Ukweli Mchungu: Serikali Haiwezi Kuendesha SGR Kwa Watanzania Tuliopo. Tujifunze Kutoka Kwenye Mwendokasi

Tusikubali SGR ifike huko. BINAFSISHA mara MOJA kama anavyosema Waziri Mbarawa
Ukisikia hivyo tayari kuna watu wamepewa mlungura, je wakurugenzi wa shirika watakuwa ofisini kufanya nini?
 
1722225146909.png

Posho ya hivyo vikao ni fedha ya kutosha mabasi kadhaa
 
ALIEKWAMBIA MWENDO KASI INAENDESHWA NA SERIKALI 100% NI NANI? UDART SIO SERIKALI NDUGU NI KAMPUNI TANZU, NDIO MAANA MABASI YAO HAYANA PLATE NUMBER YA SU, NA KODI YA IMPORTATION WANALIPA
Kampuni Tanzu maana yake ni subsidiary. Kwa mfano TBL walikuwa na Darbrew iliyokuwa inatengeneza pombe ya Chibuku.

Kwa Serikali kuwa na 85% dhidi ya 15% za say Simon Group haiifanyi UDART kuwa kampuni tanzu, bali inakuwa ni kampuni inayoendeshwa kwa ubia (Public Private Partnership).

Yeyote mwenye zaidi ya 51% hutambulika kama majority shareholder na ndiyo huendesha kampuni au kufanya maamuzi makubwa
 
Mjinga namba moja punguza uchafu wako kichwani, unafikiri udart ni wajinga basi zao ziwe na namba za kiraia badala ya SU?
View attachment 3055631
Yaani registration number ya mabasi unadhani ndiyo kielelezo cha ownership? Mbona TISS na Police wana magari mengi tu yako kwenye private numbers. Na mengine yako kwenye hata namba za nchi za nje.

Elimu ni tatizo hapa
 
Inasikitisha sana. Ina maana sasa imeshakubalika kuwa serikali haitakuwa tena na uwiano katika mipango ya kitaifa maendeleo (national integrated development planning)? Serikali ya CCM imejenga SGR kwa gharama kubwa sana inayojumuisha mass passenger transportation component. Halafu serikali hiyo hiyo inapanga kutumia gharama kubwa tena kujenga expressway kwenye corridor hiyo hiyo kama vile hii ni nchi yenye uchumi wa dunia ya kwanza! Inahitaji miundombinu shindani kuwapa raia wake “wide choice”! Tena kwa mikopo zaidi!

What’s going on? Umuhimu wa kugawa pesa za umma za maendeleo kwa sekta mbali mbali kwa uwiano sahihi umetupiliwa mbali? Sasa kila Rais anataka kufanya “miradi yake” kuwapiku wenzake wa awamu zingine? Yaani, tunakubaliana na wajinga/wapumbavu waliozuka na kutamalaki miaka hii wanaofikiri Rais bora ni yule “mwenye maono; anayebuni miradi ya ‘kimkakati’”?

Halafu hayo mahangaiko ya kutaka SGR ionekane ikisafirisha abiria ni ujinga mwingine usioelezeka. Taaluma zimetupiliwa mbali enzi hizi! Watu hawajiulizi ilikuwaje reli zetu za awali za TRC na TAZARA zikafikia hapo zilipo? Bahati mbaya hakuna documentary clip ya TAZARA watu waone ilivyokuwa wakati TAZARA inazinduliwa ikiwa brand new na kila kitu kimekamilika.

Kiuchumi, gharama ya kuendesha treni ni kubwa sana inaweza kufidiwa tu na kiwango kikubwa cha usafirishaji mizigo mizito (bulky) kwa umbali mrefu (=>1000km). Vinginevyo, inabidi abiria watozwe nauli kubwa sana kufidia gharama za uendeshaji na faida kidogo. Tanzania miaka yote gharama za safari za treni ya abiria (TRC/TZR) zimekuwa zikifidiwa (subsidised) na safari za treni ya mizigo. Ulaya waliachana na mchezo wa cross-subsidisation miaka mingi tu. Nauli za abiria katika treni ni ghali kuliko za mabasi.

