Sasa akili zao zilivyo fupi, chakula kinatoka Bara.. na Wazenji wengi hawana kazi za maana nikimaanisha hakuna mzunguko wa hela unaoeleweka ukiweka pembeni shughuli za Utalii na Uvuvi.
Pingine huna habari na unapiga ramli. Waulize wenzio huko jee hiki chakula Zanzibar wanagaiwa bure? Haya unayosema ni kinyume chake, kwani Zanzibar ikiamua kuacha kununua bidhaa za Tanganyika, na hili linawezekana,Tanganyika itakosa soko kubwa la bidhaa zake.
Ukizungumzia kutokuwa na kazi za maana na hakuna mzunguko wa pesa pia hujui kinachoendelea na wala hujui nadharia ya uchumi. Wewe kwa ujuzi wako unadhani uvuvi ma utalii sio kazi zinazoeleweka? Kama ni hivyo ni kazi gan zinazoelewka?
Mazao yao hayo ya karafuu, mwani etc havitoshi kuingiza kipato kwa mtu mmoja mmoja.
Bado una akili za kuambiwa. Hivyo karafuu na mwani kuwa havitoshi ndo iwe basi? Hujawaona Wazanzibari wakifanya shughuli nyingine?
Ikumbukwe karibu nusu yao wapo huku Bara.. wakipewa uhuru wao na sisi tunawatimua huku warudi kwao hivyo overpopulation itakuwepo na ufinyu wa resources lazima uzidi kuwadidimiza.
Hapa ndo unazidi kuonesha kutojua. Nani kakwambia population inadidimiza taifa? Hivi leo China imedidimia? Unaijua population ya China?
Jitahidi kufanya utafiti kabla kuandika. Sio kila jambo huandikwa.