Ukweli Mchungu: Serikali Haiwezi Kuendesha SGR Kwa Watanzania Tuliopo. Tujifunze Kutoka Kwenye Mwendokasi

Inasikitisha sana. Ina maana sasa imeshakubalika kuwa serikali haitakuwa tena na uwiano katika mipango ya kitaifa maendeleo (national integrated development planning)? Serikali ya CCM imejenga SGR kwa gharama kubwa sana inayojumuisha mass passenger transportation component. Halafu serikali hiyo hiyo inapanga kutumia gharama kubwa tena kujenga expressway kwenye corridor hiyo hiyo kama vile hii ni nchi yenye uchumi wa dunia ya kwanza! Inahitaji miundombinu shindani kuwapa raia wake “wide choice”! Tena kwa mikopo zaidi!

What’s going on? Umuhimu wa kugawa pesa za umma za maendeleo kwa sekta mbali mbali kwa uwiano sahihi umetupiliwa mbali? Sasa kila Rais anataka kufanya “miradi yake” kuwapiku wenzake wa awamu zingine? Yaani, tunakubaliana na wajinga/wapumbavu waliozuka na kutamalaki miaka hii wanaofikiri Rais bora ni yule “mwenye maono; anayebuni miradi ya ‘kimkakati’”?

Halafu hayo mahangaiko ya kutaka SGR ionekane ikisafirisha abiria ni ujinga mwingine usioelezeka. Taaluma zimetupiliwa mbali enzi hizi! Watu hawajiulizi ilikuwaje reli zetu za awali za TRC na TAZARA zikafikia hapo zilipo? Bahati mbaya hakuna documentary clip ya TAZARA watu waone ilivyokuwa wakati TAZARA inazinduliwa ikiwa brand new na kila kitu kimekamilika.

Kiuchumi, gharama ya kuendesha treni ni kubwa sana inaweza kufidiwa tu na kiwango kikubwa cha usafirishaji mizigo mizito (bulky) kwa umbali mrefu (=>1000km). Vinginevyo, inabidi abiria watozwe nauli kubwa sana kufidia gharama za uendeshaji na faida kidogo. Tanzania miaka yote gharama za safari za treni ya abiria (TRC/TZR) zimekuwa zikifidiwa (subsidised) na safari za treni ya mizigo. Ulaya waliachana na mchezo wa cross-subsidisation miaka mingi tu. Nauli za abiria katika treni ni ghali kuliko za mabasi.

Baada ya mageuzi makubwa ya kiuchumi yaliyochagizwa na IMF na Benki ya Dunia, makampuni binafsi ya malori yalivamia soko ndio ikawa mwanzo wa kudorora kwa TRC na TZR. Hakuna hatua za kisera zilizochukuliwa kubadilisha hali hiyo. Lakini viongozi wetu wamekimbilia kumwaga matrilioni ya mikopo kujenga SGR. (Sijui kama feasibility study ilifanyika). Sasa hao wanasiasa na wananchi wanaona raha kuanza kupanda treni kwenda Morogoro na Dodoma bila kujiuliza hatma ya huo mradi!

Ni hasara sana kwa nchi kama Tanzania kutekeleza mipango yake kwa propaganda za kisiasa badala ya uhalisia wa vigezo vya uchumi. It’s just a matter of time, the reality will finally settle on the SGR and ATCL, the most amazing follies that I know and still wondering at.
Tusikubali SGR ifeli kama ulivyofeli MWENDOKASI, hivi vitu vipewe SEKTA BINAFSI mara moja
 
View attachment 3017687
Mbona barabarani kuna makampuni kibao,
Makampuni kwenye SGR yawe mengi, yalipe tu kiwango fulani serikalini kisha yapige kazi.

View attachment 3017688

Tumeona kinachoendelea kwenye Mwendokasi ni aibu tu na mateso kwa abiria. Tusikubali SGR ifike huko. BINAFSISHA mara MOJA kama anavyosema Waziri Mbarawa
Mbona kama sielewi Ina maana hawakujipanga?,swali fikirishi je hakuna mpango wa biashara, (andiko la mpango wa biashara), kitaalamu ukitaka kuanzisha biashara yenye mafanikio ni lazima uwe na andiko la mpango wa biashara husika. I thought there is a business plan, a business plan is a game plan or an operation plan
 
Serikali haijawahi kufanikiwa kwenye mradi wowote kuanzia ndege,mwendokasi,madini,gesi,treni,meli,uvuvi,utalii nk. nk.

