UKWELI MCHUNGU: Wazazi wengi hawana upendo wa kweli

Wewe ni mzazi wa bara gani? Au khanisi huna kizazi?
 
Wewe ni mzazi wa bara gani? Au khanisi huna kizazi?
Ni mzazi wa bara la Afrika, wewe je? Ni khanisi au?

Kwa jinsi ulivyoandika, inaonesha unahusika na mambo niliyotaja kwenye post yangu.

Badilika, watoto siyo uwekezaji. Kumlea, kumtunza na kumsomesha ni wajibu wako kama mzazi, Wewe siyo bodi ya mikopo kwamba anatakiwa kurudisha baadae.

Jukumu la mtoto ni kuja kulea familia yake baadae, na siyo kukulea wewe, akikulea wewe ni hisani tu, siyo wajibu. Fanya kazi tafuta mali za kukufaa na kuwaachia urithi hao watoto baadae.

Acha kulewa na kufanya upumbavu kwa kutegemea kwamba unasomesha!
 
Hii nimeipenda ila wapo watu hawaijaelewa hii
 
Hujui maana ya upendo wa kweli. Ungejua, ungetambua kwamba mzazi hawezi kukutupa hata upate tatizo gani.
Na vipi kuhusu mwanamke anae zaa na mda huo kutupa mtoto vp mwanaume anae mktaa mtoto ebu tafakari
 
Upo sahihi kwa upande wa wazazi wanaowekeza kwa watoto ili badae wawageuze vyanzo vya kipato.
Unakuta mzazi mwingine anajiweza kabisa ila kwa urafi wake anawakamua watoto hata hawajajijenga vizuri kimaisha.
 
Ni kweli sababu nchi maskini watoto huzaliwa tu bila kupanga na kukubaliana Kato ya Mwanaume na mwanamke.

Huwa na impact kubwa sana kwa mujibu wa taarifa za tafiti mbalimbali.
 
Wazazi wengine wanataka kuabudiwa Yaani heshima iliyopitiliza.

Ndio maana Imeandikwa;
“Enyi wazazi msiwachokoze watoto wenu”
 
Mwanamke unakuta amekazana kujibebea mimba bila ridhaa ya Mwanaume hata kama mko ndani ya ndoa.

Sasa ikiwa ndani ya ndoa Mwanaume anaona aaah haya bana liwalo na liwe!
 
Ni kweli ,
Labda huko uzunguni Ulimwengu wa kwanza lakini huku Africa sizani.

Mimi huwa nasoma kwenye mitandao Eti mama sijui nini na nini kisha nasema mambo mengine yana apply huko Ulimwengu wa kwanza lakini wa tatu mmmnh ni ilimradi tu.
 
Mzazi mwingine anajaribu kuonesha kukupenda ukiwa unampa Hela ,
Ukiwa Huna hana Habari na wewe [emoji108][emoji108]
 
Huko Ulaya na America watoto huwa wanawashitaki wazazi wao ni kawaida sababu hakuna aliye juu ya sheria.

Tena wanawaambia mimi sijakuomba wewe mama unizae wala wewe baba [emoji108]

Na kwa hiyo tusipangiane maisha! [emoji4]
 
Watoto wengi wamezaliwa by default tu, Sasa hapo upendo utoke wapi.
 
umepiga kwenye mshono basi tegemea povu

bottom line ni kwamba hakuna yeyote anayekupenda unconditionally

upendo wowote ule ni wa faida(maslahi), kama siyo pesa, materiali basi ngono

huko ndoani ndiyo kabisa
Unconditional love utaipata Kwa Mungu tuu ..Kwa wanadamu Huku ni conditional love
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…