Ukweli mchungu: Zanzibar tunaishi kwa kudra za Tanganyika!

Ukweli mchungu: Zanzibar tunaishi kwa kudra za Tanganyika!

mleta mada ni mzanzibari. namjua kwa uzuri. siwezi ku reveal identity yake hapa na faragha za pembeni za kufahamiana naye.
Kaskazini unatetea huyo sio mzanzibar , ukileta hapa nakupa pesa kwa uthbitisho ...Mkimbizi huyo anarudi kwao December.

Ukithibitisha nakupa pesa au ID yangi ifungiwe milele.
 
Nimesikia huko Arusha kuna wadudu, sasa haka kamuungano ketu siku kakifa nahisi hao wadudu watanitoa mkuku nirudi kwetu unguja na kugawana kibanda changu!
Tumia utambulisho wa kwenu , acha kejeli ...Usipagawe na JF watu unaweza kufuatiliwa.

Tumia akili hata comments zako zinaonyesha tu .
 
Japo sisi tumekuwa ndugu, marafiki nk lkn bado muungano wetu una mapengo mengi sana. Wanufaika ni wanasiasa tu ndio wanaokula. Kizazi cha kuhoji kinakuja, tusiombee. Nawaza Katiba mpya itibu hili. Na wanaokataa katiba mpya ni kwa maslshi yao kwa hofu zao, hasa wanasiasa wetu ambso wanaamini wao ndio kila kitu
 
Huijui Zanzibar. Ungetulia tu.
Sasa wewe mwenye kuijua Zanzibar embu tuambie basi, Zanzibar tutawezaje kutoboa kimaisha siku moja huu muungano ukafia baharini?

Yaani kama hata ulinzi, usalama na umeme kwa 100% Zanzibar tunategemea msaada wa pesa za mvuja jasho wa Tanganyika, ni kipi hasa tutaweza kukiendesha sisi wenyewe?

Ukweli usemwe, mtanganyika apewe maua yake kwa kuweza kutusitiri sisi wazenji kwa miaka 60.
 
Mimi mpaka kesho najiuliza, nyinyi watanganyika mnafaidika nini na huu muungano?
Nani aliwaloga?
Hampati chochote na bado mnabebeshwa mzigo mzito wa kuihudumia Zanzibar lakini hamchoki tu.

Yaani Mzanzibar ataendelea kumdharau kila mtanganyika milele.
Kaka mbona iko wazi kabisa anaeng'ang'ania huu muungano ni CCM na sio Watanganyika. Bahati mbaya hata huko hao CCM mnao.
 
Japokuwa huu muungano ni kichefu chefu tu kwa wazanzibar lakini ukweli mchungu ni kuwa, bila huruma na upendo wa Tanganyika basi huenda Zanzibar tusiweze kutoboa hata miezi mitatu.

Kuanzia Ulinzi, Usalama mpaka umeme tunapewa bureee na watanganyika. Kodi na rasimali za watanganyika ndio zinatupa maisha wazanzibar.

Rasimali na mapato yetu ya ndani ya Zanzibar hayawezi kutosha kugharamia ulinzi, usalama, umeme na huduma zingine muhimu za kijamii kwa zaidi ya miezi mitatu, tutaangamia!
Maneno haya Zitto Kabwe Mcongoman hataki kusikia.
 
Sasa wewe mwenye kuijua Zanzibar embu tuambie basi, Zanzibar tutawezaje kutoboa kimaisha siku moja huu muungano ukafia baharini?
Yaani kama hata ulinzi, usalama na umeme kwa 100% Zanzibar tunategemea msaada wa pesa za mvuja jasho wa Tanganyika, ni kipi hasa tutaweza kukiendesha sisi wenyewe?

Ukweli usemwe, mtanganyika apewe maua yake kwa kuweza kutusitiri sisi wazenji kwa miaka 60.
Wewe ni mchaga kutoka machame upo Zanzibar kuuza vinyago toka lini umekua Mzanzibari?
 
Kaka mbona iko wazi kabisa anaeng'ang'ania huu muungano ni CCM na sio Watanganyika. Bahati mbaya hata huko hao CCM mnao.
Huko wapi ? Huyo ni mtanganyika mwenzako mchaga kutoka machame yupo Zanzibar anauza vinyago wala sio Mzanzibari
 
Sasa wewe mwenye kuijua Zanzibar embu tuambie basi, Zanzibar tutawezaje kutoboa kimaisha siku moja huu muungano ukafia baharini?
Yaani kama hata ulinzi, usalama na umeme kwa 100% Zanzibar tunategemea msaada wa pesa za mvuja jasho wa Tanganyika, ni kipi hasa tutaweza kukiendesha sisi wenyewe?

Ukweli usemwe, mtanganyika apewe maua yake kwa kuweza kutusitiri sisi wazenji kwa miaka 60.
Zanzibar watapata pesa zao na misaada kwa 100%. chakula hata bongo kinaagizwa juzi tu hapa walipiga marufuku ndizi kutoka huku Tz mkaanza kupiga kelele, mipakani mpaka wakenya wanunua chakula na vivyo hivyo watanzania wananunua kutoka nje.

Mfanyabiashara anapeleka kwany soko hata ulaya hana shobo na muungano wanu, Umeme inaweza kununua mbona Tanzania inanua? Muulize Biteko.

