Ukweli mchungu: Ukifuatilia sana mambo ya dini, utabaini kuwa "Dini ni kwa ajili ya watoto"

Mkuu ni vyema ukaelezea Mungu anapaswa kuabudiwa vipi kama ulivyosema wanakosea kuliko kupoteza muda kukosoa na kulaumu na kuwaacha wabaki na ujinga.

Pitia uzi wako then Jiulize unajenga au unabomoa?

Pia kama dini ni kwaajili ya watoto - Wakubwa wanatakiwa wawe na nini?
 
Mungu na Dini ni danganya toto.

Dini ni utapeli.

Hakuna Mungu.

Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.
 
Mkuu ni vyema ukaelezea Mungu anapaswa kuabudiwa vipi kama ulivyosema wanakosea kuliko kupoteza muda kukosoa na kulaumu na kuwaacha wabaki na ujinga.

Pitia uzi wako then Jiulize unajenga au unabomoa?
Kaka watu wa dini Wana kejeli sana,wenyewe wanajiona ndio wako sahihi sana.
 
Kaka watu wa dini Wana kejeli sana,wenyewe wanajiona ndio wako sahihi sana.
Bado sijapata solution mkuu - Malalamiko hayajengi.

Je, kipi kilipaswa kifanyike baina ya watu wa dini?

Kitu gani unadhani ni sahihi kufanyika lakini hakifanyiki na wao?
 
Bado sijapata solution mkuu - Malalamiko hayajengi.

Je, kipi kilipaswa kifanyike baina ya watu wa dini?

Kitu gani unadhani ni sahihi kufanyika lakini hakifanyiki na wao?
Kwanza wakubaliane na mawazo kinzani kwa kuyapa usikivu ,wasing'ang'anie Imani tu watumie uwezo wa kufikiri najua wengi ama karibia wote wamejengewa hofu ya kesho Yao ya kifo.wahoji vitu na sio kuvikubali tu kama vilivyo.
 
Watu wenye point kama nyie ndio tunawataka kwenye hii nchi..
na sio wafia dini
 
Mbona unajitetea sana anyway , freewill
 
Kwanza wakubaliane na mawazo kinzani kwa kuyapa usikivu ,wasing'ang'anie Imani tu watumie uwezo wa kufikiri najua wengi ama karibia wote wamejengewa hofu ya kesho Yao ya kifo.wahoji vitu na sio kuvikubali tu kama vilivyo.
Sahihi.

Uhuru siyo kufanya kila unachokitaka uhuru ni kutokulazimishwa kufanya kitu fulani - ikitokea mtu anafanya kitu kwa kulazimishwa ni mtumwa (hayuko huru).

Ukikubali dini kwa hofu - hauko huru kwasababu ile hofu imeingilia uhuru wako wa kufikiri na kuamua tayari.

Tatizo linaanzia kwenye wazo - usipokua na uwezo wa kuchuja kila wazo linalokujia katika namna fulani bhasi ni rahisi kulibadili lile wazo kuwa mtizamo.

Pia kukosoa kila wazo linalokujia kutoka kwa mtu/watu fulani bila kufikiri why wanasema hivyo? [Labda sababu za hasira, huzuni, chuki, nk...] kisha unalibadili hilo wazo linakua mtizamo - huwezi kuupata uhuru halisi pia.

Before haujaweka jambo lolote kuwa mtizamo it's better kuwa neutral - kukaa chini na kufikiri, Lasihivyo unaweza kuangukia kuamini kisicho sahihi au kupinga kilicho sahihi.

So stay neutral, Stay calm - Think what they say? Why they say? Think about what you think about them? Are you right about them? Are they right? Then decide - Act.
 
Kuna dini moja tu ya kweli duniani. Moja tu. Narudia, moja tu. Itafute kwa bidii k. ama unavyotafuta dhahabu. Kazi kwako. Chimba, chimba update hazi a. Mafanikio hayaji kirahisi.
 
Tupo pamoja kaka
 
Kuna dini moja tu ya kweli duniani. Moja tu. Narudia, moja tu. Itafute kwa bidii k. ama unavyotafuta dhahabu. Kazi kwako. Chimba, chimba update hazi a. Mafanikio hayaji kirahisi.
Ipi hiyo kaka?,je Kuna mtu ameshawai kuipata?,leta hoja kaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…