Huu niuthibitisho kuwa viongozi wajuu serikalini hawana uwezo,ujuzi wala maarifa katika kusimamia miradi na kuipeleka nchi mbele.

Kimsingi serikali yetu inatumia pesa nyingi mmmno kutufanyia kazi ndooogo sana ndomana ikipewa miradi yoote inafilisika!!

Mfano Ikulu ingepewa mradi uuendeshe ili kupata mapato ya kujihudumia ninauhakika ikulu ingegeuka gofu chakavu na watumishi wake wangelala njaa...
Nivile inajiendesha Kwa kodizetu na wanazila bila kujali maana hawana uchungu nazo
Tizama raisi anasafiri kilaleo Tena saanyingine anasafiri na wasanii ughaibuni bila kujali gharama kuubwa bila tija kwakuwa hawazitafuti pesa wanazichota tuu!!!

Kila taasisi(wizara) ya serikali ingekabidhiwa mradi mmoja kama chanzochake pekee cha pesa za matumizi na kodizetu zikatumika tuu kwa huduma nyingine kunaviongozi/mawaziri wangekondeana, wangevaa viraka na kuendesha baiskeli chakavuu.
Narudia Tena "Hatuna viongozi wenye uhodari wowote labda wakuvaa masuti na kumsifu alowapa kulayao".
TURUDI KWENYE ELIMU YETU...
Serikali kwa asili siyo ya kuzalisha, ni ya kuvuna (kukusanya kodi, ushru, tozo,... ) na kutumia.
Serikali Ina wajibu wa kuweka sera, sheria na kanuni zitakazohakikisha ustawi wa raia wake kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni ili kujiletea maendeleo.
Hata hivyo, kwa sababu ya ujinga, kutostaarabika kwa jamii, viongozi wengi wa nchi masikini (hasa za Africa) huibia mataifa yao kwa kushrikiana na wageni kupitia mikataba, miradi na kandarasi mbalimbali. Kuanzia enzi za Mangungo, mambo ni yale yale, tofauti ni hali ya teknolojia ya dunia tu. Mangungo wa siku hizi wanaweza, kusoma, kuandika na kusafiri.
Kinachotakiwa kifanyike ni kujenga uwezo wa watu wetu wa ndani badala ya kutegemea wageni. Hili lawezekana kwa wananchi kuunganisha nguvu kuchagua na kuweka viongozi wenye maono na fikra chanya, huku wakiondoa wale walio kinyume na matarajio yao.
 
SGR inatakiwa kufika Mwanza na Kigoma haraka na kusafirisha mizigo ya nchi jirani kwa haraka na tuanze kuchota pesa za majirani na kuua uchumi wa Kenya hizo ndio zilikuwa ndoto za Magu , hii ya kutubeba abiria ni ziada tu ya SGR sasa mwenyewe kaenda mbwembwe kama zote.

Inapaswa mkubwa aambiwe tukope bila hofu SGR imalizwe haraka kujengwa ifike Mwanza na Kigoma kwakuwa ni reli ya kimkakati kubeba mizigo ndio lengo mama na kuifanya bongo kama Ulaya yaani donor country. Yule mwamba hakunaga!he had royal dreams ambazo Mama amezielewa,amezibeba na anazitekeleza kwa nguvu zote !

Mbwembwe za kubeba abiria kwa buku teni hazitalipa mkopo na kwa maana hiyo tozo tulizochoka za mwanayanga zitaendelea kutudidimiza kwenye umaskini. Wakumbuke duniani tunapita tu

Mama ameweza, maua mengi kwake, Mama mitano mingine!
Hata ingefika Kisangani ambako haiwezi fika Kwa sababu kumejaa vita ,ni hivi 70% ya mzigo wote wa DRC unaenda njia Ya Lubumbashi,huko maporini hakuna kitu.

