Ukweli ni kwamba bodaboda ana fursa na anamzidi kipato Mwalimu

Ukweli ni kwamba bodaboda ana fursa na anamzidi kipato Mwalimu

Kuna mjadala unawaka Moto kwenye jukwaa la MMU kuwa Kati ya mwalimu na bodaboda yupi yupo kwenye sehemu nzuri ya kipato na kuendesha maisha yake ya kila siku.

Iko hivi :bodaboda akitulia vizuri na akajenga uamini Kwa wateja Kwa siku hakosa elfu hamsini mpaka sitini ukipiga Kwa mwezi ni mara tano ya mshahara WA mwalimu anaelipwa laki nne au 5 Kwa mwezi. Hata hivyo bodaboda pesa Yao Ina-vary ila Hawa maticha ipo fixed mpaka miaka mitano au sita atakapopanda daraja [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]. Nafunga mjadara sasa. Mwalimu ni kada ya mwisho kwenye kipato hata muuza magazeti anampita
Uko sawa, walimu waache kazi wakapige bodaboda ambayo kwa siku wataingiza elfi 50 hadi 60!!!!

Umetisha mpwayungu. Mwalimu aliyekuchapa ataipata, na siku ukipata mwanya utamtoa Uhai!
 
Bodaboda anayekunja 50K hadi 60K kwa siku anapakia mawaziri au akina nani?
Tuache kuleta uongo wa kingese kiasi hiki hapa JF.
Kila sehemu kuna rundo la bodaboda inakuwaje hadi bodaboda mmoja apate average ya 60K kwa siku? Au anabeba wahamiaji haramu au mirungi au bangi?
Mleta mada umeamua kuja kujipa mashavu hapa JF!!?
Kuna bodaboda wana vichwa vyao vya asubuhi na jioni yani go and return. Unakuta anapoamka tu saa kumi na moja ana vichwa vyake kumi vya kila siku kuwapeleka na kuwarudisha kutoka kazini.

Tufanye kila kichwa ni buku nne yani kwenda buku mbili kurudi buku mbili hapo sijapiga hesabu wa buku tano nawale wakudaka njiani na kijiweni
 
Uko sawa, walimu waache kazi wakapige bodaboda ambayo kwa siku wataingiza elfi 50 hadi 60!!!!

Umetisha mpwayungu. Mwalimu aliyekuchapa ataipata, na siku ukipata mwanya utamtoa Uhai!
Umeharibu hapo mwisho. Ujinga wa walimu haunifanyi niwachukie Bali nawadharau
 
Mshakaa na boda boda mkawauliza? Mtafute bodaboda muulize kama hiyo 50elfu anapata kwa siku.

Zamani bodaboda walipiga pesa si siku hizi, mtaani vijana wanalalama.
Yaani awe ameshakula, ameweka mafuta, apeleke hesabu kwa bosi kisha abakiwe na 50 elfu [emoji23]

Siku hizi akitoa hesabu, mafuta, na kula yake kuipata 15 tu kazi.
Nina kama mdogo wangu ambae hapo awali alishaendesha pikipiki zangu kabla ya kuachana na hii biashara kichaa.
Sijui mapato ya walimu ila nawajua bodaboda kiasi chake.
Kuna wengine wanamiliki bodaboda zao sio ya boss
 
Kuna bodaboda wana vichwa vyao vya asubuhi na jioni yani go and return. Unakuta anapoamka tu saa kumi na moja ana vichwa vyake kumi vya kila siku kuwapeleka na kuwarudisha kutoka kazini. Tufanye kila kichwa ni buku nne yani kwenda buku mbili kurudi buku mbili hapo sijapiga hesabu wa buku tano nawale wakudaka njiani na kijiweni
Inawezekana kwa siku chache kupata hiyo pesa lakini sio daily net income yake iwe 60K.
Kumbuka bodaboda haitumii maji.
Ingekuwa rahisi bodaboda kupata kipato cha 60K kwa siku graduates wasingejazana huku mtaani na kuwa ombaomba na malaya kwa kasi ya 5G.
 
Kama boda boda pikipiki ni yake anamzidi . Sababu wastani hapo ni kama 16,000/ kwa siku. Mi Namjua dereva mmoja wa boda ya mkaa analipa kila siiku 15, kwa boss wake nae anapata ya kula na kuishi. Hata wanao uza maji tu wana hela ndefu kwa siku. Mwalimu anajazia tuiton na vi semina vinginevyo ananufaika na bima ya afya na pesheni akistaafu lakini kula nyama tu kwenye bucha inabidi achungulie mfukoni sababu kg1 ni 9000/= bila viungo shida sana ajira jamani. labda awe na mshahara wa laki 8 mbele hukoo
Umeongea point. Chakula cha walimu ni ugali maharage tu tangu nikiwa mtoto. Mchele mpaka atoke town kuchukua mshahara anashuka kwenye bus na mkate mreeefuu
 
Inawezekana kwa siku chache kupata hiyo pesa lakini sio daily net income yake iwe 60K.
Kumbuka bodaboda haitumii maji.
Ingekuwa rahisi bodaboda kupata kipato cha 60K kwa siku graduates wasingejazana huku mtaani na kuwa ombaomba na malaya kwa kasi ya 5G.
Hawana mtaji wa kununua pikipiki. Saizi boxer au tvs Mpya inakimbilia million 3
 
Mshakaa na boda boda mkawauliza? Mtafute bodaboda muulize kama hiyo 50elfu anapata kwa siku.

Zamani bodaboda walipiga pesa si siku hizi, mtaani vijana wanalalama.
Yaani awe ameshakula, ameweka mafuta, apeleke hesabu kwa bosi kisha abakiwe na 50 elfu 😂

Siku hizi akitoa hesabu, mafuta, na kula yake kuipata 15 tu kazi.
Nina kama mdogo wangu ambae hapo awali alishaendesha pikipiki zangu kabla ya kuachana na hii biashara kichaa.
Sijui mapato ya walimu ila nawajua bodaboda kiasi chake.
Achana na hawa bodaboda wa vibarazani Kuna bodaboda wa bolt na uber hawa jamaa wanapata hela sana kwa siku kukunja elfu 40 ni kawaida
 
Haya tuanzie hapa
A. Mwalimu ana uwezo wa kuajiri bodaboda zaidi ya 10.
B. Mwalimu ana uwezo wa kupata fursa nyingi zaidi kupitia elimu yake.
C......
Sio kweli. Pikipiki moja tu ni mitihani
 
Back
Top Bottom