Uchaguzi 2020 Ukweli mchungu kwa Lissu, sio kila mtu anaweza kuwa Rais wa JMT

Uchaguzi 2020 Ukweli mchungu kwa Lissu, sio kila mtu anaweza kuwa Rais wa JMT

xng hua

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2016
Posts
3,302
Reaction score
5,379
Wakuu nawasalimu,

Naomba muelewe kitu kimoja kuwa sio kila mtu anaweza kuwa Rais wa JMT hili mliweke akilini. Kwa ufupi tu hata kama Lissu akishinda uchaguzi na CCM kuamua kukubali kushindwa na ku backdown 'system haiwezi kumkubali Lissu abadani. Vyovyote itavyokua hatuwezi kuongozwa na Rais mbeambea, Rais asieweza kusimama peke yake katika maamuzi.

Rais huandaliwa na kuchunguzwa uadilifu wake kwa nchi yake, nikimuangalia Lissu sioni akiwa na sifa hiyo hata robo
bora Membe, Maalim hata Mbowe. Hawa wana uadilifu kwa nchi yao kuliko Lissu

Kama nilivyosema huu ni ukweli mchungu kwa wafuasi wake ila ni bora mkajua mapema kabisa!!

Pia naomba mjifunze historia ya nchi hii nzuri, mjifunze misingi ya uendeshaji wa nchi hii nzuri pia mjifunze sera mbalimbali zinazotumika kitaifa na kimataifa za nchi hii nzuri.
 
Unaweza kuwa na hoja lakini hujatuwekea wazi udhaifu wa Lissu uko wapi? Mbona ni mzalendo tuu?
CCM wametaka kumnunua mara nyingi ili kumnyamzisha lakini alibaki kuwa mpinzani kwa maslahi mapana ya Taifa hili ili aliondolee ndwele ya maumivu ya CCM
 
Kwa maslahi hayohayo ya taifa, Lissu hawezi kuwa rais hata kwa siku1
Ndio CCM ilishindwa kumnunua ila mabeberu waliweza tena kwa kujipeleka mwenyewe sokoni..
Ni vile tuu taasisi ya urais imeshuka heshma miongoni mwetu lakini trust me haijashuka heshma kwe mfumo hata chembe.
 
Uraisi mtu lazima afanyiwe vetting ya nguvu awe CCM au Upinzani .Sababu kugombea Ni kutaka vyombo vya dola viwe chini yake .Haviwezi kukubali kuwa chini ya mtu ambaye vetting ripoti yake mbaya .Vitaiba au kukimbia hata na masanduku ya kura au kumtangaza wanayemuona anafaa hata Kama hakushinda

Lisu vetting report yake ya vyombo vya dola bila Shaka hahitaji kuambiwa anaijua vizuri
 
kwa maslah hayohayo ya taifa lisu hawezi kua raisi hata kwa siku1
ndio ccm ilishindwa kumnunua ila mabeberu waliweza tena kwa kujipeleka mwenyewe sokoni..
ni vile tuu taasisi ya uraisi imeshuka heshma miongoni mwetu lakini trust me haijashuka heshma kwe mfumo hata chembe
kama urais ni taasisi kwanini asiweze; la msingi ni hiyo taasisi kuongozwa kwa kutumia sheria mama - katiba na huyo kiongozi kuifuata, mengine ni ya ziada. Ila kama uraisi ni mtu (an individual) then unaweza ukaona kuwa hataweza kwa mawazo yako, na mwingine ataona kuwa ataweza.
 
Unaijua presidential power ya JMT?
 
Ni hivi, Magufuli hawezi ushindani wa kisiasa na hatakaa aweze. Hizi nyimbo zenu ni baada ya kujua Magufuli hataweza kushindana na Lissu kwa hoja, hivyo mnaanza kutengeneza mazingira ya Lisu kutokugombea. Kama nchi hii ingekuwa na hizo sifa za uhakiki, basi JK au Magufuli mwenyewe wasingekuwa marais wa nchi hii.

Tunasema hivi, tunataka tume huru ya uchaguzi kwa amani, ili mshindi halali ndio atangazwe, tumechoka kuongozwa kwa shuruti na ccm.
 
kwa maslah hayohayo ya taifa lisu hawezi kua raisi hata kwa siku1
ndio ccm ilishindwa kumnunua ila mabeberu waliweza tena kwa kujipeleka mwenyewe sokoni..
ni vile tuu taasisi ya uraisi imeshuka heshma miongoni mwetu lakini trust me haijashuka heshma kwe mfumo hata chembe

Unaongea haya kwakuwa una maslahi binafsi na madaraka ya Magufuli, na ccm kwa ujumla. Hivyo unajua iwapo itaondoka madarakani utarudia umasikini uliotoka nao kijijini. Ww ni mwanaume mtu mzima, jifunze kujitegemea badala ya kutegemea wanaume wenzio.
 
