Ukweli mchungu: Zanzibar tunaishi kwa kudra za Tanganyika!

Ukweli mchungu: Zanzibar tunaishi kwa kudra za Tanganyika!

Pesa zipo hata zile zilizotolewa kwa ajili ya athari za covid19 zilifika bara .

Nchi ngapi ndogo zinajiendesha? Hapa Tz wenyewe bajeti inatoka nje..Sio fikra duni maana hata TZ inategemea wahisani kwani TZ ina deni la shIling ngapi? 😛 😛

Unakataa hoja ya mikopo wakati nchi yako Tz inakopa daily hata kenya wana dEni kubwa , umesoma kweli au shule ndio tatizo. sukari inatoka nje watu wanagawana , je unajua biashara zinazofanyIKa bandari bubu ya Tongoni TANGA na zanzibar , huku tonnes za vyakula zinapita .

Fursa ipi ya kibiashara ? still vipingamizi vya kodi ni vile vile , toa mazao peleka zenji kama ni bure ...Wanaona soko ndio wanapeleka zenji kwa kufauta taratibu zote .

Tatizo lako ni uelewa !
Mimi nimesema hivi.
Hicho unachosema ni misaada mara zote ni mikopo (utapaswa kulipa) na kina mtego (kuna masharti). Je, Zanzibar tunakopesheka kirahisi?
Na je tuna uwezo wa kulipa?

Wakopeshaji hawaji bure bure, wanaweza kuja kuikopesha SMZ ili mwisho wa siku Zanzibar ishindwe kulipa na visiwa vipigwe bei.

Mwisho kabisa, fahamu Serikali ya muungano ni moja ya taasisi inayoongoza kuikopesha pesa SMZ, na mara nyingi SMZ wanashindwa kulipa na serikali ya muungano inapotezea kisiasa kwa kusema ni ruzuku, pesa ya maendeleo au kuingizwa kwenye kasma ya bajeti ya mambo ya muungano.
 
Zanzibar ni nchi mpaka hapo , anakopa kwa uwezo wake atapata mikopo kutoka kwa nchi za Asia kulingana ukaribu wao ...Mega porject ila na nyie mjiandae kurudisha pesa ya uanzishwaji wa BOT.
Zenji wataheshimika zaidi watafika mbali , wana bandari lango la biashara haswa sisi ndugu zao wa kanda ya pwani tutafanya nao biashara sana.
Zanzibar ilikuwepo kabla ya TZ ikaporwa .
 
Wanasem Wazenji kwamba wakipewa uhuru wao, watawaita Waarabu wa Dubai na Oman wapabadirishe hapo pawe kama Dubai...

Sasa akili zao zilivyo fupi, chakula kinatoka Bara.. na Wazenji wengi hawana kazi za maana nikimaanisha hakuna mzunguko wa hela unaoeleweka ukiweka pembeni shughuli za Utalii na Uvuvi.

Mazao yao hayo ya karafuu, mwani etc havitoshi kuingiza kipato kwa mtu mmoja mmoja.

Ikumbukwe karibu nusu yao wapo huku Bara.. wakipewa uhuru wao na sisi tunawatimua huku warudi kwao hivyo overpopulation itakuwepo na ufinyu wa resources lazima uzidi kuwadidimiza.

I wish siku ifike kila mtu abebe chake.
Hakuna mwarabu ht mmoja ataeitwa, watakuja wenyewe....infact watarudi kuja kuijenga zanzibar yao baada ya kuikimbia. Na waliikimbia baada ya mapinduzi na muungano uso tija kwa wazanzibari. Wanasubiri kwa hamu hio siku ifike
 
Nakwambia hivi, Tanganyika kwa sasa ndio inatusitiri sisi wazanzibar. Bila Tanganyika hatuna ulinzi, usalama wala umeme.

