Hao waliopewa mandate wamepewa na nani? Chaguzi zetu sasa hivi zimetawaliwa na ushenzi, ukatili na uhayawani wa wazi, hao waliopewa mandate inaonekana ndio hao wanaoagiza huo uchafu. Haiwezekani wenye mandate wapewe na hao hao wanaopaswa kushindana, kwa vyovyote watawabeba wanaowachagua ili waendelee kulinda maslahi yao binafsi.
Hao wenye mandate unaowasema, ni wahuni fulani wasioweza kujitegemea, hivyo wako sehemu wanamteua mtu atakayewapa ulaji. Hicho kikundi cha wahuni wanaojiita wenye mandate, ndio huingiza nchi kwenye machafuko kwa ajili ya maslahi yao. Fahamu ya kuwa ccm sio chama cha kizazi hiki, ndio maana kinatumia mabavu, ukatili na unyama, ili kuendelea kukaa madarakani kwa shuruti bila ridhaa ya wananchi walio wengi. Sasa hivi watu hawataki kujitokeza tena kupiga kura, kisa kuna wahuni fulani wanaojifanya wana mandate, kwa kulazimisha kukiweka madarakani chama kisichokubalika na kizazi hiki.