Wakuu salama,
Leo nataka tuguse ule ukweli mchungu ambao jamii yetu inaukwepa sana, hasa linapokuja suala la misiba ya ndoa zetu za kiafrika.
Hivi mshawahi kukaa chini na kuchunguza kwa makini vilio vya wanawake wengi wa zama hizi waume zao wanapofariki? Ukichunguza kwa jicho la ndani kabisa, utagundua kitu kimoja: Mwanamke anapofiwa na mume, asilimia 80 ya kilio chake siyo maumivu ya kuondokewa na mtu anayempenda, bali ni hofu ya maisha na kupoteza "Boya" lililokuwa linamvusha kwenye dhoruba za kiuchumi.
Huu ndio ukweli wenyewe kwa mujibu wa uhalisia wangu wa macho:
1. Kilio cha "Mtegemezi" vs Kilio cha "Mpenzi"
Kwenye ndoa nyingi, mwanaume ndiye kila kitu (The Provider). Yeye ndiye anayejua kodi inalipwaje, chakula kinaingiaje, na maisha yanaendaje. Sasa huyu mtu akifa, ghafla ulimwengu wa mwanamke unasimama. Kile kilio cha "Mume wangu umeniachia nani?" tafsiri yake halisi ya kiuchumi siyo mapenzi, bali ni: "Nani atakayebeba hizi ada za shule, nani atalipa madeni, na kiwango changu cha maisha (Standard of Living) kitaendaje sasa?" Anacholilia pale ni maisha yake ya baadaye, siyo roho ya marehemu.
2. Mume Akishaacha Mali, Kilio Kinasimama Mapema sana
Angalieni misiba ya wanaume walioacha mahekalu, makampuni, na akaunti zilizoshiba. Mwanamke analia siku ya kwanza na ya pili kufanya "wajibu wa kijamii" ili wasimseme. Siku ya tatu akili ishahamia kwenye "Hati za viwanja ziko wapi?", "Wanasheria wanasemaje?", na kupanga nguo za black kulingana na fashion. Hapa hapotezi mtu, anapoteza tu mlinzi wa status yake, lakini kwa sababu ana uhakika wa kifedha, maumivu yanakuwa sifuri.
3. Ukiona Mwanamke Analia kwa Uchungu wa Kifo, Ujue Mshkaji Kafa Kapa!
Hapa ndipo penye siri. Ukiona mwanamke analia hadi anazimia na kugaragara chini, ukichunguza sana unakuta marehemu amefariki akiwa hana mbele wala nyuma—kaacha madeni ya vikoba na kodi ya nyumba inaisha mwezi ujao. Kile kilio kikubwa siyo cha mahaba, ni hofu ya kurudi kuanza upya sifuri ("Ground Zero") na mzigo wa watoto juu. Ni kilio cha umaskini unaomnyemelea.
Rai Yangu kwa Wanaume Wenzangu hapa JF:
Acheni kufa kishujaa huku mkiacha "Maboya" nyuma yenu. Hakikisha unatafuta fedha na kuweka misingi thabiti, lakini kubwa zaidi, mfundishe mkeo jinsi ya kusimamia na kutafuta fedha. Vinginevyo, siku ukitangulia mbele ya haki, ujue utakuwa umepoteza maisha yako peke yako, huku yeye akililia tu kupoteza "Boya.
Asanteni