Karafuu iliyokuwa inatupa jeuri ilishakufa kitambo sana, na kwa uvivu wetu tumeshindwa kuifufua, na sasa tunasikia huko Tanganyika mlishaanza kuotesha na kuvuna karafuu yenu kwa fujo.....

Bandari ya Zanzibar iko mahututi maana kila jirani yetu (Beira, Mombasa, Comoro, Eritrea, Djibout, Dar, Mtwara, Tanga) alisha imarisha bandari yake, Zanzibar hatuna tena upekee wa kibandari....

Zanzibar tumebakia na Utalii pekee yake (ambao ni wa msimu, na watalii wenyewe wengi huanzia bara au kumalizia bara maana huko wako huru kuvaa chochote, kula mwaka mzima (huku kula hadharani kipindi cha Ramandan ni mwiko!), kula chochote (hata kitimoto), kunywa chochote(pombe), hapa Zanzibar watalii wanapita kwa siku zisizozidi tatu (kushangaa mchanga mweupe wa beach ambao umegundulika umejaa vilivyo kule Tanganyika (Kigamboni), kutafuna machoko wakizenji na kubwia unga kwa uhuru kisha kusepa zao). Bahati mbaya sana na huo utalii pekee hautoshi kuendesha maisha ya wazanzibar zaidi ya 1.5milioni kwa siku zaidi ya 90.

Yote kwa yote, mmasai ameshaingia Zanzibar na sasa anataka kutawala utaliii wote.

Nasema hivi, Zanzibar bila Tanganyika twafaa!
Mtanganyika anatujali mnooo.
We unadhani bandari ipo mahututi kwa sababu gani we mzanzibari wa mchongo!!!?
 
Mapato kikodi ya Zanzibar,
Mwaka 2021/2022,bilioni 374.2
Mwaka 2022/2023 bilioni 579.5
Mwaka 2023/2024 bilioni 565.8
Katika Mwaka wa Fedha uliokwisha wa makusanyo ya bilioni 565.8 wastani wa makusanyo ni 47 bilioni kwa mwezi.

Katika Mwaka wa Fedha 2023/2024 bajeti ya Zanzibar ni 2.8 trilion: trilion 1.3 matumizi ya kawaida na 1.5 trilioni ni maendeleo.Una finance vipi bajeti ya 2.8 trilioni kwa makusanyo ya 565 bilioni kwa Mwaka?.Kama sio pesa zinahamishwa kutoka Tanzania bara kufanance bajeti ya Zanzibar?.au mnataka kuniambia mnakwenda kukopa 2.3 trilioni kila mwaka kwa makusanyo ya 565 bilioni??.

Kiuchumi huu muungano unaumiza sana upende wa Tanzania bara,ni basi tu Watanganyika wengi ni matahira tusio jitambua na kufatilia mambo.Zanzibar haiwezi ku survive bila Tanganyika watakufa vibaya sana.takwimu zinaongea.
 
Japokuwa huu muungano ni kichefu chefu tu kwa wazanzibar lakini ukweli mchungu ni kuwa, bila huruma na upendo wa Tanganyika basi huenda Zanzibar tusiweze kutoboa hata miezi mitatu.

Kuanzia Ulinzi, Usalama mpaka umeme tunapewa bureee na watanganyika. Kodi na rasimali za watanganyika ndio zinatupa maisha wazanzibar.

Rasimali na mapato yetu ya ndani ya Zanzibar hayawezi kutosha kugharamia ulinzi, usalama, umeme na huduma zingine muhimu za kijamii kwa zaidi ya miezi mitatu, tutaangamia!
jamani si mna wajomba zenu arabuni huko? au ndio mlisema ma hizbu chotara
 
Japokuwa huu muungano ni kichefu chefu tu kwa wazanzibar lakini ukweli mchungu ni kuwa, bila huruma na upendo wa Tanganyika basi huenda Zanzibar tusiweze kutoboa hata miezi mitatu.

