Ukweli ni kwamba bodaboda ana fursa na anamzidi kipato Mwalimu

Wengi watakuambia kakunja 30000 ila hawajui mafuta ya shiling ngapi yametumika
unajua mahesabu ya kwenye makaratasi na mdomoni ni tofauti na uhalisia inawezekana kuna boda boda anaweza pata 50 on daily basis lakini ni wachache sana bodaboda walio wengi ni 20 tzs
 
688k Kama huna loan board
 
Hao madam na pombe unaweka pension wapi?ushawishi ni mkubwa sana wewe.
Unaongelea watoto wajinga wajinga.

Ila kuna bodaboda watu wazima na wanaendesha familia bila tatizo.

Suala la kujikatia bima na kuweka pensheni sio la bodaboda peke yake.

Informal sector yote hawana huo utaratibu. Na hela wanapata ya kutosha tu.
 
Kama kitu hujui kaa kimya, usikaririshwe na maneno ya mtaani. kuna walimu wanakunja Zaid ya mil 1.5 kwa mwezi, anaweza kukopa Zaid ya mil 50 akafanyia biashara. Lakini kubwa Zaid maisha ni namna mtu amejipanga sio kipato anachopata, kuna watu wanalipwa kidogo na wamepiga hatua kuliko wanaolipwa vizuri.
 
Mwalimu gn huyo anakunja hiyo, madeni tupu wananuka
 
Unaongelea watoto wajinga wajinga.

Ila kuna bodaboda watu wazima na wanaendesha familia bila tatizo.

Suala la kujikatia bima na kuweka pensheni sio la bodaboda peke yake.

Informal sector yote hawana huo utaratibu. Na hela wanapata ya kutosha tu.
Kabisa kiongozi Hawa shida Yao wanakariri maisha
 
Mmmmh mbona naiona ndogo sana mkuu.
Ndogo kama unaenda kuhonga na kuleweya na marafiki, ila kwa maisha ya mjini hicho ni kipato kinaendesha familia ambayo ina amani na furaha na msikitini au kanisani wanaenda kushukuru Mungu kwa riziki wanayopata

Kumbuka

Mjini fungu la mchicha mia mbili Kuna sehemu wanauziwa shilingi mia

Fungu la nyanya elfu moja Kuna sehemu wanauziwa mia tatu na mjini

Sahani ya wali maharage na nyama shilingi elfu tatu mia tano Kuna sehemu wanauziwa buku tu na ubora ulele

Suruali ya jeans 👖 ya elfu sabini Kuna sehemu wanauziwa elfu kumi na tano

So ukiwa mjini uliza wenyeji utafurahi
 
Hizi alfu hamsini ni mahesabu ya uhalisia,au kwenye makaratasi?
 
Nadhani ulimaanisha Exposure..na haipatikani shule tu mdogo angu, hata hapa ipo tatizo ni ugeni 👍
Jibu hili kama aliyejibiwa yuko sawa kichwani basi hatuwezi kumuona kesho, lazima ajinyongelee mbali.
 
Vitu vingine ni kichekesho em pita kijiwe cha bodaboda apo waulize anaetaka kuajiriwa na serikali awe mwalimu au aendelee na iyo bodaboda utapata majibu ajira usawa huu uidharau et useme boda boda inalipa.
 
Primary to sekondari
Mwalimu wa sekondari anaye anza ajira anaanza na TGTS D ambayo ni Tsh 790,000/= ambapo baada ya miaka mitatu anapandishwa na kulipwa Tsh.990,000/= na kila baada ya miaka 3 anapdishwa na wapo wanalipwa 3mil + sasa hiyo ya laki nne sijui huwa mnamuongelea mwalimu yupi huwa nawaona ni wajinga fulani hivi msio soma mnao bwabwaja msio yajua
 
Mimi boda ambae napiga madili yangu kwa siku nakunja themanini had laki na nusu siku ikiwa poa
Sasa we boda mwenzangu endelea kusubili abiria wa kugombania kijiweni ukiitafuta buku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…