Ukweli mchungu: Zanzibar tunaishi kwa kudra za Tanganyika!

Inawezekana kipindi kile cha ujamaa miaka ya 1960's Mwalimu aliona Zanzibar ipo kimkakati na itapelekea manufaa kwa Tanganyika, masuala ya usalama, uchumi na siasa zilikua sababu chache.

Na pia Zanzibar waliona hivyo kuwa na muungano pamoja na Tanganyika.

Pengine ilikua ni hatua za mwanzo ya kile viongozi wale waasisi kuiunganisha Africa, wakiwa na fikra Kenya, Uganda n.k zitajiunga siku moja.

Walikuwa na sababu za kujiunga.

Kinachopelekea vijana leo wakose kuelewa kwa nini huu muungano ukawepo ni kwa sababu wazee wale na sisi vijana wa sasa tunatofautiana katika maono.
 
Kabla ya kuitwa nchi, kabla ya ukoloni, walikufa? Chkua time.
Zanzibar iliimarishwa sana na Sultani kupitia kilimo (minazi na karafuu), biashara (mashariki ya mbali na Ulaya), mlango bahari (bandari) na Utumwa (watanganyika wenye nguvuu!). Hivyo matunda ya hayo yote ndio yalizaa Zanzibar yenye maisha bora kipindi kileeeee.....

Sasa zama zimebadilika ndugu hapa Zanzibar, Utumwa (ni hadithi za kale), Kilimo (mikarafuu na minazi imezeeka mnoo na kufa, haizai na haiuzi tena), Bandari (imebakia kuwa kijiwe cha waswahili kupiga soga na kucheza bao) na biashara (karibu wapemba wote walishakimbilia Tanganyika kwenda kuchuuza, hata Bakheresa anajuta kwanini aliwekeza kule Fumba, Zenji imebakia ukata mtupu, ubaooo!!)

Ingizo jipya ni utalii, hili halikuwa ni deal kipindi kile cha ukoloni au baada ya mapinduzi, limechipuka zaidi miaka 1990s baada ya mtanganyika kufungua codes za kiuchumi kupitia utalii. Bahati mbaya mnoo kwa sasa nalo limeingia ruba, maana mmeru, muarusha, mchaga na Mmasai wameshaliteka huko Zanzibar.

Mswahili (Dr. Hussein wa mkuranga) akabuni jipyaa la uchumi wa buluuu. Ni blah blah tupu, mswahili haelewi kitu, watanganyika ndio wanakamatia fursa uchwara kibishi.
 
Ukiondoa issue za kiusalama (nipe nikupe) inaonekana hakukuwa na kitu kingine chochote cha maana.
Mkuu tunaelezwa deal la muungano lilikuwa limekaa kimchongo kimchongo. Mtawala mmoja yeye alidai ni kama alitapeliwa na alipostuka tu yakawa mengine.
Yote kwa yote, road map inaonekana ilikuwa tuje kufikia kuwa na nchi moja (Zenji imezwe na kuwa mkoa wa Tanganyika!) bahati mbaya hilo halijafikia mpaka leo, lakini bado lipo milele.
 
Hakuna kitu kizuri kama kuwa na shukrani!.
P
Lakini Zitto Kabwe juzi katoa takwimu zinaonyesha tofauti, kwamba Tanganyika tunadaiwa na Zanzibar ma trilioni ya Dollar. Kwamba tukikopa nje tunawapa 4% ya pesa za mikopo anadai sio sawa, na Nafasi za uwakilishi tunawapunja ndani na nje ya nchi. Anadai kiuchumi Zanzibar wangejitegemea ingekuwa zaidi ya Dubai. sasa sijui maana yule mchumu msomi, au anaendeshwa na mihemko ya ACT apate kura za huruma zanzibar.
 
Zanzibar inatufanyia ujajsusi mkali. Inapenyeza watu hadi kwenye nyadhfa za juu inakamua resources itakavyo na watanganyika wapo tu.

Tutakuja kukumbuka tumechelewa
Yericko Nyerere
Pascal Mayalla
 
How?
Logic?
Hoja za Zitto ni duni sana.
Ngoja nizijibu hapa.

Sawa Tanganyika wakikopa nje wanatupa Zanzibar 4% ya pesa ya mkopo na Tanganyika wanachukua 96% ya pesa ya mkopo lakini hapo hapo wakati wa kulipa mkopo Tanganyika inalipa zaidi ya 99% ya mkopo wote, sasa hapo nani anafaidika zaidi na mkopo?