Kuanzia Ulinzi, Usalama mpaka umeme tunapewa bureee na watanganyika. Kodi na rasimali za watanganyika ndio zinatupa maisha wazanzibar.

Rasimali na mapato yetu ya ndani ya Zanzibar hayawezi kutosha kugharamia ulinzi, usalama, umeme na huduma zingine muhimu za kijamii kwa zaidi ya miezi mitatu, tutaangamia!
Ungekuwa unaongea haya kama Tanganyika ndio wangekuwa wanalalamika.

Umewahi ona wapi kisiwa kikashindwa kujiendesha?

Mwisho aliyeandika hapa ni Mtangangika anajitoa ufahamu tuu
 
Tuna mambo 22 ya Muungano,maana yake ni kuwa tuna Wizara karibu 5 zinahusuka na Muungano moja kwa moja; ulinzi,sheri na katiba,Fedha,mambo ya ndani, utumushi, uchukuzu.

Kwa makusanyo ya Zanzibar ya Bilioni 565? isiyoweza kukidhikuu support bajeti yao wenyewe watatoa wapi hela za kuchangia katika bajeti za hizo Wizara za Muungano.

Wazanzibar kaeni kimya tu,maana mnaigharimu sana Serikali kuliko mnavyo dhania.
 
Inawezekana kipindi kile cha ujamaa miaka ya 1960's Mwalimu aliona Zanzibar ipo kimkakati na itapelekea manufaa kwa Tanganyika, masuala ya usalama, uchumi na siasa zilikua sababu chache.

Na pia Zanzibar waliona hivyo kuwa na muungano pamoja na Tanganyika.

Pengine ilikua ni hatua za mwanzo ya kile viongozi wale waasisi kuiunganisha Africa, wakiwa na fikra Kenya, Uganda n.k zitajiunga siku moja.

Walikuwa na sababu za kujiunga.

Kinachopelekea vijana leo wakose kuelewa kwa nini huu muungano ukawepo ni kwa sababu wazee wale na sisi vijana wa sasa tunatofautiana katika maono.
Mkuu ulichosema ni kweli kabisa, sababu za huu MUUNGANO zilikuwa zimeegemea katika siku moja kuiona THE UNITED STATES OF AFRICA (USA) na mpango wa Nyerere, Nkuruma na Gaddafi ilikuwa kuziona nchi zinazokaribiana kikanda zinaungana kwanza kurahisisha muunganiko wa Afrika nzima hapo baadae, ndiomana unaona baada ya lengo hilo kufa na kubaki nadharia tu miaka yote hii zaidi ya 60 hakuna maelewano mazuri ya kijumuiya EAC, ECOWAS, SADC's etc kila nchi inafanya kitu inachoona kina faida nacho.
Malengo ya wazee na vijana wa sasa ni tofauti, vijana hawaoni umuhimu wa huu muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiwa Zanzibar ni sovereign country while Tanganyika is not. Kama ni MUUNGANO bhasi kuwe na serikali 3 au moja tu itakayoiwakilisha TANZANIA.
 
Ungekuwa unaongea haya kama Tanganyika ndio wangekuwa wanalalamika.

Umewahi ona wapi kisiwa kikashindwa kujiendesha?

Mwisho aliyeandika hapa ni Mtangangika anajitoa ufahamu tuu
Usiongee kwa maneno,ongea kwa takwimu.zanzibar inafanana kwa vitu vingi na visiwa vya Seychelles & Comoro hali za kiuchumi za hizo nchi unazijua?.uchumi wa Zanzibar ni mdogo hawezi kujiendesha watakuwa maskini wa kutupwa.
 