Hakuna siku mtakuja kupata faida kwenye hiyo Sgr ya kupigia picha na Kukamatwa wajinga.
 
82% ya shehena za Mizigo zinazohudumiwa na Bandari ya Dar es Salaam kwa ajili ya Nchi jirani zinakwenda/kutoka Nchi 3 tu. Nazo ni JK Kongo, Zambia na Rwanda. Jumla ya Tani 8.2M zilipita Bandari ya Dar kwenda/kutoka Nchi jirani - DRC 3.4M- Zambia 2M- Rwanda 1.5M Shehena za Mizigo ya Nchi jirani kupitia Bandari zetu imekua kwa 28%
View attachment 3017736View attachment 3017737

Sijui huyo mnayemuita Shujaa au sijui mbeba maono alikuwa anatumia vigezo gani katika kuamua SGR iende Mwanza.
Hata ingeenda DRC via Kigoma au Burundi hakuna kitu utaleta Wala haitakuja kupata faida.

70% ya mzigo wa DRC unaenda Lubumbashi na sio huko kwingine

Mzigo uliobaki unagawanyoka kati ya central corridor na Northern Corridor so no way hiyo cosmetics Sgr itakuwa kuleta faida.

Huyo shujaa wenu alijenga Ili kuwapumbaza wasio na akili na Kwa taarifa Yao tuu watazisi kuwa maskini Kwa sababu Serikali itakuwa Inachukua kodi Yao na yangu kuendesha limradi linaloleta hasara.

Unajiuliza hivi hii Nchi ilikuwa inahitaji Sgr Kwa wakati huu? Hupati majibu ila wajinga Sasa walishangilia.
 
Tusikubali SGR ifeli kama ulivyofeli MWENDOKASI, hivi vitu vipewe SEKTA BINAFSI mara moja
Itakufa tuu,hata tukiwapa private operators hakuna Cha maana itabeba so lazima ijifie kifo Cha mende

Ukitaka isife tuendelee kuchukua Kodi na kuiendesha,Sasa huu utakuwa ni upumbavu
 
Barabarani kuna uwezekano wa gari kupita muda wowote, wala haupangiwi muda wa kuanza safari. Treni zinategemea njia moja, kupishana hadi kituo maalum, yaani treni moja ikae isubiri hadi nyingine ipite ndio iendelee na safari. Kwa mtindo huo hakutakuwa na uokoaji wa muda, maana Dar-Morogoro inaweza ikachukua masaa matano
Uthibitisho ni SGR kuanza kwa safari za DAR-MORO asubuhi na jioni tu kwa siku.
 
Inasikitisha sana. Ina maana sasa imeshakubalika kuwa serikali haitakuwa tena na uwiano katika mipango ya kitaifa maendeleo (national integrated development planning)? Serikali ya CCM imejenga SGR kwa gharama kubwa sana inayojumuisha mass passenger transportation component. Halafu serikali hiyo hiyo inapanga kutumia gharama kubwa tena kujenga expressway kwenye corridor hiyo hiyo kama vile hii ni nchi yenye uchumi wa dunia ya kwanza! Inahitaji miundombinu shindani kuwapa raia wake “wide choice”! Tena kwa mikopo zaidi!

What’s going on? Umuhimu wa kugawa pesa za umma za maendeleo kwa sekta mbali mbali kwa uwiano sahihi umetupiliwa mbali? Sasa kila Rais anataka kufanya “miradi yake” kuwapiku wenzake wa awamu zingine? Yaani, tunakubaliana na wajinga/wapumbavu waliozuka na kutamalaki miaka hii wanaofikiri Rais bora ni yule “mwenye maono; anayebuni miradi ya ‘kimkakati’”?

Halafu hayo mahangaiko ya kutaka SGR ionekane ikisafirisha abiria ni ujinga mwingine usioelezeka. Taaluma zimetupiliwa mbali enzi hizi! Watu hawajiulizi ilikuwaje reli zetu za awali za TRC na TAZARA zikafikia hapo zilipo? Bahati mbaya hakuna documentary clip ya TAZARA watu waone ilivyokuwa wakati TAZARA inazinduliwa ikiwa brand new na kila kitu kimekamilika.