Baada ya mageuzi makubwa ya kiuchumi yaliyochagizwa na IMF na Benki ya Dunia, makampuni binafsi ya malori yalivamia soko ndio ikawa mwanzo wa kudorora kwa TRC na TZR. Hakuna hatua za kisera zilizochukuliwa kubadilisha hali hiyo. Lakini viongozi wetu wamekimbilia kumwaga matrilioni ya mikopo kujenga SGR. (Sijui kama feasibility study ilifanyika). Sasa hao wanasiasa na wananchi wanaona raha kuanza kupanda treni kwenda Morogoro na Dodoma bila kujiuliza hatma ya huo mradi!

Ni hasara sana kwa nchi kama Tanzania kutekeleza mipango yake kwa propaganda za kisiasa badala ya uhalisia wa vigezo vya uchumi. It’s just a matter of time, the reality will finally settle on the SGR and ATCL, the most amazing follies that I know and still wondering at.
Wabongo hutakuja kujuwa wanataka nini, hata kufunguliwa rasmi bado wala mwaka kupita financial report kutoka tumeanza... unajuwa sana huu mradi malengo yake kwamba utafika mpaka Mwanza, na dry port zipo kwa malengo ya mizigo na hizi ni train za umeme sio Fuel zenye gharama kubwa hebu tujivunie kidogo. Huko duniani train kila sehemu halafu unakuja hapa unasema duniani train bei kubwa kuliko gari, acha kupotosha watu nenda Malaysia panda train unaweza kusema bure hapo Dubai tu tumia Metro compare na gari trip moja ya gari Metro unaweza kwenda hata mara 3.
 
Mzigo utoke wapi huko kwenye vinchi vina uchumi kama Mwanza? Wakati mnashauriwa msijenge kwanza mlitegemea nini? Bado maumivu yanakuja mbona mapema sana
Mnashauriwa na nani? hata bwawa la Nyerere tuliambiwa tusijenge tumejenga shida iko wapi. Acheni roho mbaya mkienda nje mnapiga picha mko kwenye ma train mmejengewa hapa mmeanza na roho ya kwanini. Binadamu hata umpeleke peponi atauliza huko juu hakuna VIP Pepo....
 
JNHPP ni mradi ambao Samia hakuwa na namna zaidi ya kuukamilisha kwa sababu aliukuta umeshakaribia nusu na tayari ulishateketeza fedha nyingi za Watanzania.

Ukweli ni kuwa mradi wa JNHPP ulikuwa uamuzi wa hovyo kuwahi kutokea. Kwanza unakuja na athari kubwa ya kimazingira. Ushauri wa wataalamu ulipuuzwa. Mradi ukajengwa kwa kulazimisha.

Karibu miti milioni nne imekatwa. Eneo la msitu la kilometa za mraba 1,500 limeharibiwa (deforestation).

Yaani, Serikali iliamua kujenga mradi wa umeme wa maji kwa kuharibu vyanzo vya maji.

Hivi sasa kuna mabadiliko ya tabia nchi. Mvua hazinyeshi. Mto Rufiji umekuwa mkavu. Je, sio athari za kuharibu msitu wa Selous.

Mtangulizi wa Rais Samia, Dk John Magufuli, alipoingia madarakani, alikuta mradi mkubwa wa gesi Mtwara. Nchi ilikuwa ina tabasamu kuelekea uchumi wa gesi.

Fedha zaidi ya Sh11 trilioni zilizotumika kujenga JNHPP, nusu yake tu ungewekezwa kwenye gesi Mtwara, sasa hivi nchi ingekuwa na umeme wa gesi, nishati ya kupikia ya gesi na kufanya mauzo ya gesi nje ya nchi.

Umeme wa gesi ndio wa kisasa. Umeme wa maji sio wa uhakika. Ndio maana mara kwa mara nchi ikitetereka kidogo kupata mvua, umeme unakuwa shida.

Changamoto ya umeme wa maji na kukauka kwa mabwawa ya kuzalishia umeme ndio matokeo ya nchi kuingia mikataba ya hovyo ya IPTL na Richmond kwa sababu ya uhitaji wa umeme wa dharura.

Pamoja na kutambua hayo, bado Serikali ya Magufuli ikafanya uamuzi wa kujenga mradi wa umeme wa maji.

