazi kwamba, kuteuliwa kwa Kinana kuwa Mtendaji Mkuu wa CCM Taifa, akirithi mikoba iliyomshinda, Wilson Mukama, kumetutia ganzi baadhi yetu ambao kwa muda mrefu tumekuwa ‘mashabiki’ au waumini wa kuchagiza kwa njia ya kalamu na wakati mwingine katika mijadala ya wazi kwamba, taifa lilikuwa na haja ya kutafuta mabadiliko ya uongozi kutoka nje ya chama tawala.

Sitaki kuwa miongoni mwa wapenda mabadiliko ambao kwa njia za kujifariji au za kujipa matumaini hewa wameingia katika mkumbo wa jumla jumla wa kumbeza Kinana kwa namna wanayotaka kuuaminisha umma wa Watanzania kwamba, mtu huyo anaweza akasukumwa kirahisi kwa namna ile ile ilivyopata kuwa kwa watangulizi wake kadhaa waliopata kushika wadhifa huo.

siku zote nilikuwa nikiamini kwamba, ukatibu mkuu kwa Kinana ilikuwa ni silaha moja ya maangamizi kwa vyama vya upinzani ambavyo naamini vinapaswa kuendelea kupewa fursa ya kuaminiwa na kukomaa.

Kinana anaendelea kubakia kuwa tishio kubwa kwa ustawi wa upinzani ambao ni rutuba muhimu kwa maendeleo ya demokrasia na misingi ya utawala bora.

Hili ndilo ambalo naamini wapinzani wanapaswa kulitazama na kulitafakari nyakati hizi wanapoendesha harakati zao za kukabiliana na maguvu ya dola na haya mapya ya hoja ambazo aghalab zitaongozwa na Kinana nyakati hizi taifa linapojiandaa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa miaka mitatu ijayo.

Haitoshi kwa kina Freeman Mbowe, Profesa Ibrahim Lipumba, James Mbatia, Dk. Willibrod Slaa na Zitto Kabwe kumbeza Kinana na timu ya watendaji wake eti kwa hoja nyepesi na zisizo na mashiko za ufisadi au uchafu wa jumla jumla wa CCM.

Wapinzani na wachambuzi wa mambo wanapaswa kujua na kutambua kwamba, Kinana ni mwanasiasa wa vitendo, msomaji mzuri wa vitabu, ripoti, taarifa, magazeti, msikilizaji na msikivu mzuri wa mambo mepesi na mazito kuliko alivyokuwa ‘utopia’ Mukama anayeamini na kuzitetea nadharia zisizotekelezeka.

Si hilo tu, wapinzani wanapaswa kutambua kwamba, historia yake ya uaskari alioutumikia miaka 20 hadi mwaka 1972 akifikia cheo halisi cha jeshi cha Kanali ikimhusisha na mafunzo mahususi ya kimkakati ni sehemu ya mambo ambayo yanatawala nidhamu ya kazi ya aina ya kipekee iliyomfanya Kinana akawa jemedari wa mapambano ya CCM tangu mwaka 1995 hadi leo.

Wachambuzi wa mambo, nikiwamo mimi mwenyewe ambao siku zote tumekuwa tukiiona CCM kuwa chama kinachokufa kwa maana ya kuchungulia kaburi, tunapaswa kuanza kutafakari upya mawazo yetu hayo, nyakati hizi Kinana alipopewa dhamana ya kuwa mtendaji wake mkuu.

Tutakuwa wendawazimu iwapo tutamlinganisha Kinana na Mukama na kusahau kwamba huyu aliye kilingeni leo ndiye aliyemuongoza Benjamin Mkapa katika mapambano makali ya kisiasa mwaka 1995, zama Augustine Mrema alipokuwa tishio la kwanza la kweli dhidi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu.

Alikuwa ni Kinana aliyefanya kazi kubwa katika kipindi chote cha kampeni akiratibu na kuongoza kampeni zote za Mkapa zilizomjumuisha pia Mwalimu Nyerere katika mazingira ambayo wengi walikuwa wakiamini CCM ilikuwa katika mwelekeo wa anguko la kihistoria.

Kinana ambaye kabla ya mwaka 1995 alikuwa tayari amepata kuwa Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Waziri wa Ulinzi alitumia vyema mbinu za medani na zile za kidemokrasia na kidiplomasia kumjengea uhalali Mkapa ambaye wakati huo alikuwa mwanasiasa ambaye hakuwa akijulikana sana.

Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba, siku chache tu baada ya kuingia Ikulu kwa mara ya kwanza mwaka 1995, kwa sababu ama ya ulevi wa madaraka au kwa kutingwa na kazi za kimamlaka, Mkapa alisahau kazi kubwa aliyofanyiwa na Kinana.

Ni katika kipindi hicho cha kati ya mwaka 1995 na 2000 ndipo nilipokutana kwa mara ya kwanza na mara kadhaa na Kinana nyumbani kwake Masaki, jijini Dar es Salaam ambako nilipata fursa ya kumsikiliza na kuufahamu upeo mkubwa wa kuona mambo aliokuwa nao mwanasiasa huyo.