Kiuchumi, gharama ya kuendesha treni ni kubwa sana inaweza kufidiwa tu na kiwango kikubwa cha usafirishaji mizigo mizito (bulky) kwa umbali mrefu (=>1000km). Vinginevyo, inabidi abiria watozwe nauli kubwa sana kufidia gharama za uendeshaji na faida kidogo. Tanzania miaka yote gharama za safari za treni ya abiria (TRC/TZR) zimekuwa zikifidiwa (subsidised) na safari za treni ya mizigo. Ulaya waliachana na mchezo wa cross-subsidisation miaka mingi tu. Nauli za abiria katika treni ni ghali kuliko za mabasi.

Baada ya mageuzi makubwa ya kiuchumi yaliyochagizwa na IMF na Benki ya Dunia, makampuni binafsi ya malori yalivamia soko ndio ikawa mwanzo wa kudorora kwa TRC na TZR. Hakuna hatua za kisera zilizochukuliwa kubadilisha hali hiyo. Lakini viongozi wetu wamekimbilia kumwaga matrilioni ya mikopo kujenga SGR. (Sijui kama feasibility study ilifanyika). Sasa hao wanasiasa na wananchi wanaona raha kuanza kupanda treni kwenda Morogoro na Dodoma bila kujiuliza hatma ya huo mradi!

Ni hasara sana kwa nchi kama Tanzania kutekeleza mipango yake kwa propaganda za kisiasa badala ya uhalisia wa vigezo vya uchumi. It’s just a matter of time, the reality will finally settle on the SGR and ATCL, the most amazing follies that I know and still wondering at.
Kuwa na maono siyo kuelekeza pesa nyingi kwenye "white elephant projects"
Wanasiasa wetu wengi ni majuha yanayoimba na kushangilia kwa gharama ya jasho la walalahoi, huku wakifuata viongozi kama kundi la nyumbu bila kujali hatari inayoweza kuwa mbele.
Ujinga huu unaanzia kwa wananchi ambao wanahitaji kuelimishwa na kujengewa ujasiri wa kuamua kwa akili huru.
 
Mbona kama sielewi Ina maana hawakujipanga?,swali fikirishi je hakuna mpango wa biashara, (andiko la mpango wa biashara), kitaalamu ukitaka kuanzisha biashara yenye mafanikio ni lazima uwe na andiko la mpango wa biashara husika. I thought there is a business plan, a business plan is a game plan or an operation plan
Hata Mwendokasi ina Business Plan lakini je unaridhika na performance yake? Tatizo ni kwamba hatuna watu wetu ambao wako committed kwenye utendaji na matokeo. Wengi wa Watanzania ni wezi walevi, wavivu, upendeleo, siasa nk
 
Wana ahirisha kufikiri Kwa nafsi a. k. a kujizima data
 
Serikali kwa asili siyo ya kuzalisha, ni ya kuvuna (kukusanya kodi, ushru, tozo,... ) na kutumia.
Serikali Ina wajibu wa kuweka sera, sheria na kanuni zitakazohakikisha ustawi wa raia wake kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni ili kujiletea maendeleo.
Hata hivyo, kwa sababu ya ujinga, kutostaarabika kwa jamii, viongozi wengi wa nchi masikini (hasa za Africa) huibia mataifa yao kwa kushrikiana na wageni kupitia mikataba, miradi na kandarasi mbalimbali. Kuanzia enzi za Mangungo, mambo ni yale yale, tofauti ni hali ya teknolojia ya dunia tu. Mangungo wa siku hizi wanaweza, kusoma, kuandika na kusafiri.
Kinachotakiwa kifanyike ni kujenga uwezo wa watu wetu wa ndani badala ya kutegemea wageni. Hili lawezekana kwa wananchi kuunganisha nguvu kuchagua na kuweka viongozi wenye maono na fikra chanya, huku wakiondoa wale walio kinyume na matarajio yao.
SI KWELI...Jifunze kidogo kupitia nchi zinazopaa kiuchumi mf. China, Japan, Brazil,N. Korea... Nchi nyingi makini serikali zao huendesha kwa ufanisi miradi muhimu mf. Umeme,maji,usafiri kama treni,ndege nyingine ni kwa ubia mfana madini,utalii nk.
sisi hakuna mradi wakiuzalishaji serikali imeonesha umakini na ufanisi zaidi ni umaskini wa fikra na ufisadi!! Hata elimu imewashinda
 
View attachment 3017687
Mbona barabarani kuna makampuni kibao,
Makampuni kwenye SGR yawe mengi, yalipe tu kiwango fulani serikalini kisha yapige kazi.

