Ni hivi, Magufuli hawezi ushindani wa kisiasa na hatakaa aweze. Hizi nyimbo zenu ni baada ya kujua Magufuli hataweza kushindana na Lissu kwa hoja, hivyo mnaanza kutengeneza mazingira ya Lisu kutokugombea. Kama nchi hii ingekuwa na hizo sifa za uhakiki, basi JK au Magufuli mwenyewe wasingekuwa marais wa nchi hii. Tunasema hivi, tunataka tume huru ya uchaguzi kwa amani, ili mshindi halali ndio atangazwe, tumechoka kuongozwa kwa shuruti na ccm.
Sasa hivi tunaomba waweke Tume Huru,hawana hoja wamebaki kudai Tume ni Huru huku wakifahamu fika wamejaza makada na wakereketwa wa chama au ni wananchama wao.Halafu unawaambia Watanzania kuwa wanaapishwa kutenda haki,hivi mechi ya Simba na Yanga unaweza kumweka Jerry Murro kuwa refa au Kaburu?
Kuna masuala nchi hii yanafanyika sifahamu ni kwa maslahi ya nani hasa?Polisi wanazuia wapinzani kufanya siasa wakati jukumu lao ni kutoa ulinzi halafu bado tunapongezana kwa sheria kukiukwa?Mambo ni mengi muda mfupi,ila watawala wasidhani kuwa Watanzania wataendelea kuwa wapole kama mwana kondoo wa sadaka/matambiko hadi milele?
Tuna nafasi nzuri ya kurekebisha nchi yetu kwa manufaa ya wote,tukaendelea na ujenzi wa Taifa kwa UMOJA wetu kwa kuruhusu michakato huru ya kupata viongozi,bila kujali ni kutoka chama gani,bora ni Mtanzania mwenye sifa aidha za Urais,Ubunge,Udiwani,Wenyeviti wa Vijiji/Vitongoji bila mizengwe.
Tanzania bila hujuma za kura inawezekana, serikali, vyama vya siasa na wadau wa uchaguzi wakae pamoja,waunde Tume ya Uchaguzi ya maridhiano ituvushe uchaguzi wa 2020, baada ya hapo turejelee mchakato wa Katiba Mpya ya Watanzania,tusonge mbele tukiwa na mshikamano aliotuasa Baba wa Taifa Mwl.J.K.Nyerere.Usanii wa kushinda chaguzi kwa kishindo huku tukifahamu kuwa tunaongopa ni DHAMBI ya mauti ambayo watawala wengi huwageuza mioyo yao kuwa migumu.
Hatutalipa kisasi,msiogope kushindwa kihalali,tutawaenzi kwa mazuri mliyotenda ila tuacheni wananchi wawe waamuzi wa viongozi wanaowapenda ili AMANI idumu,AMANI ni zao la HAKI na HAKI ni kama MAFUTA,ukiyatia kwenye maji yatazama lakini baadaye HUELEA na kujitenga na maji.Tenda wema uende zako,usilazimishe SHUKRANI,tutakukumbuka kwa.
Watanzania wenzangu,Maamuzi ni yetu.Tuchague kwa HEKIMA na tulinde kura zetu matokeo halali yapatikane kwenye ngazi zote za uongozi.Haki Huliinua Taifa,dhuluma Huangamiza.