Zitto anasema Tanganyika inadaiwa na Zanzibar kwa kuwa wakati wa kuanzishwa kwa benki kuu (BOT) Zanzibar ilitoa mtaji wake.
Okay, Zanzibar tulitoa mtaji, je ulikuwa ni mtaji wa thamani gani?
Je, tangu kipindi hicho Zanzibar imechangia kiasi gani katika kugharamia kuendesha BOT?
Je, kipindi kile wakati BOT ikijiendesha kwa hasara kubwa mno, mtaji wa uliowekwa na Zanzibar wakati wa kuanzishwa kwa BOT uliwezaje kubakia salama?
Je, tangu kipindi hicho BOT ikiwa taasisi mfu (kufirisika) imefufuliwa mara ngapi kwa pesa za watanganyika?
Hivi tunakumbuka kipindi cha Azimio la Arusha na vita ya Kagera namna BOT ilivyofirisika? Zanzibar tuliwahi tena kutoa mtaji?

Kuhusu BOT Zitto anapaswa kufahamu tu, uanzishwaji wake kipindi kile ulikuwa umekaa kisiasa (ili kutoa huduma) kama taifa kuwa na taasisi yenye kuratibu sarafu na takwimu za kiuchumi lakini haikuwa kama taasisi ya kibiashara ya kuzalisha faida za kipesa. Na hicho ndio kipindi ambacho Zanzibar ilifaidika zaidi kwa kuwa ilikuwa ukiuza karafuu kimataifa, na BOT ikaiwezesha mnoo Zanzibar kufanikisha hilo.

Tofauti na hapo Zitto anapaswa kuizungumzia BOT ya kuanzia miaka ya 1990s wakati sera za kiuchumi zikiwa zimebadilika huku ikiwezeshwa kufanya kazi zake kwa ufanisi kwa pesa za watanganyika.
 
Nakubaliana nawe, ila nilipomsikia Zitto nilijua ni siasa zao tu, unajua huu ndio msimu wa wao wanapulizia dawa kabla ya mavuno.
 
Yaani Akili ya Zitto inawaza kuwa sehemu ya mtaji wa kuanzisha BOT uliotolewa na Zanzibar ilikuwa kama mtego ili Zanzibar ije ifaidike kiholela kupokea pesa za bure bure kutoka Tanganyika, wakati kiuhalisia Zanzibar ilikuwa ina shida kweli kweli ya uwepo wa BOT ili iweze kuuza karafuu zake kiuhakika (export) na kuagiza mizigo kutoka nje kupitia bandari(import) na kweli ikaneemeka mnoo kipindi kile kuliko hata Tanganyika.

Zitto anajifanya hajui sera za uanzishwaji wa BOT kipindi kile ni tofauti kabisa na sera za uendeshaji wa BOT zama hizi.

Zitto ni njaa sana.
 
Aseee ,ivi ulikuwa wapi mdaa wotee asee

Mmoja wa Mzanzibari mwenye akili.nahisi unaDNA za Bara wewe .si bure Shehee

Njoo Arusha nikupe kiwanjaa ukae hukuu

Kikinuka wala hutokuwa na shida Tajiri
 
Aseee ,ivi ulikuwa wapi mdaa wotee asee

Mmoja wa Mzanzibari mwenye akili.nahisi unaDNA za Bara wewe .si bure Shehee

Njoo Arusha nikupe kiwanjaa ukae hukuu

Kikinuka wala hutokuwa na shida Tajiri
Hahahahaha...huyu atakuwa Bwana HAMZA wa mwanasheria wa ATCL
 
Ila Zanzibar ina potential kubwa sana. Kuishi chini ya kivuli cha Tanganyika ni kujichelewesha.
Potential gani hiyo?
Itaje tuone.
Usitaje bandari,hakuna ataeshushia mzigo huko kwani hatakuwa na mahali pa kuupitisha.
Karafuu,mwani&nazi hazitawafanya wakidhi mahitaji.
Watalii hawawezi kwenda kuona bahari tu.
Vivutio vipo huku Tanganyika...kule huenda kupumzika tu.
Option yao ni moja tu....kuwa colony la mtu.
 
Kwani tukimwita hata Nyoka wewe huko Tanganyika unaumia kitu gani? Kabla 1964 Hakuna kitu kilitoka Tanganyika labda wachumaji karafuu kutoka Tabora
 
ULE MCHANGA ULICHANGANYWA NA MSHUA WETU.....YULE MWINGINE SIJUI ALIKUWA WAPI..!
 
Kabla uvamizi mbona tukijiendesha ?
 

Mwarabu yuko Loliondo aje kufanya nini Zanzibar?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…