Maswali ni mengi mno, unawezaje kujenga mradi wa umeme wa maji katika nchi ambayo tayari ina gesi ya kutosha?

Kuutelekeza mradi wa gesi Mtwara, ilikuwa kumkomoa nani? Hii hulka ya Rais akiingia madarakani anatelekeza miradi ya mtangulizi wake inaumiza mno wananchi.

Ingekuwaje Rais Samia angeamua kutoendelea na JNHPP? Fedha za Watanzania zingetolewa maelezo gani? Yatolewe maelezo ya kutelekezwa gesi Mtwara na miradi mingine yote ambayo ipo njiani miaka saba sasa.

Mwisho tuhoji; miti milioni tatu iliyokatwa Msitu wa Selous kupisha mradi wa JNHPP, ilipelekwa wapi? Iliuzwa? Fedha ilikwenda wapi? Uchunguzi maalum unahitajika katika hili.

Kuna harufu kubwa ya ufisadi wa miti milioni tatu iliyokatwa Selous.
 
Ndio kwanza asubuhi subiria Giza liingie
 
Paragraph ya 3 na 5 kuna maswali yako
 
View attachment 3017687
Mbona barabarani kuna makampuni kibao,
Makampuni kwenye SGR yawe mengi, yalipe tu kiwango fulani serikalini kisha yapige kazi.

View attachment 3017688

Tumeona kinachoendelea kwenye Mwendokasi ni aibu tu na mateso kwa abiria. Tusikubali SGR ifike huko. BINAFSISHA mara MOJA kama anavyosema Waziri Mbarawa
Kwani inayoendesha SGR na DART ni serikali au kampuni za serikali? Shida ni serikali kutosimamia vizuri kampuni zake kuanzia uteuzi wa waziri mwenye dhamana bodi na wakurugenzi wa makampuni yake. Sasa kwa msingi huo unafikiri serikali kama hiyo inaweza kuwapa watu gani mashirika yake waendeshe kama sio kugawa tu kwa watu watawapa maslahi vigogo wa serikali. Kwanza tunahitaji serikali yenye nia na utashi kutumikia umma wa wananchi. Hapo tutaona na mashirika yake yakikabidhiwa kuendeshwa kwa watu sahihi wenye weledi. Mbona magufuli alipokua kiongozi hata mbuzi wale wa mtaani hawakuingia ovyo barabara za mwendo kasi? Sasa vurugu zikasnza alipokufa hadi vituoni kuna wafanyakazi wanaleta tiketi zao binafsi kuuza. Mfumo wa tiketi ukafa. Wanaharibu kusudi utaratibu waweze kuibia umma.
 
Mimi nadhani hauko serious kabisa, hata wewe ukiwa unakiwanja unajenga nyumba utasafisha sehemu na kama kuna miti utakata lakini lengo ni nyumba. Naomba usikariti kuhusu Gas maana wewe unadhani kwa sababu una Gas Mtwara basi utaitoa tu na kuitumia. Lazima ujuwe Gas inachimbwa kwa gharama na ni kampuni za nje zinafanya kazi hiyo sio serikali sisi hatuna uwezo kipesa wala ufundi. Pia lazima ujuwe Gas inaisha pia sasa kufanya muendelezo ni lazima uchimbaji uaendelee kwa maisha ya mradi huo, visima huwa vinakauka.

Kwa hiyo unataka kusema baada ya mradi huu ndio mvua hazinyeshi tena? be serious sio juzi tu mlikuwa mnalalamika na mafuriko au Rufiji ya Africa kusini. umeme ulikuwa unakitaka kila siku malalamiko watu wanawasha mitambo malalamiko kisa walisema mazingira. Kina nani hao walisema mazingira sisi tusikate miti kwa miradi yetu muhimu ila waa wazalishaji wakubwa wa Carbon dioxide na Gas zingine zenye kuharibu mazingira wamefumba macho kwakuwa ndio engine ya uchumi wao kuzalisha unakuja kulaumu miti.
 
