Ukweli ni kwamba bodaboda ana fursa na anamzidi kipato Mwalimu

Ukweli ni kwamba bodaboda ana fursa na anamzidi kipato Mwalimu

Hahahahahaaa,umenikumbusha mbali sana.
mbona wako wenye nyumba, naona hapa watu wanachanganya kuna tofauti kubwa ya Boda wa Mjini Kariakoo, Goms, Magomeni Chanika, kinondoni n.k na wa vijijini wabeba mkaa na maji na samakii na wanotembeza nyama kwenye bucha. Inategemea wako walevi na makini na wengine hawajiongezi tu.

Saa 10 usiku mpaka saa 12 asubui boda tayari kesha sambaza nyama bucha kibao na hela ndefu anayo mfukoni anapumzika na kuja kujazia tu baadae, ndio maana utana boda nae pikipikiyake anatoa ajira kwa jamaa wa dei waka. kijiweni kama daladala

Na vijijini kuna hela ndefu ila mafuta bei mbaya hamna sheli. Huko bush maji buku na boda trip 1 anabeba dumu 6. we unafikiri trip ngapi anapiga,na maji anachota bure kisimani na kwenye bomba shs 200


Kifupi tu posta , Kisutu uko trip za Buku chache sana. Ndio maana hata pamoja na kukamatwa na kupigwa mizinga na traffic hawatokii, kuna hela kule.

Jirani yangu hapa ana boda lake sasa ivi yeye hataki abiria tena anasomba mkaa tu mpaka kajenga ana mke watoto 4 na sasa ana stoo kwenye nyumba yake na gunia linakaa siku 2 tu. Hana kazi nyingine.
 
Mpwayungu aka kidagaa mmoja[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] nahisi yale makofi ya uso uliyopata pale ulipofunaniwa na headmaster unaongoza binti wa ticha hayajakuacha salama .
Ndio maana unawachukia walimu
Hhhahaha ivi kumbe
 
Sasa 50000 unaona ni hela kubwa ya kumuuliza mtu anaijua?? Ninaongea sababu ninawafahamu baadhi vizuri na wengi ni marafiki zangu na ninakesha nao usiku mzima kazini kwangu na niwateja wakubwa as ofisi yangu ipo pembeni ya kijiwe chao. So ninarudia tena bodaboda kupata 50000 kwa siku inawezekana ila mchawi wao ni hawana nidhamu ya pesa period.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hajui huyo ni mshamba
 
Ni kweli kabisa mkuu, wengi hawana exposure katika bodaboda 10 unakuta waliomaliza std 7 hata 3. Hata ukiongea nao unaona kabisa huyu hana malengo na maisha kabisa as anajua kesho ataingia road atapata tena hela so hana haja hata kuweka akiba hata akiumwa hana hela ya matibabu.

Kuna siku nilikuwa nawahi makumbusho kwenye training natokea mbezi mwisho, rafiki yangu alinipeleka na bodaboda na hakutaka hata mia kisa tuu ofisini kwangu ndio wanapokula na kupiga stori usiku wanavyokesha imagine ni sh ngapi kapoteza plus muda. Siku wakiwa na nidhamu ya hela ndio watakapofanikiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Hhhahaha eti e
 
Hizo hesabu yeye hapigi kabisaa eti muda sijui nini.
Kuna mzungu nikiwahi mpakia(ni rafiki), nikimfikisha ananiuliza abiria wengine mpaka hapa unawalipisha sh ngapi kwa sasa kisha analipa.
Hakuna ushkaji kwenye biashara.
Yeah sure
 
Kuna mjadala unawaka Moto kwenye jukwaa la MMU kuwa Kati ya mwalimu na bodaboda yupi yupo kwenye sehemu nzuri ya kipato na kuendesha maisha yake ya kila siku.

Iko hivi :bodaboda akitulia vizuri na akajenga uamini Kwa wateja Kwa siku hakosa elfu hamsini mpaka sitini ukipiga Kwa mwezi ni mara tano ya mshahara WA mwalimu anaelipwa laki nne au 5 Kwa mwezi. Hata hivyo bodaboda pesa Yao Ina-vary ila Hawa maticha ipo fixed mpaka miaka mitano au sita atakapopanda daraja [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28].

Nafunga mjadara sasa. Mwalimu ni kada ya mwisho kwenye kipato hata muuza magazeti anampita
Unambwato
 
Mimi nilivyoanza mwanzo nilikuwa nashangaa,masaa mawili au matatu mfuko umetuna bila kuhesabu naanza asubuhi napiga supu chapati ya 4000+soda1000+maji 1000= ni 6000

Mchana nlikuwa nakula biriani ya 4000+ maji 1000+soda 1000 na kutokana na jua mchana nakunjwa maji mengi inafikia mpaka 2000 inakuwa =7000

Jioni mchemsho pale kijwangwani kwa halima wa 2000 na chapati mbili na soda ya 1000 na maji ya 1000= 4000
So nakuja kushtuka nimenenepeana na nimekuwa mzito sanaa kitambi paaa ila akiba ya pesa sinaaa.....
Hesabu ya boss 10,000 kila sikuu.

So biashara hii inakupa pesa ya uhakika na haraka haswa ukiwa muaminifu ila kama unaendekeza mambo utajikuta hakuna kitu unafanya.
Kabisa enjoy mkuu
 
Back
Top Bottom