Zanzibar ni nchi mpaka hapo , anakopa kwa uwezo wake atapata mikopo kutoka kwa nchi za Asia kulingana ukaribu wao ...Mega porject ila na nyie mjiandae kurudisha pesa ya uanzishwaji wa BOT.
Zenji wataheshimika zaidi watafika mbali , wana bandari lango la biashara haswa sisi ndugu zao wa kanda ya pwani tutafanya nao biashara sana.
Zanzibar ilikuwepo kabla ya TZ ikaporwa .
Tangu 1964 mpaka sasa Zanzibar ni nchi, na hakuna nchi iliyozuiwa au inayozuiwa kuja kuwekeza mega projects Zanzibar hata sasa. Kwa kifupi suala la uwekezaji sio jambo la muungano. Sasa jiulize, kwanini hao unaosema hawajaja mpaka sasa, kwanini uamini kuwa muungano ukifa watakimbilia kuja kuwekeza Zanzibar?

Kuhusu pesa za mtaji wa uanzishwaji wa BOT zilizotolewa na Zanzibar tulishajibu humu JF. Labda turudie tu kusema.
Thamani ya zile pesa za mtaji ni kiasi gani kiasi cha kuamini ni pesa nyingi?
Mkataba ulitaka Zanzibar ilipwaje fidia?
Zanzibar ni lini tuliwahi kutoa hata senti tano ya uendeshwaji wa BOT?
Faida za kuanzishwa kwa BOT Zanzibar tutawezaje kuzirudisha ikiwa tutadai turudishiwe mtaji wetu?
Hasara ambayo mara kwa mara uliikumba BOT kiasi cha kuathiri mtaji wake wa awali zinafidiaje mtaji wa Zanzibar?
Zanzibar tulitoa lini tena kiasi kingine cha mtaji kuweza kuifufua BOT wakati ilipokuwa imedorora?

Kwa sasa ukanda wa Afrika mashariki Bandari zipo nyingi na zimeendelezwa. Zanzibar hatuna tena upekee wa bandari, tumedorora. Hata sasa bandari iko chini ya SMZ, haihitaji muungano uvunjike ili ipanuke, haina msaada mkubwa sana kama zamani.

Kuhusu undugu, biashara na ushirikiano wa Zanzibar na bara (sio pwani tu), umekuwepo kabla ya ukoloni, wakati wa ukoloni, wakati wa uhuru, kwenye huu muungano na hata baada ya huu muungano, haina issue yoyote kwenye hii hoja yangu. Hapa tunazungumzia jinsi muungano unavyotusitiri wazenji kupitia pesa za wavuja jasho wa kitanganyika.
 
Usiongee kwa maneno,ongea kwa takwimu.zanzibar inafanana kwa vitu vingi na visiwa vya Seychelles & Comoro hali za kiuchumi za hizo nchi unazijua?.uchumi wa Zanzibar ni mdogo hawezi kujiendesha watakuwa maskini wa kutupwa.
Punguani mmja wewe, unadhani Seychelles ni LDC kama Tanzania?

Takwimu zipi? Kama sio Bara kuiba pesa ya Zanzibar,Wanaweza kuwa na Bajeti ya Trilioni 2 Kwa mwaka ,Kitu gani watashindwa kugharania hapo?
 
Hakuna mwarabu ht mmoja ataeitwa, watakuja wenyewe....infact watarudi kuja kuijenga zanzibar yao baada ya kuikimbia. Na waliikimbia baada ya mapinduzi na muungano uso tija kwa wazanzibari. Wanasubiri kwa hamu hio siku ifike
Kwani Zanzibar tulishaacha kuimba mapinduziiiii, daima!
Unadhani tunaimba vile ili kujifurahisha eeeeh?

Tunamaanisha, mwarabu tulimuondoa milele, hatutaki arudi tena pale, na akirudi tutampindua tena. Hiyo ndio dhana kamili ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar.
 