Kwani inayoendesha SGR na DART ni serikali au kampuni za serikali? Shida ni serikali kutosimamia vizuri kampuni zake kuanzia uteuzi wa waziri mwenye dhamana bodi na wakurugenzi wa makampuni yake. Sasa kwa msingi huo unafikiri serikali kama hiyo inaweza kuwapa watu gani mashirika yake waendeshe kama sio kugawa tu kwa watu watawapa maslahi vigogo wa serikali. Kwanza tunahitaji serikali yenye nia na utashi kutumikia umma wa wananchi. Hapo tutaona na mashirika yake yakikabidhiwa kuendeshwa kwa watu sahihi wenye weledi. Mbona magufuli alipokua kiongozi hata mbuzi wale wa mtaani hawakuingia ovyo barabara za mwendo kasi? Sasa vurugu zikasnza alipokufa hadi vituoni kuna wafanyakazi wanaleta tiketi zao binafsi kuuza. Mfumo wa tiketi ukafa. Wanaharibu kusudi utaratibu waweze kuibia umma.
Acha kuleta uchuro wa huyo Magufuli wako, tukishamzika Chato na maujinga yake
 
View attachment 3017687
Mbona barabarani kuna makampuni kibao,
Makampuni kwenye SGR yawe mengi, yalipe tu kiwango fulani serikalini kisha yapige kazi.

View attachment 3017688

Tumeona kinachoendelea kwenye Mwendokasi ni aibu tu na mateso kwa abiria. Tusikubali SGR ifike huko. BINAFSISHA mara MOJA kama anavyosema Waziri Mbaraw
Hata baskeli tu huna lakini lawama nyiingiiii kama zote.
Wenzako hatupandi hayo.
 
View attachment 3017687
Mbona barabarani kuna makampuni kibao,
Makampuni kwenye SGR yawe mengi, yalipe tu kiwango fulani serikalini kisha yapige kazi.

View attachment 3017688

Tumeona kinachoendelea kwenye Mwendokasi ni aibu tu na mateso kwa abiria. Tusikubali SGR ifike huko. BINAFSISHA mara MOJA kama anavyosema Waziri Mbarawa
hiyo ni akili ya kikoloni sana, na ni ya kijijini.
 
Wabongo hutakuja kujuwa wanataka nini, hata kufunguliwa rasmi bado wala mwaka kupita financial report kutoka tumeanza... unajuwa sana huu mradi malengo yake kwamba utafika mpaka Mwanza, na dry port zipo kwa malengo ya mizigo na hizi ni train za umeme sio Fuel zenye gharama kubwa hebu tujivunie kidogo. Huko duniani train kila sehemu halafu unakuja hapa unasema duniani train bei kubwa kuliko gari, acha kupotosha watu nenda Malaysia panda train unaweza kusema bure hapo Dubai tu tumia Metro compare na gari trip moja ya gari Metro unaweza kwenda hata mara 3.
Kama una taaluma ya transport economics tunaweza kujadili. Kama sivyo tutaishia kwenye propaganda za kisiasa. Fact ni kuwa gharama (per passenger kilometer) za kuendesha treni ya abiria ni kubwa kuliko za Basi. Isipotolewa ruzuku, nauli huwa juu (Ulaya/Marekani).

Treni huwa na ufanisi mkubwa likisafirisha mizigo mingi kwa umbali mrefu (>1000 km). Gharama kwa tonne kilometer hupungua kwa kadiri mzigo na umbali unavyoongezeka. Kuna hesabu zake.

Treni la abiria kwenda Morogoro na Dodoma lina tija ndogo sana kiuchumi na nina hakika litaendeshwa kwa ruzuku kwa muda mrefu sana. Reli ikikamilika hadi Mwanza na safari za mizigo kuanza basi mwelekeo unaweza kuwa bora zaidi mradi serikali iwe makini (serious).

Kwa sasa kama wananchi hawana tatizo na SGR kusafirisha abiria kwa bei ndogo na serikali ni ina pesa, basi sawa tu. Ni kama masuala ya ndege (ATCL) yanavyoendelea. (Umuhimu wa air transport economics umetupiliwa mbali). Huwa sina kauli kwenye aina hiyo ya mitizamo. Ruzuku ni uamuzi wa serikali na ridhaa ya wananchi.
 
Back
Top Bottom