Eyce
JF-Expert Member
- Mar 16, 2016
- 7,185
- 24,330
👏🏾👏🏾👏🏾Kumbuka kwa kila kijana mmoja wa huo umri unamuona ana enjoy maisha kuna wengine 100 wa umri huo huo wanaotaabika.
Swala la mafanikio ni swala mtambuka, halina formula maalum. Kuna watu wanasulubika ujanani yote na anakuja kutusua maisha uzeeni.
Kuwa kipimo cha mafanikio yako wewe mwenyewe. Jilinganishe ulipokuwa jana na ulipo leo. Ukisema kipimo cha maendeleo yako kiwe mafanikio ya wengine unaweza jinyonga maana kuna watu wanajua hasa kuonyesha jeuri ya pesa.
Mwisho na la muhimu zaidi, usithaminishe maisha ya mtu kwa kile anachokionyesha mitandaoni ama kwenye sehemu za starehe. Huko kuna maigizo tu.
Mkuu umeongea. Vijana hustling sio mchezo ndio maana vijana wanajiua sana siku hizi na wengine wanaingia kwenye mambo ya ajabu ili Tu waishi good life
Na ubaya hao wanaowapa ushauri sijui kwa nini msilime, mfuge, mfanye biashara etc, wao wana mitaji ila hata uthubutu wa kuanzisha kibanda cha M pesa hawana. Wanasubiria kuiba ili wajenge nyumba za kupangisha ambazo ni safe businesses