View attachment 3017688

Tumeona kinachoendelea kwenye Mwendokasi ni aibu tu na mateso kwa abiria. Tusikubali SGR ifike huko. BINAFSISHA mara MOJA kama anavyosema Waziri Mbarawa
Wahujumu wakubwa ni wafadhili wa CCM na majangili ya nchi
 
SI KWELI...Jifunze kidogo kupitia nchi zinazopaa kiuchumi mf. China, Japan, Brazil,N. Korea... Nchi nyingi makini serikali zao huendesha kwa ufanisi miradi muhimu mf. Umeme,maji,usafiri kama treni,ndege nyingine ni kwa ubia mfana madini,utalii nk.
sisi hakuna mradi wakiuzalishaji serikali imeonesha umakini na ufanisi zaidi ni umaskini wa fikra na ufisadi!! Hata elimu imewashinda
Huku ukiiba unaenda kui-support CCM unakuwa kwenye safe side
 
Ndiyo maana serikali imekaribisha wawekezaji! Serikali inahitaji wabia!
 
SI KWELI...Jifunze kidogo kupitia nchi zinazopaa kiuchumi mf. China, Japan, Brazil,N. Korea... Nchi nyingi makini serikali zao huendesha kwa ufanisi miradi muhimu mf. Umeme,maji,usafiri kama treni,ndege nyingine ni kwa ubia mfana madini,utalii nk.
sisi hakuna mradi wakiuzalishaji serikali imeonesha umakini na ufanisi zaidi ni umaskini wa fikra na ufisadi!! Hata elimu imewashinda
Hili lazima tuli implement na huo ndiyo ukweli mchungu
 
SI KWELI...Jifunze kidogo kupitia nchi zinazopaa kiuchumi mf. China, Japan, Brazil,N. Korea... Nchi nyingi makini serikali zao huendesha kwa ufanisi miradi muhimu mf. Umeme,maji,usafiri kama treni,ndege nyingine ni kwa ubia mfana madini,utalii nk.
sisi hakuna mradi wakiuzalishaji serikali imeonesha umakini na ufanisi zaidi ni umaskini wa fikra na ufisadi!! Hata elimu imewashinda
Nakubaliana na wewe kabisa.
Hapo kuna ubia (sekta binafsi), hivyo kinachoendesha pale ni hiyo element ya ownership (sekta binafsi).
Hata usalama wa taifa bila uwepo wa mikataba na wenye nchi wakiwa na nguvu (sekta binafsi) ya ndani (siyo magabacholi) bado unakuwa shakani.
Ni lazima mataifa ya Afrika, Tanzania ikiwemo yajenge uchumi na usalama kupitia raia wake wa asili na walio wengi (weusi), vinginevyo hakutakuwa na maendeleo endelevu, zaidi sana ni kuimarisha utumwa wa kiuchumi.
Usalama na miradi ya maendeleo bila raia weusi wenye nguvu za kiuchumi bado ni changamoto.
Ni muhimu kutofautisha taifa na nchi.
Taifa la Tanzania ni watu weusi zaidi na hivyo kujenga taifa ni kuwajenga watu weusi walio wengi, kinyume chake ni kubomoa taifa.
Nchi ya Tanzania ni eneo tu linalokaliwa na hao watu.
Bila kuwawezesha hao weusi kifikra na kiuchumi, maendeleo ya taifa itakuwa ndoto.
Wengi wenye fikra za kukariri wataona huu ni ubaguzi, lakini ni ukweli mchungu.
 
Ubishi tu kwa usichojua, haya bisha tena
Screenshot_20240729-063152_Gallery.jpg

Nitajie CEO wa UDART halafu uniambie nani alimteua? Siyo mnaandika tu JF bila kujua
 
Back
Top Bottom