Tangu wakati huo hadi wakati wa kampeni za mwisho za mwaka 2010, niliendelea kukutana kwa nyakati fupi fupi na Kinana na mara kadhaa nikawa mtu wa kufuatilia na kuzisikiliza kwa makini, habari zake kutoka ama kwa marafiki au maadui zake wa kisiasa.

Sikushangazwa hata kidogo niliposikia tena kwamba, Mkapa alilazimika kumuangukia tena Kinana na kumuomba aongoze tena kampeni zake mwaka 2000 kabla ya Kikwete naye hajafanya kile alichofanya mtangulizi wake alipomuomba mwanasiasa huyo adhibiti joto la kiti cha urais mwaka 2010.

Uwezo wake mkubwa wa kisiasa, umakini wake na upeo mkubwa alionao katika kuona na kuchambua masuala ya siasa, uchumi na jamii ndivyo vitu ambavyo kwanza kwa nyakati tofauti vimepata kumfanya Kinana awe Mbunge wa Jimbo la Arusha kwa miaka 10, Mbunge wa Afrika Mashariki na Spika wa Bunge hilo.

Si ajabu hata kidogo kwamba, hata kabla ya kufikia huko, ni Kinana huyo huyo ambaye alipata kuwa Mwakilishi wa Kidiplomasia wa Rais wa Tanzania katika eneo la Maziwa Makuu na kabla ya hapo akiwa Mwenyekiti wa Mawaziri wa Ulinzi wa Nchi za Kusini Mwa Afrika (SADC) zama akiwa Waziri wa Ulinzi katika Serikali ya Awamu ya Pili iliyokuwa ikiongozwa Rais Ali Hassan Mwinyi.

Uzoefu wake katika siasa za kiraia unaanzia mwaka 1972 wakati alipostaafu jeshi akiwa Kanali baada ya kulitumikia kwa miaka 20 ndiyo ambao amekuwa akiutumia kama silaha kubwa ya kukijua chama chake na pengine kumfanya awe mmoja kati ya watu wachache ambao wamepata kuwafanyia kazi marais wote wane wa Tanzania.

Anarithi mikoba ya Mukama akiwa mmoja wa wanasiasa wachache wa CCM wa rika ile ile la kina Kikwete ambaye alilikimbia na kulikana kundi la mtandao mwaka 2005 ambalo baadhi yetu tunaamini kuwa, ndilo lilisababisha kuzaliwa kwa siasa mpya za kupakana matope, kuzushiana na kuhujumiana ndani na nje ya CCM.

Lakini pengine kubwa katika yote hayo anaingia madarakani huku akiwa na hazina ya uzoefu mkubwa wa kuongoza mapambano dhidi ya vyama vya upinzani na kushinda katika mazingira ambayo aghalab yamekuwa yakiacha vidonda visivyopona kwa wapinzani tangu mwaka 1995. Huyu si mtu wa kumpuuza au kumbeza hata kidogo.
Tunakushukuru mleta uzi kwa uzi huu nadhani ili upigane vita kwa uhakika ni lazima ujue uwezo na udhaifu wa adui yako kwa haya tunazidi kumjua kinana na kubuni mbinu mbadala za kupambana nae. Pamoja na sifa zote lakini bado kitu kimoja umeacha kuzungumza kuhusu udhaifu wa kinana. Hata hivyo pamoja na sifa zote ulizompamba lazima pia ukubali kwamba saliweza kufanikiwa kisiasa katika kipindi ambacho Watanzania wengi tulikuwa bado tumelala usingizi kwenye siasa za nchi hii. Kumbuka kuwa kwa sasa kumekuwa na mabadiliko makubwa sana kuhusu siasa za nchi hii ambazo kwa vyovyote vile Kinana si mzoefu wa siasa za sasa. Lakini pengine kubwa zaidi ni kwamba, tofauti na miaka ya nyuma kizazi hiki ni cha tofauti sana kukubali siasa za kina Kinana. Hiki ni Kizazi ambacho mi nakiita Critical generation. Kinana hana uzoefu na kizazi hiki na nina uhakika kwamba anafahamu kuwa siasa za sasa ni changamoto kubwa kwake kama katibu mkuu wa CCM. Vijana wanakwambia fashion ya sasa ya siasa ni CDM. M4C ndio story ya mjini ndio maana kwenye mikutano yake anaishia kubeba wamama kwenye malory baada ya kuwalipa elfu mbilimbili. Na hili halihitaji Ph.D kuelewa fanya tu personal observation utaona ni akina nani wanahudhuria mikutano ya CCM na CDM. Mi nakaa na vijana vijiweni na vyuoni vijana wanakwambia CCM ya sasa ni aibu kuizungumzia mbele ya watu au kuhudhuria mkutano yake labda unywe kidogo uende kama mwenda wazimu. Kwa mazingira kama haya Kinana ana kazi ya ziada kuivusha CCM 2015 na anaweza akajikuta anafeli zaidi ya mtangulizi wake. Unajua CCM walizoea vyama vya upinzani vya msimu, Sasa CDM imewashika pabaya ndio maana mpaka wanachanganyikiwa wabunge wao wanaliomba bunge lifute maandamano, na wanasahau kama waliyaweka wao kikatiba kama haki, haya yote ni kauli za mfa maji, wanatapatapa CCM hoi. Nawasilisha
 
Back
Top Bottom