Tatizo linalowasumbua Wazanzibar ni kutaka watengane na Bara ili wajiuze kwa Mwarabu.
Wanafikiri Mwarabu atawapa kila kitu bure!
 
umeandika vitu vingi na kuchanganya mambo. Tuchambue.
Ndio. Ni kwa sababu kuna haja ya kufanya hivyo ili kujenga hoja.
Hoja yangu ni kuhusu wema wa watanganyika kutufadhili wazenji kiuchumi kupitia muungano. Ni ukweli halisi, muungano huu ni kichefu chefu kwa wazanzibar wengi (kwa sababu umenyang'anya uhuru wa Zanzibar, na kupandikiza hadi ugalatia zenji), lakini ni ukweli muungano huu pia umetuneemisha wazanzibar kiuchumi, tunaishi kirahisi kabisa kwa mgongo wa watanganyika.
Hapa ndo sikubaliani kwani hakuna hoja. Hivi Wazanzibari tunaishi kirahisi kwa mgongo wa Watanganyika ? Weka ushahidi wa hili. Huenda hujui kinachoendelea na unasikia maneno yasiyo na ushahidi. Hakuna siku, mimi nasema, Wazanzibari wameishi kwa mgongo wa Watanganyika, na haitotokea. Sababu kubwa ni kwamba Watanganyika hawana moyo huo.
Suala la kihistoria, ni kweli Zanzibar imekuwepo muda mrefu zaidi (lakini ikiwa ni vipande vipande vya visiwa, ni Sultani pekee aliyekuja Zanzibar na kuviunganisha kuwa nchi kiutawala huku akivimiliki kama mali yake binafsi, na hii sio sifa njema ya kujivunia wazanzibar, na ndio maana tulimpindua na mpaka leo tunaimba Mapinduzi daima).
Unapozungumza haya ni kama hujui yaliyotokea hata Tanganyka na kwengineko. Hivi wakoloni walipokuja walikuja kugawa pesa au kutawala? Hivi Nyerere na Karume walikuja kugawa pesa au kutawala?

Hili la mapinduzi naomba nikukumbushe, kama umesahau, kwamba Zanzibar ilidai uhuru kutoka kwa Mwingereza, kwani Wazanzibari (Waafrika na Waarabu) walitawaliwa na Mwingereza, na ndo maana wote- Waafrika na Waarabu- walidai uhuru kwa Mwingereza. Na ni Mwingereza aliyekabdhi bendera ya uhuru tarehe 10 Disemba, 1963. Mara nyingi ukweli huu hausemwi. Unajua ni kwanini? Jiulize halafu huenda utapata jibu.

Nimeyaweka niliyoyaweka kukunesha kwamba Zanzibar inaweza kujiendesha yenyewe, tofauti na unavyotaka watu tuamini.
Kwa sasa ukanda wa Afrika mashariki Bandari zipo nyingi na zimeendelezwa. Zanzibar hatuna tena upekee wa bandari, tumedorora. Hata sasa bandari iko chini ya SMZ, haihitaji muungano uvunjike ili ipanuke, haina msaada mkubwa sana kama zamani.
Hili la bandari ungeliwacha, limekupita kimo. Hivi unajua kwanini Tanganyika inataka kujenga bandari Bagamoyo, sehemu iliyo pua na mdomo na Zanzibar? Jitahidi kufunika kombe ili mwanaharamu apite. Kuna mambo huyajui kwani wewe si mjuzi.
Kuhusu undugu, biashara na ushirikiano wa Zanzibar na bara (sio pwani tu), umekuwepo kabla ya ukoloni, wakati wa ukoloni, wakati wa uhuru, kwenye huu muungano na hata baada ya huu muungano, haina issue yoyote kwenye hii hoja yangu. Hapa tunazungumzia jinsi muungano unavyotusitiri wazenji kupitia pesa za wavuja jasho wa kitanganyika.
Mkuu sasa nimejiridhisha kwamba hujui kuchambua kilichoandikwa. Nilipozungumzia biashara nlkuwa najibu hoja yako uliyodai Zanzibar haina kazi za maana na hata biashara haina, hivyo inaishi kwa mgongo wa Tanganyika.

Zawadini
 
Back
Top Bottom