Ukweli ni kwamba bodaboda ana fursa na anamzidi kipato Mwalimu

Ukweli ni kwamba bodaboda ana fursa na anamzidi kipato Mwalimu

Aliyekwambia walimu wote wamesomeshwa na Loan Board au wana Makato ya benki ni nani

Sent using Jamii Forums mobile app
Anyway asilimia tisini walisoma Kwa mkopo kada ya ualimu wengi wametokea Familia masikini hivyo wanategemea mkopo. Fanya vyovyote ila kama hadaiwi loan board basi take home ni laki Sita. Na huyo wa tgts d3 ni sayansi wa art ni tgts 1 pesa Yao take home ni ndogo
 
wateja wakubwa wa hao bodaboda ni walimu vip kuhusu walimu wenye boda boda zao wanaletewa pesa kwa kutwa huku wakidaka mishaara?
Pia Kuna bodaboda wana pikipiki zaidi ya Tatu wamegawa nawanaletewa hesabu
 
D ni 4 yrs
E ni 3yrs
Kwaiyo mwalimu aliyekaaa kazini miaka 7 anakuwaa amefika F ww unaongele umri wa kustaafu hapa.....Haya mambo unayajua lakini au wewe ni bodaboda

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu mbona unakuwa kama hazimo. Nani kakudanganya madaraja yanapanda tu kama mountaineer. Unapanda daraja baada ya miaka mitano. Mwalimu aliyeanza na tgts D1 baada ya miaka kumi anakuwa F nahapo kama atakizi sifa za kupandishwa daraja maana wengine wana makosa ya kinidhamu. Hata hivyo mbona unakimbilia degree tu kwani wa certificate in primary education sio walimu. Mwalimu wa certificate shule ya msingi anapewa laki Tatu na sabini take home. Sasa Kwa mshahara huu sibora niwe muokota makopo tu
 
Au una ndugu yako mwalimu ana mshahara wa laki tatu? Kama yupo mwambie akasome apayte kshahara kadogo hadi mil 2 kwa mwrzi
Hakuna mwalimu yoyote yule wa sekondari au primary au wakufunzi wa vyuo vya Kati wanalipwa million mbili take home
 
Kuna mjadala unawaka Moto kwenye jukwaa la MMU kuwa Kati ya mwalimu na bodaboda yupi yupo kwenye sehemu nzuri ya kipato na kuendesha maisha yake ya kila siku.

Iko hivi :bodaboda akitulia vizuri na akajenga uamini Kwa wateja Kwa siku hakosa elfu hamsini mpaka sitini ukipiga Kwa mwezi ni mara tano ya mshahara WA mwalimu anaelipwa laki nne au 5 Kwa mwezi. Hata hivyo bodaboda pesa Yao Ina-vary ila Hawa maticha ipo fixed mpaka miaka mitano au sita atakapopanda daraja [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28].

Nafunga mjadara sasa. Mwalimu ni kada ya mwisho kwenye kipato hata muuza magazeti anampita
Yawezekana lakini hebu ngoja....

Mwalimu anafanya kazi masaa 7 kwa siku tano kwa wiki.... Boda akifanya kazi kwa masaa hayo hapindui

Mwalimu ana likizo ya mwaka.... Boda akienda likizo kaumia

Mwalimu akiugua mshahara uko palepale.... Boda akiugua kaumia

Mwalimu akipata dharura bado mpunga unaingia.....

Na kikubwa zaidi, mwalimu anaweza kumiliki na kuendesha bodaboda akitaka lakini boda hawezi kuwa mwalimu

Haya nayo mkayatazame

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Kipimo cha hoja yako yamkini ni dhaifu sana,hatuwezi kupima nani anazidi kipato mwingine kwa kuhesabu nani anapata pesa nyingi kwa mwezi....ila tunaweza kuangalia mambo anayofanya kwa kutumia pesa mfano kujenga, kulima, kufuga, biashara, usafiri, kusomesha, family standard nk....hapo si rahisi bodaboda kumkuta mwalimu labda atakuwa mwalimu wa enzi za kale lakini kwa sasa walimu si viwango vya bodaboda......
 
Khabisa ili iwaongezee mshahara walimu, wanaishi kama mambwa
Nimegungua mkuu wewe ni mwalimu umejaribubkutumia njia hii ya uwasilishaji.

Mimi enz zile tunasoma waliokuwa wa kwanza kiwilaya, kukata au tarafa(wale vipanga) walikwenda ualimu.

Mwisho wa siku vilevile waliishia kuishi maisha duni.


Hata Marais walioshika nchi, mawaziri walimu wameendelea kudharau ualimu.

Wakiambiwa suala ya kuwaongezea mishahara, mawaziri wanasingizia hata kada zingine wanastahili.

Binafsi niligundua kuanzia wathibiti ubora(quality assurer wengine ni empty vichwani. Nilishuhudia wakitoa pumba wakati flani. Hawa hapo zamani waliitwa wakaguzi.

Kuna walimu very intelligent huwezi kuamini. Lakini serikali yao inawaacha wafanye uzalendo miaka na miaka
 
Kuna watu waliikataa kuwa walimu enzi hizo kwa kejeli kuwa walimu ni maskini...leo hii nafsi inawauma sana sasa kila siku wanaanzisha nyuzi za kuwaponda walimu lakini hamna namna walimu wengi sana kwa sasa wamepiga hatua kubwa sana ki maendeleo, wamesalia walimu wachache sana ambao wako nyuma ki maendeleo
 
Kipimo cha hoja yako yamkini ni dhaifu sana,hatuwezi kupima nani anazidi kipato mwingine kwa kuhesabu nani anapata pesa nyingi kwa mwezi....ila tunaweza kuangalia mambo anayofanya kwa kutumia pesa mfano kujenga, kulima, kufuga, biashara, usafiri, kusomesha, family standard nk....hapo si rahisi bodaboda kumkuta mwalimu labda atakuwa mwalimu wa enzi za kale lakini kwa sasa walimu si viwango vya bodaboda......
Kifupi mwalimu na mshahara mdg anafanya mambo makubwa.. asilimia kubwa watoto wa walimu wanasoma shule Bora nchini.

Na wanachokosa walimu ni zile allowance sio kitu kingine. Kwa mfano.

House allowance

Transport allowance

Water bills

Electricity bills

Extra Duty allowance (hapa anafanya duty nyingi tu) Pamoja na teaching

Nk.

Serikali inasingizia kuwajengea nyumba kumbe ni kamba na fix miaka na miaka. Haiwez kuwajengea nyumba walimu wote nchini ni ndoto
 
Maisha hayana formula ni wewe kujituma na kutochaguakazi Kuna wale wenzangu wanaozunguka na bahasha za kaki miezi Hadi miaka wabadilike
 
Back
Top Bottom