Ni hivi, Magufuli hawezi ushindani wa kisiasa na hatakaa aweze. Hizi nyimbo zenu ni baada ya kujua Magufuli hataweza kushindana na Lissu kwa hoja, hivyo mnaanza kutengeneza mazingira ya Lisu kutokugombea. Kama nchi hii ingekuwa na hizo sifa za uhakiki, basi JK au Magufuli mwenyewe wasingekuwa marais wa nchi hii. Tunasema hivi, tunataka tume huru ya uchaguzi kwa amani, ili mshindi halali ndio atangazwe, tumechoka kuongozwa kwa shuruti na ccm.
Lisu akuna wakuweza kumzuia kugombea isipokua chama chake.
nani aljua ccm ingempitisha JPM na sio lowasa au membe?
tuelewane pale linapokuja swala la kiinchi lazima watu wenyeakili na walopewa mandates kusimama Ustawi wa nchi wafanye uhakiki hii aijalishi mgombea anatoka wapi.
 
Sisi Watanzania wazalendo ndyo tutakaomchagua Lissu tena kwa kura nyingi sana zitakazompa ushindi,huo ujinga wako peleka Lumumba wanakokupa buku saba!
Atagombea kama mgombea binafsi? Maana wamiliki wa CDM wanachaguo lao tayari, Nyalandu. Ni mtu ambaye wanaamini hatowasumbua kwenye kampeni financially
 
Sidhani kama uko sahihi.Watu pia waliamini aliyeko madarakani asingeweza lakini mambo yanakwenda.Nadhani huwezi kumuhukumu mtu bila ya kumpa fursa.

Unachopaswa ni kumuunga mkono ili uthibitishe kama kweli hawezi.Otherwise,utakuwa umeweka vipimo vyako we mwenyewe ambavyo si general standards.
 
Sidhani kama uko sahihi.Watu pia waliamini aliyeko madarakani asingeweza lakini mambo yanakwenda.Nadhani huwezi kumuhukumu mtu bila ya kumpa fursa.Unachopaswa ni kumuunga mkono ili uthibitishe kama kweli hawezi.Otherwise,utakuwa umeweka vipimo vyako we mwenyewe ambavyo si general standards.
ukishaaminiwa na system amna shida hata usipo amini wewe na wenzako

embu soma izo para 2za mwisho kwe bandiko langu
 
Uraisii mtu lazima afanyiwe vetting ya nguvu awe CCM au Upinzani .Sababu kugombea Ni kutaka vyombo vya dola viwe chini yake .Haviwezi kukubali kuwa chini ya mtu ambaye vetting ripoti yake mbaya .Vitaiba au kukimbia hata na masanduku ya kura au kumtangaza wanayemuona anafaa hata Kama hakushinda

Lisu vetting report yake ya vyombo vya dola bila Shaka hahitaji kuambiwa anaijua vizuri

Ukweli ni kwamba ccm haina tena uwezo wa kushindana kwa njia ya box la kura. Hivyo vyombo vya dola vinavyoendesha vetting inaonekana ni wanaccm watupu, ndio maana vetting yao majibu ni lazima uwe mwanaccm. Hiyo ya kukimbia na mabox ya Kutana kunajisi chaguzi za nchi hii zimekuwa wazi sana chini ya awamu hii, kwahiyo inaonekana hayo ni maagizo ya hivyo vyombo vya dola. Ni hivi, mgombea wetu upinzani ni huyo huyo Lissu, hivyo vyombo vya dola vitake, visitake lakini habari ndio hiyo.
 
ukishaaminiwa na system amna shida hata usipo amini wewe na wenzako

embu soma izo para 2za mwisho kwe bandiko langu

Hakuna mwenye uhakika na hilo.System ipi?Vyombo vya dola?Nafasi ya wananchi kuchagua viongozi wao iko wapi?Lolote linaweza kutokea,usiwe na uhakika sana
 
kama urais ni taasisi kwanini asiweze; la msingi ni hiyo taasisi kuongozwa kwa kutumia sheria mama - katiba na huyo kiongozi kuifuata, mengine ni ya ziada. Ila kama uraisi ni mtu (an individual) then unaweza ukaona kuwa hataweza kwa mawazo yako, na mwingine ataona kuwa ataweza.
Tatizo watu wa Lumumba hawaelewi kuwa urais ni taasisi. Vyombo vya ulinzi na usalama ni sehemu mojawapo ya vyombo vinavyotumiwa na taasisi hiyo. Havihusiki kikatiba ku-influence nani awe kiongozi wa taasisi hiyo. Wanaofanya hivyo ni wananchi kupitia sanduku la kura. Kwa hiyo, yeyote yule anayechaguliwa na watu ndiye anayekuwa rais na vyombo husika sharti vimtii. Kwa hiyo hakuna pingamizi lolote kikatiba kwa TL kuwa rais.
 
Back
Top Bottom