Mikoa kibao ya karibu kama kupitia Dar, Tanga, Mtwara ....Basi kama lango la bidhaa hata magendo zenji ni namba moja ..

Hamna logic kwa vile kuvunja muungano sio ugomvi ushirikiano upo pale pale , unaweza kutoka bara ukaomba uraia kule kw kufuata taratibu, zanzibar ina diaspora wengi nje kuliko huku bara...Nchi za Asia wapo kibao ndugu zao wapo mikao ya pwani kwa sana maana wanafanana.

Biashara zipo pale pale watalii wataingia na wakule wtakuja huku.
 
Huyo jamaa znz Asp ni mchaga kutoka machame yupo Zanzibar anauza vinyago
Nionyeshe mzanzibar wa asili ili nikuonye mgeni wa kuja Zanzibar!
Wazanzibar wote ni watu wa kuja, Zanzibar haina mwenyewe, kihistoria ni kisiwa cha uvuvi, utumwa na ulanguzi. kuanzia Mzee Karume mwenyewe (mnyasa), Maalim (mshiraz wa kutoka Oman) mpaka Dr. Hussein (kutoka Mkuranga)

Sifa kubwa (na mbaya) ya Mzanzibar ni kubagua na kutumikisha, ubaguzi ni kama ngozi kwa mzanzibar. Mshirazi (mpemba!) atambagua mswahili (muunguja!) na muunguja atamdidimiza (mtumikisha) mpemba. Ngoma pia ipo siku itageuka. Yaani Zanzibar tumekaa kuviziana tu.
 
Nionyeshe mzanzibar wa asili ili nikuonye mgeni wa kuja Zanzibar?
Wazanzibar wote ni watu wa kuja, kuanzia Mzee Karume mwenyewe (mnyasa), Maamlim (mshiraz wa kutoka Oman) mpaka Dr. Hussein (kutoka Mkuranga)

Sifa kubwa (na mbaya) ya Mzanzibar kubagua na kutumikisha, ubaguzi ni kama ngozi kwa mzanzibar. Mshirazi (mpemba!) atambagua mswahili (muunguja!) na muunguja atamdidimiza (mtumikisha) mpemba. Ngoma pia ipo siku itageuka. Yaani Zanzibar tumekaa kuviziana tu.
Nimekuuliza toka lini umekua Mzanzibari?
 
Wanasem Wazenji kwamba wakipewa uhuru wao, watawaita Waarabu wa Dubai na Oman wapabadirishe hapo pawe kama Dubai...

Sasa akili zao zilivyo fupi, chakula kinatoka Bara.. na Wazenji wengi hawana kazi za maana nikimaanisha hakuna mzunguko wa hela unaoeleweka ukiweka pembeni shughuli za Utalii na Uvuvi.

Mazao yao hayo ya karafuu, mwani etc havitoshi kuingiza kipato kwa mtu mmoja mmoja.

Ikumbukwe karibu nusu yao wapo huku Bara.. wakipewa uhuru wao na sisi tunawatimua huku warudi kwao hivyo overpopulation itakuwepo na ufinyu wa resources lazima uzidi kuwadidimiza.

I wish siku ifike kila mtu abebe chake.
Mimi nataka tu siku moja huu muungano uvunjike ili wabaki kwao tuone wwtafsnya maajabu gani ..watu wanapewa kila ain y a upendeleo lakin hawaridhiki
 
Nionyeshe mzanzibar wa asili ili nikuonye mgeni wa kuja Zanzibar!
Wazanzibar wote ni watu wa kuja, Zanzibar haina mwenyewe, kihistoria ni kisiwa cha uvuvi, utumwa na ulanguzi. kuanzia Mzee Karume mwenyewe (mnyasa), Maalim (mshiraz wa kutoka Oman) mpaka Dr. Hussein (kutoka Mkuranga)

Sifa kubwa (na mbaya) ya Mzanzibar ni kubagua na kutumikisha, ubaguzi ni kama ngozi kwa mzanzibar. Mshirazi (mpemba!) atambagua mswahili (muunguja!) na muunguja atamdidimiza (mtumikisha) mpemba. Ngoma pia ipo siku itageuka. Yaani Zanzibar tumekaa kuviziana tu.
Kwa hiyo na wewe ni Mzanzibari wa kuja au vipi ?
 
Ni sawa na kusema Tanzania bila ya misaada ya Ulaya isinge toboa.

Hivi kuna kisiwa duniani hakiwezi jiendesha wenyewe?.
Namshangaa huyu mpenda misaada ya bure. Hivi Zanzibar kabla ya 1964 ilikuwa inaishi vipi? Au hivyo visiwa vingi tu vinavyojitegemea wenyewe vinajiendesha vipi?

Na akumbuke tu kuwa Zanzibar ilikuwa mbele zaidi kielimu na kimaendeleo kabla ya muungano.
 
Nimesikia huko Arusha kuna wadudu, sasa haka kamuungano ketu siku kakifa nahisi hao wadudu watanitoa mkuku nirudi kwetu unguja na kugawana kibanda changu!
Shehee Wadudu wa huku ni Marasi
So hilo ni brand tu bro ya kazi zao wasikutishe waa amani sana Dingi hao Jomba
 
Back
Top Bottom