Ukweli mchungu na sababu za kusimamishwa kwa Chama jr

Chama ana dharau sana, Hana LA maana halafu anajiona Iniesta.

Mbona Kuna wachezaji wakubwa walipita kwa heshima zao?

Waachane naye!
Viongozii wapo tayari ila chama ametega mtego wa kuvunjiwa mkataba apewe Pesa nyingi...hapo ndio kuna ugumu kwa viongozi

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 

Medhod Alicheza Simba nambari tano, Saba halafu nane akibadilishana na gaga. mda mrefu alicheza 5 siyo Sita. Sita ilichezwa na wengi akina bakri iddy, iddy selemani, ramadhani lenny maufi. Nico bambaga na Hussein MASHA ambaye baadae alienda namba nane baada Juma Amir kuondoka Simba.

Hata mechi ya mwisho kuchezea Simba, ambapo tayr tetesi za Method kuhamia Yanga zili trend, Method alikuwa akizomewa na kusukumwa na mashabiki aende zake Yanga, mechi hiyo ilikuwa Simba na Reli ambapo Simba ilipigwa 2 kwa moja. Simba iliongoza reli ikachomoa na kupiga mbili kupitia David Mihambo na Mwanamtwa ambao wote baadae walikuja kuhamia Simba.

Kwa Saidi Mwamba upo sahihi kama nilivyosema kuanza kucheza namb 5 Uganda kipindi cha mashindano ya africa mashariki
 
Vingi ulivyoviandika ni vitu vya kizushi na kufikirika. Kwa mfano.

1. Mchezaji kuomba kuvunja mkataba wake inakuwaje kuwa ni kosa la kinidhamu?

2. Mchezaji agomee mazoezi inakuwaje bado awe anapangwa kila mechi?

3. Mchezaji akosane na kocha wake inakuwaje bado kocha huyo huyo ahakikishe ana mpanga kila mechi?
 
Viongozii wapo tayari ila chama ametega mtego wa kuvunjiwa mkataba apewe Pesa nyingi...hapo ndio kuna ugumu kwa viongozi

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
Hii nayo ni fix tu. Hakuna ukweli hapo.
Mchezaji anapotaka yeye kuvunja mkataba haiwezekani tena yeye huyo huyo ashinikize kulipwa pesa. Anayetaka kuvunja mkataba ndio anawajibika kulipa fidia au kupoteza haki za maslahi yake na sio tofauti.
 
Mkuu chama ameomba kuvunja mkataba mwenyewe hii ipowazi

2- hii imetokea Ile siku ya mechi ya waydad na haina shaka katika ilo wewe ndio hukuona ujeri wa chama

3- baada ya kugomea mazoezi ya viungo kocha wa viungo alimfata baadae kumwambia utovu wa nidhamu wa chama....pia nikwambe usichokijua kama saido asingekuwa na Kadi tatu za njano chama asingeanza mechi Ile na asingecheza kabisa

Siongei udaku mkuu it's real

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Hii nayo ni fix tu. Hakuna ukweli hapo.
Mchezaji anapotaka yeye kuvunja mkataba haiwezekani tena yeye huyo huyo ashinikize kulipwa pesa. Anayetaka kuvunja mkataba ndio anawajibika kulipa fidia au kupoteza haki za maslahi yake na sio tofauti.
Jitahidi uwe unasomea vizuri mkuu naona ujaelewa kabs..

Ipo hivi mchezaji anapoomba kuvunja mkataba kama timu inaona wa muhimu lazima imtulize ili achane na hiyo dhamira kwamaana wambembeleze kama alivyofanya akidhan watambembeleza tahamaki wakamkubali kwamba avunje ila asubir msimu wa dirisha kubwa hapo ndipo chama alipoanza vituko

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Kiukweli CHAMA kama Simba kachez Sana, nasi tunamshukuru.... Hakutakiwa kumaliza vibaya hapo kajidanganya nasi tuko tayari aende hata Yanga kwani yeye sio wa kwanza walikuwepo kina Morison Leo wako wap?

Aende anakotaka, umri ushamkimbia halafu anatuletea zengwezengwe huyu Mzambia Wala sio mtaanzania... Wana Mbeya tupo tayari kumpokea Airport Songwe na kumsindikiza mpaka Tunduma!
 
Anajivunia na historia insha'Allah kikao kitaamua vyema

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Kama unasema Method alicheza Simba namba 5 basi huenda umemuona akicheza mwishoni mwa carrier yake pale Msimbazi, nakumbuka kwenye mechi dhidi ya Yanga mwaka 1990 Yanga alivyofungwa 1-0 kwa goli la faulo ya mbali la Mavumbi Omari, Method alicheza no 6 huku Gaga akicheza 8,wakati huo hao uliowataja hawakuwepo Simba isipokuwa Lenny aliyekuwa anakuja na kuondoka Simba (maana kuna kipindi alikuwa anaenda kucheza Uarabuni na wachezaji wengine kama Idd Pazi),Ingawa Method alikuwa kiraka anayeweza kucheza namba zote isipokuwa kipa,no 6 ndiyo ilimtambulisha tangu akiwa Umiseta Kanda ya kusini (wakati huo akisoma Mtwara Tech) hadi alivyoenda Arusha Tech pia ambapo akiwa Arusha alicheza AICC na huko alikuwa akicheza no 6, Method Mogella alikuwa kiungo mwenye ball control ya hali juu sana,alipohamia Yanga ndio nikamwona akicheza no 5 but unapotaja jina Method Mogella picha ya kwanza inayokujia ni kiungo na sio beki wa zamani.Wengi hawajui kuwa kuwa Method Mogella ndiye mchezaji mahiri aliyecheza Simba huku akiwa ni shabiki lialia wa Yanga huku Thomas Kipese naye ni mchezaji mahiri aliyecheza Yanga huku akiwa mnazi mkubwa wa Simba,pia wengi wanafikiri Method Mogella aka yake ilikuwa" fundi' kwa sababu ya umahiri wake kiwanjani,huyu alikuwa mchezaji aliyekuwa fundi by profession akiihitimu Chuo cha ufundi Arusha
 
Mlipeni pesa zake hao viongozi ndio wanawadanganya kila kukicha mtu anadai pesa mnasema maswala ya nidhamu...hata usajiri wake ulisumbua kisa mlitaka kumkopa wakati yeye anazijua hizi Team zetu.. acheni janja janja mpeni pesa yake yote anayoidai Simba sio mnampa kesi moja baada ya ingine...
 
Nadhani chama alitakiwa apewe "senkyuu" msimu jana ulipomalizika lakini hawajachelewa kumpa mkono wa kwa heri tena kwenye dilisha dogo hili ili wapate mbadala wake wa kudumu, hiyo itatoa funzo zuri kwa wachezaji wengine kubaki kwenye nidhamu zao
 
Sio apangwi ni hapangwi.

Aise uandishi huu unatia mashaka na elimu ya mtu.
 
Heshima kwenu wazee wetu
 
Subiri nikwambie kijana wakati Benchika anakuja Simba aliomba amsikilize Kila mchezaji mmoja mmoja shida yake na alisema kama kuna mchezaji anawadai mlipeni la sivyo hawezi pata namba kwenye kikosi, wachezaji wote walipewa bonansi zao hizi sasa Simba hakuna mchezaji anayedaiwa

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…