Tafakari upya.
Tukivunja muungano, Zanzibar tutapata wapi pesa za kuendesha serikali na kutoa huduma za kijamii kwa uendelevu ikiwa kwa sasa hivi tu hatuwezi kulipa hata umeme wa Tanesco?
Hivi hujui kwa sehemu kubwa uendeshaji wa SMZ kibajeti unategemea ruzuku kutoka serikali ya muungano, ambayo ni pesa inayokusanywa zaidi kutoka kwa mvuja jasho wa kitanganyika?
Hivi unajua bajeti ya ulinzi na usalama ya serikali ya muungano inayotumia ili kuilinda Zanzibar?
Hoja ya kusema, muungano ukivunjika basi Zanzibar tutapata pesa za misaada za kutosha kwa 100% ni hoja ya kimaskini, kijinga na kipumbavu zaidi iliyojaa vichwani mwa wazenji wengi. Ni fikra duni kupita maelezo. Yaani wazenji wakisikia Tanzania imepewa pesa za misaada wanadhania ni pesa za sandakalawe, hawajui hizo sio pesa za bure (nyingi ni mikopo) na wanaozitoa wana akili mara kumi yetu (ni mtego wa hatari), na wanaozitoa wamesoma ramani ya kuvutiwa na fursa bwerere zilizopo Tanganyika kuliko Zenji.
Mwisho fahamu tu, sio muungano ndio unaofanya vyakula viletwe kuuzwa Zanzibar bali fursa za kibiashara ambazo ziko wazi na huru kwa taifa lolote lile. Hata muungano usingekuwepo bado watanganyika wangepeleka kuuza vyakula Zenji. Issue ni uwezo wa SMZ kuweza kuwahudumia wazenji kijamii bila msaada wa serikali ya Muungano uko chini mnoo, haufiki hata 30%